Magufuli akomaa na wenye Malori

Magufuli akomaa na wenye Malori

Kama umeangalia ITV Jioni umeingia chaka hizo zilikuwa habari za wiki na Pinda alishatoa order kuwa utaratibu wa zamani utumike na ndiyo mgomo ukaishia hapo.

Lakini waziri Mkuu alisema hawataruhusu, wazidishe mzigo.
 
Umeona eeh!!!! Anaona ile kutajwa tajwa kama potential candidate wa 2015 ndiyo hiyo inaanza kusepa taratibu sasa kaamua kukomaa kivyake vyake!!!
Huku unakokwenda unakwenda kwenye kiza kinene.
 
kwani ishu kwa sasa ni kugomea barabarani au ni faini wanayotakiwa walipe wakizidisha mzigo?

labda kama wamezuiliwa barabarani naweza kuungana na PM, lakini kama wanataka kulazimisha wazidishe mzigo nitawaona washenzi.
 
RELI ya kati na Tazara na zile nyingine zirudishwe ili kuokoa kuharibika kwa Barabara....
 
Barabara ya Mandela imejengwa miaka michache iliyopita, na sasa imeanza kuharibika kwa sababu ya uzito wa mizigo kwenye magari. Hapa Mh.Magufuli lazima ajue kitu kimoja, pamoja na uzito unaozidi, lakini pia, wanaojenga hizi barabara wanazijenga kwa kiwango cha chini sana!

Kwa nini barabara ya Mandela ambayo inatumiwa na malozi? hoja ya magufuli inazidi kuwa na nguvu kuwa tatizo ni malori.
 
Waziri wa Miundombinu na Ujenzi Mheshimiwa John Magufuli amesema kwamba atasimama na msimamo wake kuyapiga marufuku magari ya mazigo kutokugoma barabarani.Waziri Magufuli amesema kwamba anashangaa kutokana na lawama anazobebeshwa kufuatia mgomo unaoendelea na kudai kuwa amefanya hivyo kwa kufuata sheria na kuongeza kuwa analazimika kuchukua hatua hizo ili kulinda barabara zisiharibiwe Nchini.Na zaidi amewataka wamiliki wa malori kwamba milango iko wazi wanaweza kwenda mahakamani kama wanahisi wameonewa.

Yap, kwa sababu wenye malori wanaweza kutumia vibaya uamuzi wa PM. Wasizidishe mzigo wakati issue yao inashughuliwa
 
Watanzania tumuunge mkono Magufuli kwa maendeleo endelevu katika sekta ya barabara.
 
Kwenye ujenzi anajitaidi sana kusimamia lkn watanzania sisi ndo shida,rushwa za watu wa mizani na mizigo kuzidi ndo tatizo,tusimkatishe tamaa bali tumtie moyo kwa faida ya vizazi vijavyo.

Na kwa vile PM amewaruhusu kwa kuangalia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mgomo kuendelea na siyo kwa sababu wana haki, ni vema wenye malori wakazingatia sheria ambazo Magufuli anazisimamia.
 
Mandela road kiwango cha chini, una uhakika? Halafu pesa zilitoka European Union, wakaleta Mhandisi Mshauri wenyewe, Tanroads walihusika tu kama Clerks of works! Ikumbukwe kuwa kazi iliyofanyika Mandela Road ni kazi bora kabisa kwa uwezo wetu, huku tukizingatia kama tungekuwa na uwezo tungeongeza ili kuongeza tabaka la materials zile, lakini hatukuweza kuongeza, basi design imebaki ya tani angalau 40 hivi! Kwa kifupi Mandela road waliweka overlay, na siyo ujenzi from the scratch/beginning.

Tani 40, kwa hiyo hakuna Barabara yeye uwezo wa kuhimili hiyo 5% ya Pinda? Magufuri ana kosa gani? Au basi ni serikali ya kipuuzi. Kila kiongozi Ana bei yake kwa hawa traders.
 
Watanzania tumuunge mkono Magufuli kwa maendeleo endelevu katika sekta ya barabara.

Kweli kabisa, lakini pia tukumbuke kuwa PM kuruhuru malori yaendelee na utaratibu wa zamani hakuwa na maana ya kupingana na Magufuli , bali kuzuia uwezekano wa athari kuwa kubwa. PM alisisitiza masimamo wa kutoyaruhusu kuzidisha uzito.
 
Kama umeangalia ITV Jioni umeingia chaka hizo zilikuwa habari za wiki na Pinda alishatoa order kuwa utaratibu wa zamani utumike na ndiyo mgomo ukaishia hapo.
Mkuu kwanza heshima yako mimi nipo karibu kuja kukusabai ila hii post ni ya leo sasa hapa sijui ni nani mkweli kati ya hawa wa tatu Pinda,Magufuri,na matoa mada!salamu zao huko!!!!
 
Magufuli nnchizi.
huwezi kukomalia sheria inayovuruga jamii nawe unajisifu kusimamia sheria.

Kwani hiyo sheria kaitunga yeye,nadhani aliapa kulinda sheria hiyo kama jamii inaona ni sheria mbaya taratibu zifuatwe kuifuta.
Magufuli anatekeleza wajibu wake na hao wahindi na waarabu hawawezi kwenda mahakamani,kwa sababu hajavunja sheria ya nchi,labda kama wanamshitaki Pinda.
 
Naona uzi huu https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=7558182 ulianzisha maalumu kumchafua Magufuli.

Miradi ya malori ni ya vigogo. Lakini pia nadhani wapenda urais 2015 wanaanzisha propaganda za kupunguza makali ya nyota ya Magufuli kutokana na utendaji wake wa kazi.

Nimeona hadi waandishi wa habari walivyoriti tukuio la mgomo wa malori wakilenga Magufuli binafsi bila kujadili sheria husika wala hoja ya Magufuli juu ya uharibifu wa barabara utokanao na magari kuzidisha uzito.

Pamoja na kwamba mtu hakosi kasoro zake, lakini nyota ya Magufuli haina mfano. Pinda analijua hilo, kikwete hali kadhalika.

Naomba nasi tumpe nafasi. Kwani tatizo liko wapi? Wamiliki wa malori wafuate sheria iliyotungwa na Bunge letu tukufu, tena ikasainiwa na Rais; sheria aliyoapa kuilinda. Sasa siwaelewi wanomlalamikia Magufuli wanataka atendeje kazi yake?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Magufuli anajua sheria ingawa hakusoma sheria, waliosoma sheria ndio wanapindisha sheria, hua sielewi? Hivi huyu aliyempinga Magufuli si ndio aliyesema, "Wapigeni tu kwasababu sisi kama serikali tumechoka"? Pamoja na upungufu wake mzee wa makilomkita bado namsifu hua anasimamia anachokiamini!
 
Back
Top Bottom