Magufuli amekosea wapi, mbona 'anachuja' haraka?

Magufuli amekosea wapi, mbona 'anachuja' haraka?

Mwanzoni mwa utawala wake ilikuwa kila gazeti linamwandika yeye tena vizuri. Vijiwe vyote kuanzia vya kahawa, daladala, bar na maofisini story alikuwa ni yeye tena watu wakimsema kama malaika mkombozi.

Ghafla upepo ukabadilika, watumishi wakaanza kukosoa utumbuaji majipu, wafanyabiashara wakakosoa mbinyo wake kwenye kodi, wanasiasa wakahoji style yake ya uongozi. Wananchi wa kawaida wakanigwa na maisha magumu (ingawa hawa bado wamebakiza kaimani fulani). Vyombo vya habari wanalalamikia kuminywa uhuru wao.

Kiujumla upepo unavuma vibaya kwa JPM naye ameshakiri ugumu wa kiti chake mpaka akasema angejua asingegombea urais. Je, rais wetu amekosea wapi mpaka hali imegeuka mapema hivyo?
Eti kachuja? Kachuja saizi kona zote wanamuishi Magufuli yuko tu akili mwa watu.
 
1. Wakwepa kodi hawataki hata kumuona na ndio walikuwa wasemaji saaana mtaani maana walikuwa wanatumia vilivyo
2. Wezi kupitia watumishi hewa pressure juu hawajui wataishia wapi maana mafaili yao yanaandaliwa
3. Wezi wa hela za mikopo ya wanafunzi eimu ya juu walikuwa kelele nyingi mtaani sasa matumbo joto wakimuona kwenye tv wanatamani wapige magoti waombe msamaha
4.Wapiga kelele za kisiasa wamekosa ajenda, maana umaarufu wao ilikuwa ni kutukana serikali ndo wanapata umaarufu
5. Machangudoa wameshusha bei saa hii hata wakito kwa buku wanakosa wateja, hela za magumashi zimeminywa
6. Maguest house yaliyokuwa yanalaza short time kuuza kitanda mara 5 usiku mmoja sasa kwishney
7. Msululu wa watumishi wa umma kwenda kufanya shopping dubai week end sasa Emirates wamepunguza safari za kuja kubeba wezi Tanzania
8. Wauza unga wameingi kibano kiasi umaarufu wao mtaani wanauogopa kama ukoma
TANGU UHURU, SERIKALI AWAMU YA PILI NA YA NNE NDO ZILIKUWA MAARUFU KUPINDUKIA KWA KUWA YOTE YALIYOTAJWA HAPO JUU YALIPATA CHAT ZA JUU KWA GHARAMA YA UCHUMI WA TAIFA. KWA HIYO WAHUSIKA WOTE HAO WAKIFYATA MKIA UJUE TU PUBLICITY YA SERIKALI INAYOJALI WANYONGE HAIWEZI KUWA MAARUFU, MAANA HAO HAWANA UWEZO HUO WA KUCHEZEA AIRTIME ZA TV/RADIO NA KULIPIA KURASA ZA MAGAZETI. HAVUMI LAKINI YUPO. UKIMTAFUTA UTAMPATA
 
Urais ni fikra sio nguvu,pushups ziliashiria matumizi ya nguvu.
Urais hautaki mabishano na asiyekuwa rais.
Urais unataka rais awe na utii wa sheria na katiba.
Ukiminya mtu mdomo utaonekana unamuonea,uonevu unafanya usipendwe na wengi.
Rais wetu amekuwa na sifa mbaya ambazo wanazozieneza ni wanaccm mfano.Rais hashauriki hii si kauli nzuri toka kwa chama chako.
mh.aliharibu tangu ile siku kule kigamboni alipouliza NITUMBUEEE.........wananchi nao wakajibu TUMBUAAAAA.
hapo sasa pongezi zikaanza kudrop day after day mpaka leo hii siku inapita husikii jina la mh.katika radio wala TV.
 
Mpinga Ukut** Nchi imemshinda sababu ya Woga hata sijui anatishwa na nini
 
Zile push ups na waliozishangilia walionyesha upeo mdogo sana wa kufikiri
 
Viongozi wa vyama vya upinzani kukosa hoja za mshiko (maslahi mapana kwa jamii) ni kithibitisho Rais utendaji wake uko makini.

Mwanzo wa utawala wake aliweka vigezo vya utendaji (akitafsiri kaulimbiu yake hapa kazitu kwa vitendo). Wateule wake kwa sasa ndo kazi yao.
 
Mpinga Ukut** Nchi imemshinda sababu ya Woga hata sijui anatishwa na nini
Born in Austria in 1889, Adolf Hitler rose to power in German politics as leader of the National Socialist German Workers Party, also known as the Nazi Party. Hitler was chancellor of Germany from 1933 to 1945, and served as dictator from 1934 to 1945. His policies precipitated World War II and the Holocaust.
 
Jibu hoja utakuwa umemsaidia yeye na taifa, mashambulizi kwa mtu aliyeonyesha kile kinachoonekana hayasaidii
Rais alikuwa kwenye vichwa vya habari alipokuwa akitoa maagizo. Sasa ni zamu ya watendaji kuchacharika. Wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa wilaya, wa mikoa na mawaziri ni habari kila pembe ya nchi. Ulitaka rais aseme nini tena?
 
Back
Top Bottom