mdukuzi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 20,017
- 49,168
Katika sifa kadhaa za mgombea urais kwa tiketi ya ccm huwa ipo ya awe na uzoefu wa masuala ya kimataifa.
sifa hii kwa JPM ilifumbiwa macho,
Nyerere baada ya kusoma nchini alikwenda makerere Uganda na baadae uingereza kunoa Bongo mwinyi alishawahi kukaa Misri ubalozini kwa miaka kadhaa,Mkapa ndio usiseme canada na marekani amekaa sana,JK ziara zake nje ya nchi akiwa foreign affairs minister kwa miaka kumi na miaka kumi ya urais wake ni sawa na kukaa nje miaka mitano,(siungi mkono,it was too much)
JPM alikanyaga Dar es salaam kwa mara ya kwanza mwaka 1984 alipokuwa anakuja kujaza fomu ya kujiunga na UDSM,tangu hapo hajawahi kukaa nje ya nchi kwa zaidi ya mwezi mmoja Amezunguka vichochoro vyote vya Tanzania alipokuwa waziri wa ujenzi akikagua barabara,kazi aliyoiweza kuliko mawaziri wote tangu uhuru .
Back to the point,mimi nimezaliwa Dar Es Salaam na enzi za ujana wangu nilikuwa najiona mtoto wa mjini sana ila siku nilipokanyaga Manhattan mwaka 2002 nilijiona ni mshamba sana kila kitu nilikiona ni kipya na tangu siku hiyo nikajua Dar Es Salaam sio jiji bali ni mji tu.
Wazungu wanakitu wanaita exposure , huwa ni shule tosha kwa tuliosoma zamani tunajua ,mtu wa mtwara kuchaguliwa sekondari wilaya ya Ngara japo kwa upande mmoja ilichangiwa na uhaba wa shule ila ilitusaidia sana,kwa sasa kuna wanafunzi wanazaliwa ndani ya wilaya x,primary mpaka sekondari anasomea ndani ya wilaya hiyohiyo na chuo cha ualimu hapo hapo na anakuja kufundisha shule ndani ya wilaya hiyohiyo ,huyu anakosa exposure atakuwa mshamba tu.
Pia kwa waliopitia vyuo vikuu vya Tanzania mtagundua kuwa lecturers walipata elimu yao nchini bila kwenda nje ya nchi huwa wanakamata sana wanafunzi wakati wa mitihani kuliko walimu waliosomea nje.(sina uhakika kama kutumbua majipu yanhusiana na kukosa exposure )
JPM anasema anataka Tanzania iwe nchi ya viwanda sasa nashangaa itakuwaje nchi ya viwanda wakati anawakimbia wazungu ambao ndio wenye technology ya viwanda,kama hadi pampas za watoto tunaagiza tukubali hatuwezi kujenga viwanda bila kuwa karibu na wazungu,awakaribishe wakae mezani waongee dili win win based business,wanatuhitaji pia bado tunawahitaji,ndio maana Nyerere na kuwatimua kote waingereza alifia kwao akukubali kufia Muhimbili
Pia JPM amekaliliwa akisema Dar ndio kioo cha Tanzania ndio maana anataka kujenga daraja toka cocobeach mpaka ocean road,hii ni kukosa exposure,nchi za watu maendeleo huwa yanakuwa balanced na pia fursa zinakuwa balanced kila sehemu kupunguza msongamano wa watu kwenye miji fulani,kuna baadhi ya nchi watu hawataki kuishi miji mikuu kwani fursa ziko kila kona,Juzi tumesikia kuwa Obama atakuwa rais wa pili wa marekani kuishi washngtone baada ya kustaafu na hii ni kwa sababu watoto wake bado wapo shule,other wise angerudi kwao chicago,JK wakati anakabidhi ikulu na kutuaga kuwa anarudi kijijini helicopter ilimpeleka Msoga mchana jioni akarudi nayo Dar.
Tanzania sio Dar tu
Pia exposure inasaidia kuimprove lugha za kigeni,hili sitaki kuliongelea sana hapa nisije kuchafua jukwaa