Magufuli 2015-2020: Matarajio ya uchumi na changamoto zake

Uchambuzi:

· Kama tulivyokwisha ona, ‘concessional loans’ ina unafuu kwa maana ya riba (chini ya asilimia moja i.e 0.75%, fixed), deni linaiva baada ya miaka 40; na kunakuwa na grace period ya muda mrefu (miaka kumi) kabla deni halijaanza kudaiwa.

· Lakini tumeona pia kwamba kwa miaka ya hivi karibuni, vyanzo hivi vya mkopo vimekuwa vikizidi kupungua kutokana na ‘creditos’ kuamua kujiondoa taratibu kwa sababu mbalimbali. Reaction ya serikali imekuwa ni pamoja na kuhamia kwenye vyanzo vyenye gharama na pia masharti makubwa zaidi, na pia kutegemea sana soko la ndani la deni la taifa (Domestic Debt). Kwa mfano, Mwaka 2013, Serikali ilikopa DOLA milioni 600 kutoka Standard Bank ya Uingereza (Rejea sakata la EGMA na Benki ya Stanbic).

- Kwa mfano, tukiangalia gharama za mikopo (cost of debt), kwa mwaka 2010, Weighted Average Interest (Interest Rate) ya mikopo yote ya nje ilikuwa ni 0.4%. Kufikia mwaka 2015, Weighted Average Interest ilifikia 1.9%.

· Kwa mujibu wa Medium term Term Debt Management Strategy (2010), deni la nje lilifikia TZS takribani Trilioni saba. Kufikia Mwezi June 2015, deni la nje lilifikia USD 12.1 Billion, ambayo ilikuwa ni sawa na TZS takribani 25 trillion. Na kwa mujibu wa ripoti ya Benki Kuu (February 2016), deni la nje limefikia $15.6 Billion, ambayo ni sawa na takribani TZS Trilioni 33. Kwa mwaka 2010, deni la nje lilichukua 71% ya deni lote la taifa, na kufikia June 2015, takwimu hii ilishuka kidogo na kufikia (69%). Lakini kwa mujibu wa ripoti ya (BOT), kufikia mwezi Januari 2016, deni la nje limefikia 79% ya jumla ya deni lote la taifa. Masuala muhimu matatu hapa:

- Moja ni kwamba – katika kipindi cha miaka mitano tu, deni la taifa liliongezeka kwa karibia MARA SABA.

- Pili, ndani ya miezi sita tu (June 2015 hadi December 2016), deni la taifa liliongezeka kwa $1.4 Billion, sawa na karibia TZS Trilioni Tatu.

- Tatu, deni la nje linazidi kuchukua sehemu kubwa ya jumla ya deni lote la taifa. Jamno la kutoa wasiwasi katika hili ni kwamba, tofauti na zamani ambapo sehemu kubwa ya deni la taifa ilikuwa ni concessional loans (low interest, fixed interest rate, long grace period, long maturity), ongezeko la deni la nje katika kipindi kuanzia 2009, limeambatana na vyanzo vingi vya ‘non-concessional and commercial”.

· Kwa mujibu wa benki kuu (BOT), katika kipindi cha (January 2015 hadi January 2016), Serikali ya Rais Magufuli ililipa jumla ya $401 million ya deni la taifa (Debt servicing) (sawa na takribani TZS bilioni 870 za walipa kodi). Kati ya hizi, 58% ilikuwa ni malipo ya ‘principal’ peke yake, na kiasi kilichobakia ikiwa ni malipo ya interest. (Katika hili rejea athari zitokanazo na mabadiliko ya kuachana na mikopo yenye gharama na masharti nafuu i.e concessional loans).

· Katika kipindi hicho hicho cha January 2015 hadi January 2016 pekee, serikali ilikopa jumla ya $1.6 billion, sawa na karibia TZS Trilioni 3.5. Kati ya hizi, $1.3 (TZS karibia 2.8 trilioni) zilienda kwenye shughuli za serikali kuu, na kiasi kilichosalia $300 milion zilienda kwenye sekta binafsi (sawa na karibia TZS bilioni 600).

· Kwa mujibu wa ripoti ya BOT (February 2016), Kwa kipindi cha mwezi mmoja tu (December 2015 hadi January 2016), deni la nje liliongezeka kwa $67 (ikiwa ni karibia sawa na TZS bilioni 145). Kwa mwezi huo huo, serikali ililipa deni la nje $49 million (sawa na karibia TZS bilioni 105). Kwa maana hii, katika kipindi hicho hicho, TZS bilioni 145 ziliingia ndani ya nchi kama mkopo/deni la nje kwa mkono wa kushoto, na hapo hapo TZS bilioni 105 zikatoka kwa mkono wa kulia kama malipo ya deni la nje


4.12 Costs and Risks Indicators (Deni la Nje)


Jedwali #3

Risk Indicator

2010

2015

Cost of Debt:

1. Weighted Average Interest Rate.


0.4%

1.9%.

2. Refinancing Risk

*Debt Maturing in one year (out of total debt).



6.2%






4.7%

3. Interest Rate Risks


*Total Amoung of Debt Refixing (%)

*Average Time to Refixing (Interest Rates) – Number of years.




6.2%




19.3 Years






23%




14.7 years.



UCHAMBUZI WA JEDWALI #3:


· Cost of debt (Gharama za mkopo wa nje).


Hapo juu tunaona kwamba Weighted Average Interest Rate (wastani wa riba) kwa mwaka 2010 ulikuwa ni 0.4%. Wastani huu uliongezeka hadi 1.9% miaka mitano baadae (2015), ikiwa ni ongezeko la zaidi ya mara tano. Tukumbuke kwamba sehemu kubwa ya ongezeko hili ni la mikopo ambayo vyanzo vyake ni vya kibiashara kuliko ‘concessional’.


Refinancing Risk


Deni linaloiva katika kipindi cha mwaka mmoja kati ya deni lote kwa mwaka (2015) ilikuwa ni 4.7%, ikilinganishwa na mwaka 2010 ambalo ilikuwa ni 6.2% ya jumla ya deni lote kwa kipindi hicho. Hili ni punguzo la 1.5%. Kwa kuangalia juu juu inaonekana walipa kodi wamepata ahueni lakini uhalisia haupo hivyo. Jumla ya deni la nje (2010) ilikuwa ni takribani TZS 6.7 trilioni. Kwa maana hii, deni lililokuwa linaiva ilikuwa ni jumla ya TZS takribani 415 billioni. Kwa mwaka 2015, deni la nje lilifikia takribani TZS 25 trilioni. Kwa maana hii, deni lililokuwa linaiva ilikuwa ni karibia TZS 1.2 trilioni. Kwahiyo wakati kulikuwa na punguzo la 1.5% katika kipindi hicho, kwa upande wa fedha za walipa kodi, kulikuwa na ongezeko la zaidi ya TZS trilioni moja. Rejea mjadala wa refinancing risk huko juu.


Interest rate risk

Kufikia mwaka 2010, jumla ya deni ambalo lilikuwa linahitaji ‘refixing of interest rate’ kutokanana kuiva ilikuwa ni 6.2% ya jumla ya deni lote. Hii ilikuwa ni sawa na karibia TZS 415 billion. Kufikia mwaka 2015, kiwango hiki kilifikia 23%, ambayo ilikuwa ni sawa na karibia TZS trilioni 6 (trilioni sita). Tukirejea mjadala wa awali juu ya gharama/hatari ya ‘roll over of debt’, maana yake ni kwamba kufikia kipindi husika, TZS karibia trilioni Sita zilikuwa zinasubiri kuwa rolled over kwa riba ya juu zaidi kuliko awali wakati mikopo husika ilipochukuliwa na serikali.



Katika sehemu inayofuata tutajadili:

Kwanini tunapaswa kuwa na wasiwasi zaidi juu ya hali ya deni la nje.

Historia ya deni la nje.
 
Sura ya TANO:


Katika sehemu hii ya mwisho, tutajadili deni la nje katika maeneo makuu matano kama ifuatavyo:


Kwanza tutajadili kwa kifupi kwanini tuna haja ya kuwa na wasiwasi zaidi juu ya hali ya deni la nje.


Pili tutaangalia historia fupi ya deni la nje kuanzia miaka ya 1970s hadi kipindi hiki cha sasa.


Tatu tutaangalia mikopo husika imekuwa ikielekezwa zaidi katika sekta gani za kiuchumi na kijamii.


Nne tutaangalia athari (impact) ya mikopo kutoka nje katika maeneo mbalimbali ya kijamii na kiuchumi.


Kijamii, tutaangalia athari za deni la nje katika maeneo yafuatayo:

· Ukweli kuhusu hoja kwamba kila nchi ina kopa/ina madeni

· Uhusiano wa kukua wa deni la nje na jitihada za kutokomeza umaskini.

· Uhusiano wa kukua kwa deni la nje na pengo baina ya ‘wenye nacho’ na wasio ‘nacho’.

· Uhusiano wa kukua kwa deni la nje na idadi ya watanzania wanaoshi na utapiamlo.



Kiuchumi tutaangalia athari za deni la nje katika maeneo yafuatayo:

· Uhusiano wa kukua kwa deni la nje na ‘diversification’ ya uchumi.

· Uhusiano wa kukua kwa deni la nje na Kushuka/kushuka kwa thamani ya bidhaa ghafi zinazouzwa nje (Commodity Devaluation) na kuporomokoa/kupanda kwa thamani ya Sarafu ya nchi ( Depreciation of Currency):


Na mwisho tutajadili kasi ya kukua kwa deni la taifa na jinsi gani nchi inakabiliwa na hatari (risk) ya kuingia katika mgogoro mkubwa wa Kiuchumi. Katika hili, tutafanya tathmini ya ‘debt sustainabililty’ kwa kuangalia maeneo makuu mawili:


· Iwapo katika muda ujao wa kati (2016-2021), Serikali itakuwa na uwezo wa kuimarisha mapato ya kodi ili kuwa na nafasi nzuri ya kulipa deni la nje bila ya kuathiri majukumu yake mengine kwa walipa kodi.


· Iwapo katika muda ujao wa kati (2016-2021), ‘export performance’ yetu itakuwa katika hali nzuri ya kuongezea taifa pato la kigeni la kutosha kuwezesha serikali kulipa deni la nje bila ya kuathiri majukumu yake mengine kwa walipa kodi.


5.1 Kwanini tunapaswa kuwa na wasiwasi zaidi na hali ya deni la nje kuliko deni la ndani? Tulijadili hili katika sehemu ya nne. Baadhi ya masuala tuliyojadili ilikuwa ni pamoja na yafuatayo:


· Kwanza – tuliona kwamba deni la nje ni ‘more risky’ kuliko la ndani, kutoka na masuala kama vile ‘exchange rate risk’, nk.


· Pili – tuliona kwamba deni la nje linatoboa tundu kubwa zaidi kwenye ‘fiscal system’ ya nchi kuliko deni la ndani.


· Tatu – tuliona kwamba deni la nje lisipodhibitiwa vizuri, linaweza kuwa mzigo mkubwa kwa vizazi vya baadae.


· Nne – tulijadili kwamba deni la nje linaondoa sovereignity (uhuru) wa nchi, katika Nyanja zote za kiuchumi na kijamii.

· Tano tukasema kwamba tofauti na deni la ndani, deni la nje linapelekea ‘a financial imbalance’ baina ya uchumi wa ndani na ‘the rest of the world. Tulijadili suala hili katika muktadha wa ‘current account deficit’ kwenye sehemu ya NNE.



5.2 Historia fupi ya deni la nje (1970s hadi kipindi cha sasa)


Miaka ya 1970s & 1980s, Tanzania ilikopa fedha nyingi kutoka vyanzo vya nje, kiasi kilichofikia $6.3 billion. Kati ya mikopo hii, 50% ilikuwa ni mikopo ya moja kwa moja kutoka mataifa makubwa yaliyoamini sera ya ujamaa chini ya Azimio la Arusha (1967), nchi kama Sweden n.k; asilimia nyingine thelathini (30%) ilitoka kwenye multilateral institutions tulizojadili katika sehemu ya NNE (kwa mfano World Bank nk); na kiasi kilichosalia (20%) kilitoka kwenye sekta binafsi nje ya nchi. Kwa ujumla wake, kama tulivyogusia awali, sehemu kubwa ya vyanzo hivi vilikuwa ni vya gharama nafuu kwa maelezo tuliyoyaona awali – long debt maturity, low and fixed interest rate, long grace period, nk.


Ndani ya Kipindi kifupi sana, nchi ilianza kuona matokeo na mafanikio iliyotokana na mikopo husika kutoka nje. Pamoja na mengineyo serikali ilifanikiwa kupunguza umaskini wa kipato, wananchi walipata huduma ‘bora’ za kijamii, uchumi ulizalisha ajira kwa wananchi, nk. Tuangalie mifano michache ya mafanikio yaliyojitokeza:


· Kufikia mwaka 1987, taifa likiwa limefikisha jumla ya idadi ya watu milioni ishirini. Kufikia kipindi hiki, watoto zaidi ya million tatu na nusu walikuwa mashuleni (shule za msingi), ambazo zilifikia zaidi ya 10,000 nchi nzima katika kipindi kifupi.

· Kila kijiji kilijengwa angalau shule moja ya msingi.

· Idadi ya wanafunzi waliomaliza darasa la saba iliongezeka kutoka (20%) mwaka 1971 na kufikia 90% mwaka 1983.

· Nchi ilifanikiwa kujenga viwanda vingi huku sehemu kubwa ya ujenzo wa viwanda, hasa ‘mass goods industries’, vikijengwa kwa fedha za ndani. Viwanda hivi vilitoa ajira kwa watanzania wengi na pia vilichangia pato la taifa.

· Pia kufuatia mkakati wa ‘Elimu ya watu wazima’, nchi ilifanikiwa kufikisha ‘literacy rate’ ya kiwango cha 85%, kiwango ambacho kilikuwa ni cha juu kuliko nchi nyingine zote barani Afrika.

· Vile vile yalikuwepo maeneo mengine mengi ambayo kulikuwa na mafanikio makubwa, kwa mfano afya. Kwa mfano, idadi ya watoto waliokuwa wanafariki chini ya umri wa miaka mitano ilishuka hadi 220 kati ya kila watoto 1,000 (mwaka 1970) na kufikia watoto 170 (mwaka 1988). Nk nk.


Muhimu:

Serikali iliweza kuboresha maisha ya watanzania kwa kiwango kikubwa ndani ya miaka 10-15, kwa mkopo wa nje uliofikia takribani $7 billion.


Kama tutakavyojadili baadae, ndani ya MIAKA MITANO TU (2009-2013), serikali ya awamu ya TANO chini ya Rais Jakaya Kikwete ilikopa kiasi cha $ 10 bilioni, kiasi ambacho ni mara tatu ya kiasi kilichokopeshwa na Serikali ya awamu ya Kwanza kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi. Tumeona jinsi gani mikopo chini ya serikali ya awamu ya kwanza ilileta faida kwa wananchi.


Swali linalofuata ni je:


Mikopo ya zaidi ya TZS trilioni 20 kwa kipindi cha miaka mitano tu (2009-2013) utakuwa na maslahi gani kwa vizazi vya baadae?


Ni ngumu kubaini kwa sababu kuna kila sababu ya kuamini kwamba hatukukopa kwa kufuatana na ‘fiscal discipline principles’. Fiscal Discipline inasheria zake, moja wapo ikiwa ni ‘Golden Fiscal Rule’. Kanuni hii inaelekeza ‘policymakers’ kuhakikisha kwamba ‘in any given economic cycle’, serikali inakopesha fedha kwa ajili ya matumizi ya ‘uwekezaji’ (investment) kuliko katika matumizi ya kawaida. Lengo kuu katika hili ni kuakikisha kwamba iwapo inatokea mzigo wa deni unaangukia kizazi cha baadae, basi kizazi hicho nacho kije kulipa madeni ambayo manufaa yake yanaonekana. Lakini kwa mujibu wa ripoti za Benki ya Dunia, sehemu kubwa ya mikopo hii ilikwenda kwenye matumizi ya kawaida.



5.2.1 Msukosuko wa kiuchumi miaka ya sabini na themanini:

Baada ya mafanikio haya chini ya Serikali ya awamu ya kwanza, uchumi ukaingia katika mgogoro mkubwa. Zipo sababu nyingi zilizopelekea hali hiyo, lakini sababu za msingi ni pamoja na kuporomoka kwa bei ya mazao ghafi - ‘commodity prices’ ambayo ilikuwa ndio tegemea kubwa la mapato ya kigeni kwa nchi. Hali hii pia ikaambatana na ongezeko kubwa la riba kimataifa. Kwa vile nchi ilikuwa bado inategemea sehemu kubwa ya mikopo kutoka nje, ongezeko la riba haikuwa habari njema kwa taifa, kwani athari yake kwa mikakati ya uchumi na maendeleo ikawa ni kubwa.


Kuanzia kipindi cha mwisho ya 1970s na mwanzoni mwa miaka ya 1980s, nchi ikajikuta kwenye deni kubwa lisilostahimilika. Kwa mfano kufikia miaka ya 1990s, hali ilifikia kuwa mbaya kiuchumi kutokana na serikali kulazimika kutumia zaidi ya 27% ya mapato (fedha za walipa kodi) kulipa deni la nje, hivyo kuathiri uwezo wa serikali kuhudumia wananchi. Kutokana na hali kuzidi kuwa mbaya, serikali ikalazimika kuingia katika makubaliano na World Bank na IMF juu ya mikakati ya kuokoa uchumi wa taifa ili usitumbukie kwenye shimo kubwa zaidi na kuwa na athari kubwa zaidi. Msaada huu ukaja na masharti mbalimbali, ikiwa ni pamoja na serikali kutakiwa kubana matumizi, kulegeza masharti ya kiuchumi na kibiashara nk.


5.2.2.1 Athari zilizojitokeza:


· Idadi ya watanzania maskini ikaongezeka, kwa mfano – wananchi waliokuwa wanaishi chini ya dola mbili kwa siku ikaongezeka kutoka watanzania milioni 25 mwaka 1993 na kufikia watanzania milioni 33 mwaka 2000.

· Idadi ya watoto waliokuwa wanamaliza elimu ya darasa la saba ikaporomoka kutoka 90% hadi 50%.

· Idadi ya watanzania wenye utapiamlo ikaongezeka kutokea milioni sita mwaka 1991 na kufikia milioni 13 mwaka 2000.

· Ukosefu wa ajira ukashamiri kutokana na masharti ya World Bank/IMF yaliyolazimisha serikali kupunguza matumizi hata yale yaliyohusishwa uwezezaji na ujenzi.

· Kushamiri wa sekta isiyo rasmi (informal sector) kufuatia tatizo la ukosefu wa ajira nk.


Kufuatia hali hii, iliyoambatana na kasi ya kuongezeka kwa deni la taifa, nchi wahisani zikaingia makubaliano na serikali ya Tanzania ya kusamehe sehemu ya madeni ya nje lakini pia kwa masharti juu ya jinsi gani fedha zinazo samehewa zitumiwe na serikali. Haya yalitokea katika muktadha wa ‘Highly Indebted Poor Countries Intiative’ (HIPC) miaka ya mwisho ya 1990s hadi mwanzoni ya 2000. Kufuatia mkakati huu, uchumi wa nchi (hasa uchumi mpana wa nchi – macro economy) ukaanza kurejea katika afya, huku kiwango cha kodi za wananchi zilizokuwa zikienda kulipa deni la nje kikushuka na kufikia 2% ya GDP kwa kipindi cha 2001-2013, kutoka zaidi ya 27% miaka ya 1990s.


Katika sehemu inayofuata tutaangalia, je:

Kwa sasa hali ipo vipi?

Mikopo imekuwa ikielekezwa sekta gani?
 
5.2.1 Hali ya Sasa Ipo Vipi?


Kama tulivyoona awali, mafanikio katika uchumi mpana (kasi kubwa ya kukua kwa uchumi/GDP growth rate wastani wa 7% kwa miaka kumi na tano mfululizo/2000-2015), bado hali ya umaskini nchini haijabadilika. Kwa mfano idadi ya wananchi wanaioshi na utapiamlo inazidi kuongezeka, idadi ya watanzania wanaoishi chini ya Dola mbili kwa siku inazidi kuwa kubwa nk.


Kama tulivyoona awali, kufikia Mwezi January Mwaka huu wa 2016 deni la nje limefikia $15.6 billion, ambayo ni sawa na karibia TZS trilioni 34. Sehemu kubwa ya deni hili iliongezeka katika kipindi kifupi cha miaka mitano wakati wa utawala wa Rais Kikwete (2009-2013). Tuliona kwamba katika miaka mitano tu, deni la taifa liliongezeka kwa dola za kimarekani Bilioni 10, ambapo kwa leo ni zaidi ya TZS trilioni 20.


Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, kati ya mwaka 2007 na 2013, kiasi cha dola za kimarekani milioni 980 (leo zaidi ya $trilion 2) kutoka Benki ya Dunia zilielekezwa katika miradi ya kupambana na umaskini ‘support credit’, ikiwa ni sawa na 63% ya mikopo yote ya World bank katika kipindi hicho. Lakini kwa mujibu wa Benki ya Dunia, sehemu kubwa ya mikopo hii ilienda kugharamia ‘matumizi ya kawaida’. Si ajabu tathmini ya mikopo mingi ya aina hii (2003-2013) inaonyesha kwamba wakati kasi ya kukua kwa pato la taifa (GDP) imekuwa ni ya kutia moyo sana katika kipindi husika (wastani wa karibia 7%), kasi hii haikuwa na matokeo chanya katika juhudi za kupunguza umaskini tofauti na ilivyotarajiwa.


Katika kipindi cha miaka ya 2007-2013, asilimia hamsini (50%) ya mikopo ya nje ilikuwa ni kutoka Benki ya Dunia. Vyanzo vingine vilikuwa ni Multilaterals kama AfDB and IMF (24%), sekta binafsi nje ya nchi (17%) ambayo kama tulivyoona mikopo yake huwa ni ya gharama kubwa, huku mikopo iliyosalia (8%) ikiwa ni kutoka moja kwa moja kutoka kwenye serikali nyingine.


Katika kipindi hiki pia (2013), serikali ilitoa ‘Hati Fungani” yenye thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 600 (sawa na zaidi ya TZS Trilioni 1.2) kupitia Benki ya Standard Chattered ya nchini Uingereza. Gharama ya mkopo huu haipungui 6% pamoja na Libor ambayo kwa sasa ni takribani 2%, na kufanya jumla ya gharama kuwa ni 8%. Mkopo huu unatakiwa kuwa umeshalipwa na serikali ya Tanzania ndani ya miaka kumi ijayo.


5.3 Je Mikopo ya Nje inaelekezwa katika Sekta gani?


Kwa mujibu wa takwimu za kila mwezi za Benki kuu (BOT), katika kipindi cha hivi karibuni, sehemu kubwa ya deni la nje imekuwa ikielekezwa katika sekta zifuatazo:


· Usafiri na Mawasiliano (Transport and telecommunications) karibia 23%

· Balance of Payments & Budget Support (karibia 17%)

· Agriculture (Karibia 4%)

· Energy and Minerals (Karibia 17%)

· Industries (Karibia 2%)

· Social Welfare and Education (Karibia 14%)

· Finance and Insurance (Karibia 4%)

· Real Estate and Construction (Karibia 4%)

· Others (Karibia 14%)

JUMLA KUU 99%



Kinachoshangaza ni kwamba sekta ya KILIMO, ambayo ndio sekta mama ya uchumi wa nchi kwa maana ya kubeba sehemu kubwa ya nguvu kazi ya nchi (sio chini ya 70%); sekta yenye mchango mkubwa kuliko sekta zote katika pato la taifa (GDP); na sekta inayochangia kiasi kikubwa cha mapato ya fedha za kigeni yanayohitajika kulipa deni la nje na kuhudumia pia wananchi, bado mikopo ya nje inayoelekezwa katika sekta hii ni kidogo sana kama tunavyoona hapo juu (4%). Matokeo yake ni kwamba licha ya umuhimu wa sekta hii katika maendeleo ya viwanda na uchumi kwa ujumla (rejea mjadala wetu wa awali), kasi ya kukua kwa sekta hii haijawa ya kuridhisha kwa kipindi cha miaka 15 iliyopita (chini ya 4% kwa mwaka, huku tukijipongeza na wastani wa 7% kwa mwaka).


Sekta nyingine muhimu ni za Elimu na Afya. Takwimu za Benki Kuu zinaonyesha kwamba sekta hizi zimekuwa zikipata kiasi kikubwa cha mikopo ya nje (14%). Lakini cha ajabu ni kwamba, kasi ya kukua kwa sekta hizi, kasi ya kila sekta haizidi 1% kwa mwaka. Maana yake nini? Maana yake ni kwamba fedha zinazopelekwa katika sekta hizi zinaenda zaidi kwa ajili ya matumizi ya kawaida kuliko miradi ya maendeleo/uwekezaji.


Sekta nyingine ni ya Viwanda. Tulitarajia sekta hii kupewa kipaumbele na fedha za nje, hasa kutokana na mikakati ya serikali ya kuipeleka Tanzania kuwa nchi ya Viwanda. Lakini tofauti na matarajio haya, ni 2% tu ya mikopo ya nje ndio inapelekwa katika sekta hii. Mbaya zaidi, hata bajeti ya mwaka huu wa fedha (2016/17) nayo imetenga kiwango kidogo sana cha fedha kwa ajili ya sekta hii muhimu (TZS bilioni 82 tu).


Kama tulivyojadili huko nyuma, ni vigumu kwa taifa kuingia katika uchumi wa viwanda bila ya kuwekeza vya kutosha kwenye sekta hizi tatu muhimu - kilimo, elimu na afya.


Hapo juu tunaona kwamba sekta za ‘Usafiri na Mawasiliano’ zinaongoza katika kupokea mikopo mingi ya nje. Pamoja na umuhimu wa sekta hizi, ‘impact’ (athari) ya uwekezaji katika sekta hizi kwa maisha ya watanzania bado sio ya kuridhisha. Mbali ya hili, miradi mingi ya ‘public private partnership’ (PPP), miradi mingi imekuwa ikifanyika ndani ya sekta hizi. Bila ya uangalifu, taifa linaweza kuingia katika matatizo makubwa kiuchumi, hasa kulemewa na deni la nje. Hii ni kwa sababu, kama tutakavyoona punde, miradi ya PPP inachochea deni la taifa.


Sekta ya Nishati na Madini.


Sekta hii imekuwa ikipokea kiasi kikubwa cha mikopo kutoka nje (17%). Pia kasi ya kukua kwa sekta hii imekuwa ni kubwa katika kipindi cha (2010-2015), mara nyingine kuliko wastani wa kukua kwa uchumi (7%). Kwa maana hii, sekta kama hizi ndio zinazobeba mafanikio ya kukuwa kwa uchumi wa taifa kwa kasi kubwa (wastani wa 7% kwa kipindi cha 2010-2015). Lakini uhalisia uliopo ni kwamba mapato yatokanayo na sekta ya madini, mafuta, gesi, yataendelea kunufaisha watu wachache (wawekezaji wan je na ‘elites’ wa ndani/wanasiasa), hivyo kuzidi kuongeza pengo baina ya walio nacho na wasionacho. Hii ni kwa sababu, uwekezaji katika sekta hii unahitaji nguvu kazi chache for the revenues produced; pia sekta hii ni ‘capital driven’ kuliko ‘labour driven’. Sekta hizi ni maarufu kwa kuwapa wawekezaji na elites njia za kuhodhi rasilimali husika pamoja na faida zitokanazo na rasilimali hizo, kuliko umiliki au manufaa kuwa distributed across the population.


Dhahabu na Uchumi wa Wananchi:

Katika hali ya kawaida, kufikia kipindi hiki, ilitakiwa tuwe tunavuna matunda ya kupanda mbegu ya ‘Dhahabu” kunyanyua uchumi wa wananchi, hasa kilimo.


Kumekuwepo na mijadala mbalimbali kuhusu jinsi gani Tanzania inaweza kugeuka kuwa na uchumi wa gesi. Huku ni kujidanganya. Kwanza, itachukua miaka mingi kabla ya wananchi kuanza kunufaika na gesi. Lakini muhimu zaidi ni kwamba – Tanzania haiwezi kutegemea gesi kujenga uchumi wake kwa muda mrefu, badala yake gesi itaweza kutumika kama kichocheo cha kukuza sekta nyingine za uchumi. Kwa mfano, gesi inaweza kutumika kama nishati kusaidia uzalishaji viwandani n.k. Katika hili tukumbuke pia kwamba rasilimali za aina hii zina madhara yake pia. Kwa mfano:


- Ni jambo la kawaida kwa nchi maskini kuingia katika migogoro na vita baada ya rasilimali kama hizi kupatikana.


- Lakini muhimu pia ni kwamba – nchi nyingi maskini zinazogundua rasilimali hizi hugeuka kuwa na serikali kandamizi na zisizojali haki na demokrasia. Hii ni kwa sababu mapato ya gesi au mafuta yanaiwezesha serikali iliyopo madarakani kuacha kutegemea kwa kiasi kikubwa kodi za wananchi, suala ambalo ni muhimu katika kujenga uwajibikaji wa serikali kwa wananchi, suala ambalo pia linasaidia ‘legitimacy of the party/government in power to be tested between elections. Rasilimali hizi huondoa yote haya kwani chama tawala na serikali yake kinapata uwezo wa kutumia utajiri wa nchi kutoa ‘generous welfare’ kuhonga wananchi, lakini pia kunyonga demokrasia, nk.







Katika sehemu inayofuata, tutajadili dhana ya Public – Private Partneship na athari zake kwa uchumi wa nchi kama Tanzania.
 
5.4 Ubia Wa Sekta ya Umma na Binafsi – Public – Private Partnerships (PPPs) na Athari zake kwa Walipa Kodi/Deni la Taifa.


Miradi ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi - Public – Private Partnerships (PPPs) huchukua sehemu kubwa sana ya uwekezaji wa sekta ya miundo mbinu. Miundo mbinu ni pamoja na ile ya mawasiliano (telecommunications), nishati, bandari, barabara, reli, maji nk. PPPs zimeendelea kupata umaarufu mkubwa kwa sababu zinawezesha ‘debt repayments’ za nchi kutoonekana kwa urahisi kwa wananchi na hata kwa wawakilishi wao bungeni. Miongoni mwa PPP schemes maarufu ni pamoja na “The Private Finance Initiative” ya Uingereza.


Taasisi za aina hii zinasaidia sekta binafsi kutoka mataifa makubwa kuwekeza katika nchi maskini lakini kwa masharti kwamba serikali za nchi maskini zitoe ‘guarantee’ ya malipo kwa wawekezaji bila ya kujalisha hali ya uchumi itageuka vipi baade. Pia serikali za nchi maskini hutakiwa kujifunga (commit) ‘to bail out the private operator’ kama biashara itakwenda kombo. Kwa namna hii, PPPs zinakuwa na athari ile ile kwenye fiscal system ya nchi kama ilivyo kwa mikopo kwa sababu kimsingi serikali bado inakopa moja kwa moja, lakini tofauti na mikopo mingine, ‘payment obligations’ za serikali under PPP projects huwa hazionyeshwi kwenye takwimu za deni la nje la taifa.


Miradi ya PPP kwa kawaida hugharimu zaidi serikali kuliko ambavyo serikali ingeamua kukopesha yenyewe kutoka vyanzo vingine na kuwekeza katika miradi hiyo hiyo kwa mfano ujenzi wa miundo mbinu nk. Hii ni kwa sababu mikopo hii inatoka kwenye sekta binafsi, na kama tulivyojadili awali, ni mikopo yenye vyanzo gharama kubwa, na ukiachilia gharama zinazohusiana na viwango vya riba, pia private contractors huwa wanahitaji faida kubwa sana na vile vile ‘negotiations’ mara nyingi huwa zinapendelea sekta binafsi kuliko serikali husika.


Kwa mujibu wa utafiti wa Griffiths et al (2014), [“Financing for development post 2015: Improving the contribution of Private Finance”]:


“PPPs are the most expensive way for governments to finance infrastructure, ultimately costing more than double the amount than if the investment had been financed with bank loans of bond issuance”.


Katika hili, Mchumi Maximilien QueyRanne kutoka dawati la “Fiscal Affairs” la Mfuko wa kimataifa wa fedha (IMF), anaongeza kwamba:


“the fiscal risks of PPPs are potentially large because they can be used to move spending off budget and bypass spending controls and move debt off balance sheet and create contingent and future liabilities. They also reduce budget flexibility in the long term.”


World Bank pia kupitia utafiti wake huru hivi karibuni (World Bank’s independent evaluation Group) ilibaini kwamba kati ya miradi 442 ya PPP iliyo chini ya uangalizi wake, tathmini ya athari za miradi hii katika kutokomeza umaskini ilifanyika kwenye miradi tisa tu (sawa na 2%). Vile vile, tathmini juu ya ‘fiscal impact’ ya miradi hii ya PPP ilifanyika kwenye miradi 12 tu (sawa na 13%). Pamoja na haya yote, cha ajabu ni kwamba ‘debt payment obligations’ zinazotokana na miradi ya PPP bado huwa haipo covered katika ‘Debt Sustainability assessments’ zinazofanywa na World Bank/IMF. Maana yake ni kwamba, uhalisia juu ya obligations za malipo ya mbeleni ni kiasi kikubwa zaidi cha fedha za walipa kodi kuliko kile kinachowasilishwa kwenye ‘Debt Sustainability assessments.’


5.4.1 Tanzania, Deni la Nje na Public - Private Partnerships (PPPs)


Mikopo ya nje kwa mwaka 2013 (iliyozidi TZS trilioni 3.5) na ilihusisha miradi miwili ya PPP. Leo hii, Serikali ya Tanzania ina ‘three hidden obligations’ zilizotokana na mikataba ya nyuma ya PPP. Miradi hii ni ya Umeme ambayo ilikua implemented kwa ajili ya kuiuzia serikali (Tanesco) umeme ‘at a pre-determined price’, ambayo ni guaranteed na serikali ya Tanzania (Kodi za wananchi). Mradi wa kwanza ulikuwa ni IPTL, na mradi wa Pili uliofuatia ukawa ni ule wa Songas.


Kwa mujibu wa mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali (CAG) mwaka 2007/2008, miradi hii miwili ilikuwa inaigharimu Tanesco 90% ya mapato yake na kufanya Tanesco kulemewa na mzigo mkubwa wa purchase agreements ambazo hazikuzingatia Public Procurement ACT pamoja na regulations zake. Lakini kama vile hiyo haitoshi, bado serikali ya ikaingia mkataba na Kampuni nyingine ya Richmond/Symbion/Dowans mwaka (2007/2007).


Kutokana na kulemewa na miradi hii ya kinyonyaji, mwaka 2009 Tanesco ililazimika kuongeza ‘tarrifs’ kwa 40%, lakini bado shirika hili likaendelea kujiendesha kwa hasara. Kwa mujibu wa ripoti ya IMF (2013), ruzuku ya serikali kwa tanesco iligharimu serikali 10% ya fedha za walipa kodi, na sehemu kubwa ya fedha hizi zilienda kulipia ‘inflated costs’ za miradi hii ya PPP ya uzalishaji wa umeme. Kwa maana hii, ruzuku ya serikali (10% ya kodi za wananchi kila mwezi) ilikuwa ni ruzuku kwa makampuni binafsi yaliyowekeza kupitia PPPs, na sio ruzuku kwa walipa kodi, ambao ndio wanaostahili kufaidika na ruzuku husika. Kwa mfano, inasemekana kwamba malipo ya fedha za walipa kodi kwenda IPTL ni TZS bilioni nane kwa mwezi.


5.5 Hoja kwamba Kila nchi Inakopa na Nchi Yetu Bado Inakopesheka


Hoja hii ni maarufu sana, hasa miongoni mwa wanasiasa hasa pale wanapobanwa kuelezea uhalali wa kasi kubwa ya kukua kwa deni la taifa. Kuna ukweli kwamba kukopa au kuwa na deni ni suala la kawaida kwa taifa au serilai yoyote. Lakini kusema hivyo haina maana kwamba kila nchi inayokopa inakwa na ‘guarantee’ kwamba itaweza kurejesha mikopo husika kwa wakati, lakini pia, bila ya kuathiri maisha ya wananchi ambao ndio wanaowajibika kulipa mikopo hiyo kupitia kodi na tozo mbalimbali juu yao na serikali. Kwa maana nyingine, kuna viashiria vinavyotumika kufanya tathmini iwapo deni la nchi lipo “sustainable’ au hapana. Tutajadili viashiria hivi baadae kidogo.


Lakini kwa sasa tuseme tu kwamba – ukweli kuhusu ‘sustainability’ ya deni la taifa, hasa deni la nje, ni lazima liambatane na takwimu. Kwa mfano, ushahidi kwamba serikali/nchi ina uwezo wa kumudu deni la taifa ni kwa kuangalia kiasi cha malipo yanayoenda kulipa madeni (Debt Servicing) ‘as percentage of government revenues’.takwimu ya Kama kweli Serikali au nchi ina uwezo wa kumudu madeni yake, ni lazima hili lionekane katika takwimu inayoonesha ‘debt servicing as a percentage of government revenues’.


Iwapo takwimu hii inapungua mwaka hadi mwaka, ni ishara kwamba serikali/nchi inalimudu deni la taifa vizuri. Lakini iwapo takwimu hii inaongekeza mwaka hadi mwaka au inagota katika kiwango kimoja kwa miaka mingi, hii ni ishara kwamba nchi/serikali inalemewa na haiwezi kumudu deni la taifa. Vinginevyo, kupungua kwa ‘debt servicing as a percentage of government revenues’ huwa ni matokeo ya serikali kutumia vizuri mikopo husika kwa kuwekeza (investment) katika shughuli ambazo zinazalisha mapato makubwa ya Kodi, hivyo kuiweka serikali katika nafasi nzuri ya kupunguza deni la nje kw kasi ya kuridhisha.


Kwa maana nyingine, matumizi mazuri ya mikopo itakayopelekea ‘sustainability’ ya deni la nje ni pamoja na kuhakikisha kwamba mikopo husika inawekezwa katika sekta zitazochochea kasi ya kukua kwa uchumi (GDP growth), lakini pia shughuli hizi za kiuchumi ziweze pia kuzalisha kodi za kutosha. Iwapo haya yatafanyika kikamilifu, malipo ya deni na nje (as percentage of government revenues) yataendelewa kushuka mwaka hadi mwaka. Vinginevyo iwapo malipo ya deni la nje kwa kutumia kodi za wananchi (as percentage of GDP) hayashuki mwaka hadi mwaka na badala yake yanaendelea kuongezeka, hii ni dalili kwamba mikopo husika haina manufaa ya maana kwa walipa kodi.


Katika sehemu inayofuata, tutajadili kwa undani Uhusiano baina ya:


· Kasi ya kukua kwa deni la nje

· Kasi ya kukua kwa uchumi (GDP), na

· Kasi ya kutokomeza umaskini.
 
5.5.1 Uhusiano baina ya:


· Kasi ya kukua kwa deni la nje

· Kasi ya kukua kwa uchumi (GDP), na

· Kasi ya kutokomeza umaskini.


Katika hali ya kawaida, kasi ya kukua kwa deni la taifa inatakiwa iendane na kasi ya kukua kwa uchumi ambao matokeo yake yanaonekana kwa wananchi kwa maana ya maisha bora kijamii na kiuchumi. Kwa kipindi cha miaka mingi sasa, uchumi wa Tanzania umekuwa na sifa mbili kati ya hizo tatu (kasi kubwa ya kukua kwa deni la taifa na kasi kubwa kukua kwa uchumi). Katika kipindi cha miaka kumi na tano (2000-2015), kasi ya kukua kwa uchumi imekaribia 7% kwa mwaka. Sambamba na kasi hii ya kukua kwa uchumi, deni la taifa limeendelea pia kukua kwa kasi kubwa. Lakini yote haya mawili hayajawa na matokeo ya kurudhisha kwenye kasi ya kupungua kwa umaskini.


· Ni sababu gani zinazopelekea uwepo wa hali hii?

Zipo sababu kuu mbili. Sababu ya kwanza tumeshaelezwa na Benki ya Dunia kwamba – Mikopo mingi ya nje inachochea kasi ya kukua kwa uchumi kwa njia ya ku ‘finance’ “Consumption” kuliko “Investments” ndani ya nchi. Kwa vyovyote vile, matumizi ya aina hii ya mikopo ya nje haiwezi kusaidia kasi ya kutokomeza umaskini.


Lakini ipo sababu ya pili. Wakopeshaji wa nje (lenders) wamekuwa wakivutiwa na kasi kubwa ya kukua kwa uchumi ambayo tayari wameikuta ipo.


Uhusiano wa kasi ya kukua kwa uchumi na kasi ya kupunguza umaskini Tanzania umekuwa ni wa mbali sana. Kwa mujibu wa ‘World Development Report’, kwa hali ya sasa, uchumi wa Tanzania utahitaji kukua kwa mara tano zaidi ya sasa ili kuondoa wananchi wote wanaoishi chini ya dola mbili kwa siku. Kwa maana hii, tutafanikiwa kutokomeza umaskini iwapo uchumi wa nchi utakuwa kwa 35% kwa mwaka. Hili sio jambo rahisi kutokea. Uhalisi huu unatukumbusha juu ya umuhimu wa kufanya mabadiliko makubwa katika mfumo wetu wa uchumi ili kasi inayowezekana sasa iweze kusaidia kupungua umaskini. Kasi ya 7% kwa mwaka inawezekana kutokomeza umaskini iwapo serikali itakuwa imejipanga vyema. Wadau wa maendeleo walidhihirisha hili wakati wa kuanza kwa Malengo ya Milenia mwaka 2000.


Vinginevyo katika hali ya sasa, World Development Report inaonyesha kwamba GDP growth rate ya 7% kwa mwaka inapunguza umaskini kwa 0.7% tu. Pia idadi ya wananchi wanao ondoka kwenye kundi la umaskini kwa kila ongezeko la 1% ya GDP Per Capita ni 0.2%.


Pamoja na nchi kuendelea kukopa fedha nyingi kutoka nje, kwa kipindi cha miaka 25 - (1988-2013), idadi ya watanzania wanaoishi chini ya Dola mbil kwa siku imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka, ingawa idadi hiyo ilipungua kidogo mwaka 2013. Hii ni kwa mujibu wa World Development Report:


Jedwali #4

MWAKA

IDADI YA WANANCHI WANAOISHI CHINI YA $2 KWA SIKU

1988

Milioni 25

1995

Milioni 30

2005

Milioni 36

2010

Milioni 36

2013

Milioni 35


5.6 Kasi ya kukua kwa deni la nje na pengo baina ya ‘wenye nacho’ na wasio ‘nacho’.


Katika hali ya kawaida, Pengo baina ya walio nacho na wasio nacho linatakiwa pungua kwa kadri nchi inavyozidi kupokea mikopo kutoka nje ya nchi. Lakini uhalisia nchini Tanzania ni kwamba – kwa kadri deni la nje linavyozidi kushika kasi, na pia kwa kadri pato la taifa (GDP) linavyozidi kupaa, ‘income inequality’ nayo inazidi kuongezeka. Kwa mfano, katika kipindi cha 2000-2012, wastani wa kipato cha ‘the richest 10% Tanzanians” kiliongezeka kwa $2,300, huku wastani wa kipato cha “the poorest 40%” kikiongezeka kwa $250 tu katika kipindi hicho hicho.


5.7 Kasi ya kukua kwa deni la nje na idadi ya watanzania wanaoshi na utapiamlo.


Katika hali ya kawaida, deni la nje likiendelea kukua kwa kasi kubwa na kuambatana na kasi kubwa ya kukua kwa uchumi (GDP), taifa halipaswi kuendelea kuwa na tatizo la utapiamlo miongoni mwa wananchi wake. Lakini tofauti na hili, idadi ya watanzania wanaoishi na matatizo haya ya kiafya imezidi kuongezeka mwaka hadi mwaka.


Jedwali #5 (FAO):

MWAKA

IDADI YA WATANZANIA WANAOISHI NA UTAPIAMLO

1988

Milioni 7

1995

Milioni 11

2005

Milioni 14

2010

Milioni 17

2013

Milioni 18


5.8 Uhusiano wa kukua kwa deni la nje na ‘diversification’ ya uchumi.


Deni la nje linatakiwa kupunguza utegemezi wa nchi kwenye ‘primary commodities’ miaka nenda miaka rudi. Uwekezaji/Matumizi mazuri ya mikopo ya nje yanatakiwa kusaidia nchi kuondokana na uchumi unaotegemea mapato ya fedha za kigeni kwa kuuza bidhaa zile zile kama mazao y abiashara na madini. Tofauti na hili, nchi husika inabakia kuwa ‘vulnerable’ to events kama vile natural disastes, kuporomoka kwa bei za ‘primary commodities’ kwenye soko la dunia, na hata depletion of resources (madini, gesi, mafuta) kwanini rasilimali hizi hazipo milele.


Kwa Tanzania, primary commodities zinaendelea kuchukua sehemu kubwa ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi (Exports). Bei ya bidhaa hizi – kwa mfano Dhahabu, Shaba, Kahawa, Chai, na mazao mengine ya biashara zimekuwa zikiyumba mara kwa mara, bei zake hazitabiriki na haziimariki. Kushuka kwa bei ya bidhaa inapelekea mapato ya serikali (fedha za kigeni) pia kupungua lakini pia, kuporomoka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya dola. Hali hii inapelekea kuongezeka kwa deni tunalodaiwa nje kama tulivyojadili awali.


5.10 Uhusiano baina ya kasi ya kukua kwa deni la nje na Kushuka kwa thamani/bei ya bidhaa ghafi zinazouzwa nje (i.e. Commodity Devaluation) na kuporomoko kwa thamani ya Sarafu ya nchi (i.e. Depreciation of Currency)


Kuporomoka kwa bei ya bidhaa ghafi katika soko la dunia ina athari kubwa kwa malipo ya deni la nje. Hii ni kwa sababu, nchi inayotegemea bidhaa za aina hii (primary commodities) hujikuta ikipata mapato kidogo zaidi ya fedha za kigeni. Kupungua kwa mapato ya kigeni, husababisha sarafu ya ndani (kwa mfano TZS) kushuka thamani (currency depreciation) dhidi ya sarafu za kigeni, hasa dola ya kimarekani. Hapa tukumbuke kwamba sehemu kubwa ya deni letu la nje lipo katika sarafu ya Dola za kimarekani, kwani tuliona kwamba kufikia Januari 2016, asilimia 79 ya deni la taifa ilikuwa ni deni la nje. Taifa linategemea fedha za kigeni kulipa madeni yake ya nje.


Katika hali hii, kushuka kwa thamani ya shillingi dhidi ya dola kunafanya deni la nje liongezeke. Sababu zinazofanya deni la nje kuongezeka ni kwamba – thamani ya shilingi ikishuka dhidi ya dola, ili tulipe kiasi kile kile cha deni katika sarafu ya “dola”, tunahitaji kupata fedha nyingi zaidi za ndani (rejea mjadala juu ya exchange rate risk), suala ambalo litailazimisha serikali aidha kuongeza viwango vya kodi inayotoza wananchi au serikali italazimika kupunguza matumizi yake kuhudumia wananchi ili kulipa ongezeko la deni la nje.


Kwa kawaida, Benki ya Dunia na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) huwa wanatabiri (projections) kiasi gani serikali/nchi itatumia kiasi gani cha fedha za walipa kodi kulipa deni la taifa/au malipo ya deni yanachukua kiasi gani cha mapato ya serikali(kodi). Lakini moja ya mapungufu makubwa ya mashirika haya katika kufanya utabiri wa aina hii ni kwamba, tathmini na utabiri wao huwa hauzingatii athari ya kushuka kwa bei ya ‘primary commodities’ katika soko la dunia. Suala hili linafanya ‘projections’ nyingi za aina hii ziwe ‘underestimated’ katika kukadiria mzigo wa deni la taifa kwa walipa kodi.



Katika sehemu inayofuata tutajadili:

Je tutaweza kustahimili?

Tunapimaje sustainability ya deni la nje?
 
5.12 Deni la nje na mapato ya Kodi: Je tutaweza kustahimili?


5.12.1 Tunapimaje sustainability ya deni la nje?


Sustainability ya deni la taifa inaweza kufanyiwa tathmini katika muktadha wa scenario zifuatazo:


· Scenario ya kwanza ni kwa kutumia IMF/World Bank baseline ambayo kwa kawaida huwa ni ‘high GDP growth’. Lakini kama tunavyofahamu, ni kawaida kusikia ‘IMF’ wakija na ‘down graded projections of economic growth’ baada ya projections za awali kuonekana ni za juu zaidi.


· Scenario ya pili ni kwa kuangalia uwezekano wa uchumi kukumbwa na ‘one major economic shock’. Mara nyingi hii huwa ni ‘devaluation of the currency’ - kupungua kwa thamani ya sarafu ya ndani/shilingi kufuatia kushuka kwa thamani ya ‘primary commodities’ kwenye soko la dunia.


· Mwisho ni scenario ya kasi ndogo ya kukua kwa uchumi/lower GDP growth tofauti na ile iliyotarajiwa.


Viashiria kwamba nchi ipo hatarini kuingia katika mgogoro wa deni la taifa:

Viashiria vikuu ni vitatu:


· Kwanza, malipo ya baadae (muda wa kati ujao) ya deni la nje kuwa ni zaidi ya 10% ya mapato ya kodi. Lakini kama takwimu hii haipo, basi iwapo deni la nje tayari ni zaidi ya 40% ya pato la taifa (GDP).

· Pili, deni kuwa mgizo mkubwa kwa pato la taifa, kwa maana ya kuwa ni zaidi ya 30% ya pato la taifa (GDP).

· Tatu, deni kubwa la taifa kuambatana na ‘current account deficit’, inayozidi (-5%) ya pato la taifa (GDP).


Katika sehemu inayofuata, tutapitia ‘scenarios’ tulizoona hapo juu (rejea sehemu ya 5.12.1), moja bada ya nyingine kwa lengo la kupima ‘sustainability’ ya deni la nje.


5.12.1.1 SCENARIO ONE - High GDP Growth


Kwa mujibu wa makadirio ya mfuko wa fedha wa kimataifa (IMF), ndani ya miaka michache ijayo, Serikali ya Tanzania itajikuta ikianza kutumia 10% ya mapato yake (kodi) kwa deni la taifa. Kama tulivyojadili huko juu, kwa kiwango hiki, maana yake ni kwamba nchi ipo katika hatari ya kukabiliwa na ‘unsustainable’ external debt.


Katika kishiria hiki cha kwanza, tuliona kwamba mbadala wake ni kiashiria kingine ambacho ni ‘uwiano wa deni la nje la pato la taifa’. Tuliona kwamba nchi inakuwa katika hatari ya kutumbukia katika mgogoro wa deni la nje iwapo deni la nje limefikia 40% ya pato la taifa (GDP). Tukichukulia pato la taifa kwa sasa (GDP) ambalo limeshafikia takribani TZS trilioni 100, na tukichukulia kiwango cha deni la nje ambalo sasa limekaribia TZS trilioni 34, tunaona kwamba hatupo mbali sana kufikia 40% kama uwiano wa deni la nje na pato la taifa (GDP). Hii ni kwa sababu, kwa kufuatana na kiashiria hiki, kwa sasa deni la nje ni kama 34% ya GDP, huku deni la hili likiongezeka kwa kasi kubwa kuliko pato la taifa (GDP).


Tukichukulia kiashiria cha pili hapo juu kwamba ikiwa jumla ya deni la taifa (ndani na nje) ikifikia 30% ya pato la taifa ni ishara ya hatari mbeleni, kwa kuangalia jumla ya deni la taifa (TZS trilioni 42) na pato la taifa (TZS trilioni 100), maana yake ni kwamba tumeshavuka 30% threshold, na tunapoelekea kuna hatari kubwa. Kwa mujibu wa IMF, nchi inakuwa salama tu iwapo deni lake la taifa lipo chini ya 50% ya pato la taifa (GDP). Lakini tukizingatia ukweli kwamba kasi ya kukua kwa deni la taifa inaendelea kuwa kubwa na kuliko kasi ya kukua kwa pato la taifa (GDP), hatupo mbali sana kufikia kiwango hiki cha 50%.


Kiashiria cha tatu na cha mwisho kinahusisha ‘current account deficit’, kwamba ikiwa ni (-5%) ya pato la taifa (GDP) au zaidi, ni ishara kwamba deni la taifa halipo ‘sustainable’. Kwa miaka karibia yote tangia uhuru, ‘current account deficit’ ya Tanzania imerekodiwa kuwa zaidi ya (-5%). Kwa mfano wastani wa kipindi cha 1970 - 2005 ilikuwa ni (-9%), huku wastani wa 2011-2015 ukiwa ni (-11%). Huko nyuma tulijadil kwamba ingawa suala la current account deficit ni jambo la kawaida kwa kila nchi, lakini hali hii ikiambatana na deni kubwa la taifa, huwa ni dalili ya deni la taifa kutokuwa ‘sustainable’. kama ilivyo kwa deni la taifa, current account deficit pia ina viashiria vyake vya kupima iwapo ipo ‘sustainable’ au hapana. Sustainability ya current account inategemeana na sustainability ya deni la taifa.


Tukirudi kwenye hoja ya awali kidogo, tuliona kwamba kwa mujibu wa IMF, ndani ya miaka michache ijayo Serikali ya Tanzania itaanza kulipa takribani 10% ya mapato yake (kodi) kwa deni la taifa. Kwa mujibu wa IMF, kwa hali hii, serikali itahitaji kuongeza mapato yake yafikie 19.5% ya GDP kwa kipindi cha 2015-2019 na 20.3% ya GDP ifikapo mwaka 2024 ili deni la taifa liendelee kuwa sustainable. Lakini kwa kuangalia uhalisi uliopo sasa, ni vigumu kubaini iwapo tutafanikiwa kufika huko kwani hivi sasa mapato ya kodi (as percentage of GDP) yanaendeleo kuwa chini ya 15% ya pato la taifa (GDP). Kwa maana hii, Serikali ipo nyuma kwa karibia 5% kufikia makadirio husika ya IMF. Hata takwimu za Serikali kupitia Waziri wa Fedha, Dr. Mpango akiwasilisha (Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa 2016-2021) bungeni zinaonyesha kwamba katika kipindi cha miaka 2 hadi mitatu ijayo, matarajio ya serikali ni kukusanya 17% tu ya pato la taifa.


5.12.1.2 SCENARIO TWO - One Economic Shock Scenario (Currency Devaluation)


Kwa mujibu wa IMF, iwapo itatokea economic shock moja wapo hapo katikati (kwa maana ya devaluation ya TZS dhidi ya Dola kutokana na kushuka kwa bei ya primary commodities kwenye soko la dunia), malipo ya deni la taifa (as percentage of government revenue) yatavuka 14% of mapato ya kodi. Kama tulivyokwisha jadili, miaka 50 baada ya uhuru, Tanzania bado inategemea fedha zake nyingi za kigeni kutoka katika mauzo ya ‘primary commodities’ nje ya nchi. Bei ya bidhaa hizi kwenye soko la dunia kwa mfano katika kipindi cha mwaka 2014-2015 ilipungua, na kupelekea ‘currency devaluation’ (rejea mjadala wa awali juu ya hili). Kuporomoka kwa bei ya bidhaa hizi kulipelekea kupungua kwa mapato ya serikali, lakini mbaya zaidi ni kwamba ‘devaluation’ ilipelekea thamani ya deni la nje kuongezeka. Na kama tulivyojadili kwamba IMF/World Bank huwa hawazingatii athari za suala hili katika ripoti zao za ‘kutathmini deni la taifa”, mzigo wa deni ni lazima utakuwa tayari ni mkubwa kwa walipa kodi kuliko inavyoelezwa.


5.12.1.3 SCENARIO THREE – Kasi ndogo ya kukua kwa uchumi (GDP) kuliko matajario


Kwa jinsi hali ilivyo nchini hivi sasa, uwezekano wa kasi ya kukua kwa uchumi kupungua katika miaka michache ijayo ni mkubwa, hasa kuelekea mwaka 2020. Iwapo hali hiyo itajitokeza, malipo ya deni la taifa (as percentage of government revenue) yatavuka 20%. Tukifikia kiwango hiki, nchi itakuwa haikopesheki tena hali hiihali itayapolekekea kuibuka kwa mgogoro mkubwa wa kiuchumi.
 
6. Sehemu ya Sita – Hitimisho


Mjadala wetu ulijikita katika muktadha wa serikali mpya ya awamu ya tano kwa kuangalia matarajio ya wananchi na changamoto za serikali. Serikali hii imeingia madarakani ikiwa na mzigo mkubwa wa kutimizia matarajio ya wananchi walio wengi. Matarajio haya yametokana na maendeleo makubwa ya kisiasa na kidemokrasia nchini ambayo yamepelekea wananchi wengi kuzidi kupata fursa ya kuelewa haki zao za kisiasa, kiuchumi na kijamii, pamoja na umuhimu wa kutumia mfumo wa kisiasa uliopo (demokrasia ya vyama vingi) kuonyesha kiu na shauku yao ya kutafuta mabadiliko ya kweli (kupitia sanduka la kura). Kwa kila namna, uchaguzi wa mwaka 2015 ulikuwa ni uchaguzi wa “Mabadiliko”. Baada ya uchaguzi huo wa kihistoria, serikali iliyopo madarakani inatakiwa kutumia vyema kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-2020) kuthibitishia wananchi kwa vitendo kwamba ni kweli ilidhamiria kuletea wananchi walio wengi mabadiliko ya kweli.


Tulijadili jinsi gani Serikali ya awamu ya tano imeanza kazi kwa kasi kubwa ya kujaribu kutimiza matarajio ya wananchi. Katika kufanya hivyo, tuliona kwamba serikali imeanza kwa kuweka kipaumbeke katika maeneo makuu matatu ambayo – Kwanza ni kurudisha nidhamu katika mfumo wa fedha za umma; Pili ni kuziba mianya ya ukwepaji kodi na ufisadi; na tatu, ni Kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ya fedha za walipa kodi.


Tuligusia matarajio ya wananchi pamoja na changamoto zake katika pembe tatu – kwanza iliku ni bajeti ya 2016/17 ambayo ni ya kwanza chini ya serikali ya awamu ya tano; pili ilikuwa ni Mpango wa pili wa Maendeleo wa Taifa 2016/17-2021/22; na Tatu ilikuwa katika majukumu ya serikali ya katika uchumi wa taifa ambapo tulibaini majukumu makuu matatu.


Mjadala uliendelea mbele zaidi na kujadili ngazi mbili kubwa za serikali katika nchi ambapo tuliona kwamba ni ngazi ya serikali kuu na ngazi ya serikali za mitaa. Katika muktadha huu, tulifanya tathmini ya mgawanyo wa majukumu makuu matatu ya serikali tuliyoyaona, baina ya ngazi hizi kuu mbili za serikali. Mgawanyo wa majukumu hayo ulizingatia vigezo vya ‘efficiency and effectiveness’, ambapo tuliweza kubaini ni majukumu yepi yabakie katika serikali kuu na majukumu yepi yabakie kwenye serikali ngazi ya halmashauri/manispaa.


Baada ya kugawanya majukumu haya, ukafuatia mjadala juu ya ‘taxation and revenue’ powers baina ya ngazi hizi kuu za serikali, na jinsi gani ngazi hizi zinaweza kugawana mamlaka ya kodi na mapato, pia kwa kuzingatia vigezo vya ‘efficiency and effectiveness, huku lengo kuu likiwa ni kuhakikisha kwamba maslahi ya wananchi walio wengi yanaboreshwa, na hivyo matarajio ya serikali ya mabadiliko (2015-2020), kuweza kutimia.


Baada ya hapo, mjadala ulihamia kwenye ‘deni la taifa’. Hapa tuliweza kuona umuhimu wa kutenganisha mjadala, uchambuzi na tathmini ya deni la nje na deni la ndani ya nchi. Tulifanikiwa kuona jinsi gani serikali hii iliyobeba msalaba wa ‘Mabadiliko’ inakabiliwa na changamoto kubwa, hasa hatari iliyopo mbeleni kutokana na kasi ya deni la taifa kuzidi kuwa kubwa huku takwimu zikionyesha wazi kwamba kwa miaka 55 ya uhuru, kasi hii ya kukua kwa deni la taifa haijawa na uhusiano wowote na kasi ya kutomea kwa umaskini nchini.


Katika mjadala, tuliweza kupitia viashiria mbalimbali vya kutuonyesha uhalisia juu ya hatari kubwa iliyopo mbeleni kiuchumi. Matarajio ni kwamba mjadala huu utakuwa ni wenye afya na wa kujenga, hasa katika kubadilishana mawazo juu ya nini kifanyike ili kupambana na changamoto zilizopo, kwa manufaa yetu kama taifa.
 
Naomba mniwie radhi, takwimu za kwenye majedwali zimetoka vibaya. Nitafanya marekebisho kisha kuwasilisha.
 
Mkuu Mchambuzi ahasante sana kwa bandiko hili linalofikirisha sana

Ningeomba ufafanuzi kutoka bandiko lako namba 23
Unasema kwa mujibu wa BOT sehemu ya deni la Taifa inaelekezwa maeneo mbali mbali

Ukatokea mfano wa sekta ya (transportation and telecommunication)
Kwa upande wa Transportation nadhani huo ni uwekezaji ambao kupima 'return' yake kwa muda mfupi si kazi rahisi

Tatizo langu lipo katika telecommunication. Kuna private players wengi ikiwemo serikali
Huduma zake zimekuwa za kibishara badala ya huduma za kawaida

a) Nini mchango wa sekta hii katika uchumi wa nchi kwa sasa?
b) Ni kwanini waziri aseme tunahitaji viwanda 5 vya bia na siyo eneo kama telecommunications? Nadhani kulikuwa na mjadala na DAR si LAMU kuhusu hili

Ahsante
 
Mkuu Mchambuzi ahasante sana kwa bandiko hili linalofikirisha sana

Ningeomba ufafanuzi kutoka bandiko lako namba 23
Unasema kwa mujibu wa BOT sehemu ya deni la Taifa inaelekezwa maeneo mbali mbali

Ukatokea mfano wa sekta ya (transportation and telecommunication)
Kwa upande wa Transportation nadhani huo ni uwekezaji ambao kupima 'return' yake kwa muda mfupi si kazi rahisi

Tatizo langu lipo katika telecommunication. Kuna private players wengi ikiwemo serikali
Huduma zake zimekuwa za kibishara badala ya huduma za kawaida

a) Nini mchango wa sekta hii katika uchumi wa nchi kwa sasa?
b) Ni kwanini waziri aseme tunahitaji viwanda 5 vya bia na siyo eneo kama telecommunications? Nadhani kulikuwa na mjadala na DAR si LAMU kuhusu hili

Ahsante

Nguruvi3,
Asante kwa hoja za kufikirisha. Naomba nijadili hoja zako kwa mpangilio ufuatao:

1. Miundo Mbinu ya barabara na mchango yake katika kutokomeza umaskini.
2. Mchango wa Sekta ya Mawasiliano katika kutokomeza umaskini.
3. Uwekezaji wa Viwanda vya Bia.
4. Mwisho, risks kuhusiana na miradi ya ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi, hasa katika sekta ya miundo mbini.

1. Miundo Mbinu ya barabara na mchango yake katika kutokomeza umaskini.

Nakubaliana na hoja yako kwamba kupima 'economic returns' za ujenzi wa miundon mbinu ya barabara katika kipindi kifupi sio kazi rahisi. Lakini kwa mfano Rais akiulizwa, ulikuwa waziri wa ujenzi kwa miaka mingi sana, na sekta hii imekuwa sana chini ya uongozi wako, je, mchango wake katika au juhudi zako zimechangia nini katika kasi ya kupunguza umaskini? Tujaribu kutafuta japo mwanga katika hili.

Mjadala juu ya uhusiano baina ya uwekezaji sekta ya miundo mbinu umekuwepo kwa muda mrefu sana hata katika ngazi ya jumuiya ya kimataifa inayojihusisha na maendeleo ya nchi maskini. Katika miaka ya 1990s, kulijitokeza 'two schools of thought' katika suala hili:

*Kwa upande mmoja, wao walihimiza juu ya umuhimu wa kuwekeza katika sekta ya miundo mbinu ili kuchochea kasi ya kukua kwa uchumi, ambayo waliamini kwamba itakuwa na matokeo chanya katika kasi ya kupunguza umaskini.

*Kwa upande wa pili, wadau wengi walianza kuingia na shaka ambapo kwa mujibu wa ripoti moja ya Department For International Development (DFID) ya nchini Uingereza, Mwaka 2002, wadau hawa walisema mambo makuu mawili:

(i). Ingawa miundo mbinu ni muhimu kwa ajili ya kuongeza kasi ya kukua kwa uchumi, uwekezaji wake ulikuwa na 'little relevance to poverty reduction'. Walitumia maneno haya haya 'relevance...'.
(ii). Actual benefits zitokanazo na uwekezaji katika miundo mbinu zilikuwa ni kidogo kuliko matarajio (kwa maneno yao, actual benefits were less than expected).

Miundo mbinu iliyofanyiwa tathmini ilikuwa ni ile ya Barabara, Reli, Bandari, na Viwanja vya ndege.

Miaka kadhaa iliyopita, kulifanyika utafiti juu ya suala hili hili la 'mchango wa sekta ya miundo mbinu katika kutokomeza umaskini'. Utafiti huo ulifanyika nchini Indonesia. Iligundulika kwamba barabara za majimbo "provincial roads" zilichangia kuongeza vipato na ajira kwa wananchi. Kwa mujibu wa utafiti huo, 1% of investment ya barabara za majimbo ulihusisha umaskini kupungua kwa 0.3% katika kipindi cha miaka mitano.

Tukumbuke kwamba hizi ni barabara za kwenye majimbo, ikiwa ni pamoja na feeder roads. Kwa maana nyingine, ni barabara ambazo nchini kwetu zipo chini ya serikali za halmashauri, na sio zile za Tanroads ambazo ndio zimekuwa zikichukua sehemu kubwa ya mikopo na kodi za wananchi. Katika hili turudishe kumbukumbu zetu pia katika mjadala wetu wa awali juu ya mgawanyiko wa majukumu baina ya ngazi kuu mbili za serikali, pamoja na mgawanyiko wa mamlaka juu ya mapato na matumizi kwa vigezo vya efficiency & effectiveness katika kuboresha maisha ya wananchi.

Maswali ya kutafakari:

(i) Je, barabara za Tanroads zinasaidia kujenga national integration of the economy au zinaendeleza mfumo ule ule kwa miaka zaidi ya hamsini wa kuelekeza mazao na rasilimali bandarini kwenda kuuza nje?

(ii) Je, kufuatia uwekezaji mkubwa wa barabara hizi za tanroads, whats the return to farmers - ambao ndio wanaobeba kulipa madeni yaliyotokana na mikopo husika?

(iii) Hizi barabara zimeongeza productivity ya wakulima?

(iii) Hizi bababara zime influence vipi bei ya mazao katika soko la ndani na la nje kwa manufaa ya mkulima (sio manufaa ya middle men na final consumer)?

(iv) Kufuatia ujenzi wa hizi barabara, soko la bidhaa za mazao ya biashara limekuwa bora zaidi kwa wakulima huko nje?

Kwa miaka kumi iliyopita, Sekta ya ujenzi imeendelea kukua kwa wastani wa zaidi ya asilimia KUMI, kiwango cha juu kuliko wastani wa kasi ya kukua kwa uchumi wa nchi (7%). Lakini kilimo, sekta ambayo ndio nyumbani kwa maskini, na ambapo uwekezaji wa miundo mbinu ndio unalenga kutokomeza umaskini, sekta hii katika kipindi hicho hicho imekuwa kwa wastani usiozidi 4%. Je hii inatuambia nini?

Ni kwamba kasi ya kukua kwa uchumi haina uhusiano wowote na kasi ya kupungua kwa umaskini kwa sababu kama tulivyoona katika bandiko la msingi huko juu, kasi kubwa ya uchumi (7%) inabebwa na sekta nyingi ambazo hazina uhusiano wa maana na kilimo.

2. Sekta ya Mawasiliano na Mchango wake kupunguza umaskini

Mawasiliano ni sekta nyingine ambayo pia inahusisha uwekezaji wa miundo mbinu. Kwa miaka kumi iliyopita, kasi ya kukua kwa sekta hii imekuwa ni kubwa (wastani wa zaidi ya asilimia kumi). Lakini kama tulivyoona, sekta ya Kilimo ndio nyumbani kwa maskini walio wengi Tanzania.

Maswali ya kutafakari:
(i) Lakini iwapo kasi ya kukua kwa sekta ya kilimo kwa miaka kumi iliyopita (wastani) haikuvuka 3%, huku sekta ya mawasiliano kasi yake ikifikia karibia 15%, tunawezaje kusema kwamba sekta ya mawasiliano ilikuwa na mchango katika kupunguza kasi ya umaskini nchini?

(ii) Je, sekta ya mawasiliano imeondoa 'market constraints' sekta ya kilimo kwa kiwango gani ambacho we can quantify and prove kwamba maisha ya mkulimu yameboreshwa?

Sekta ya mawasiliano inachangia 2.3% tu ya pato la taifa (GDP), huku kilimo kikichangia takriban 30%. Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, kasi ya kukua kwa sekta ya mawasiliano ilikuwa ni zaidi ya 10%, huku kwa upande wa kilimo iliendelea kubakia chini ya 4%. Tutawezaje kusema kwamba sekta ya mawasiliano imekuwa na mchango kwenye sekta ya Kilimo?

3. Ujenzi wa Viwanda Vya Bia:
Kwa mtazamo wangu, serikali imeweka kipaumbele katika viwanda hivi kutokana na mchango wake katika kodi. Pengine katika projections zao za mapato ya kodi, come what may, vilezi will deliver to government coffers. Sioni kitu kingine muhimu zaidi katika mkakati husika.

Vinginevyo kama tulivyoona katika mjadala wetu juu ya Viwanda, kabla ya wimbi la 'privatization' viwanda vya bia vilichangia national integration of the economy kwa kiasi kikubwa kuliko sasa. Kwa mfano, palikuwepo vertical and horizontal linkages baina ya viwanda hivi na suppliers wa inputs mbalimbali ambao walikuwa ni watanzania. Baada ya privatization, such linkages aidha zilipungua au kutoweka kabisa.

Tunahitaji kuhoji 'multiplier effect' ya viwanda vitano vya bia kwenye uchumi wa nchi.

4. Miradi ya Ubia Baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (Public Private Partnership Projects):

Tulijadili awali kwamba miradi ya aina hii ni 'risk' kubwa on the future debt crisis. Tuna mikakati ya kutumia PPPs katika miradi yetu mbalimbali. Tuliona mifano ya PPPs Tanzania ni pamoja na IPTL, Songas, na Symbion. Huko nyuma tulikuwa na mradi mwingine wa "City Water" ambao Edward Lowassa akiwa Waziri wa Maji, alivunja mkataba kuokoa fedha za walipa kodi baada ya kubaini athari zake baadae. Pengine tufafanue tena athari husika:

Sekta binafsi inajenga miundo mbinu kwa serikali kama vile bomba la mafuta/gesi, barabara, madaraja, reli, bandari, viwanja vya ndege, power plants nk. Katika ujenzi huu, serikali inaingia katika makubaliano kwamba ita 'guarantee' kufanya a set of payments kwa muda utakaokubaliwa. Pia, serikali inakubali kubeba mzigo incase mradi unaenda kombo.

Kwa maana hii, PPPs hizi zinakuwa na practical effect ile ile kama ambavyo serikali ingekopa yenyewe na kujenga kwani bado ni walipa kodi ndio watakaofanya malipo husika kwa private provider. Kilicho tofauti ni kwamba, chini ya huyu provider wa sekta binafsi, kwa vile haijengwi moja kwa moja na serikali, hii inatoa fursa kwa serikali to keep the debts off the balance sheet na kufanya kama vile the government owes less kuliko uhalisia. Kwa kuweka payment obligations za aina hii off the balance sheet, inakuwa ni vigumu kwa wananchi na hata wawakilishi wao (wabunge) kujua the magnitude of the national debt.

Utafiti unaonyesha kwamba PPPs zina gharimu zaidi walipa kodi kuliko ambavyo serikali ingeamua kukopa kutoka vyanzo vingine na kuwekeza katika miradi husika. Hii ni kwa sababu, pamoja na mengine, private sector borrowing ni gharama zaidi (mikopo yenye masharti ya kibiashara), private contractors huwa wanataka profits kubwa na negotiations katika miradi ya aina hii mara nyingi favors the private sector kuliko walipa kodi.

Tafiti zinaonyesha kwamba miradi ya aina hii inagharimu walipa kodi zaidi ya mara mbili kuliko ambavyo ingeigharimu serikali kama ingetafuta vyanzo vingine vya mkopo moja kwa moja. Tuna haja ya kuwa makini kila mara tunaposikia serikali ikieleza juu ya PPP projects. Miradi hii ipo katika sekta nyingi tu, nje ya miundo mbinu.
 
Mchambuzi ahsante, bado ninatatizika kidogo hapa.
1. Katika kukuza kilimo, hii ni pamoja na kujenga barabara kuwafikia wakulima ambao mchango wao ni 30% kwa mujibu wa bandiko.
Swali, kwani lengo ni kuwafikia wakulima tu au kuwafikia na kuleta unafuu?

Ninauliza hivyo kwasababu ukisoma bandiko lako,, mikopo mingi imeelekezwa katika ujenzi wa barabara. Kwanini kama lengo ni kuleta matokeo chanya kwa sekta ya kilimo, kusiwe na mkakati wa kufufua reli ambayo inaweza kurahisisha uchukuzi kutokana na gharama zake kuwa ndogo?

Kwanini tunaelekeza pesa za mikopo katika barabara, nini logic ya jambo hili?
 
Mchambuzi ahsante, bado ninatatizika kidogo hapa.
1. Katika kukuza kilimo, hii ni pamoja na kujenga barabara kuwafikia wakulima ambao mchango wao ni 30% kwa mujibu wa bandiko.
Swali, kwani lengo ni kuwafikia wakulima tu au kuwafikia na kuleta unafuu?

Ninauliza hivyo kwasababu ukisoma bandiko lako,, mikopo mingi imeelekezwa katika ujenzi wa barabara. Kwanini kama lengo ni kuleta matokeo chanya kwa sekta ya kilimo, kusiwe na mkakati wa kufufua reli ambayo inaweza kurahisisha uchukuzi kutokana na gharama zake kuwa ndogo?

Kwanini tunaelekeza pesa za mikopo katika barabara, nini logic ya jambo hili?
Nguruvi3,

Kwa miaka zaidi ya 20 sasa uwekezaji katika sekta hii ya barabara umechukua sehemu kubwa sana ya mikopo ya nje (fedha za walipa kodi). Na uwekezaji huu umepelekea sekta hii kukua kwa kasi kubwa, kwa mfano kwa zaidi ya miaka kumi, kasi ya kukua kwa sekta hii ni zaidi ya 10% (over and above 7%, ambayo ni national average katika kipindi hicho hicho). Swali linalofuata ni je:

*Growth in road infrastructure generates profitability and productivity katika sekta gani za uchumi?

Tumesha jiridhisha kwamba profitability and productivity haiendi kwenye sekta ya Kilimo. Kwa maana hii, productivity and profitability is not captured by those who finance the infrastructure investments (wakulima).

Umeuliza swali la msingi sana, je lengo ni kuwafikia au kuwaletea unafuu wakulima?

Kwa mtazamo wangu, lengo kuu ni kuwafikia wakulima just like in the old days kwa maana ya kwamba, mauzo ya mazao ya biashara yanahitajika sana na taifa ili kuleta fedha za kigeni. Lakini pili, mazao haya (ya biashara) yanahitajika sana na mabepari wa nje. Kwa maana hii, by default, ujenzi wa miundo mbibnu ya barabara unalenga barabara ambazo zinarahisisha further integration ya mkulima na international economy kuliko integration with the national economy. Tazama barabara nyingi za Tanroads zinapita kwenye maeneo ya mazao ya kilimo na pia madini kuyapeleka bandarini. All other benefits are secondary.

Kuhusu suala la reli, inaweza kutusaidia, lakini again, itatusaidia to integrate our national economy au kuzidisha integration of our farmers to the international economy? National integration itakuja ikiwa mikakati ya Viwanda vya ndani utakuwa na mafanikio.

Vinginevyo, we are not supposed to make agriculture important for life. This sector has to become less important in terms of GDP contribution kwa maana ya kwamba kupunguza 30% to somewhere under 10%, lakini kuongeza the Shilling contribution. Kwa mfano, tukichukulia GDP yetu ya sasa kuwa around 100 trillion Shillings, ina maana mchango wa kilimo kwa sasa (around 27/26%) katika GDP ya sasa, ni plus/minus ni kama TZS trilioni 27. Kwanini tunaendelea na 80/20 principle ambapo we use more resources to gain less badala ya kutumia the 20/80 principle meaning kutumia less resources to gain more, kwa kufanya kwa mfano 10% contribution ya Kilimo on GDP ichangie TZS trilioni 50?

By doing so, we will make kilimo less important kwa maana ya mchango wa asilimia, lakini more important kwa mchango wa Shillingi. We need to make agriculture less important in the future but we can only manage to do so by making it more important today.
 
BAJETI YA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO 2016/2017

Katika mjadala wetu, tumegusia juu ya umuhimu wa Serikali kuweka kipaumbele katika sekta Afya ili kufanikisha mkakati wake wa kuongeza kasi ya kupunguza umaskini nchini.

Hatimaye bajeti ya wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa mwaka ujao wa fedha (2016/17) imetangazwa na kupitishwa na bunge. Jumla ya fedha za walipa kodi zilizotengwa kwa ajili ya Wizara hii muhimu ni TZS Bilioni 845. Kati ya fedha hizo, karibia 60% zimeelekezwa kwenye matumizi ya ‘Maendeleo’.

Swali muhimu ambalo tunapaswa kujiuliza ni je:

· Kiasi hiki cha Bajeti kinaendana na matarajio ya wananchi kuwa bajeti ya kwanza ya Serikali ya awamu ya Tano itakuwa na sura ya mabadiliko?

Punde tutaangalia kwa undani swali hili muhimu. Lakini kabla ya kufanya hivyo, turejee kidogo masuala muhimu tuliyogusia katika bandiko la msingi. Tuliona kwamba:

Umaskini miongoni mwa wananchi wengi kwa miaka zaidi ya hamsini ya uhuru umechangiwa sana na mapungufu ya serikali katika kuweka kipaumbele kuendeleza sekta muhimu zifuatazo:

- Sekta ya Afya

- Sekta ya Elimu

- Sekya ya Kilimo

Vile vile tulijadili kwamba uzoefu wa nchi mbalimbali duniani unaonyesha kwamba nchi zilizopiga hatua kubwa kimaendeleo zilifanikiwa kufanya hivyo baada ya kuwekeza kwa nguvu kwenye ‘mtaji watu’ (Human Capital). Tukasema kwamba Human Capital ni kirutubisho muhimu cha ujenzi wa uchumi imara na wenye matokeo katika maisha ya wananchi. Na tukaona kwamba - Human Capital inajengwa na nguzo kuu mbili: AFYA na ELIMU, huku pia suala la LISHE likiwa ni sehemu muhimu katika mlinganyo huu.

Kwa miaka zaidi ya hamsini ya uhuru, sekta ya Afya bado haijapewa uzito unaostahili, suala ambalo limeendelea kukwamisha juhudi za kupambana na umaskini nchini. Ushahidi wa hili unaonekana wazi kwa kutizama mchango wa Sekta ya Afya katika pato la taifa (GDP). Kwa mfano, hivi sasa, mchango wa sekta hii kwenye Pato la Taifa (GDP) ni chini ya asilimia mbili, (1.5% to be specific).

Suala hili ni la kustaajabisha kidogo kwa sababu, kwa mujibu wa ripoti za Benki Kuu (BOT), “Ustawi wa Jamii” ni miongoni mwa sekta ambazo imekuwa ikipokea fedha nyingi kutoka nje kwa njia ya mikopo (deni la taifa). Lakini pamoja na uhalisia huu, bado ‘growth/productivity’ ya mikopo hii (kwa wastani wa miaka kumi iliyopoita) ni ndogo sana, karibia 1.6%. Vile vile mchango wa sekta hii kwa pato la taifa (GDP) licha ya fedha nyingi za mikopo ya nje kuelekezwa huko, kama tulivyoona ni mdogo sana katika kipindi cha miaka kumi iliyopita (wastani wa 1.5%).

Tukitazama sekta nyingine zinazopokea mikopo mikubwa kutoka nje, kwa mfano Sekta ya Usafiri na Mawasiliano ambayo kwa mujibu wa Benki kuu, inapokea 23% ya mikopo yote ya nje), growth/productivity ya mikopo hii ni kubwa, zaidi ya 10% kwa wastani wa kipindi husika. Hivyo hivyo kwa sekta namba mbili katika kupokea mikopo ya nje (Nishati na Madini ambayo inapokea 17% ya mikopo ya nje), productivity ya mikopo husika kwa wastani ipo juu, zaidi ya 10%. Tubabaki kujiuliza, kuna nini katika sekta muhimu kama ya Afya?

Awali tuliona kwamba katika moja ya Vipaumbele vinne vya Mpango wa Maendeleo (2016/17-2020/21), lipo eneo la “Kufungamanisha Maendeleo ya Uchumi na Maendeleo ya Watu”. Katika hili, yanatajwa maeneo makuu muhimu ya ujenzi wa mtaji watu (Human Capital) ambayo ni Elimu na Afya. Lakini kwa bajeti hii ya 2016/17, hatuoni dalili yoyote ya kufanikiwa kwa malengo husika katika mpango wa maendeleo uliotangazwa bungeni hivi karibuni.

Lakini hili suala lisitushangaze sana. Hii ni kwa sababu ni jadi kwa serikali ‘not to walk the talk’. Kwa mfano, katika bandiko letu la msingi tulijadili Azimio la Abuja (2001) juu ya Kuboresha Afya za Wananchi. Tulisema kwamba Azimio hili lilikutanisha Viongozi kutoka nchi za Umoja wa Afrika (AU) wakiambatana na wataalam na washauri wao juu ya masuala ya Afya, ambapo kwa pamoja walitia saini ya makubaliano kwamba ili kuboresha Afya za wananchi na kumarisha Mtaji Watu (Human Capital), kila Serikali itenge kiasi kisichopungua asilimia 15 (kumi na tano) ya Bajeti yake ya Afya kila mwaka. Serikali ya Tanzania ilishiriki kutia saini makubaliano husika.

Tukasema licha ya such commitment, kutokana na sababu zisizoeleweka, Serikali ya Tanzania haijawahi kutekeleza hata chembe ya azimio hili. Hivyo tukahimiza kwamba kwa vile serikali kupitia mpango wake wa maendeleo imedhamiria kukuza Raslimali Watu nchini, ni vyema ikawaonyesha wananchi kwamba bajeti yake ya kwanza ya Afya ni bajeti ya MABADILIKO, na hivyo kukidhi matarajio ya wananchi. Ili kufanikisha hilo, tukashauri kwamba kwa mwaka ujao wa fedha, Serikali inapaswa kutenga Kiasi kisichopungua TZS Trilioni 4.4 (ikiwa ni sawa na asilimia 15) ya Bajeti nzima ya TZS Trilioni 29.5 kwa ajili ya Wizara/Sekta ya Afya.

Swali linalofuata ni je:

· Serikali imetenga kiasi gani cha fedha kwa ajili ya Wizara hii ya muhimu (Afya)?

Kama tulivyoona, kiasi cha fedha kilichotengwa ni TZS bilioni 845, ambayo ni sawa na 2.8% tu ya bajeti nzima ya TZS Trilioni 29.5.

Wananchi wengi (hasa maskini) walikuwa na matumaini kwamba Uchaguzi wa TANO wa Vyama Vingi (2015) utakuwa ni uchaguzi wa ''mabadiliko.'' Lakini kinyume chake, mwenendo uliopo unaonyesha kwamba serikali ya awamu ya tano bado ni yenye kufuata mfumo ule ule unaoshadidia mambo YALE YALE kufanywa kwa namna ILE ILE na yenye matokeo YALE YALE kwa maisha yao kwa miaka zaidi ya Hamsini ya uhuru.

Katika sehemu inayofuata, tutaangalia kwa undani swali letu la msingi huko juu kwamba:

· Je ni kiasi gani hasa cha matumizi ya fedha za walipa kodi ndicho sahihi zaidi kwa ajili ya Sekta ya Afya nchini?

Ili kupata jibu kwa Swali hili, tunapaswa kwanza kuzingatia changamoto za Afya zilizopo katika jamii/nchi yetu. Kwa mfano, matatizo ya HIV/AIDS, utapiamlo, Malaria, nk. Kutokana na umuhimu wa kuzingatia changamoto zilizopo, tunalazimika kupanua zaidi swali letu na badala yake kuhoji:

· Je tunahitaji kutenga kiasi gani cha fedha kibajeti kwa ajili ya sekta ya afya kwa kufuatana na ‘epidemiological profile ya nchi yetu?

Kwa kuingiza suala la ‘epidemiological profile’ katika kutafuta jibu, tunaanza kuona umuhimu wa ‘siasa’ katika kufanikisha malengo husika, hasa ‘political will’. Kwa mfano, dunia ilifanikiwa kugundua chanjo ya kutokomeza ugonjwa wa “Polio” zaidi ya miaka 60 iliyopita lakini licha ya uwepo wa tiba ya ugonjwa huu kwa muda mrefu, ilichukua miaka mingi sana kwa baadhi ya nchi duniani, Tanzania ikiwepo kuamua kutokomeza janga hili.

Kwa maana hii, kiasi cha fedha za kutenga kwa ajili ya bajeti ya sekta ya Afya kitategemea sana na ‘hamu yetu kama taifa/what we aspire to do as a nation’. Iwapo tunakubaliana na hili, basi pia tutakubaliana kwamba swali letu hapo juu linahitaji kupanuka tena na kuchukua sura mpya kama ifuatavyo:

· Je tunahitaji kutenga kiasi gani cha fedha kibajeti kwa ajili ya sekta ya afya kwa kufuatana na ‘epidemiological profile ya nchi yetu ‘relative to the level of health status that we aspire as a nation’?

Tukisoma between the lines na pia kutafakari swali hili kwa kina, tutaona kwamba hata swali hili bado halijakidhi kiwango cha kutoa majibu ya kutusaidia kutatua suala husika. Hii ni kwa sababu, kunaibuka suala lingine la ‘inputs’ na ufanisi wa ‘inputs’ mbalimbali zinazohitajika kuboresha sekta ya afya nchini, hivyo kuwa na matokeo chanya kwa wananchi kwa maana ya ‘Afya Bora’ (tofauti na bora afya). Inputs tunazozungumzia hapa ni pamoja na ‘capacity’ ya watumishi waliopo sasa sekta ya afya, tekinolojia iliyopo/inayotumika, upatikanaji wa dawa pamoja na ubora wa dawa husika, nk. Haya yote yata athiri matokeo ya matumizi ya fedha zitakazo tumika, kwa maana ya ubora wa afya za wananchi.

Vile vile, katika hili, tunaona kwamba kuna namna nyingi zaku ‘organize’ matumizi ya hizi ‘inputs’. Suala hili lina athari kiasi cha fedha kitacho hitajika katika usimamizi na utekelezaji wa malengo husika. Iwapo tunakubaliana katika hili, basi pia tutakubaliana kwamba tunatakiwa kubadili tena sura ya swali letu la hapo juu:

· Je tunahitaji kutenga kiasi gani cha fedha kibajeti kwa ajili ya sekta ya afya kwa kufuatana na ‘epidemiological profile ya nchi yetu ‘relative to the level of health status that we aspire as a nation’, na kwa kuzingatia ufanisi wa inputs za afya tulizojadili?

Kama tulivyogusia, ufanisi wa ‘inputs’ ni suala muhimu sana. Lakini pia suala lingine muhimu ni gharama/bei ya ‘inputs’ husika. Nchi zenye mafanikio makubwa ya uchumi wa soko huria wenye matokeo makubwa kwa wananchi walio wengi, na zenye ‘large economies of scale’ zina uwezo wa kuzalisha madawa na vifaa vya afya kwa idadi kubwa (mass production) kwa gharama ndogo.

Mbali ya suala hili, pia lipo lingine muhimu ambalo ni hali ya ‘soko la ajira’ na ‘mfumo wa elimu’ kwani haya yana athari kubwa katika viwango vya mishahara kwa wataalam wa afya wanaotegemewa kuboresha afya za wananchi. Kwa maana hii, kiasi cha fedha kitachohitajika kutumiwa kwa ajili ya Sekta hii lazima kitabadilika kuendana na bei ya ‘inputs’ tulizojadili awali. Iwepo tunakubaliana hapa, basi pia tutakubaliana kwamba tunahitaji kupanua zaidi swali letu la hapo juu:

· Je tunahitaji kutenga kiasi gani cha fedha kibajeti kwa ajili ya sekta ya afya kwa kufuatana na ‘epidemiological profile ya nchi yetu ‘relative to the level of health status that we aspire as a nation’, na kwa kuzingatia ufanisi wa inputs za afya tulizojadili zitakazo patikana kwa gharama/kwa bei z/iliyopo?

Kufikia hapa tunaweza kusema kwamba sasa swali letu limejitosheleza, na majibu yake yatatusaidia. Lakini tukitafakari kwa kina kuhusu changamoto zinazoikabili Sekta yetu ya Afya, tutaona kwamba swali letu bado lina mapungufu kidogo. Kwa mfano, tumeangalia sekta ya Afya tu, na hatujazingatia mahitaji mengine ya kijamii yanayotegemea kodi hizo hizo za wananchi kama vile elimu, miundo mbinu, maji nk. Kwahiyo pamoja na umuhimu wa sekta ya afya, tunahitaji pia kuzingatia ‘the best alternative use of the available resources’ tukizingatia uhalisia uliopo juu ya ‘limited resources available vis a vis unlimited wants’.

Hivyo basi tunalazimika tena kupanua zaidi swali letu la hapo juu:

· Je tunahitaji kutenga kiasi gani cha fedha kibajeti kwa ajili ya sekta ya afya kwa kufuatana na ‘epidemiological profile ya nchi yetu ‘relative to the level of health status that we aspire as a nation’, na kwa kuzingatia ufanisi wa inputs za afya tulizojadili, huku pia tukitilia maanani gharama/bei za inputs husika kwa bei za wakati huo, na kwa kuzingatia umuhimu wa matumizi mbadala ya fedha (hadimu/limited) kufuatana na mahitaji mengine (unlimited wants) ya kijamii nje ya sekta ya afya?

Kufikia hapa ni muhimu tukasema kwamba ukweli uliopo ni kwamba - jamii yoyote itataka serikali yake iweke kipaumbele kikubwa kwenye kuboresha mfumo wa afya ndani ya taifa.

Kufikia hapa, turejee tena kwenye swali letu la msingi kwamba:

· Je ni kiasi gani hasa cha matumizi ya fedha za walipa kodi ndicho sahihi zaidi kwa ajili ya Sekta ya Afya nchini?

Tumeona kwamba ili kupata majibu, tunalazimika kuzingatia factors mbalimbali ambazo zitatupa different results towards lengo husika. Factors tulizojadili ni ‘epidemiological profile ya nchi yetu; level of health status that we aspire as a nation’; ufanisi wa inputs muhimu kwenye sekta ya afya kwa kukitilia maanani pia gharama/bei za wakati huo; na pia kwa kuzingatia umuhimu wa matumizi mbadala ya fedha (hadimu/limited) za walipo kodi kwa ajili ya matumizi mengine (unlimited wants) ya kijamii nje ya ‘Afya’.

Kwa kufanya hivyo, tutakuwa katika nafasi nzuri zaidi to determine kiwango halisi (fedha za bajaeti) tunachohitaji kwa ajili ya kuwekeza na kuendeleza sekta yetu ya Afya na kupata matokeo chanya kwa maana ya Afya bora kwa wananchi, na sio bora afya kwa wananchi.
 
Naona hapa sisi wengine tutabakia wasomaji tu ingawa sina hakika wapo wengi watakaosoma hiki kisima cha hekima kwa ujumla wake. Asante sana Mchambuzi, wewe ni kichwa, endeleza hizi juhudi za kuelimisha bila kuchoka.
Naam ni kisima haswa! Mkuu Mchambuzi, kuna suala la bajeti ulilosema asilimia 60 ya Bilioni 840 ni pesa za maendeleo. Unaweza kutupa mchanganuo wake?

Afya ni huduma hivyo maendeleo yake yana malengo tofauti. Kisha nitaweka senti sumuni
 
Naam ni kisima haswa! Mkuu Mchambuzi, kuna suala la bajeti ulilosema asilimia 60 ya Bilioni 840 ni pesa za maendeleo. Unaweza kutupa mchanganuo wake?

Afya ni huduma hivyo maendeleo yake yana malengo tofauti. Kisha nitaweka senti sumuni

Nguruvi3,

Kwa mujibu wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (2016/17), takribani TZS Bilioni 500 kati ya TZS bilioni 845 ndio zilizotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Binafsi sijaweza kuona mchanganuo husika katika bajeti hii, lakini kwa mujibu wa maelezo ya NGO ya ‘Policy Forum’, pamoja na mengineyo, serikali inatajaria kuboresha hospitali za rufaa nchini. Pia kuna mgao wa ajili ya benki ya damu (TZS Bilioni 5) kwa mikoa ya Mara, Geita, Kigoma, Mwanza na Simiyu; Ukarabati wa miundo mbinu ya afya katika hospitali mpya tano za wilaya; na uwekaji wa mfumo wa mionzi wa kidijitali katika hospitali mbili za rufaa na saba za mkoa; Vile vile, serikali imetenga kiasi cha TZS Bilioni 3 kwa ajili ya manunuzi ya vifaa tiba kwa ajili ya taasisi ya saratani ya Ocean Road, TZS Bilioni 2 kwa ajili ya taasisi ya mifupa muhimbili na TZS Milioni 876 kwa ajili ya hospitali ya Bugando, Mwanza.

Vinginevyo kwa mujibu wa Hotuba ya bajeti (2016/17), serikali imeweka vipaumbele katika maeneo makuu kumi na tano kama ifuatavyo:

1. Kuimarisha Huduma za Kinga, Tiba, kuongeza usawa katika utoaji wa huduma za afya na kupunguza vifo vya wanawake wajawazito,

2. Kuimarisha upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya umma vya kutolea huduma za afya,

3. Kuimarisha miundombinu kwenye vyuo vya mafunzo ya afya kwa lengo la kuongeza udahili na upatikanaji wa rasilimali watu,

4. Kuendeleza ujenzi, upanuzi na ukarabati wa miundombinu ya kutolea huduma za afya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Benjamini Mkapa - Dodoma, Taasisi ya Saratani Ocean Road, Hospitali Maalum za Mirembe na Kibong’oto; pia Hospitali za Rufaa za Kanda za Bugando, KCMC, Mbeya na Mtwara.

5. Kuimarisha mazingira ya ubia na ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi (PPP) katika utoaji wa huduma za afya,

6. Kuimarisha huduma za lishe na upatikanaji wake katika jamii na vituo vya kutolea Huduma za Afya,

7. Uimarishaji wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kuboresha huduma za afya.

8. Kuendelea na utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa katika Sekta ya Afya.

9. Kuhamasisha wananchi kwa nia ya kuongeza idadi ya wanaojiunga na Mifuko ya Bima za Afya.

10. Kuzuia na kukabiliana na ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto ikiwemo kupambana na mimba na ndoa za utotoni;

11. Kuimarisha na kupanua juhudi za kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuhamasisha uanzishwaji wa SACCOS na VICOBA vya wanawake, kuwapatia elimu ya ujasiriamali, biashara na kuwaunganisha na vyombo vya fedha ikiwemo Benki ya Wanawake Tanzania na Mfuko wa Maendeleo wa Wanawake;

12. kuimarisha miundombinu ya Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi kwa lengo la kuongeza udahili wa wanafunzi ili kuwapatia maarifa na stadi za kuwajengea uwezo wa kujitegemea na kuinua hali za maisha yao na taifa kwa ujumla

13. Kuwajengea uwezo watumishi wa maendeleo ya jamii wa Halmashauri ili kuchochea ari na mwamko wa wananchi wa kutumia rasilimali zilizopo katika kuongeza kipato kwa jamii hasa vijana na wanawake;

14. Kuimarisha haki, ulinzi na usalama wa wazee pamoja na kukarabati makazi ya wazee, shule za maadilisho na mahabusi za watoto na kuwapatia chakula; na

15. Kuwezesha mapitio ya sheria na kanuni mbalimbali zinazokinzana na haki za wanawake na watoto ambazo ni: Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971, Sura ya 29 na marekebisho yake ya mwaka 2002; Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya mwaka 2004; Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009; na Kanuni za Mirathi Na. 279 za mwaka 1963

Pamoja na vipaumbele tajwa, tukiangalia bajeti ya TZS Bilioni 845, ambapo takribani TZS Bilioni 518 ni kwa ajili ya maendeleo, sawa na kama 61% ya bajeti yote. Kiasi hiki ni kidogo sana kufanikisha malengo tajwa.

Suala lingine muhimu la kuzingatia ni kwamba, kati ya fedha hizi TZS Bilioni 518 zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo, TZS Bilioni 198, kama 31% ya fedha zote kwa ajili ya Maendeleo zinatarajiwa kutoka vyanzo nje ya nchi. Kwa mtafaruku uliojitokeza baina ya Serikali ya sasa na wahisani, hasa kufuatia ukanzamizaji wa haki za binadamu na demokrasia nchini, ni vigumu kuwa na uhakika kwamba kiasi hiki cha fedha kutoka nje kitapatikana.

Awali tulijadili juu ya umuhimu wa serikali kuzingatia makubaliano ya kutenga kiasi cha kutosha (Bajeti) kwa mujibu wa Azimio la Abuja (2001) juu ya sekta ya Afya. Azimio hili lilitaka serikali kutenga sio chini ya 15% ya bajeti zake za taifa kila mwaka kwa ajili ya Sekta ya Afya. Kitendo cha kutenga TZS 845 Billioni ni kinyume cha makubaliano husika, kwani kiasi hiki ni asilimia isiyozidi tatu ya bajeti nzima (2.8% to be eact). Jambo hili ni la kushangaza kidogo hasa ikizingatiwa kwamba Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP II) unaonyesha asilimia kumi na tano 15 kama lengo la serikali kwa mwaka 2020.

Pia katika bandiko #33 tulijadili juu ya umuhimu wa serikali kuangalia suala la ‘rasilimali fedha’ kwa ajili ya sekta hii muhimu in a ‘holistic manner’, ambapo tulichambua swali la msingi kwamba je:

Je ni kiasi gani hasa cha matumizi ya fedha za walipa kodi ndicho sahihi zaidi kwa ajili ya Sekta ya Afya nchini?

Udadisi wetu ukatufikisha kwenye swali lifuatalo kama kikomo:

·Je tunahitaji kutenga kiasi gani cha fedha kibajeti kwa ajili ya sekta ya afya kwa kufuatana na ‘epidemiological profile ya nchi yetu ‘relative to the level of health status that we aspire as a nation’, na kwa kuzingatia ufanisi wa inputs za afya tulizojadili, huku pia tukitilia maanani gharama/bei za inputs husika kwa bei za wakati huo, na kwa kuzingatia umuhimu wa matumizi mbadala ya fedha (hadimu/limited) kufuatana na mahitaji mengine (unlimited wants) ya kijamii nje ya sekta ya afya?

Kufikia hapa nadhani nimejaribu kujibu swali lako kwa kadri ya uwezo wangu (swali kuhusu “mchanganuo” wa bajeti ya Afya 2016/17 kama ilivyowasilishwa).

Ili kuamsha mjadala, naomba niongeze neno kidogo katika bandiko linalofuata hapo chini.
 
Sekta ya Afya nchini imejengwa na ‘a three tier system” kama ifuatavyo:

· Basic Clinics, Dispensaries – Ngazi ya KWANZA

· District Hospitals – Ngazi ya PILI

· Referral Hospitals and Specialty – Ngazi ya TATU (mifano ya Hospitali za Rufaa ikiwa ni pamoja na Muhimbili, KCMC, Bugando, Mbeya); na (mifano Speciality ikiwa ni pamoja na Taasisi ya Moyo, Taasisi ya Kansa nk).

Serikali ya Awamu ya TANO, Serikali inayotarajiwa kuwa ni ya ‘Mabadiliko’ inatakiwa kuwa na ufahamu kwamba mfumo huu inakabiliwa na changamoto zifuatazo:

Pamoja na kwamba aslimia sabini na tano (75%) ya mahitaji ya afya kwa wananchi yapo katika ngazi ya KWANZA (i.e. basic clinics and dispensaries), huku asilimia ishirini na tano (25%) mahitaji ya afya ya wananchi yakiwa katika ngazi ya JUU (i.e. referral hospitals and specialty), katika upangaji wa bajeti za Wizara ya Afya miaka nenda miaka rudi, serikali huwa haitengi fedha kwa kufuatana na mahitaji haya. Badala yake, asilimia 75% ya ‘resources’ (madawa, vifaa, mishahara, posho, education and training, nk) huwa zinapelekewa kwenye ngazi ya juu (referral hospitals na Specialties). Hali hii kidogo ni ya kushangaza kwa sababu zifuatazo:

Kila siku, ‘major outpatient diseases’ nchini (magonjwa ambayo huwa hayahitaji mgonjwa kulazwa zaidi ya kuonana tu na daktari) ni yafuatayo:

· Malaria; Acute Respiratory Infection ; Numonia ; Kuhara; Eye infection; Skin Infection; Anaemia; na UTI.

· Magonjwa ya kulala hayapo mengi kama yale ya ‘out patients’ na yanajumuisha pamoja na ugonjwa kama vile malaria, TB, Ukimwi, nk.

Hoja ya msingi hapa ni kwamba asilimia tisini ya magonjwa yote Tanzania yanaweza kupatiwa tiba katika vituo vya afya/ngazi ya chini katika mfumo tuliojadili huko juu (dispensaries and clinics), iwapo ngazi hii ya afya itapatiwa wataalam tena wa kawaida sana, vifaa (very basic) kama vile vya diagnosis pamoja na madawa. Lakini kwa vile Serikali haifanyi hivyo kwa maana ya kutenga ‘enough resources’ kwa ajili ya ngazi hii ya awali ya Afya, matokeo yake ni wataalam wengi wanakosa motisha ya kutumikia ngazi za chini na badala yake wanarundikana katika ngazi za juu tulizojadili awali, hali inayopelekewa ‘too much manpower chasing too few resources’.

Swali linalofuata ni je, Kwanini Serikali imekuwa inafanya hivyo?

Pengine ni kwa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na:

Kwanza - Serikali inaona kuna umuhimu wa kutumia fedha nyingi ‘to train’ wataalam wa Afya ili waende kutoa huduma za Afya katika ngazi za chini i.e. district hospitals, and clinics and dispensaries, ndio maana kila mwaka fedha nyingi za walipa kodi zinatengwa kwa ajili ya kutekeleza hilo.

Pili – inawezekana serikali inawekeza zaidi katika ngazi za juu kwa sababu bado hakuna ‘Health Insurance Market’ nchini yenye uwezo wa kuwasaidia wananchi walio wengi kwa sababu wengi ni maskini, hence they cannot insure themselves against the risk of serious illnesses, injury and the consequent need for very expensive treatment. Kutokana na uhalisia huu, serikali inaona kuna haja ya kutenga fedha nyingi kwenye ngazi ya juu (Referral hospitals and specialty hospitals – moyo, saratani, n.k), kuliko ngazi za chini.

Lakini majibu haya yanazua mjadala/maswali kadhaa. Kwa mfano:

Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi (2007-2017), nchi bado inakabiliwa na uhaba mkubwa wa wataalamu wafuatao (Clinicians, Nurses, Pharmacists, Lab technicians, Radiographers, Therapists nk.). Kwa mujibu wa Mpango huo, watalaam wa aina hii waliopo ni kama 30% tu ya idadi inayohitajika. Mpango huo wa maendeleo (2007-2017) unaendelea kuainisha kwamba, kufikia mwaka (2007), nchi ilikuwa na takribani vyuo sita tu (Medical Schools), na kati ya hivyo, serikali ilikuwa na chuo kimoja tu, huku sekta binafsi ikiwa na vyuo vitano.

Nje ya Vyuo rasmi (Medical Schools), nyingi ya ‘training institutes’ zilikuwa ni aidha za Sekta binafsi au NGOs. Licha ya serikali kutenga fedha nyingi kwa ajili ya kuendeleza mfumo wa aya ngazi ya juu, je ni kwanini bado imeshindwa kujenga vyuo vya kisasa kwa ajili ya kujenga na kuendeleza wataalam nchini? Bila ya kufanya hivyo, ‘output’ ya wataalam wa afya (kuanzia ngazi ya cheti hadi degree) itaendelea kuwa ni kidogo sana to bridge na HR deficit in the sector. Pia pamoja na fedha nyingi (resources) kuendelea kuelekezwa ngazi za juu in the 3 tier system, ni kwanini bado magonjwa mengi makubwa yanahitaji serikali kupeleka wagonjwa kutubiwa nje ya nchi. Kwanini Fedha zinazotengwa kila mwaka

Pia lipo tatizo la ukosefu wa ‘update of health work force skills’, hasa katika ngazi za chini.

Kuna another concern, Miaka nenda, miaka rudi, pamoja na fedha nyingi kutengwa kwa ajili ya kuendeleza manpower in the health sector, bado uwiano baina ya daktari na wananchi (Doctor to Patient Ratio) kitaifa na kwa mkoa mmoja mmoja inaendelea kuwa katika kiwango kile kile cha juu tofauti na inavyopendekezwa na World Health Organization (WHO).

Leo hii, karibia 50% ya hospitali zote nchini ni za NGOs, huku nusu iliyobakia ikiwa ni mchanganyiko wa zile za serikali na zilizo chini ya sekta binafsi.

Wananchi walio wengi bado wanaishi vijijini (sio chini ya 70% of the population). Karibia 25% ya clinics na dispensaries zote nchini ni za NGOs, huku zilizobakia zikiwa ni zile chini ya serikali. Nyingi ya clinics & dispensaries zipo vijijini. Lakini kama tulivyokwisha ona, ni asilimia 25% tu ya bajeti ya serikali ndio uelekezwa kwenye mahitaji ya vijijini ambako sio chini ya 70% ya watanzania ndio wanaishi.Ndio maana,sekta ya afya katika ngazi hizi za Clinics na Dispensaries hasa ambazo zipo chini ya Serikali zinaendelea kukabiliwa na uhaba wa wataalam, vifaa, na madawa. Matokeo yake ni kwamba, 70% ya Watanzania wanategemea huduma za afya zinazotolewa na NGOs, Waganga wa Kienyeji, huku wengine wengi wakiamua ‘kupotezea’ matatizo mengi ya kiafya, na kumwachia ‘mungu’.

Pia lipo tatizo la Madaktari wengi wanaosomeshwa na fedha za walipa kodi kutumia muda wao mwingi kutoa huduma za afya katika hospitali binafsi, kuliko kule walipoajiriwa na serikali na wanapolipwa na fedha za walipa kodi. Serikali haijaonyesha mikakati ya kutatua tatizo hili, bila ya kuathiri motisha ya madaktari wetu kuendelea kuwahudumia wananchi walio wengi.
 
Nipo part I, naomba source ya data zako hasa kwenye statistics.
Kama ni utafiti uliofany wewe mwenyewe, naomba methodology uliyoitumia .... like your sample size, sampling method etc... (sehemu ya afya)
 
Mkuu , siku za nyuma sekta ya afya ilijengwa katika 'four tier system'
1. Clinic na dispensaries (zahanati)
2. Hospitali za Wilaya
3. Hospitali za mikoa
4. Hospitali za rufaa na zile maalum

Kwasababu zisizoeleweka kitaalamu awamu ya nne ikapandisha hadhi hopsitali za mikoa kuwa za rufaa. Hili halikuzingatia maana halisi ya hospitali za rufaa

Jambo hili limekuwa na matokeo haya

1. Kupoteza nguvu za hospitali za mikoa ambazo hazikidhi haja ya kuwa kuwa za rufaa
Hospitali za mikoa zimekosa eneo lake kama ulivyoonyesha 'three tier system'

2. Kudoroa hospitali za mikoa kumepelea ongezeko la 'mzigo'hospitali za rufaa/maalam.

3. Ongezeko la hospitali bila mpangilo limezaa tatizo la 'resource allocation' .
Kwa hali hiyo, huduma zinazotolewa na hospitali za rufaa ni za kiwango cha chini.

Kutokana na hospitali za rufaa kushindwa kumudu shughuli (ufinyu wa bajeti) kinyume na azimio la Abuja, eneo muhimu la 'maendeleo' katika sekta hii limesahaulika

Maendeleo ya sekta ya afya ni katika maeneo 3, kukinga, kuzuia na kuponya

Kukinga (primary health care) ni eneo muhimu linalogusa magonjwa yanayokingwa kwa chanjo au elimu ya msingi (kama Child and maternal health care)

Kuzuia ipo katika eneo la magonjwa yanayozuilika si kwa kinga au matibabu bali elimu ya umma. Hapa ni pamoja na yale ya milipuko, kuhara, malaria n.k.

Kutibu ni kwa maradhi(tofautisha na magonjwa) yanayohitiji tiba kutokana na asili yake

Pamoja na bajeti finyu, hata kama azimio la Abuja lingefuatwa bado tuna tatizo nchini.

Kazi za kitaalamu ima zinafanywa na wataalam kisiasa au zinafanywa na wanasiasa

Maendeleo ya sekta ya afya si ujenzi wa majengo kama wizara ya ujenzi au miundo mbinu bali ni kupunguza , kukinga na kuzuia magonjwa/maradhi ili kuondoa 'strain' katika bajeti ya wizara kwa miaka ijayo.

Hivyo,mkazo unatakiwa uwe katika afya ya msingi ili kuzuia, kukinga na kuponya

Hatuhitaji hospitali za rufaa kila kona bila ufanisi. Tunahitaji hospitali za rufaa chache kikanda ili zipate resource za kutosha, na sehemu kubwa iende katika kuimarisha ngazi za chini. Tunaweza kuwa na Ligula, Muhimbili, Bugando, KCMC, Dodoma na Mbeya tu

Sehemu kubwa ya resource iende ngazi za chini ikilenga kukinga,kuzuia na kuponya.

Nitachangia suala la vyuo vya afya na umuhimu wake
 
Back
Top Bottom