Magufuli aitia Wizara hasara ya Bilioni 2

Magufuli aitia Wizara hasara ya Bilioni 2

Maghufuli hachafuliki kirahisi hivyo mkuu, chama chake kikimpirisha kugombea urais, Mbowe, SLAA wote watampa kura.
 
Magufuli alitimiza wajibu wake kwa taifa. Hizi mahakama zetu zina watendaji wasio wazalendo. Wameshaona udhaifu wa serikali kwa nini wasishirikiane na wenye meli na kutengeneza Escrow yao pia.
 
Magazeti ya leo yanaripoti kuwa mahakama ya Tanzania imeamuru serikali kuwasilisha mahakamani zaidi ya bilioni 2 kama fidia ya samaki maarufu kama samaki wa Magufuli.Hii imetokana na serikali kushindwa kesi hiyo iliyounguruma kwa mda mrefu,Swali la Kizushi:Hivi kwa nini serikali "haishindagi" kesi kubwa kubwa

Tatizo sio suala la kesi lakini ukurupukaji wa huyu bwana Magufuri na sababu kubwa ni kutaka kufanya kazi kwa kutumia masikio ya watu yanam-back up vipi! Misifa misifa tu!!
 
Magazeti ya leo yanaripoti kuwa mahakama ya Tanzania imeamuru serikali kuwasilisha mahakamani zaidi ya bilioni 2 kama fidia ya samaki maarufu kama samaki wa Magufuli.Hii imetokana na serikali kushindwa kesi hiyo iliyounguruma kwa mda mrefu,Swali la Kizushi:Hivi kwa nini serikali "haishindagi" kesi kubwa kubwa

Kwenye kesi kuna dili vile vile
 
Mambo yalivyo nchi yetu ya wagagagigikoko, hata hawa majangili wanaotumalizia tembo siku wakikamatwa na kupelekwa mahakamani watatushinda na tutawalipa fidia kwa kutuulia tembo wetu.WTF?
 
ndio maana hata sikushangaa mwanasheria mkuu kuchaguliwa yule masaju maana nae ni dizaini hiyo hiyo

masaju alishawai kushindwa kuamua kesi ndogo sana ya kikazi iliyokuwa inamkabili mwenyekiti wa tawi wa chama cha wafanyakazi wa shirika moja huko Arusha ikabidi afafanuliwe sheria na mwenyekiti huyo wa Tawi
 
masaju alishawai kushindwa kuamua kesi ndogo sana ya kikazi iliyokuwa inamkabili mwenyekiti wa tawi wa chama cha wafanyakazi wa shirika moja huko Arusha ikabidi afafanuliwe sheria na mwenyekiti huyo wa Tawi

mkuu namfahamu sana yule jamaa ni kilaza wa sheria sana na ameshaingiza nchi kwenye majanga mengi sana
 
Hapa mchezo ukute ushatengenezwa wa kupiga hela hamna kitu hapo uhuni tu,
 
Samaki wana thamani ya USD720,000 na meli ina thamani ya USD 2.5m. Jumla ni USD 3.22m ambayo ni zaidi ya sh. 5.4billion. Ni muhimu ikaeleweka hivo. Si sh 2 billion kama msemavyo
 
Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam imetoa amri ya Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kuiachia meli ya 'Tawariq 1' na tani 296.3 za samaki yenye thamani ya zaidi ya 2bn / - mali ya raia wawili wa China, Hsu Chin Tai na Zhao Haquing.

Raia wa China walikuwa wameshtakiwa kwa kufanya shughuli za uvuvi katika eneo maalum la uchumi (EEZ) la Tanzania. Barua iliyosainiwa na Msajili wa Mahakama Kuu ya Desemba 17 mwaka jana, wito kwa serikali kutimiza ahadi zake kupitia hati ya kiapo iliyotolewa na Godfrey Nanyaro na Katibu Mkuu wa wizara tajwa, Charles Nyamlundana. Kiapo juu ya barua alisema kwamba kama mshtakiwa hautakuwa na hatia katika mahakama ya serikali kulipa gharama ya samaki ambayo ni 2,074,249,000 / - ndani ya siku 30 tangu kuachiwa kwao baada ya kutopatikana na hatia. Barua pia ilionyesha nakala ya amri hiyo iliyoongozwa samaki na kuuzwa. Ili ilitolewa na Jaji Radhia Sheikh Desemba 11, 2009.

Mapema Septemba 1 mwaka jana, mawakili wa utetezi kuwasilishwa barua ya ushahidi mbele ya msajili wa mahakama tajwa. Katika barua hiyo mawakili waliiomba mahakama kurudisha ushahidi wa watuhumiwa uliyowasilishwa na Mahakama Kuu katika kesi ya 38 ya 2009 mbele ya Jaji Sheikh wakati wa kesi.

Mwaka 2009 watuhumiwa wawili na wengine 36, walishtakiwa mbele ya mahakama kwa kosa la kufanya shughuli za uvuvi katika ukanda wa uchumi wa Tanzania na kuhukumiwa kifungo cha miaka 20.

Lakini walikata rufaa kwa mahakama ya Rufaa ambayo ilitengua uamuzi wa Mahakama Kuu na kuwaachia huru watuhumiwa. Mara baada ya hapo walikamatwa tene na kushtakiwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Agosti 14, mwaka jana na DPP alitupilia mbali mashtaka!

chanzo: the guardian
 
Wakuu wetu wamekuwa wafanyabiashara na familia zao sasa sijui nani atatutetea sisi wanyonge...maana kila mahali wapo na familia zao, mihimili yote ni yao.. tanzania imebaki ya watu mafukara na masikini,,, wao sio wenzetu tena labda ni wazungu wa ulaya sijui wamekuwa waarabu wa dubai, au sijui wahindi wa india... TTanzania haina mwenyewe tena!!! Watanzania wanatia huruma hawanamtetezi popote pale ndani ya ardhi yao... Tutashindwa kila mahali!!!!
 
Hapo kuna kitu, hizo hela zinaliwa na hao hao jamaa, wameona sehemu ya kupigia hela imekuwa ni shida, yaaan hawa jamaa daaah kweli wezi wanambinu za kila aina, naaamini hizo pesa wanazila wao tu.

ukipata nafasi kula, ukikosa kuwa mkosoaji wa chama tawala.
 
Hahaaa, mkuu wewe umekuwa wazi juu ya lengo la mada hii, ni kutaka tu kumchafua MAGHUFULI. Watanzania siyo wajinga kiasi hicho wanajua kazi nzuri ya Maghufuli, tunajua uwezo wa Maghufuli, tunajua msimamo wa Maghufuli. Hatudanganyiki,

Nchi hii inao wanasheria nguli kabisa. Ikiwa serikali au kiongozi mwenye maamuzi serikalini atataka serikali ishinde kwa hakika kesi kama hii TZ ingeshinda na gharama za kesi ingelipwa. Lakini kwa vile kuna nia ya kuonyesha kuwa Magufuli hafai ndio ikasukwa ili serikali ishindwe na Magufuli aonekane chanzo cha kushindwa. Sijui kama WaTZ mmesahau kesi ya Richmond ambayo ilifanyika somewhere Ulaya. Kwa makusudi mazima serikali pamoja na mafisadi wakati ule waliifanya siri kubwa sana na kupeleka utetezi hafifu ili serikali ishindwe na ionekane kuwa kamati ya bunge wakati ule ilikosea na waliochukuliwa hatua kutokana na ile kashfa ya richmond labda walionewa. Na ndivyo ilivyotokea baada tu ya mahakama kuamua serikali imeshindwa ndipo hapo serikali yetu sikivi ilipotangaza kuwa tumeshindwa na wamiliki wa richmond. Watu mpaka leo wanajiuliza kwa nini serikali ilifanya siri wakati imeshtakiwa ili hali miezi michache serikali hiyo hiyo ilishtakiwa na kampuni fulani ya maji na ikatangazwa sana na serikali ikaweka wazi kwamba wameandaa utetezi wa kutosha na kweli mwishoni serikali ilishinda. Kwa nini hiyo ya richmond haikuwa hivyo???
 
Mahakama zenyewe hizi hizi zinazopokea kila kitu??

Mimi binafsi naamini kabisa kuna shida ya wanasheria wetu wa wizara kuwa legelege, mahakama kuwa corrupt na wafanyabiashara kutumia mianya ya corruption kufanikisha mambo yao... kibaya zaidi siku hizi wanasiasa hasa wa chama tawala wamekua ni madalali wakuu wa wafanyabiashara kwenye kununua haki

I find it difficult kwamba hii kesi bado ilikua inanguruma wakati wale jamaa walikua hawana vibali vya kuvua samaki kwenye maji ya Tanzania

Anyway, tutapigwa hadi tutie akili na tuamue kusimama kwa ajili ya Tanzania
Tatizo hawa viongozi wetu wengi wao wanafanya maamuzi kwa jazba ili wapate sifa bila kuchukua ushauri wa kisheria pale wanataka kuchukua hatua yeyote, ndiyo maana tunajikuta tunashindwa kesi nyingi au tunatoa mianya ya kugeuziwa kibao na kushitakiwa sisi. Jaji hawezi tu kutusaidia tu kwasababu yeye ni mtanzania mwenzetu anatizama sheria ndiyo anatoa hukumu ndiyo maana tunaambiwa mahakama zinatoa maamuzi siyo haki.
 
hii si mara ya kwanza Magufuli kuitia hasara serikali hata kule mwanza serikali ililipa mabilioni ya pesa baada ya kuvunja kituo cha mafuta alichosema kilijengwa kwenye hifadhi ya barabara leo hii aliyevunjiwa ni mbunge wa ccm amekuwa anafanya maamuzi mengi ya kurupuka hata uuzaji nyumba za serikali pia uliingiza hasara serikalini kwani waliokuwa wakiteuliwa ilibidi wakae hotelini kwa kukosa makazi

Acha jazba kama aliwahi kukukwaza, Magufuli huwa hakurupuki kule Mwanza kesi ilikuwa ya kushinda na tena mapema tu, alipohamishwa mambo yale ya kina Jaji Ruhangisa yakafanyika serikali ikapigwa chini, ndo maana hata baada ya kushinda yule jamaa hakuruhusiwa na Jiji kujenga pale alianza kama kujenga tena wakavunja!!

Kesi ya Samaki kila kitu kilikuwa hadharani kabisa, Magufuli katoka kina Ruhangisa tena wakazama na mambo yao Serikali imepigwa chini!!! hivi wewe huna macho, masikio,akili ya kufikiri n.k.

Nyumba za Serikali ilikuwa ni azimio la serikali nzima likibarikiwa na baraza la mawaziri na tena hata kipindi cha miaka ya 1960 serikali iliunda tume ya akina Adu ili kuondokana na gharama za kuhudumia kuchunguza serikali kumiliki nyumba au nyumba za serikali ziuzwe yakaletwa mapendekezo ya kuuza na kujenga nyumba mpya na ndicho kinafanyika leo!


Naomba nikuulize nitajie kesi tano tu za maana kabisa kabisa ambazo serikali imewahi kushinda kila mtanzania akasifia utendaji kazi wa serikali (tano tu).
 
Back
Top Bottom