Magufuli amekosea wapi, mbona 'anachuja' haraka?

Magufuli amekosea wapi, mbona 'anachuja' haraka?

Born in Austria in 1889, Adolf Hitler rose to power in German politics as leader of the National Socialist German Workers Party, also known as the Nazi Party. Hitler was chancellor of Germany from 1933 to 1945, and served as dictator from 1934 to 1945. His policies precipitated World War II and the Holocaust.

So what? Do want war? Then try to start one.
 
Kuna sababu kama 4 hivi naziona ndizo zinazomfanya achuje haraka hivi:

1. Kushindwa kwake kudili na majipu (wala rushwa wakubwa) na kubaki kuangaika na kesi za kuku. Hii imejionyesha kwa yeye kunywea kwenye swala la Lugumi, Wezi wa Escrow (kutekeleza maamuzi ya Bunge), kuendelea kukumbatia viongozi majizi, HSC na mambo kama hayo.

2. Kuendesha nchi pasipo kufuata utawala wa sheria. Anajiona yeye ndio ultimate decision maker wa kila kitu na hakuna anayejua zaidi yake. Sasa watu wameamua kumuacha afanye kazi zoootee peke yake.



3. Nchi kukosa muelekeo wa kiuchumi. Hii inapelekea kuwa na hali ngumu pasipo sababu. Bado anaangaika na kodi za machinga na mama Ntilie, wakati kule kwenye madini wanawaanchia wazungu wanachukua madhahabu na Almasi bureee kabisa. Hana vyanzo vipya vya kodi zaidi ya kumbana mwananchi wa kawaidi.

4. Kunyima Uhuru wa habari. Hii imejionyeshwa kupitia kukataa kuonyesha Bunge Live kwa sababu ya kuogopa wananchi kuona serikali yake ikikosolewa. Yeye anataka kusifiwa tu, ukimkosoa ni shida.
"Kila anaekosoa SERIKALI yangu ujue huyo ni shetani" ova
 
Mangikule ameleta mambo ya Hitler na world war II ya nini hapa? Ask him not me!
Tulia, poa moto kwanza...umepanic na bado hutaki kujitathmini. Hitler hakuzaliwa na wazo la kuwa dikteta.

Hebu rejea ulichoandika. (So what. Do want war. Then try to start one).
 
Akiwa Singida kwenye miaka 34 ya CCM alisema chama kwanza mengine baadaye.Tafakari.Hapo ndipo nilipomalizia yale niliyokuwa nayafikiria.............
Na wakati anapewa kiti alitamka, kiongozi au taasisi ya serikali isipomtambua kiongozi wa chama ata-deal naye/nayo
 
Sa hv ana piga kazi za kutumia akili ambazo waandishi wetu hawana uwezo nazo kuzifanya ziwe taarifa.

Huwezi kuanzisha viwanda huku unapiga maneno vyombo vy habari
 
Mzigo ushamshinda, au nyie hamjashtuka??? Zile CT Scan na MRI za Muhimbili magumshi tena, pale Bugando ndo walishasahau kabisa
 
Hivi kwa nini wazee walisema mzigo mzito mpe Mnyamwezi na hawakusema mpe Msukuma? Najiuliza tuu
 
Mwanzoni mwa utawala wake ilikuwa kila gazeti linamwandika yeye tena vizuri. Vijiwe vyote kuanzia vya kahawa, daladala, bar na maofisini story alikuwa ni yeye tena watu wakimsema kama malaika mkombozi.

Ghafla upepo ukabadilika, watumishi wakaanza kukosoa utumbuaji majipu, wafanyabiashara wakakosoa mbinyo wake kwenye kodi, wanasiasa wakahoji style yake ya uongozi. Wananchi wa kawaida wakanigwa na maisha magumu (ingawa hawa bado wamebakiza kaimani fulani). Vyombo vya habari wanalalamikia kuminywa uhuru wao.

Kiujumla upepo unavuma vibaya kwa JPM naye ameshakiri ugumu wa kiti chake mpaka akasema angejua asingegombea urais. Je, rais wetu amekosea wapi mpaka hali imegeuka mapema hivyo?
Akiachia democracy tu,mambo yatemwendea unono otherwise atakwama
 
M
kutaka kukibeba chama cha mapinduzi,ndiyo gharama kubwa aliyeifanya mpaka kupoteza umaarufu wa kisiasa!
Magufuli amekosea kuziba nafasi ya mafisa na wakwepa ushuru nakurudisha uwajibikaji kazi. Hadi mafisadi yanaanzisha maoperation yasiyo na akili haaaahaaa. Magufuli chapa kazi tu Mungu yupo pamoja nawe. Amina
 
Siamini kama duniani kwa sasa hivi kuna nchi ina Rais hewa kama huyu wa kwetu!
 
Back
Top Bottom