Magufuli amekosa exposure

Magufuli amekosa exposure

Katika sifa kadhaa za mgombea urais kwa tiketi ya ccm huwa ipo ya awe na uzoefu wa masuala ya kimataifa.

sifa hii kwa JPM ilifumbiwa macho,
Nyerere baada ya kusoma nchini alikwenda makerere Uganda na baadae uingereza kunoa Bongo mwinyi alishawahi kukaa Misri ubalozini kwa miaka kadhaa,Mkapa ndio usiseme canada na marekani amekaa sana,JK ziara zake nje ya nchi akiwa foreign affairs minister kwa miaka kumi na miaka kumi ya urais wake ni sawa na kukaa nje miaka mitano,(siungi mkono,it was too much)

JPM alikanyaga Dar es salaam kwa mara ya kwanza mwaka 1984 alipokuwa anakuja kujaza fomu ya kujiunga na UDSM,tangu hapo hajawahi kukaa nje ya nchi kwa zaidi ya mwezi mmoja Amezunguka vichochoro vyote vya Tanzania alipokuwa waziri wa ujenzi akikagua barabara,kazi aliyoiweza kuliko mawaziri wote tangu uhuru .

Back to the point,mimi nimezaliwa Dar Es Salaam na enzi za ujana wangu nilikuwa najiona mtoto wa mjini sana ila siku nilipokanyaga Manhattan mwaka 2002 nilijiona ni mshamba sana kila kitu nilikiona ni kipya na tangu siku hiyo nikajua Dar Es Salaam sio jiji bali ni mji tu.

Wazungu wanakitu wanaita exposure , huwa ni shule tosha kwa tuliosoma zamani tunajua ,mtu wa mtwara kuchaguliwa sekondari wilaya ya Ngara japo kwa upande mmoja ilichangiwa na uhaba wa shule ila ilitusaidia sana,kwa sasa kuna wanafunzi wanazaliwa ndani ya wilaya x,primary mpaka sekondari anasomea ndani ya wilaya hiyohiyo na chuo cha ualimu hapo hapo na anakuja kufundisha shule ndani ya wilaya hiyohiyo ,huyu anakosa exposure atakuwa mshamba tu.

Pia kwa waliopitia vyuo vikuu vya Tanzania mtagundua kuwa lecturers walipata elimu yao nchini bila kwenda nje ya nchi huwa wanakamata sana wanafunzi wakati wa mitihani kuliko walimu waliosomea nje.(sina uhakika kama kutumbua majipu yanhusiana na kukosa exposure )

JPM anasema anataka Tanzania iwe nchi ya viwanda sasa nashangaa itakuwaje nchi ya viwanda wakati anawakimbia wazungu ambao ndio wenye technology ya viwanda,kama hadi pampas za watoto tunaagiza tukubali hatuwezi kujenga viwanda bila kuwa karibu na wazungu,awakaribishe wakae mezani waongee dili win win based business,wanatuhitaji pia bado tunawahitaji,ndio maana Nyerere na kuwatimua kote waingereza alifia kwao akukubali kufia Muhimbili

Pia JPM amekaliliwa akisema Dar ndio kioo cha Tanzania ndio maana anataka kujenga daraja toka cocobeach mpaka ocean road,hii ni kukosa exposure,nchi za watu maendeleo huwa yanakuwa balanced na pia fursa zinakuwa balanced kila sehemu kupunguza msongamano wa watu kwenye miji fulani,kuna baadhi ya nchi watu hawataki kuishi miji mikuu kwani fursa ziko kila kona,Juzi tumesikia kuwa Obama atakuwa rais wa pili wa marekani kuishi washngtone baada ya kustaafu na hii ni kwa sababu watoto wake bado wapo shule,other wise angerudi kwao chicago,JK wakati anakabidhi ikulu na kutuaga kuwa anarudi kijijini helicopter ilimpeleka Msoga mchana jioni akarudi nayo Dar.

Tanzania sio Dar tu
Pia exposure inasaidia kuimprove lugha za kigeni,hili sitaki kuliongelea sana hapa nisije kuchafua jukwaa
Acha JPM afagie na kupanga nyumba yake kwanza ili siku ataanza kwenda huko nje baada ya kufagia na kupanga nyumba yake vizuri ili akaongeze huo ujuzi mwingine ili akirudi aboreshe zaidi. Ni kukosa busara kuanza kwenda kutembelea tembelea majirani wakati nyumba yako ni chafu. Sipingani na wewe.
 
Kwahyo aende US, China kufanyaje labda zaidi ya kutembeza bakuli. Bila kujijenga ki ndani na kuimarisha mambo ya ndani ka elimu, miundo mbinu hata ahamie China nothing will change sasa nyie waumini wakuwa dependence ndo mnataka awe mzururaji mbona mlikuwa MNA mnanga mkwere
aende akaibe au akanunue technology
 
Sikatai ila hao tangia wawekeze wameacha technology gani kama huko migodini je niwa Tanzania wangapi wanaruhisiwa kupata hyo knowledge wanayoitumia ka sikuajiri experts kutoka nchini kwao na Watanzania kuwa vibarua tu. Nenda huko gesi ilipovumbuliwa ka kuna Mtanzania ana ruhusiwa kijua kinachoendelea. China, Singapore, Taiwani, south Korea tulikua almost the same ila nao wametuacha mbali. Wale walirndeleza internal capability, innovation na Ku ji invest kwenye elimu na kupata experts. Ili kuendelea lazima tuendeleze wazawa kwa kuwazesha. Na tutumie foreign experts kubenefit nchi sio makampuni yao
mkapa na JK walitumia vibaya exposure yao wakawa vibaraka wa wazungu wakachemsha JPM awekinyume nao awakomalie wazungu wasitunyonye kila mtu afaidike
 
aende akaibe au akanunue technology
Yeye ataibàje bila kuwa na vision ya kitaifa ya kimaendeleo na Ku invest kwenye technical change na implementations ya issue zetu. Bila hivo kamwe tusipovifuata hatutapiga hatua hata akia nje ya nchi. Aanzie ndani
 
mkapa na JK walitumia vibaya exposure yao wakawa vibaraka wa wazungu wakachemsha JPM awekinyume nao awakomalie wazungu wasitunyonye kila mtu afaidike
Jk yeye alikua ka ndege angani na kula bataz had kubembea
mkapa na JK walitumia vibaya exposure yao wakawa vibaraka wa wazungu wakachemsha JPM awekinyume nao awakomalie wazungu wasitunyonye kila mtu afaidike
Jk yeye alikua ka ndege angani na kula bataz had kubembea kah magufuli akomae na huku ndani
 
Hii exposure ni mdudu gani? Mbona hao ulio wasifia wako na huo mdudu ndoo wametufikisha hapa tulipo.afadhali tuwe na raisi asiye kuwa na hilo dubwasha exposure kutuletea matapeli uchwala (wawekezaji)ndoo maana siku moja nilisema watz ni dead head.kuna njia nyingi za kujikwamua bila kuwategemea wazungu.mmoja mmoja, makundi.mwisho,tunavusha taifa
 
Ww ulioandika mm cjakuelawa unamaanisha nini kama lugha ya kingereza cc sio waingereza wananchi tunataka vitendo na uchapakazi ndio maana tuliokua na viongozi wabovu kwa kuangalia kingereza anagalia wabunge wameishia kidacho cha nne tazama wanavyotoa mada zilizomakini wakati hao walisoma masomo ya juu na mavyeti kibao wanafanya utumbo kila cku.mtu hajatoa mada wala kijibu hoja mpaka kikao kinakwisha na kingereza kama amezaliwa nacho acha hizo kingereza nikama lugha nyingine.cc tunataka kiongozi atakaeweza kuingoza vile tunavyotaka wananchi hasa wakipato cha chini nafikiri tumempata maraisi watatu wamepita lkn hawawezi kumfikia Magufuli ni mtu aliyejitolea muanga juu ya nchi yake.Mungu mpe maisha marefu.
 
Ww ulioandika mm cjakuelawa unamaanisha nini kama lugha ya kingereza cc sio waingereza wananchi tunataka vitendo na uchapakazi ndio maana tuliokua na viongozi wabovu kwa kuangalia kingereza anagalia wabunge wameishia kidacho cha nne tazama wanavyotoa mada zilizomakini wakati hao walisoma masomo ya juu na mavyeti kibao wanafanya utumbo kila cku.mtu hajatoa mada wala kijibu hoja mpaka kikao kinakwisha na kingereza kama amezaliwa nacho acha hizo kingereza nikama lugha nyingine.cc tunataka kiongozi atakaeweza kuingoza vile tunavyotaka wananchi hasa wakipato cha chini nafikiri tumempata maraisi watatu wamepita lkn hawawezi kumfikia Magufuli ni mtu aliyejitolea muanga juu ya nchi yake.Mungu mpe maisha marefu.
mtoa mada hajaongelea kuhusu masuala ya lugha bali technology ya wenzetu kuwa ipo juu kuliko afrika
 
Haaa haaaa umenifurahisha eti Vasco alipondoka na Chopa kwenda Msoga asubuhi jioni karejea nayo Dar haaa haaa Mzee wa kubembea hataki mambo mazuri ya mkini yampitie kando.
 
Rais wetu anajua matatizo yetu. Yaani kutatua matatizo ya ndani ya nyumba yako mpaka uende kwa jirani? Mathalan ndani hakuna chumvi wala sukari na chanzo cha ukosefu huo unakijua kuwa mkeo anachepusha matumizi ya lazima na kupeleka kwenye upatu. Hapo bado unahitaji msaada wa jirani?

Na JK ulikuwa unamfagilia safari zake ilikuwaje ??AU wakati ule Chumvi na sukari ilikuwa inapatikana nje ya nchi??
 
Kwani Mhe, Magufuli Masters yake aliipata wapi? Mimi sijasafiri kwenda nchi yeyote ile, lakini najitahidi kuufahamu ulimwengu kwa njia ya Internet. Tuseme Mhe. Magu naye haijui kutumia mtandao!
 
Rais wetu anajua matatizo yetu. Yaani kutatua matatizo ya ndani ya nyumba yako mpaka uende kwa jirani? Mathalan ndani hakuna chumvi wala sukari na chanzo cha ukosefu huo unakijua kuwa mkeo anachepusha matumizi ya lazima na kupeleka kwenye upatu. Hapo bado unahitaji msaada wa jirani?
Mbona JK alipofululiza safari za nje ulimuunga mkono
 
Aise, kooote nimependa hiyo paragraph ya mwisho, kwamba sio wote wanaopenda kuishi mjini (hasa Dar) na mfano ulioutoa ni JK kuchukuliwa na chopa from Dar to Msoga (nadhani hapa ulitaka kutonesha kua sio wote wanaopenda kuishi Dar) lakini mara baada ya onesho hilo la Chopa to Msoga, jioni akageuza to Dar with the same Chopper; hi nimeipenda sana.
 
Tulitaka rais anaejua matatizo us wananchi wake, exposure ya nin!! Kikete kakimbia huko nchi iinaingia mifukonmwa watu, angekua lowasa toka aapishwe mpaka tuadhisha siku100 angekua bado germany anatibiwa nanlii
 
Back
Top Bottom