Magufuli anachukua nchi kimya kimya Octoba

Magufuli anachukua nchi kimya kimya Octoba

upo nyuma ya muda wewe
na km hutaki mabadiliko basi jua kuwa hayakusubiri wewe .
 
MAGUFULI: KIONGOZI WA AINA YAKE
Sipendi sana kujadili watu. na hapa najadili katabia tu nilikokaona kwa kiongozi huyu.
Magufuli ni kiongozi wa ajabu. Ameanza kuliongoza taifa kiaina. Magufuli ameishachukua form ya kuomba kugombea urais kwa tiketi ya CCM kutoka kwa tume ya taifa ya uchaguzi NEC. Nilijua kuwa atachukua form kutoka NEC baada ya kuichukua na nishtukia naona picha za misafara ya waliomsindikiza. Sijui walijuaje? Kama angetangaza kuwa siku fulani na saa fulani atachukua form sijui watu wangekuwa kiasi gani?

Yeye ameishakamilisha kazi ya kuwapata wapiga kura wa kumdhamini. Majuzi nilishtukia yuko Bukoba mjini amekuja kutafuta wapiga kura wa kumdhamini. Watu wachache walijua na wengine nilisikia wakilalamika kuwa kwa nini haikutangazwa ili wakafurike. Naona anatumia mtindo wa CHEMA CHAJIUZA KIBAYA CHAJITANGAZA. Nao (mtindo wake) una maana kubwa kwa nchi yetu, maana kelele zimetufikisha pabaya. Nakumbuka wakati wa Mkapa ilikuwa kama hivi hivi. gazeti la Uhuru siku ile amechukua form habari ilitoka kushoto chini ya ukurasa wa mbele ikiwa na kichwa cha habari '------ Na Mkapa achukua form' Ilikuwa habari ya mengineyo. Niliyaona 1995. Nayaona na 2015.

Gwamaka mdogo wangu endelea kupiga rangi upepo hivi ni kweli safari ya magufuli kwenda NEC ilikuwa siri? Ndiyo maana mpk JK akaamua kumsindikiza? Kuna kitu kimoja ambacho CCM mkikubali uwezo wa kumobilize watu mpo chini ukilinganisha na chadema kuna sababu nyingi kupoteza mvuto na organization mbovu ya viongozi wenu.
yawezekana kuna mengi ya ndani ya chama chako huyafahamu ila hali ni mbaya sana ila wanajikaza kisabuni.
 
Usisahau kuwa ni huyo huyo anaesimamia ujenzi wa daraja la Kigamboni.

Ambalo mmeshindwa kulimalizia baada ya pesa yake kuichota na kuipeleka kwenye maandalizi ya kampeni yake
 
Mwaka 1995 (Wakati wa Mrema ni tofauti kubwa sana na leo )kipindi kile Mwalimu JK ilibidi azunguke nchi nzima kumpigia debe Mkapa,Mrema alipata zaidi wanasheria baada ya kuwa na akina Mabere Marando,Masumbuko Lamwai nk wanachama wa Ccm na viongozi hawakumfuata wengi hivi (kama EL)Kipindi kile vyombo vya habari hawakumpa Mrema 'Coverage 'ya kutosha pia kulikuwa hakuna Social media kama sasa.EL atakuwa Unguja kubomoa ngome ya Ccm trh 17,Pemba yenyewe ni ngome nzito ya CUF ambayo ata Mwalimu JK hakuweza kuibomoa hii maana yake ni kuwa SS HAMAD ataanza kusherehekea saa 8 mchana !!!Bara sherehe tutaanza jioni saa 1.
kama hatakuelewa tena, asubiri tarehe 25 October 2015 ili tumdhibitishie
 
Atachukua nchi kwa kutumia sanduku la kura,au goli la mkono,au atatumia nguvu ya dola?fafanua vizuri!
 
Nilicheka sana jana vijaana wakiimba ....kama sio Kikwete Lowasa tungempata wapi.............
 
Magufuli hawezi kuchukua nchi kama unavyodhani.
Mwaka huu mgumu sana kwa CCM.
 
Back
Top Bottom