Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Uwanja wa Kambarage Shinyanga: Dkt. Magufuli asema Miaka 5 haitoshi, mpimeni kwa miaka 10

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,982

C746F510-B3B4-4199-9FE5-2942CF8687AB.jpeg



Leo kishindo cha awamu ya tano kitakuwepo uwanja wa Sabasaba Kambarage ambapo mgombea wa CCM, Dkt. John Pombe Mafufuli atakuwa jukwaani kunadi sera zake.

Dkt. Magufuli: Miaka 5 haitoshi, nipimeni kwa miaka 10

MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli leo Septemba 3, 2020 amefanya mkutano wa kampeni za kuomba kura katika mkoa wa Shinyanga pamoja na kuwanadi wagombea ubunge katika majimbo sita ya mkoa huo na madiwani.

Mkutano huo umefanyika katika Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, ambapo pamoja na mambo mengi aliyoyaeleza kwa wafuasi, wanachama wa CCM na wananchi waliohudhuria uwanjani hapo, Dk. Magufuli amesema kwamba changamoto za nchi haziwezi kumalizwa kwa siku moja, hivyo hawezi kupimwa kwa miaka mitano pekee bali ameomba aongezewe muda mwingine ili apimwe utendaji wake kwa miaka 10.

Dk. Magufuli pia ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo, serikali itanunua ndege nyingine tano ikiwemo moja ya mizigo itakayokuwa inasafirisha bidhaa mbalimbali za wakulima na wafugaji kwenda nje ya nchi.

“Msinipime kwa miaka mitano, mnipime kwa miaka 10 ili mjue utendaji kazi wangu, katika miaka mitano iliyobaki tutafanya maajabu na naamini mtatupa tena miaka mingine mitano tutafanya mambo makubwa” amesema JPM.

Yaliyofanyika Shinyanga
Akieleza baadhi ya mambo aliyoyafanya kwa kipindi cha miaka mitano kwa mkoa wa Shinyanga, Dk. Magufuli amesema serikali imetumia jumla ya Sh Bilioni 31.9 katika miradi ya afya, ikiwemo kujenga hospitali ya mkoa wa Shinyanga ambayo imegharimu Sh Bilioni 3.6 mpaka sasa, hospitali za wilaya ya Kishapu na Shinyanga zilizogharimu Sh Bilioni 3.6, hospitali ya Msalala (Sh Milioni 634), vituo vya afya 11 (Sh Bilioni 4.2) na vituo vya afya 28 (Sh Bilioni 2.08).

Pia Sh Bilioni 29 zimetumika kwenye upande wa elimu hususani elimu bure, Sh Bilioni 60.8 katika miradi ya maji, hatua za awali za ujenzi wa reli ya kisasa ya Isaka-Shinyanga-Mwanza ambapo tenda zimeanza kutangazwa.

Atakayoifanyia Shinyanga
Akieleza baadhi ya mambo yaliyomo kwenye ilani ya chama chake ambayo yatafanyika kwa mkoa wa Shinyanga kwa miaka mitano ijayo, ni pamoja na kuimarisha vyama vya ushiriki, ujenzi wa maghala na vihenga vyenye uwezo wa kubeba tani zaidi ya 30,000, kujenga vituo vya kuchakata na kuhifadhi mazao ya kilimo ikiwemo Pamba, kuongeza Uzalishaji wa mazao yatokanayo na mifugo, kuhamasisha ufugaji wa samaki kwenye maeneo kame.

Pia ujenzi wa barabara ya Kolandoto-Lalago-Mwanuzi-Olabieni Junction, Mwanangwa –Misasi-Salawe- Kahama (Km 149), Solwa-Old Shinyanga (Km 65) na Kagongwa-Bukoba-Kahama zote kwa kiwango cha lami, pamoja na ujenzi wa Uwanja wa ndege ili ndege ziweze kutua.

Vile vile, Kuimarisha mfumo wa kisera ili wananchi wanufaike na rasilimali za nchi ikiwemo upatikanaji wa teknolojia rahisi, mikopo, leseni na kutengewa maeneo ya kuchimba.

Changamoto
Dk. Magufuli ameeleza kuzitambua changamoto mbalimbali zinazousibu mkoa wa Shinyanga ikiwemo uhaba wa vifaa tiba na watumishi, malalamiko ya wachimbaji wa dhahabu Mwakitolyo, mkandarasi wa maji Solwa kutomaliza mradi kwa wakati, watumishi wa SHIRECU waliopunguzwa mwaka 2018 na wale waliopo kutolipwa stahiki zao, mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga kubadilisha umiliki wa vibanda katika soko kuu, stendi na soko la Kambarage bila kushirikisha wamiliki wa awali, na kilio cha kufufuliwa kiwanda cha Nyama Old Shinyanga kilichosimama tangu mwaka 2014.

Ambapo amewataka wahusika wakiwemo viongozi wa Serikali na wagombea ubunge, Patrobasi Katambi (Shinyanga Mjini) na Ahmed Salum(Solwa) kuyashughulikia.

Katambi aomba chuo kikuu, soko
Awali akiomba kura zake kwa wananchi, Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobasi Katambi (CCM) alimuomba Dk. Magufuli kuuongezea mkoa wa Shinyanga taasisi ambazo zitaongeza mzunguka wa fedha katika jimbo hilo.

“Tunahitaji chuo kikuu katika mkoa wetu, tukipata walau soko moja kubwa na stendi mpya ya kisasa tutaondoa malalamiko ya wafanyabiashara,” amesema.


Ampigia debe Katambi, aahidi kumtafutia kazi nyingine Masele

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Magufuli, amewaomba wananchi wa Shinyanga kumpa kura mgombea ubunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi ambapo pia ameahidi kumtafutia kazi nyingine aliyekuwa Mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele.

“Yale mengine ya pembeni achaneni nayo, Katambi ni kijana nampenda mpeni kura, atawavusha, jana tu nimekutana na Masele aliyekuwa Mbunge wa hapa wala sina tatizo, mimi ni Rais nitamtafutia kazi nyingine, ukishakuwa Rais Makazi yapo mengi tu

“Masele nitamtafutia tu kazi ya kwenda kufanya, ukishakuwa Rais kazi ni nyingi, hata leo kuna nafasi ya Mtu mmoja anafanya ovyoovyo huko, Katambi ameacha Ukuu wa Wilaya Dodoma Makao Makuu kuja kuomba kura Shinyanga anawapenda, Katambi ukichaguliwa usibadilike kama wengine”,
amesema Magufuli.

Pamoja na hayo Magufuli ameelezea mipango ambayo anatarajia kuikamilisha katika Mkoa wa Shinyanga iwapo atarejea madarakani baada ya uchaguzi.

“Hapa Shinyanga tumetekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa hospitali, zahanati na mradi mkubwa wa kusafirisha umeme kutoka Iringa hadi Shinyanga ambapo itafika mahali tatizo la umeme litakuwa ni ndoto, kwani tumepeleka umeme katika vijiji 136 vya mkoa huu,” alisema huku akiahidi kukamilisha pia miradi mbalimbali ya barabara mkoani humo.


======
PICHA KUTOKA SHINYANGA:

727D443C-8609-4F6A-84C0-8B30E06DC641.jpeg

83E5686A-6C89-485B-979B-6851CE3204E5.jpeg

29F0E18E-EB53-4B6C-9C07-E96BF5382551.jpeg

635C0C5F-8522-4F7A-91E2-2823B138EFFE.jpeg

59F6D6A5-0945-428C-A3C2-BDAB18C88408.jpeg

EC1ED336-648E-45B3-AD8F-B30B7FEE5C9F.jpeg


Rais Magufuli akimnadi Patrobas Katambi (picha ya chini)

4697F240-112F-48DC-B893-E5435D009849.jpeg


Rais Magufuli akijimwaga na msanii Chege Chigunda 👇🏾

B863C17D-A070-4987-B9FA-41EE72BB2494.jpeg




JPM%2BAKIWASILI%2B2.jpg

Dk. Magufuli akiwasili katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga (Credit:Michuzi Blog)






MWENYEKITI%2B-SHY.jpg

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa akizungumza na wananchi wakati akimkaribisha Mgombea Urais wa chama hicho, Dk. John Magufuli katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga

WABUNGE%2BSHY.jpg

Wagombea ubunge katika majimbo sita ya mkoa wa Shinyanga na wa Viti Maalum wakiwa jukwaani na Mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli wakiomba kura kwa wananchi
ccm%2B-wananchi.jpg

Baadhi ya wafuasi wa chama cha CCM waliohudhuria kwenye uwanja wa Kambarage wakifuatilia sera kutoka kwa wagombea wao
wananchi%2B-jukwaani.jpg


Maelfu ya wafuasi wa CCM na wananchi wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga

WANANCHI%2B2.jpg


wananchi%2Bccm.jpg

Wananchi na wana CCM waliojitokeza kwenye uwanja wa Kambarage wakifuatilia mkutano huo


wananchi%2Bmajukwaani.jpg
 
Watanzania tumeshuhudia maiti za watanzania wenzetu zikiokotwa kwenye fukwe zikiwa zimefungwa mawe na vyuma na nyingine zikiwa kwenye viroba.

Watanzania, tumeshuhudia wenzetu wakitekwa na kupotezwa, wafanyabiashra wakifilisiwa,.

Tumeona ndugu na jamaa zetu wakifunguliwa makesi makubwa na yasiyo na dhamana.

Huyu mtu hatufai kabisa.
 
Back
Top Bottom