Mkuu mimi si tatizo hata kidogo ila naomba nikueleweshe kama ifuatavyo:
1. Kesi yenyewe ni Kesi ya Bausi and others kesi namba 39 ya mwaka 1997.
2. Werema enzi hizo akiwa wakili mwaminifu kabisa wa Serikali - ndo hapa nikasema inategemea kina nani wanahusika ktk kesi hiyo
3. Angalia hata mjomba wake yeye Werema aitwaye Munanka alibomoa nyumba ili kupisha Ujenzi - angalia leo hii hiyo barabara inavyowasaidia mamilioni ya Watanzania! Na tena barabara hiyo inataka kupanuliwa iwe njia sita kuanzia Dar es Salaam mpaka Morogoro ( Morogoro Expresway, 200km) kama upo ktk road reserve usijenge au kuendeleza utabomolewa tu, nafikiri mushauri na huyo mwenzako (Wantabe) anaelialia na road reserve ya Morogoro road
4. Mugongo Fimbo tena professor wa Land Law pale UDSM akiwaongoza wenzake , lakini wakashindwa - hicho ndo nataka unielewe na si vinginevyo na wala usipotoshe ninachokuelekeza !
5. Magufuli ni Waziri pekee anayesimamia sheria hasa road reserve na ndo maana unaona miradi mingi inajengwa na bila hivyo ni ndoto kuyapata haya yanayotokea ya Ujenzi wa barabara mfano: Mwenge-Tegeta, Morocco-Mwenge, Kamata - Rangi Tatu ( juzi tu wameboa nyumba), barabara ya mabasi yaendayo kwa kasi n.k
6. Bila kuwa jasiri - Wizara ya Ujenzi ni ngumu sana kutekeleza Majukumu hasa ukizubaa na kufuata hizi porojo porojo za wanasiasa uchwara
7. Ndo maana utaona Magufuli mambo yake yanaenda - lakini pia huwa anawakumbusha wananchi, kama umeonewa unaenda mahakamani.
8. Mkuu mpaka hapa kama hujanielewa basi na wewe utakuwa mbulula!
Aidha, ukae ukijua watu wanakula rushwa sana sana si ajabu kuona kesi nyingi za wazi wazi kushinda kwa upande wa Serikali unakuta eti Serikali imeshindwa. Mfano kipindi kile Magufuli akiwa Ujenzi alibomoa kile kituo cha mafuta Mwanza, wale jamaa wakaishitaki Serikali na wakaja kushinda kipindi Magufuli amehamishiwa Wizara nyingine la sivyo wasingeweza kushinda, na ndo maana utaona ile sehemu waliyobomolewa walitaka kuendelea na Ujenzi wa kituo cha mafuta wakapigwa stop!!!!! Kuna kitu hapo kilienda isivyo hebu jiulize kulikoni.
Pia, kaa ukijua wabunge wote wa CCM na wale wa Upinzani wanazijua sana sana hizi sheria so Magufuli asingekuwa anavunja sheria mbele ya bunge wakimnyamazia.