Wengi wetu tumekuwa tukijiuliza ni kwanini Mhe John Magufuli anakosa ujasiri wa kujiuzulu hata pale wakubwa zake wanapoonyesha dhahiri kutofautiana naye hadharani kimsimamo na kiutendaji. Leo makala moja katika gazeti la Mawio Toleo Na 0067 la Oktoba 31-Nov 06, 2013 limeweka hadharani miongoni mwa sababu hizo kuwa ni matumizi ya sheria "batili" licha ya majigambo yake ya miaka zaidi ya 13 kuwa anafuata sheria.
Katika video zilizoambatanishwa Mhe John Magufuli anaonekana alikidanganya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akijibu hoja za makadirio ya wizara yake na pia katika kujibu maswali ya wabunge mmoja mmoja kuhusiana na suala la hifadhi ya barabara. Cha kushangaza licha ya kusema uongo bungeni, mbunge muuliza swali na wengi ambao wananchi wao wamevamiwa ardhi na makazi yao kinyume cha sheria na Tanroad kwa shinikizo la Mhe Magufuli walinywea na kushindwa kumchukulia hatua zozote za kibunge.
Aidha katika video mojawapo Mhe Magufuli anakiri kuwa mahakama ndicho chombo cha kutafisiri sheria, kwa kuwa tayari mahakama zetu zimeshafanya kazi hiyo kupitia hukumu iliyoambatanishwa. Hivyo Magufuli kama mtu muungwana na mwenye sifa ya kufuata sheria kama wengi wetu tunavyodhani hana budi kutii amri ya mahakama na kukuabli kwa hiarai yake mwenyewe na kuiagiza Tanroad ikaondoe mabango na mawe waliyoapanda mita 120 kutoka katikatia ya barabara Kuu ya Morogoro pande zote mbili.
Vivyo hivyo umefika wakati wabunge wetu wakaacha mtindo wa kuburuzwa na huyu mbabe na badala yake watumie madaraka waliyonayo kupitia kifungu 63 cha Katiba ya nchi kuhakikisha kuwa Waziri huyu anatimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria ziliziotungwa na bunge bila ya kuwaathiri wananchi kijamii, kisaikolojia na kiuchumi.
DR. MAGUFULI AKIFAFANUA KUHUSU HIFADHI YA BARABARA - YouTube
DR.MAGUFULI NA UFAFANUZI KUHUSU HIFADHI YA BARABARA - YouTube