Magufuli akomaa na wenye Malori

Magufuli akomaa na wenye Malori

Waziri wa Miundombinu na Ujenzi Mheshimiwa John Magufuli amesema kwamba atasimama na msimamo wake kuyapiga marufuku magari ya mazigo kutokugoma barabarani.Waziri Magufuli amesema kwamba anashangaa kutokana na lawama anazobebeshwa kufuatia mgomo unaoendelea na kudai kuwa amefanya hivyo kwa kufuata sheria na kuongeza kuwa analazimika kuchukua hatua hizo ili kulinda barabara zisiharibiwe Nchini.Na zaidi amewataka wamiliki wa malori kwamba milango iko wazi wanaweza kwenda mahakamani kama wanahisi wameonewa.
Heshima niliyokuwa nimeinyakua toka kwako Mh. Magufuri huenda nikairudisha na ziada. Huyu Pinda kazoea kupindisha sheria.
 
Barabara ya Mandela imejengwa miaka michache iliyopita, na sasa imeanza kuharibika kwa sababu ya uzito wa mizigo kwenye magari. Hapa Mh.Magufuli lazima ajue kitu kimoja, pamoja na uzito unaozidi, lakini pia, wanaojenga hizi barabara wanazijenga kwa kiwango cha chini sana!
Ndumila kuwili usiye na mbele wala nyuma!
 
Magufuli wewe ni kiongozi makini japo wasiojua sheria wanazani unakurupuka lkn sisi wachache tunaeshimu kazi yako,usikate tamaa songa siku moja watanzania watakuelewa, maana wenye malori ni walewale tabaka lilelile.

Watakao muelewa ni viongozi wenzake ambao wanataka kutoana macho wenyewe kwa wenyewe utafikili wameingiliana kwenye masilahi yao.
 
Magufuli wewe ni kiongozi makini japo wasiojua sheria wanazani unakurupuka lkn sisi wachache tunaeshimu kazi yako,usikate tamaa songa siku moja watanzania watakuelewa, maana wenye malori ni walewale tabaka lilelile.

Umenena. Tatizo watanzania hatupendi kufuata sheria. Tunatunga sheria halafu tunapindisha kwa visingizio vya kijinga tu. Eti mgomo wa malori umeathiri uchumi. Uchumi wa nchi my ass. Sishangai wakisema hivyo kwa sababu wao ndo wamiliki wa malori ndiyo maana wanalia uchumi wao umeathirika.
 
Siasa kwenye mambo ya msingi tuweke pembeni jamani,magufuli hongera sana kwa kazi nzuri
 
Kwanini wasimalize kama watu wazima badala ya kulialia kwenye vyombo vya habari?
 
Magufuli nnchizi.
huwezi kukomalia sheria inayovuruga jamii nawe unajisifu kusimamia sheria.

hasimamii sheria anasimamia barabara zisiharibike kwa kufuata sheria ya barabara inataka nini kifanyike.
 
barabara hazina viwango hata wadai yapite magari ya robo tani kuharibika ni kulekule
 
Ni kweli Mkuu the matter is ready resolved kwa maamuzi yake kupigwa chini yeye ndo aende mahakamani wala siyo upande ulioshinda uende!La zaidi kaandamwa na waandishi wa habari matokeo yake kazima simu zote zinazojulikana official hapatikani kabisa!
Hii kauli ni outdated. Maamuzi yameshafanywa na Waziri Mkuu, inabidi aongee na hao wenye malori na wala hawaendi mahakamani.
 
Ndumila kuwili usiye na mbele wala nyuma!

Umeandika kwa kukurupuka kama vile umekabwa na mwiba wa samaki, jenga hoja na uache viroja, karibu JF na upunguze ushamba wa kuchangia mada!
 
Piga kazi kama PM anakusumbua achana naye hana future katika uongozi wa taifa hili, sharia kwanza na kwa wote bila mawaaa, hongera dk Magufuli.
 
Kama anauchungu si aimarishe reli kwani nani asiyejua kuwa tz ndiyo yenye maroli mengi kuliko nchi nyingine jirani zenye reli kutoka bandarini? Mnaua reli makusudi ili mfanye biashara na maroli yenu leo mnageukana!
 
Hawa wahuni wasiendelee kuharibu barabara! Pia ujenzi wa barabara uchunguzwe upya
 
Bandarini? wewe kweli uko weekend.
mkuu nahisi umenielewa vibaya simaani mzani uwekwe bandarini kupima meli bali uwekwe kupima maloli yaliyochukua mzigo bandarini kuelekea mikoani na nchi jirani, kibaha ni mbali sana
 
tatizo si yeye ni maccm mezake yanayo mjazaga ujinga kwa kumpigia makofi wakati akitaja barabara za tanzania....
 
Safi sana J Pombe,komaa sababu ukilegea barabara zikahalibika,vizaz vingi vitakukumbuka kwa uzembe,barabara zikidumu utakumbukwa kwa kusimamia sheria,achana na midomo,komaa kama ulivyofanya kwenye vivuko,kelele ni zamda tu,
 
Hii kauli ni outdated. Maamuzi yameshafanywa na Waziri Mkuu, inabidi aongee na hao wenye malori na wala hawaendi mahakamani.

Unaweza kuona watanzania tulivyokuwa na fikra finyu ya kufikiri.
Magufuli ni mtu mwelewa na anayeona mbali, Wenye malori ni kama malori yenyewa akili ndogo
Huyu baba anatetea kitu chenye manufaa na anajua sio siku nyingi shida ya barabara itarudi tena Tanzania. Kutoka Dar mapaka Mwanza itachukua wiki moja kama ilivyokuwa zamani. Barabara zilojengwa ni mikopo bado haijalipwa, wenye malori hawajali uharibifu wanaofanya.Jamani hizi barabara hazitadumu ka Magufuli akipuuzwa
 
MAGUFULI 2.JPG
 
Back
Top Bottom