Magufuli amekosea wapi, mbona 'anachuja' haraka?

Maskini Magufuli ana nia njema sana na nchi hii tatizo sijui ni mbinu anazotumia au ni wanaomshauri binafsi kuna vitu namuelewa sana ingawa hili la uhuru wa vyombo vya habari simuelewi kabisaaaaa
****
NINGEKUWA MAGUFULI VYOMBO VYA HABARI NINGEVIPA UHURU ZAIDI NA ULINZI MAALUM, MAANA NDIVYO VINAVYOFUNUA UOVU ULIO CHINI KABISA / AU KUJIFICHA.

unless otherwise tunashindwa tambua dhamira yake ya ndani.
 
Ili uthibitishe haya maneno yako kuwa Magufuli kachuja au lah nenda mtaani alafu ukikuta kikundi cha watu tamka haya maneno kuwa "Magufuli hafai".. Kitachokutokea kutoka kwa wananchi usisite kuja kutuambia ata kama ukiwa ICU.

Huko kitaani kwenu kwa washua nini?
 

Nafuatilia kauli ya Nyerere ya Makabila ambayo hayawezi kushika urais Kama ilikuwa ya kweli. Mojawapo lilikuwa ni hili la Huyu Jamaa.
 
Mbona mtoa post na wachangiaji hamjielewi? kwa miezi 7 aliyoyafanya ni makubwa sana, lakini ni muda mfupi kubadilisha nchi na watu kufaidi au kupata ahueni ya maisha, halafu budget ndo hiyo kwanza hata haijapita mmeanza kelele, kumbukeni wafanyabiashara pia wanataka kua juu ya serikali kwa kuficha sukari ili wajipangie bei, JPM bado anajipanga kwa mambo mengi , utumbuaji ( kuwasimamisha watu Kazi) lazima iwe kazi endelee mpaka tuheshimiane.
 

Povu la nini? Si ujibu tu hoja kisha jenga hoja ya kutokubaliana na hoja hiyo kwamba Rais wetu mtukufu utukufu wake na sifa zinazidi kupanda juu na si kushuka? Kadiri unavyotukana unaonyesha udhaifu wako
 
....

.....njaa haina simile !!!
 
Dhulma ndo inamtafuna, na itaendelea kumtafutana hadi akwishe kabisa!
 
Hizi story nyingine nafikiri hapa sio mahali pake, hii ipeleke kijiweni kwenu utapata majibu haraka sana
 
Tatizo ni kuwa ameshindwa kufanya kazi kimfumo zaidi ya ziara za ghafla sasa zikikosekana anaonekana kama yupo hayupo. Ziara za ghafla ndio zimemtambulisha na yeye kajitambulisha nazo. Hivyo ni lazima aendelee kufanya ziara za ghafla ili watu wajue yupo shida ni kuwa sehemu za kwenda ghafla zikikosekana hapo itakuwa ni shida itabidi aanze hata kwenda mikoani
 
Kwa mjadala mzuri naomba unapochangia, jikite kwenye hoja sio kujikita kwenye itikadi za vyama. Mheshimiwa Magufuli Ni rais WA wote, akifanya vyema sote tunanufaika, ikitokea amefanya vibaya huwezi kukwepa sehemu ya matokeo hayo.
Lengo ni kutaka kuwa na nchi ambayo kila mmoja anatimiza majukumu na wajibu wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…