Magufuli 2015-2020: Matarajio ya uchumi na changamoto zake

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,850
9,405
Utangulizi

Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais J.P.Magufuli (CCM) imeanza kuwatumikia wananchi kwa kipindi cha (2015-2020) kwa mujibu wa katiba ya JMT(1977).

Vipaumbele vikuu vya serikali ya awamu ya tano ni pamoja na:

·Kurudisha nidhamu katika mfumo wa fedha za umma
·Kuziba mianya ya ukwepaji kodi na
.Kubana matumizi ya fedha za umma.

Sambamba na haya, serikali pia (kupitia waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango, Dr. Mpango), imewasilisha sura ya bajeti ya mwaka 2016-17 pamoja na mapendekezo ya Mpango wa pili wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano (2016/2017 – 2020/2021).

Tutajadili matarajio ya kiuchumi chini ya Rais Magufuli na Changamoto zake kwa kipindi cha 2015-2020. Tutafanya hivyo kwa muktadha wa dhana ya “Mabadiliko” tarajiwa ya Wananchi wengi, hasa maisha yao KIUCHUMI.

Wananchi wengi (hasa maskini) wanatumaini Uchaguzi wa TANO wa Vyama Vingi (2015) katika dhana ya ''mabadiliko'' utaondoa mfumo unaoshadidia mambo YALE YALE kufanywa kwa namna ILE ILE na yenye matokeo YALE YALE kwa maisha yao kwa miaka zaidi ya Hamsini ya uhuru.

Mjadala wetu umegawanyika katika sehemu kuu SITA:

Sehemu ya Kwanza

Tutajadili Matarajio ya wananchi Kiuchumi tukiyangalia katika maeneo makuu mawili:

(1) Sura ya Bajeti ya Kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano (2016-17) na Mapendekezo ya Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano (2016/17-2020-2021).

(2) Tutajadili matarajio ya wananchi kwa undani juu ya yanayopaswa kuwa ‘Majukumu ya Serikali” katika Uchumi wa Taifa.

Sehemu ya Pili
Tutajadili ngazi kuu za Serikali – (i) Serikali Kuu” na (ii)Serikali za Halmahauri.

Hapa tutaangalia kwa undani mgawanyo wa majukumu wa ngazi hizi mbili za Serikali katika kuleta ufanisi na matokea chanya kisiasa (demokrasia), kiuchumi na kijamii, kwa faida ya wananchi walio wengi.

Sehemu ya Tatu
Tutajadili Mamlaka ya Kodi na Mapato [“Taxation and Revenue powers”] katika ngazi mbili kuu za serikali – Serikali Kuu na Serikali Za Halmashauri.

Tutatazama urali “Fiscal Imbalances” katika ngazi za Halmashauri na jinsi gani changamoto zake zinapaswa kutatuliwa kwa ushirikiano baina ya ngazi mbili kuu hizi za Serikali.

Pia tutaangalia aina mbalimbali za Kodi:

– Kodi zipi zinapaswa kusimamiwa na serikali kuu;

- Kodi zipi zinapaswa kusimamiwa na Serikali ngazi za halmashauri; na

- Kodi zipi zinaweza kusimamiwa kwa kushirikisha ngazi kuu mbili.

Lengo kuu hapa ni kuleta ufanisi wenye matokeo chanya kwa maisha ya wananchi walio wengi - Kijamii, Kiuchumi na Kisiasa(demokrasia)

Sehemu ya Nne
Tutajadili hali ya “Deni la Taifa” na changamoto (zitokanazo) kwa Serikali ya awamu ya Tano katika utekelezaji wa mipango yake mbalimbali ya kibajeti na kimaendeleo.

Sehemu ya Tano

Tutajadili hali ya baadae ya uchumi katika muktadha wa deni la NJE, kwa kufanya tathmini ya mwenendo wa deni la nje.

Pamoja na mengineyo, tutajadili:


· Historia fupi ya deni la nje.

· Matumizi (kisekta) ya deni la nje.

· Athari (impact) ya mikopo ya nje katika maendeleo ya uchumi na jamii.

· Hatari (risk) iliyopo mbeleni ya nchi kuingia katika mgogoro mkubwa kiuchumi na hivyo kutoweza kukopesheka. Katika hili, tutafanya tathmini ya masuala makuu mawili:


- Kwanza ni tathimini ya Mapato ya kodi kwa kuangalia iwapo katika kipindi cha 2016-2021, mapato haya yatatosha kuiwezesha serikali kulipa madeni ya nje bila ya kuathiri majukumu ya serikali ya kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi.

- Pili, ni tathmini ya Mapato ya Fedha za Kigeni kupitia mazao ya kibiashara nje ya nchi kwa kipindi cha 2016-2021, na kuangalia iwapo mapato haya yatatosha kuiwezesha serikali kulipa madeni ya nje bila ya kuathiri uwezo wake wa kuwajibika kwa wananchi.


Sehemu ya Sita

Sehemu ya Siita itakuwa ni hitimisho la mjadala.


Bandiko linalofuata litaanza na sehemu ya kwanza:

(1) Sura ya Bajeti ya Kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano (2016-17) na Mapendekezo ya Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano (2016/17-2020-2021).

(2) Tutajadili matarajio ya wananchi kwa undani juu ya yanayopaswa kuwa ‘Majukumu ya Serikali” katika Uchumi wa Taifa.
 
1. Sehemu ya Kwanza


1.1 Sura ya Bajeti ya Kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano (2016-17).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa karibuni na waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango (Dr. Mpango) matarajio ya makusanyo na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17 ni TZS Trilioni 29.5, asilimia 24 zaidi ya bajeti ya 2015/16 (TZS Trilioni 22.5)


Mapato ya Ndani:

-Mapato ya Kodi TZS Trillioni 15.1

-Mapato yasiyotokana na Kodi pamoja na Mapato ya Halmashauri TZS Trilioni 3.36.


Mikopo ya Ndani:

-TZS Trilioni 5.4


Vyanzo Vya Nje:

-Washirika wa Maendeleo wanatarajiwa kuchangia TZS Trilioni 3.6.

-Mikopo ya Kibiashara TZS Trilioni 2.1.


1.1.1 Uchambuzi wa Sura Ya Bajeti (2016/17) Pamoja Na Matarajio Ya Wananchi:


Bajeti ya 2016/17 ni ya kwanza chini ya Awamu ya TANO ya Rais JP Magufuli.

Vipaumbele vya bajeti vipo katika maeneo makuu manne yafuatayo:


(a) Uchumi wa Viwanda.

(b) Kufungamanisha Maendeleo ya Uchumi na Rasilimali Watu.

(c) Mazingira wezeshi ya uendeshaji biashara na uwekezaji.

(d) Usimamizi wa utekelezaji wa Mipango.


Bajeti ya 2016/17 ina sura ifuatayo:

· Katika bajeti hii, fedha nyingi zaidi zimetengwa kwa ajili ya maendeleo (TZS Trilioni 11.8) ikilinganishwa na kiasi kilichotengwa kwa ajili hiyo katika bajeti ya 2015/16 (TZS Trilioni 5.7). Hii ni sawa na ongezeka la karibia TZS Trilioni 6 (asilimia 40).

·Matumizi ya kawaida yamepungua kwa asilimia 6 kutoka TZS Trilioni 17.72 (2015/16) hadi TZS trillion 16.7(2016/17)


· Utegemezi wa bajeti ya 2016/17 kutoka kwenye vyanzo vya nje (washirika wa maendeleo na mikopo ya kibiashara) ni TZS Trilioni 5.7, ambayo ni sawa na asilimia 19.3 ya Bajeti nzima.

· Mapato ya ndani (Kodi, Halmashauri na vyanzo visivyotokana na kodi) ni TZS Trilioni 18.46, sawa na asilimia 62.5 ya bajeti nzima.

· Mapato ya Kodi katika bajeti ni TZS Trilioni 15.1, ambayo ni sawa na asilimia 51.1 ya bajeti nzima.

· Mikopo ya ndani ni TZS Trilioni 5.4, ambayo ni sawa na asilimia 18.3 ya bajeti nzima.

· Mikopo ya nje na yenye masharti ya kibiashara ni TZS Trilioni 2.1, sawa na asilimia 7.1 ya bajeti nzima.

· Jumla ya fedha za Mkopo katika bajeti hii ni TZS Trilioni 7.5, sawa na asilimia 25.4 ya bajeti nzima.


Wananchi wengi (hasa maskini) wamekuwa na matumaini kwamba Uchaguzi wa TANO wa Vyama Vingi (2015) katika dhana ya ''mabadiliko'' utaondoa mfumo unaoshadidia mambo YALE YALE kufanywa kwa namna ILE ILE na yenye matokeo YALE YALE kwa maisha yao kwa miaka zaidi ya Hamsini ya uhuru.


Wananchi wanatarajia serikali yao itatumia ipasavyo kodi na tozo mbalimbali kutimiza matarajio yao maisha bora,kijamii na kiuchumi. Umaskini miongoni mwa wananchi wengi kwa miaka zaidi ya hamsini ya uhuru umechangiwa sana na ukosefu wa umakini kwa upande wa serikali katika kuendeleza sekta muhimu zifuatazo:


- Sekta ya Afya

- Sekta ya Elimu

- Sekya ya Kilimo


Uzoefu wa nchi mbalimbali duniani unaonyesha kwamba nchi zilizopiga hatua kubwa kimaendeleo zilifanikiwa kufanya hivyo baada ya kuwekeza kwa nguvu kwenye ujenzi wa maeneo muhimu kama vile ‘mtaji watu’ (Human Capital). Human Capital ni kirutubisho muhimu cha ujenzi wa uchumi imara na wenye matokeo katika maisha ya wananchi.


Human Capital inajengwa na nguzo kuu mbili: AFYA na ELIMU.


Kwa miaka zaidi ya hamsini ya uhuru wa nchi yetu, sekta hizi mbili bado hazijapewa uzito unaostahili, suala ambalo linazidi kuchochea hali ya umaskini nchini. Ushahidi kwamba serikali haiwekezi vya kutosha katika sekta hizi muhimu za Elimu na Afya unaonekana wazi kwa kutizama mchango wa Sekta hizi katika pato la taifa (GDP). Kwa mfano, mchango wa sekta ya Elimu katika pato la taifa (GDP) ni chini ya asilimia mbili ya pato la taifa (1.3%), huku sekta ya Afya nayo ikiwa katika hali hiyo hiyo (1.6%) ya pato la taifa. Udogo wa mchango huu ni kiashiria kwamba hakuna shughuli kubwa za maendeleo katika sekta hizi muhimu kutokana na kutotengewa fedha za kutosha katika bajeti zake za “maendeleo”.


KILIMO

Kilimo ni sekta nyingine muhimu katika ujenzi wa uchumi endelevu na wenye kujali maslahi ya wananchi walio wengi. Nchi zilizopiga hatua kimaendeleo duniani zilipata mafanikio kutokana na uwekeaji mkubwa katika sekta ya Kilimo.


Kwa kipindi chte cha uhuru wan chi yetu, Tanzania imeendelea kutambua umuhimu wa sekta hii ‘kinadharia’, kwa mfano kauli mbiu za ‘kilimo ni uti wa mgongo’, ‘kilimo kwanza’ 'siasa ni kilimo'' n.k. Lakini ‘kivitendo’, sekta hii bado haijapewa kipaumbele kinachostahili.


Kwa kadri nchi inavyopiga hatua kimaendeleo, Mchango wa Sekta ya Kilimo katika uchumi unapaswa kupungua baada ya sekta hii kufanikiwa kukuza sekta nyingine za uchumi wa nchi na kupunguza umaskini ndani ya jamii (tutaona kwa undani baadae). Lakini kwa Tanzania, hali haijawa na matokeo hayo kwa miaka yote 55 ya uhuru. Kwa mfano, mchango wa sekta ya Kilimo katika pato la taifa umeshuka kutoka asilimia 60 miaka ya sitini na kufikia takribani asilimia 27 leo hii. Lakini tofauti na inavyopaswa (na pia tofauti na ilivyotokea katika nchi nyingine zilizoendelea), Kushuka kwa mchango wa Kilimo katika uchumi (GDP) hakujaenda sambamba na kukua kwa sekta muhimu ya Viwanda, na pia kuiwezesha sekta hii kukuza ajira nje ya Kilimo. Leo, ajira katika sekta ya viwanda haivuki asilimia 3 (tatu). Kilimo kinaendelea kubeba nguvu kazi kubwa (zaidi ya 70%), hali ambayo haijabadilika sana katika kipindi chote cha miaka zaidi ya 50 ya uhuru.


Kama tutakavyoona baadae, ni vigumu kufanikisha uchumi wa Viwanda bila kwanza kuboresha sekta ya kilimo (hasa productivity).


Kama tulivyosema awali, mchango wa kilimo katika pato la taifa (GDP) umeendelea kushuka lakini kushuka huku hakujaenda sambamba na kuboreshwa kwa hali za wakulima) kimapato na kiuchumi kwa ujumla. Tangia uhuru (1961), sehemu ya nguvu kazi imeendelea kubakia katika kilimo chenye kipato duni, na kinachochochea umaskini.

Kama tutakavyoona mbeleni, kulazimisha mkakati wa uchumi wa viwanda bila ya kuwekeza sekta ya Kilimo ni kupoteza muda na rasilimali za walipa kodi.


Katika bandiko linalofuata, tutajadili:

Mafanikio ya Uchumi mpana wa “Nchi” na hali za “Wananchi” na uhusiano wake na sekta ya kilimo ambayo ndio mkombozi wa kweli wa wananchi.
 
1.2 Mafanikio ya Uchumi mpana wa “Nchi” na hali za “Wananchi”


Mafanikio ya uchumi mpana wa nchi yalianza kujitokeza kuanzia mwaka 2000 baada ya kipindi kirefu cha kudorora kwa uchumi wa ngazi hiyo (baadae tutajadili kwa undani dhana ya uchumi mpana wa nchi).


Kwa miaka 15 sasa (2000-2015), uchumi wa Tanzania umekuwa kwa kasi kubwa tofauti na kipindi karibia chote cha kabla ya mwaka 2000. Katika kipindi cha (2000-2015), uchumi wa taifa umekuwa kwa wastani wa karibia asilimia 7 kwa mwaka. Kwa kiwango hiki, hali ya umaskini haikupaswa kuendelea kuwa kiasi kikubwa.


Miaka 15 iliyopita wakati wa uanzishwaji wa ‘Mpango wa Maendeleo ya Milenia’ - Millenium Development Goals (MDGs), Wataalamu wa uchumi na maendeleo katika jumuiya ya kimataifa walieleza kwamba iwapo nchi maskini kama Tanzania itafanikiwa kukuza uchumi wake kwa wastani wa asilimia 7 au zaidi kwa mwaka kwa miaka kumi na tano (mwaka 2015 ulikuwa ni kikomo cha MDGs), nchi husika itafanikiwa kupunguza umaskini kwa asilimia isiyopungua hamsini (50).


Leo ni miaka kumi na tano tangia tathmini hiyo ifanyike,na kwa kipindi chote hiki, kasi ya kukua kwa uchumi wa Tanzania (wastani) imekaribia asilimia 7 kwa mwaka - kwa miaka 15 mfululizo.


Pamoja na mafanikio haya katika uchumi mpana, uchumi wa wananchi walio wengi umeendelea kuwa mgumu.

Tofauti na tathimini kwamba wastani wa kasi ya asilimia saba kwa miaka 15 mfululizo itapelekea umaskini kupungua kwa asilimia isiyopungua 50, katika kipindi husika (2000-2015), kiwango cha umaskini nchini hakijapungua kwa kiwango cha kuridhisha (haijavuka asilimia kumi).


Pamoja na haya yote,limekuwa ni jambo la kawaida kwa wanasiasa, hasa wa chama kilichopo madarakani – Chama Cha Mapindizu kuelezea wananchi juuu ya mafanikio makubwa ya serikali katika kukuza Uchumi wan chi kutokana na kasi ya kukua uchumi– wastani wa asilimia 7 (kwa mwaka, kwa miaka 15 mfululizo. Pia ni jambo la kawaida kwa mtazamo wa aina hii kujitokeza katika bajeti za kila mwaka pamoja na mipango ya maendeleo ya taifa.


Je ni kwanini hali imekuwa hivi?


Hatutakiwi kuishangaa kasi ya kubwa ya kukua kwa uchumi bila athari chanya kwa maisha ya wengi (hasa wakulima). Kama tulivyojadili, tutaweza kutokomeza umaskini iwapo tu, tutaamua kuwekeza vya kutosha kuinua ‘Productivity’ katika sekta ya Kilimo ambayo ndio uti wa mgongo wa taifa letu.


Katika miaka 15 ya mafanikio ya kukua kwa uchumi mpana wa nchi kwa wastani wa asilimia 7, kasi ya kukua kwa Sekta ya Kilimo haijavuka wastani wa asilimia nne. Kwa mfano kwa mujibu wa ripoti ya idara ya takwimu ya taifa (NBS, 2016), kwa kipindi cha Octoka 2015 hadi Disemba 2015, sekta ya kilimo ilikuwa kwa asilimia 2.6 tu.


Tunaposema Kilimo ni uti wa mgongo ina maana kuu tatu:


Kwanza, kwa karibia katika kipindi chote cha uhuru, Sekta ya Kilimo imeongoza kulipatia taifa fedha za kigeni. Pamoja na mengineyo, Mapato haya yamewezesha taifa kumudu kuagiza kutoka nje, bidhaa mbalimbali muhimu zisizozalishwa nchini, lakini pia yamesaidia serikali kuendelea kuwa na uwezo wa kulipa deni la taifa (deni la nje) na kufanya nchi kuendelea kukopesheka.Wa kushukuriwa ni Mkulima.


Pili, sekta ya Kilimo imekuwa ni chanzo kikubwa cha ajira kwa watanzania walio wengi (karibia 70% ya nguvu kazi yote nchini). Kwa maana nyingine, watanzania wengi wanategemea kilimo kumudu maisha yao (kwa maana ya kipato kukidhi mahitaji yao mbalimbali kama vile kama vile afya,elimu n.k.)


Tatu, sekta ya kilimo ni muhimu kwa kulipatia taifa usalama na uhakika wa upatikanaji wa chakula kama vile mahindi, mchele, maharage, mafuta ya kula (cooking oil), SUKARI nk.


Lakini pamoja na umuhimu huu, sekta ya kilimo imeendelea kudodora kutokana na kutopangiwa fedha za kutosha kibajeti, kutowezeshewa mazingira ya uwekezaji nk. Kinachosikitisha zaidi ni kwamba pamoja na ukweli kuwa sehemu kubwa ya walipa kodi wa nchi yetu ni Wakulima, kodi ambazo ndio zinazotumiwa na Serikali Kila Mwezi kulpa madeni ya ‘nje’, wakulima hawa hawapati lolote la maana ‘in return’, kwani takwimu za Benki Kuu zinaonyesha wazi kwamba kiasi cha mikopo ya nje kinachopelekwa kwenye Sekta ya Kilimo hakivuki asilimia nne ya jumla ya mikopo yote ya nje inayoingia nchini.


Kwa mujibu wa Ripoti ya Idara ya Takwimu ya Taifa (NBS), Sekta zinazofanya vizuri ni pamoja na Mawasiliano (ambayo kwa miezi mitatu ya mwisho ya mwaka 2015, ilikuwa kwa asilimia 23); Public Administration and Defense ambayo kwa kipindi kama hicho ilikuwa kwa asilimia 20; Sekta ya huduma za Kifedha & Bima asilimia 14, na Sekta ya Madini asilimia 11.


Pamoja na umuhimu wa sekta hizi kiuchumi kwa maana mbalimbali, mchango wa sekta hizi katika kuboresha maisha ya wananchi walio wengi kwa njia kama vile ajira nk, bado haujawa wa kuridhisha.


Katika bandiko linalofuata tutajadili kwanini uchumi wa viwanda hauwezekani bila ya kwanza kuboresha kilimo.
 
1.3 UCHUMI WA VIWANDA HAUWEZEKANI BILA KWANZA KUBORESHA SEKTA YA KILIMO


Iwapo tuna nia ya dhati ya kujenga uchumi wa Viwanda katika taifa letu ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya Watu kama inavyoainishwa ndani ya Mpango wa Pili wa Maendeleo ya taifa, hatuna budi kuipa Sekta ya Kilimo umuhimu wa kipekee.


Hapo juu tumejadili kidogo juu ya umuhimu wa sekta ya kilimo katika uchumi wa taifa.

Katika sehemu inayofuata, tutajadili mchango huo kwa kina.


Sekta ya Kilimo ina mchango mkubwa katika mchakato wa maendeleo kwa kupitia sura kuu nne kama ifuatavyo:

· Product Contribution (Mchango wa uzalishaji)

· Factor Contribution (Kigezo cha michango mingine)

· Market Contribution ( Mchango katika soko)

· Foreign Exchange Contribution (Mchango wa fedha za kigeni)


1.3.1 Product Contribution (Mchango wa Kilimo kama Bidhaa)


Maana yake hapa ni kwamba - Kilimo lazima kiwe na uwezo wa kuzalisha chakula (aina zote za vyakula), over anf above kiasi kinachohitajika kukidhi mahitaji ya wakulima (‘subsistence needs’) ili kuwezesha nguvu kazi zilizopo kwenye sekta nyinginezo nje ya sekta ya Kilimo, nazo zipate uhakika wa chakula. Nguvu kazi ya kilimo haipaswi kutumia muda wake mwingi kujilimia kwa ajili ya mahitaji tu ya dharura ya kifamilia ‘immediate need of food in the household’ (subsistence farming).


Vinginevyo bila ya uchumi kuzalisha chakula kwa wingi kukidhi mahitaji ya wananchi ‘beyond subsistence level’ and at affordable price (purchasing power), sehemu kubwa ya nguvu kazi ya taifa haitakuwa na motisha ya kutumukia (kutafuta ajira) katika sekta nyinginezo, na badala yake nguvu kazi hii italazimika kujishughulisha na ‘subsistence farming’ ili kukidhi mahitaji ya chakula kwa gharama ndogo. Hii ni moja ya sabab za msingi juu ya kwanini kwa kioindi chote cha uhuru, sehemu kubwa ya nguvu kazi bado imeendelea kubakia katika kilimo. They have ni choice kwani ‘the money economy’ sio rafik kwa wakulima walio wengi (peasants). The only way to survive imeendelea, na itaendelea kuwa ni kupitia ‘Subsistence Farming’.


Msisitizo:

Iwapo tuna nia ya kuendeleza sekta nyingine za uchumi kama viwanda, sekta ambayo ili nayo iamke, itahitaji kuvutia nguvu kazi kubwa, nguvu kazi ambayo kwa sasa motisha yake kubwa bado ipo kwenye ‘subsistence farming’, hatuna mbadala mwingine zaidi ya kwanza kuinua ‘productvity’ ya Kilimo.


Hatuwezi kufanikisha mahitaji ya chakula kwa nguvu kazi tutakayohitaji Viwandani kwa kutegemea kuagiza chakula kutoka nje kulisha nguvu kazi hii. Chakula lazima kizalishwe ndani ya uchumi wa nchi, chakula cha kutosha, over and beyond subsistence needs. Njia pekee ya kuzalisha chakula ‘beyond substistence level’ na kwa bei nafuu ni kupitia ongezeko la ufanisi wa uzalishaji wa mazao ya kilimo (agricultural productivity growth).


Ufanisi katika kilimo ukiongezeka, taifa litapata chakula kingi na cha uhakika na kwa bei nafuu.

Hali hii ikitokea, nguvu kazi iliyopo katika kilimo (subsitence farmers) haitalazimika tena kuendelea kukaa kwenye sekta ya kilimo for ‘subsistence production’. Badala yake,itahamia katika sekta ya viwanda kwa hiyari yake na kwa wingi na hivyo kutengeneza ‘surplus labour’. Katika hatua za awali za maendeleo ya Viwanda, uchumi unahitaji uwepo wa ‘Surplus Labour’ kwa sababu katika hatua za awali, wamiliki au wawekezaji wa Viwanda wanahitaji kuajiri wafanyakazi kwa mishahara ‘affordable’ kwao ili kuhakikisha kwamba kuna Return on Investment. Hii haina maana kwamba nguvu kazi Viwandani haitakiwi kuwa na maslahi bora. Maslahi bora ni suala ‘incremental’, linakuja over time. If we are to succeed and weather the storm katika hatua za awali za uchumi wa viwanda, we cant afford kufanya maslahi ya nguvu kazi Viwandani kuwa ‘radical’.


Upatikanaji wa chakula over and above ‘subsistence needs’ unajulikana kama “Marketable Surplus”. Katika hatua za awali za ujenzi wa uchumi wa Viwanda kama Tanzania, tunahitaji kuwa na ‘Marketable Surplus’. Lakini ili kuipata hii ‘surplus’, tutalazimika kuongeza ufanisi katika kilimo (improvement in agricultural productivity).


Angalizo

Marketable Surplus inatakiwa ipatikane ‘naturally’ au ‘voluntarily’. Isipopatikana kwa njia moja wapo kati ya hizi mbili, huku nguvu kazi ikiwa tayari kutumikia viwanda iwapo tu chakula kinapatikana na kwa bei nafuu, Taifa litaingia katika mgogoro mkubwa sana wa Kiuchumi.


Hii ni kwa sababu, serikali italazimika kuingilia hizi ‘market failure’ ili kuhakikisha nguvu kazi nje ya Kilimo inapata chakula cha kutosha na kwa bei nafuu. Hali hii inaweza kuilazimisha Serikali kutafuta ‘Marketable Surplus’ kwa nguvu, na ikibidi kwa ‘mtutu wa bunduki kama’ ilivyotokea nchini Japan mwaka 1867 wakati wa “Meiji Restoration” na nchini Urusi miaka ya 1920s. Zoezi la “Operesheni ya Vijiji Vya Ujamaa” nchini Tanzania katika miaka ya 1970s pia ilitokana na changamoto inayofanana nah ii kwani Serikali ilihitaji ‘marketable surplus’ kwa ajili ya kulisha nguvu kazi ya utumishi wa umma, utumushi wa chama (TANU/CCM), lakini pia taifa lilihitaji fedha za kigeni kupitia uzalishaji na uuzwaji wa Mazao ya Kilimo nje ya nchi.


Msisitizo:

Kama tulivyojadili, katika muktadha wa ujenzi wa uchumi wa Viwanda, kutakuwa na ongezeko la mahitaji ya chakula kulisha kwa wingi nguvu kazi nje ya Kilimo. Ongezeko hili lisipoenda sambamba na ongezeko la “Marketable Surplus”, athari yake ni bei ya vyakula kupanda (food inflation).


Tukumbuke, kwa Tanzania chakula ni takribani asilimia 50 ya matumizi ya wananchi wengi.

Katika hali hii, ongezeko la bei ya chakula hata kama ni kwa asilimia ndogo sana lina athari kubwa kwa nguvu kazi itakayoamua kuachana na ‘subsistence farming’ ili kwenda kutumikia uchumi wa viwanda. Bila ya uangalifu, tutakuta tunaua sekta ya kilimo kwa gharama ya kukuza sekta ya viwanda inayotegemea kilimo kutoa matokeo chanya.


Mfumuko wa bei ya chakula ‘will turn the terms of trade against the industrial sector.’

Hii ni kwa sababu, bei ya vyakula ikipanda itaathiri gharama za maisha kwa nguvu kazi iliyohamia kwenye viwanda kutoka kwenye ‘subsistence farming.’ Hili litapelekea sehemu kubwa ya nguvu kazi ya viwandani kurudi kwenye ‘subsistence farming’ ili kujipatia chakula kwa gharama nafuu. Kwa upande wa wenye viwanda - ili waweze kuifanya nguvu kazi hii iendelee kubakia kwenye Viwanda, watajikuta wakishinikizwa kuongeza mishahara ya wafanyakazi viwandani ili waweze kukabiliana na mfumuko wa bei ya chakula ‘food inflation’. Hii italazimisha wawekezaji Viwandani kuanza kufikiria mara mbilimbili kuendelea na biashara kwa sababu ‘cheap labour’ wont be ‘cheap’ anymore.


In the long run, nyongeza ya mishahara ni jambo jema na sahihi, lakini in the short run - katika hatua ya awali ujenzi wa uchumi wa viwanda, ni hatua kinzani (counter productive). Sababu ni kuwa ongezeko la mishahara katika hatua ya awali litaathiri sana ‘profits’ na ‘capital accumulation’ zinazohitajika kuendeleza viwanda in the early stage of industrialization.


Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais JP Magufuli inatakiwa kutambua kwamba bila kuwekeza katika kilimo kwa ajili ya kupata ‘Marketable Surplus’, taifa litakosa ‘marketable surplus na hivyo kuathiri juhudi zake za kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati kupitia Viwanda, ifikapo mwaka 2025.


Tuendelee kuangalia Michango mingine ya Kilimo Katika mchakato wa maendeleo iliyosalia (Factor contribution, market contribution, & foreign exchange contribution):


1.3.2 Factor Contribution

Mchango wa aina hii unakuja kwa sura kuu mbili - nguvu kazi (labour contribution) na mitaji (capital contribution) vitu ambavyo ni muhimu katika ujenzi wa uchumi wa viwanda. Hapo juu tulijadili hili.


1.3.3 Market Contribution

Moja ya sababu kubwa kwa taifa kuendeleza uchumi wa Viwanda ni pamoja na kuhakikisha kwamba Viwanda vya ndani vinazalisha bidhaa kukidhi mahitaji ya soko la ndani. Kwa maana nyingine, mafanikio ya Viwanda yatategemea sana uwezo wa wananchi (purchasing power) wa kununua bidhaa mbalimbali zitakazo zalishwa na viwanda vya ndani.


Ni muhimu serikali ikatambua kwamba, Katika hatua ya awali ya maendeleo ya Viwanda, ni lazima Sekta ya Kilimo (wakulima) iwe ndio soko kubwa la bidhaa kutoka viwandani (wateja wa bidhaa husika), hasa ikiwa ni viwanda vya ‘mass goods’ kama vile vilivyojengwa na serikali ya awamu ya kwanza. Vinginevyo bidhaa za viwandani hazitakuwa na soko la uhakika, suala ambalo litakuwa ni kikwazo kwa mikakati ya viwanda kupiga hatua. Awali tuligusia kidogo juu ya umuhimu wa kuboresha vipato vya wakulima. Ni wajibu wa serikali kuhakikisha kwamba ‘disposable income’ ya wakulima inaongezeka ili kusaidia viwanda kukua. Kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia (1979):


‘A stagnating rual economy with low purchasing power holds back industrial growth in many developing countries.”


1.3.4 Foreign Exchange Contribution

Katika hatua ya awali ujenzi wa uchumi wa viwanda, taifa linahitaji fedha za kigeni kwa kiwango cha kutosha. Katika hatua za mwanzo za maendeleo, Kilimo ni chanzo kikubwa cha fedha za kigeni kupitia ‘Primary commodity exports.’ Katika hatua za awali, mauzo ya bidhaa hizi yanasaidia serikali kufanikisha mambo makuu mawili:

-Kwanza yanawezesha nchi kupata fedha za kigeni ili kununua mahitaji muhimu yasiyozalishwa au kupatikana nchini.

-Pili, maendeleo ya Viwanda yanahitaji mikopo ya nje ya nchi (mingi ikiwa inapatikana kwa sarafu ya dola ya Kimarekani). Njia pekee na ya uhakika ya serikali kulipa mikopo hii ili nchi iendelee kukopesheka ni kwa kupitia mauzo ya bidhaa za Kilimo katika soko la kimataifa/primary commodity market.


Katika bandiko linalofuata, tutajadili:

Matarajio ya Wananchi Katika Bajeti Ya Kwanza Ya Awamu ya Tano (2016-17)
 
1.4 Matarajio ya Wananchi Katika Bajeti Ya Kwanza Ya Awamu ya Tano (2016-17):


Kama tulivyokwisha jadili, Wananchi wengi (hasa maskini) wanatumaini Uchaguzi wa TANO wa Vyama Vingi (2015) katika dhana ya ''mabadiliko'' utaondoa mfumo unaoshadidia mambo YALE YALE kufanywa kwa namna ILE ILE na yenye matokeo YALE YALE kwa maisha yao kwa miaka zaidi ya Hamsini ya uhuru.


Katika moja ya Vipaumbele vinne vya Mpango wa Maendeleo (2016/17-2020/21), lipo eneo la “Kufungamanisha Maendeleo ya Uchumi na Maendeleo ya Watu”. Katika hili, yanatajwa maeneo makuu muhimu ya ujenzi wa mtaji watu (Human Capital) ambayo ni Elimu na Afya (pamoja na lishe).


Mbali ya Mtaji Watu (Elimu, Afya na Lishe), mpango wa maendeleo unataja (japo kwa juu juu) umuhimu wa kukuza uzalishaji na tija katika Sekta ya Kilimo.


Kwa maana hii, Serikali inatambua kwamba Mtaji Watu (Afya na Elimu) na Kilimo vina umuhimu wake katika kufanikisha ujenzi wa uchumi wa Viwanda utakaochochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu.


Kwa kuangalia Mpango wa pili wa Maendeleo uliowasilisha na serikali hivi karibuni, kuna dalili njema kwamba Serikali inaelewa umuhimu wa kuweka kipaumbele katika sekta hizi tatu muhimu za Afya, Elimu na Kilimo.


Tatizo linalokabili taifa ni uzito wa utekelezaji wa maazimio mbalimbali.

Kwa mfano, yamekuwepo na maazimio mengi ya kikanda na kimataifa yanayolenga kuboresha maeneo ya Mtaji Watu (Human Capital) na Sekta ya Kilimo. Serikali ya CCM imehudhuria mikutano mbalimbali inayohusisha maazimio haya na kutia saini makubaliano husika. Serikali ya Rais JP Magufuli kama ina ya dhati ya kuleta “mabadiliko ya kweli” , haina budi katika Bajeti ya 2016/17 kutekeleza hilo kwa vitendo.


Serikali ya Rais JP Magufuli ina fursa ya kuonyesha wananchi kupitia bajeti yake ya kwanza ya ‘mabadiliko’, maazimio yafuatayo yatatekelezwa kwa ajili ya maslahi ya wananchi:


· Azimio la Kwanza ni Azimio la Maputo (2003) juu ya Kilimo na Usalama Wa Chakula (Agriculture and Food Security).


Azimio hili lilikutanisha Viongozi kutoka nchi za Umoja wa Afrika (AU) wakiambatana na wataalam na washauri wao wa uchumi na kilimo, ambapo kwa pamoja walitia saini ya makubaliano kwamba ili kuleta ufanisi katika sekta ya kilimo na sekta hii ilete mchango wa maana katika uchumi wa nchi na wananchi (kama inavyojadiliwa katika mpango wa pili wa maendeleo 2016-2020), viongozi wote walitia saini ya makubaliano kukubali kutenga kiasi kisichopungua asilimia 10 (kumi) ya Bajeti ya kila mwaka kwa ajili ya kuendeleza sekta ya Kilimo. Serikali ya Tanzania ilitia saini makubaliano haya. Kwa sababu zisizoeleweka, Serikali ya (CCM) haijawahi kutekeleza azimio hili.


Matokeo yake ndio kama tulivyojadili awali kuhusiana na hali duni katika Sekta ya Kilimo nchini.

Iwapo Serikali ya wamu ya TANO ina nia ya dhati ya kuonyesha wananchi kwamba bajeti yake ya kwanza ni bajeti ya ‘Mabadiliko”, serikali inapaswa kutenga kiasi kisichopungua TZS Trilioni 2.9 (sawa na asilimia 10 ya Bajeti nzima ya TZS Trilioni 29.5) kwa ajil ya Wizara/Sekta ya Kilimo. Kwa kufanya hivyo, Serikali itakuwa imekidhi matarajio ya wananchi walio wengi kwamba hatimaye Serikali itahakikisha kwamba inaboresha maisha yao kwa vitendo.


Ni Matarajio kwamba Serikali haitafanya hivyo kwa mwaka mmoja tu wa bajeti (2016/17) bali itaendelea kutenga kiwango hiki hiki cha asilimia 10 ya jumla ya bajeti yote katika kipindi chote cha utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa.


· Azimio la Pili ni Azimio la Abuja (2001) juu ya Kuboresha Afya za Wananchi.


Azimio hili lilikutanisha Viongozi kutoka nchi za Umoja wa Afrika (AU) wakiambatana na wataalam na washauri wao juu ya masuala ya Afya, ambapo kwa pamoja walitia saini ya makubaliano kwamba ili kuboresha Afya za wananchi na kumarisha Mtaji Watu (Human Capital), kila Serikali itenge kiasi kisichopungua asilimia 15 (kumi na tano) ya Bajeti yake ya Afya kila mwaka. Serikali ya Tanzania ilishiriki kutia saini makubaliano husika.


Lakini kutokana na sababu zisizoeleweka, Serikali haijawahi kutekeleza azimio hili.

Matokeo yake ni sekta ya afya kuendelea kuwa duni, na kuathiri nguvu kazi na wananchi kwa ujumla.


Kutelekezwa kwa sekta ya afya kibajeti na serikali pia kunaoonekana kwa kuangalia mchango wa sekta ya Afya katika pato la Taifa (GDP) ambao ni chini ya asilimia mbili (1.5% ya GDP) katika kipindi chote cha Shangwe juu ya kasi ya kukua kwa uchumi wa taifa (GDP), wastani wa asilimia 7 kwa miaka kumi na tano mfululizo (2000-2015).


Kwavile serikali kupitia mpango wa maendeleo imedhamiria kukuza Raslimali Watu, ni vyema ikawaonyesha wananchi kwamba bajeti hii ni bajeti ya MABADILIKO, na hivyo kukidhi matarajio ya wananchi. Katika kutimiza matarajio haya, kwa mwaka huu wa fedha, Serikali inapaswa kutenga Kiasi kisichopungua TZS Trilioni 4.4 (ikiwa ni sawa na asilimia 15) ya Bajeti nzima ya TZS Trilioni 29.5 kwa ajili ya Wizara/Sekta ya Afya.


Ni Matarajio kwamba Serikali haitafanya hivyo kwa mwaka mmoja tu wa bajeti (2016/17) bali itaendelea kutenga kiwango hiki hiki cha asilimia 15 ya jumla ya bajeti yote katika kipindi chote cha utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa.


· Azimio la Tatu ni Azimio la Dakar (2000) juu ya “Elimu Bora Kwa Wote.


Azimio la Dakar juu ya ‘Elimu’ lilikutanisha viongozi kutoka nchi zaidi ya ‘160’ duniani ambao pia waliambatana na watalaam na washauri wao juu ya masuala ya Elimu ambapo kwa pamoja, walitia saini makubaliano kwamba ili kuboresha Elimu na kuimarisha Rasilimali Watu kupitia Sekta hii, kila Serikali inatarajiwa kutenga kiasi kisichopungua asilimia 20 (ishirini) ya Bajeti yake kila mwaka kwa ajili ya Sekta ya Elimu. Serikali ya Tanzania ilishiriki na kutia saini makubaliano haya lakini kama ilivyo kwa maazimio mengine (rejea huko juu), Serikali ya CCM haijawahi kutekeleza azimio hili.


Kutelekezwa kwa sekta ya Elimu kibajeti kunaonekana wazi kwa kuangalia jinsi gani Sekta ya elimu ilivyokuwa katika hali mbaya na ya kukatisha tamaa. Hli hii ndio inayopelekea mchango wa sekta ya elimu katika pato la Taifa (GDP) kuwa ndogo san. Mchango wake ni wa chini ya asilimia mbili (1.6% ya GDP) katika kipindi chote cha Shangwe juu ya kasi ya kukua kwa uchumi wa taifa (GDP) kwa wastani wa asilimia 7 kwa miaka kumi na tano mfululizo (2000-2015).


Lakini kwavile serikali kupitia mpango wa maendeleo imedhamiria kukuza Raslimali Watu, ni vyema ikawaonyesha wananchi kwamba bajeti hii ni bajeti ya MABADILIKO kwa kutenga Kiasi kisichopungua TZS Trilioni 5.9 (ikiwa ni sawa na asilimia 20) ya Bajeti nzima ya TZS 29.5 kwa ajili ya Wizara/Sekta ya Afya. Kwa kufanya hivyo, Serikali itawezesha wananchi kupata mabadiliko wanayotafuta katika maisha yao kwa miaka zaidi ya 50 ya uhuru.


Ni Matarajio kwamba Serikali haitafanya hivyo kwa mwaka mmoja tu wa bajeti (2016/17) bali itaendelea kutenga kiwango hiki hiki cha asilimia 20 ya jumla ya bajeti yote katika kipindi chote cha utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa.


1.4.1 Umuhimu wa kuweka malengo ya kibajeti:


Mabadiliko ya kweli ni lazima yaendane na matumizi ya kodi za wananchi katika masuala yanayogusa moja kwa moja maisha ya wananchi walio wengi. Kuna umuhimu wa serikali kujiwekea malengo ya kibajeti, na njia nzuri na rahisi itakayosaidia kupima ufanisi na utekelezaji wa serikali wa kuboresha maisha ya wananchi ni ile itakayohakikisha kwamba malengo ya kibajeti ya kila mwaka katika sekta muhimu yanawekewa ‘benchmark’ kama tulivyojadili hapo juu. Kuna sababu ya kufanya hivyo:


Nchi zote zilizofanikiwa kuboresha maisha ya wananchi wake kupitia sekta muhimu kama Afya na Elimu zilifanikiwa baada ya kwa kujiwekea ‘benchmarks’. Na hata katika Malengo ya Milenia ya 2000-2015 – The Millenium Development Goals (MDGs), jumuiya ya kimataifa kwa kushirikiana na nchi maskini walianza kwa kuweka‘benchmarks’, hali iliyosaidia kubaini mafanikio, changamoto, na mapungufu ya malengo husika.


Hivyo tukiwa kama wananchi, tunatarajia Serikali ya awamu ya tano, kupitia bajeti yake ya kwanza (2016/17), itakuja na bajeti ya “Mabadiliko” ambayo pamoja na mengineyo, itaanza kutekeleza maazimio iliyoyaridhia huko nyuma kwa maslahi ya wananchi walio wengi (Maskini), maazimio kama vile: Maputo (Kilimo), Abuja (Afya) na Dakar (Elimu) kwa kutenga bajeti kwa sekta hizi kufuatana na benchmarks tulizojadili.

Katika bandiko linalofuata tutajadili:

Mapendekezo ya Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa wa Miaka Mitano (2016/17-2020/2021)
 
1.5 Mapendekezo ya Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa wa Miaka Mitano (2016/17-2020/2021):


1.5.1 Masuala na muhimu yaliyowasilishwa:


Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa (2016/17-2020/21) una dhima ya kujenga viwanda kwa nia ya kuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu. Maeneo ya Kipaumbele ya Mpango huu ni manne kama ifuatavyo:


· Kukuza uchumi na kujenga msingi wa uchumi wa viwanda.

· Kufungamanisha maendeleo ya uchumi na maendeleo ya watu.

· Kujenga mazingira wezeshi kwa uendeshaji Biashara na Uwekezaji.

· Kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa Mpango.


Msukumo mkubwa katika mpango huu wa maendeleo ni kuhakikisha kwamba rasilimali na fursa za nchi zinatumika vizuri katika kujenga msingi wa uchumi wa viwanda pamoja na uwezo wa kupunguza umaskini nchini.


1.5.2 Ugharamiaji wa Mpango:


Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango bungeni hivi karibuni, mpango wa maendeleo wa taifa (2016/17-2020/21) utagharimu TZS Trilioni 107, sawa na TZS Trilioni 21.4 kwa mwaka. Katika fedha hizi, Serikali inatarajia kuchangia TZS Trilioni 29.5, sawa na TZS Trilioni 11.8 kwa mwaka.


Mbali ya kutumia vyanzo vya fedha kutoka ndani ya nchi, serikali pia inatarajia kupata fedha kutoka nje kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huu. Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha:


“Uzoefu nchi nyingine unaonyesha kwamba mkakati wa Viwanda aghalabu huvutia misaada kutoka nje”.


Maana ya “Misaada” hapa ni utegemezi wa Mikopo (Deni la nje) pamoja na mitaji kutoka nje (tutajadili kwa undani deni la nje katika sehemu ya nne na ya tano). Ili kufanikisha malengo husika, Serikali inatarajia yafuatayo:


· Kasi ya kukua kwa uchumi itaongezeka kutoka asilimia 7 mwaka 2015 na kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2020.

· Uwekezaji kutoka nje (Foreign Direct Investment) utaongezeka kutoka Dola Bilioni 2.1 mwaka 2015 na kufikia Dola Bilioni 5 ifikapo mwaka 2020.

· Mapato ya Kodi (Tax Revenues) yataongezeka kutoka asilimia 12 ya pato la taifa (GDP) kwa mwaka 2015 na kufikia asilimia 17 ya pato la taifa ifikapo mwaka 2020.

· Uzalishaji wa umeme utaongezeka kutoka Megawati za Sasa (1500) na kufikia Megawati 4915 ifikapo mwaka 2020.

· Usambazaji wa umeme utaongezeka kutoka asilimia 36 ya wananchi kwa mwaka 2015 na kufikia asilimia 60 ifikapo mwaka 2020.


Pia Serikali inatarajia Mpango wa pili wa maendeleo wa taifa utaleta matokeo yafuatayo:


· Uchumi wa Viwanda Utazalisha bidhaa nyingi za kutumiwa ndani ya nchi na kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje.

· Maendeleo ya Viwanda yatasaidia uzalishaji wa ajira nyingi na zenye faida.

· Maendeleo ya Viwanda yatachochea maendeleo ya tekinolojia.

· Nchi itafikia kiwango cha “Uchumi wa Kati” ifikapo mwaka 2025.


1.5.3 Uchambuzi Wa Mpango wa Pili Wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21) na Matarajio Ya Wananchi


Uchambuzi wetu utajikita zaidi katika Uchumi wa Viwanda kwa sababu dhima ya Mpango huu ni ujenzi wa uchumi wa Viwanda. Kwa mujibu wa Mpango husika (Ikurasa wa 10), Waziri wa Fedha, Uchumi na Mpango, Dr. Mpango anajadili kwamba:


[“Mheshimiwa Spika, Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, 2016/17 2020/21, una dhima ya Kujenga Uchumi wa Viwanda ili kuchochea Mageuzi ya Kiuchumi na Maendeleo ya Watu – Nurturing Industrialisation for Economic Transformation and Human Development”. Msukumo wa Mpango huu ni kuhakikisha kuwa rasilimali na fursa za nchi zinatumika vizuri katika kujenga msingi wa uchumi wa viwanda na uwezo wa kupunguza umaskini”].


1.5.3.1 Historia Fupi ya Uchumi wa Viwanda Tanzania


Mkakati wa Maendeleo ya Viwanda sio jambo geni masikioni mwa watanzania. Ni vema tuangalie historia na uzoefu wetu kama taifa unatuonyesha nini katika hili.


Miaka 41 iliyopita (1975), serikali ya Kwanza Ya TANU chini ya Rais JK Nyerere ilikuja na mkakati wa Viwanda uliojulikana kama - “Basic Industry Strategy” (BIS) ikiwa ni BLUE PRINT ya Miaka 20 ya Maendeleo ya Viwanda (1975-1995). Kama ilivyo kwa dhima ya Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa (2016/7-2020/21), Basic Industry Strategy (1975) ililenga kujenga na kukuza uchumi wa Viwanda, kuchochea mageuzi ya kiuchumi, kuanzisha vyanzo vingine mbalimbali vya sekta ya uchumi nje ya Kilimo, kuzalisha ajira, kuleta maendeleo ya watu n.k.


Muhimu ni kwamba, kama ilivyo kwa Mpango wa Pili wa Maendeleo (2015/16-2020/21), Mkakati wa awali wa Ujenzi wa Viwanda (1975) ulilenga kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje (import substitution) kwa kulenga bidhaa zote (Consumer & Capital goods) kama vile Chuma, Kemikali nk. Kama inavyoelekezwa ndani ya Mpango wa sasa wa maendeleo, Mkakati wa Viwanda (1975) pia ulilenga maeneo ya kijiografia ambayo yalikuwa na “Comparatve Advantage” kwa maana ya uwepo/uwezekano wa kuwepo kwa Malighafi, Nishati, Miundo Mbinu nk.


Lakini kabla ya uanzishwaji wa Viwanda husika, Serikali ilihakikisha kwamba inaanza kwa kuwekeza zaidi katika uwezeshaji wa mazingira ya kukuza uchumi wa Viwanda, na ili kufanikisha lengo hilo, Serikali ilipitisha sheria zilizolenga kuchochea uwekezaji kutoka nje ya nchi (FDI), sheria zilizounda taasisi mbali mbali kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa uchumi wa viwanda n.k.


Kwa mfano serikali ilianzisha yafuatayo kwa mujibu wa Sheria:


*Shirika na Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO). Tangia awali kabisa, Serikali ilitambua mchango na umuhimu wa Sekta ya Viwanda Vidogo na vya Kati (SMEs) ni muhimu katika Uchumi wa Viwanda. Na tangia kipindi kile, ukiacha SIDO, Serikali haijawahi tena kuja na mkakati endelevu wa kusaidia Viwanda vidogo vidogo kwa mwamko ule wa awali.


*Taasisi ya utafiti kusaidia uchumi wa Viwanda – Tanzania Industrial Research and Development Organization (TIRDO). Umuhimu wa taasisi hii unajieleza wenyewe.


*Tanzania Engineering and Manufacturing Design Organization (TEMDO). Umuhimu wa taasisi hii unajieleza wenyewe.


*Tanzania Industrial Studies and Consulting Organization (TISCO). Umuhimu wa taasisi hii unajieleza wenyewe.


*Shirika la maendeleo la taifa - National Development Corporation (NDC). Shirika hili lilipewa jukumu la kusimamia uanzishaji na uimarishaji wa Viwanda nchini.


*Tanzania Investment Bank (TIB) n.k.


Tangia kipindi kile, hapajwahi tena kuwa na mkakati mpana namna hii wa Viwanda nchini.






Katika bandiko linalofuata tutajadili:

Tofauti kubwa baina ya Mkakati wa Viwanda wa(1975) na Mkakati na Mpango wa Maendeleo wa Taifa (2015/6-2020/21)
 
1.5.4 Tofauti kubwa baina ya Mkakati wa Viwanda wa(1975) na Mkakati na Mpango wa Maendeleo wa Taifa (2015/6-2020/21):


-Mkakati wa awali (1975-1995) ulikuwa ni mrefu kuliko Mkakati wa sasa kupitia Mpango wa Maendeleo wa Taifa (2015/6 - 2020/21). Mkakati wa mwaka 1975 ulifikia hatima yake chini ya Serikali ya Awamu ya Pili. Na kama tutakavyoona baadae, kipindi cha miaka 10 iliyofuatia (chini ya serikali ya awamu ya Tatu) kilishuhudia nchi ikiingia katika mchakato wa - “de-industrilization”.


-Tofauti na Mkakati wa sasa (2015/6 - 2020/21), ambao umebuniwa bila ya maridhiano ya kitaifa (National Consensus), Mkakati wa awali (1975-1995) ulihusisha maridhiano ya kitaifa. Kwa mfano, wananchi walielezwa hatua kwa hatua na kwa uwazi kupitia serikali yao, hasa juu ya ‘sacrifices’, zilizohitajika kwa taifa. Vile vile taasisi za elimu ya juu (vyuo vikuu) zilipewa fursa kuujadili mkakati na kuishauri serikali juu ya masuala mbalimbali. Hali hii ya kushirikisha umma katika masuala muhimu yanayohusiana na kodi zao na maslahi yao ilisaidia nchi kujenga utaifa/uzalendo; ilijenga ari ya wananchi ya kujitolea, kujituma, ku – ‘sacrifice’, kwa sababu wananchi walijisikia kuwa ni sehemu ya ‘suluhisho badala ya tatizo’ na hivyo kuzidi kujenga na kuwa na imani kubwa Serikali.


-Tofauti na Mkakati wa sasa, mkakati wa (1975-1995) ulizalisha tafiti na marejeo (references) mbalimbali zilizotumiwa kikamilifu na wanafunzi wa ‘Uchumi’ katika vyuo vikuu nchini. Wasomi na wanazuoni kama vile Dr. Justinian Rweyemamu, Dr. Bismark Mwansasu na wengineo walitumiwa vyema na serikali kuandaa ‘content’ mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi na jamii kwa ujumla. Nk.



1.5.5 Mafanikio ya Mkakati wa Uchumi wa Viwanda (1975-1995):

Kufuatia mkakati wa Viwanda (1975-1995), nchi ilifanikiwa kujenga na kuendeleza Viwanda vingi, mifano ikiwa ni pamoja na hii ifuatayo:


*Dar-es-salaam - Viwanda vya nguo, Vinywaji, Simenti, Vifaa vya Kilimo, Nyama za Kusindika, Sigara, Toys (kwa ajili ya kuchezea watoto) nk.


*Mwanza – Samaki, Nguo, ngozi, Pamba, mafuta n.k.


*Kilimanjaro - Kilimanjaro Machinery tools, Surgical tools,ngozi nk.


*Shinyanga – Nyama za Kusindika, nk.


*Mbeya – Vifaa vya Kilimo, Simenti, Nguo, Maziwa nk.


*Tanga – Simenti, Mbolea, Chuma, Kemikali, Mkonge, Maziwa nk.


*Morogoro – Nguo, ngozi, mafuta ya kula, Katani nk.


*Arusha – Matairi, ngozi, Vinywaji, ngozi, vifaa vya umeme nk.


*Iringa/Mufindi – Karatasi na Tancut Almasi


*Kibaha - Tanzania automobile assembly plant (TAMCO), Tractor Assembly plant, Korosho.


*Mtwara – Korosho, nk.


*Vile vile kwa upande wa Viwanda Vidogo Vidogo, SIDO kwa kushirikiana na wataalam kutoka nchi za Sweden na Netherlands, ilifanikiwa kujenga viwanda vidogo vidogo vingi (engineering workshops) vyenye ubora, utaalam, na vilivyotengeneza ajira kwa wingi kwa wananchi, mfano katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Mbeya, Arusha, na Moshi. Viwanda hivi vilijengwa mahususi kuhudumia viwanda vikubwa katika sehemu mbalimbali nchini, na hivyo kujenga na kuimarisha ‘upward and downward economic linkages.‘ Matokeo yake ikawa ni pamoja na Serikali kufanikiwa kujenga “National Integration of the Economy”, suala ambalo halipo tena. Leo hii, walaji wengi (consumers) wana ukaribu zaidi na wazalishaji wa nje (China nk), kuliko wazalishaji wa ndani.


1.5.6 Mkakati wa Viwanda (2016/17-2024/21) hauwaelezi wananchi historia inavyotakiwa.


Wananchi wana haki ya kuhoji kwanini Serikali chini ya Chama Kile Kile inarudia mambo YALE YALE miaka 41 baadae bila ya maelezo ya kina tulikosea wapi na tufanye nini ili makosa ya awali yasijirudie.


Zipo sababu za msingi za wananchi kuhoji haya. Katika sehemu inayofuata tutazijadili kwa uchache:


Serikali imekuja na mkakati wa kurudia yale yale iliyaanzisha miaka 41 iliyopita na kushindwa kuyasimamia kikamilifu ikizingatiwa, sehemu kubwa ya ‘mass goods industries’ zilijengwa kwa fedha za ndani (Kodi za wananchi).


Kizazi cha Sasa Kinapaswa kuelezwa kwamba huko nyuma tulifanikiwa pia kabla ya sisi wenyewe kubomoa mafanikio yaliyopatikana na nguvu, juhudi, na gharama kubwa (Kodi za wananchi, hasa Wakulima na Wafanyakazi)


Katika miaka ya 1970s, Tanzania ilikuwa na takribani ‘fifty five textile units, ikijumuisha ‘fully’ integrated textile mills zilizokuwa na uwekezaji (kwa thamani ya wakati ule) wa Dola za Kimarekani Milioni 500. Leo hii ni sawa na Zaidi ya TZS Trilioni moja – kwa viwanda vya nguo tu. Viwanda hivi vilitoa ajira zaidi ya 30,000 (elfu thelathini) kwa wananchi. Lakini miaka 20 baada, nchi ilikuwa na Viwanda viwili tu. Vingine vilivyobakia aidha vilikuwa vimeisha kufa au ‘privatised’.


Viongozi wengi wamekuwa wakielezea historia halisi juu ya mafanikio ya Viwanda (1975-1995) kwa kuficha ficha. Lakini Katibu Mkuu wa CCM A.Kinana katika ziara zake za kuimarisha chama (2014/2015) aliwahi kukiri mbele ya umma kwamba serikali ya chama chake ilifanya makosa makubwa katika mchakato wa ubinaifishaji wa mashirika ya umma na kuahidi wananchi serikali ya CCM italiangalia upya suala hili. Kitendo hiki kilikuwa ni cha kijasiri sana.


Ni matarajio ya wananchi kwamba Serikali itafunguka zaidi kuhusu makosa yaliyofanyika huko nyuma. Wananchi wana haki ya kuelezwa kwa kina nini kilitokea katika viwanda vyao. Kwa mfano, historia ya viwanda vya nguo (textiles) imekuwa ikielezwa kuanzia kipindi cha miaka ya tisini kama ‘base year’ kulinganisha mafanikio katika sekta hii.


Iliwahi kuelezwa kwamba uzalishaji wa ‘textiles’ uliongezeka kutokea mita za mraba milioni ‘31’ mwaka 1991 na kufikia mita za mraba milioni ‘84’ mwaka 2001. Lakini mafanikio ya kipindi kabla ya mwaka 1991 kwa sekta yamekuwa hayawekwi hadharani. Pengine ni katika juhudi za kutetea uhalali wa ‘privatization’. Kwa mfano miaka ya mwisho ya 1970s na mwwanzo ya 1980s, uzalishaji wa ‘textiles’ uliwahi kufikia mita za mraba milioni ‘92’. Rekodi hii haijawahi kuvunjwa. Hilo halielezwi.


Pamoja na mafanikio kadha wa kadha ya Mkakati wa awali wa Kuendeleza Viwanda (1975), miaka 20 baadae, bado hoja ikajengwa kwamba Viwanda vyetu vinahitaji kubinaifisishwa kwa lengo la kuongeza ufanisi zaidi na kuwapunguzia mzigo walipa kodi. Hoja hii imejirudia katika Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa (2016/17-2020/21) katika kuelezea historia ya uchumi wa Viwanda Tanzania. Katika hotuba yake, Dr. Mpango alitamka kuwa hatua ya ubinaifisishwaji ilitokana na ukweli kwamba “mashirika ya umma yalikuwa ni mzigo wa walipa kodi”.


Dr. Mpango anazungumzia Viwanda ambavyo sehemu kubwa ya gharama za ujenzi wake (mass goods industries) ilitokana na vyanzo vya ndani vya fedha (walipa kodi). Waziri Mpango anazungumzia pamoja na Viwanda vya nguo ambavyo vilizalisha ajira zaidi ya 30,000 kwa watanzania. Pamoja na juhudi za serikali kufufua viwanda vya aina hii, itakuwa ni vigumu kwa serikali kuzalisha ajira viwandani kwa kiwango hiki.


Viwanda vingine vya ‘mass production’ vilikuwa ni pamoja na Viwanda vya Bia, Sigara nk. Tofauti na hoja Serikali kwamba kulikuwa na ulazima wa kubinaifisisha Viwanda vyetu kwa utaratibu uliotumika, kwa hoja kwamba vilikuwa vikiendeshwa kwa hasara na hivyo kuwa mzigo kwa walipa kodi, Viwanda hivi (Bia na Sigara) havikuwahi kuendeshwa kwa hasara, hivyo havikuwahi kuwa mzigo kwa walipa kodi. Badala yake Viwanda hivi vilichangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa (GDP), pato la serikali (Kodi), na pia ajira nyingi kwa wananchi.


Lakini cha ajabu ni kwamba Wananchi wanaambiwa mashirika haya mawili kwa mfano TBL na TCC ni ‘success story’ ya privatization. Hii sio kweli kwani hadi siku ya mwisho mashirika haya yalipokuwa yanaondolewa mikononi mwa wenyewe (walipa kodi), yalikuwa bado yanaendeshwa kwa faida. Kwa mfano, katika miaka yake ya mwisho mwisho mikononi mwa umma (walipa kodi), TBL ilikuwa inazalisha ‘at 50% capacity’ lakini ilikuwa ikitengeneza faida. Lakini bila ya kujalisha kama shirika la umma lilikuwa linaendeshwa kwa faida au hasara, hoja ikajengwa kwamba ni lazima kubinaifisisha ili ‘kuwaondolea walipa kodi mzigo’.


Mashirika ambayo yalikuwa yakijiendesha kwa hasara nayo yakauzwa kwa bei chee kwa masharti kwamba the state (hivyo walipa kodi) ndio wabebe all the ‘liabilities’. Kwa maana hii, walipa kodi ambao maslahi yao yalikuwa kwenye mashirika haya ya umma wakapoteza ‘on both counts’.


Mbali ya kubinaifisisha viwanda ambavyo vilikuwa bado vinaendeshwa kwa faida, vile vile sensitive and strategic sectors kama vile oil refinery, madini, mabenki, na mawasiliano, nazo zikabinaifisishwa. Leo kama taifa tunapata wakati mgumu wa kufanya maamuzi au kuchukua hatua muhimu za kiuchumi kutokana na makosa haya.


Mantiki ya kiuchumi inayoongoza ‘private enterprises’ ni tofauti na ile inayoongoza ‘state enterprises’. Kwa mfano, tangu Kampuni ya Bia (TBL) ibinaifisishwe, kampuni hii imeweza kuongeza uzalishaji. Vile vile, mchango wake katika pato la taifa umeongezeka na imeweza pia kujenga viwanda vingine. Lakini serikali haielezi wananchi hatujaambiwa hadithi yote kuhusu TBL. Kwa mfano:


Kampuni ya Bia (TBL) haikuwa simply just a ‘beer plant’. Kampuni hii ilikuwa na mashamba makubwa ya ngano, majengo kwenye maeneo yenye thamani kubwa (Prime Area Properties), na pia ilimiliki ‘Brands’ kubwa kama bia ya ‘SARARI’, nk.


Wananchi wanapaswa kuelezwa – Je:


-Leo hii ni nani anamiliki brands za wananchi kama vile brand ya “SAFARI”?

-Brands husika zilifanyiwa tathmini gani kabla ya ‘privatization’?

-Leo hii nani analipwa royalty ya brands mbalimbali za wananchi?


Zipo taarifa kwamba kuna wakati bia ya ‘Safari’ ilikuwa ikiuzwa nchini Swaziland huku ikiwa imeandikwa maneno ‘Made in Swaziland’. Hili ni suala la kushangaza na kusikitisha.


Pia katika mfumo wa uzalishaji wa bia chini ya TBL, kulikuwa na ‘horizontal linkages’ baina ya TBL na viwanda vingine kama vile utengenezaji wa chupa na makopo ya bia. Inashangaza kuona kwamba ‘Linkages’ kama hizi zilikuwepo wakati kiwanda cha TBL kilipokuwa katika ufanisi wa kiwango cha chini kidogo kuliko sasa, lakini leo hii ambapo ufanisi umeongezeka sana, linkages hizi zilizotoa fursa za ajira kwa watanzania na fursa za biashara kwa viwanda vidogo vidogo vya ndani, fursa hizi hazipo tena. Wananchi wana haki ya kujua – viwanda hivi vina faida gani kwa maana ya kujenga national integration of the economy yenye kuweza kutoa fursa mbalimbali zinazoendana na up stream and down stream activities za kisekta?


Mbali ya viwanda vya nguo, bia, sigara, wananchi pia hawajaelezwa ni kitu gani kilivikumba viwanda vyao vingine vya ‘mass goods’ kama vile viwanda vya viatu, mafuta ya kupikia n.k., viwanda ambavyo sehemu kubwa ya gharama za ujenzi ilitokana na fedha za ndani (Kodi na mapato ya fedha za kigeni zilizotokana na uuzwaji wa mazao ya biashara nje ya nchi).


Mkakati wa Uchumi wa Viwanda (1975-1995) haukufeli kwa asilimia mia moja. Na hata katika maeneo tulipo feli, bado tulikuwa na uwezo wa kurekebisha, hasa kwa kuchagua utaratibu wa ‘privatisation’ wenye kuangalia maslahi ya watanzania. Kufeli kwa Viwanda mbalimbali haikuwa na maana kwamba soko lilitoweka kwa viwanda vyote. Vinginevyo wawekezaji wan je wasingekuja kuvinunua na kuwekeza. Lakini pamoja na ukweli huu, wananchi wakashuhudia (1995-2005) nchi ikiingia katika mchakato wa ‘de-industrialisation’ ambayo ilivikumba hata viwanda vilivyokuwa vinaendeshwa kwa faida, viwanda vilivyokuwa na mchango mkubwa katika pato la taifa na vilivyotoa ajira kwa wananchi.


Miaka 41 baadae, Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa unajaribu kuja na malengo yale yale. Tungetumia muda, rasilimali, na fursa vizuri, huku tukiongozwa na uzalendo, Viwanda vilivyojengwa miaka 41 iliyopita, vingine kabla hata ya Viwanda vya China, Malaysia nk, leo tungekuwa tunapanga mambo mengine tofauti na endelevu.


Katika bandiko linalofuata tutajadili:

Je, Tulikosea Wapi na Mkakati Wa Viwanda – BIS (1975-1995)?
 
1.5.7 Je, Tulikosea Wapi na Mkakati Wa Viwanda – BIS (1975-1995)?


Kwa miaka mingi, swali hili limezua mijadala mikubwa huku sababu mbalimbali zikitolewa. Tutajikita katika sababu kuu tatu ambazo ninaamini ni za msingi zaidi:


1. Sababu ya kwanza kwanini tulifeli ni kutokana na ukweli kwamba mfumo uliokuwepo (centrally planned economy) ulijaa urasimu (bureucray) badala ya msukumo wa ujasiriamali na ubunifu (entrepreneurship and innovation).


Kusema hivyo haina maana kwamba mafanikio ya uchumi ya viwanda hayawezi kupatikana chini ya ‘centrally planned economy’, bali kama tutakavyoona punde, tulishindwa kuhusisha virutubisho muhimu kama vile ujasiriamali na ubunifu katika mkakati wa awali wa viwanda.


2. Sababu ya pili ni kwamba tulitegemea ‘Kupandikiza’ (transplant) teknolojia badala ya ku ‘internalize’ tekinolojia. Hatukufanikiwa kuja na mkakati mzuri wa kuhamisha tekinolojia (technology transfer) and localize it, kama walivyofanya kwa mfano China na kwingineko katika kipindi kile kile.


3. Sababu ya tatu na pengine muhimu kuliko zote ni kuibuka kwa China Kiuchumi kuanzia miaka ya tisini.


Tusisahau kwamba Mkakati wetu wa viwanda – Basic Industry Strategy (1975) ulianza karibia wakati sawa na Mkakati wa Viwanda nchini China – The Chinesse Transformation (1978). Tofauti na sisi, China walitumia vyema mfumo wao wa uchumi (centrally planned economy) kulinda viwanda vyao na pia kuviwezesha kuhamisha tekinolijia (Technology Transfer). Pia historia inatuonyesha kwamba China ilichelewa sana kujiunga na ‘World Trade Organization’, suala lililowasaidia sana kuweza kujiandaa na uchumi wa viwanda bila ya kuingiliwa na ushindani kutoka nje.


China walifanikiwa sana katika ‘technology transfer’ na kupitia uwekezaji kutoka nje (Foreign Direct Investment). Lakini mafanikio haya yalitokana na maandalizi mazuri ya awali kama vile kuwekeza katika mtaji watu (Human Capital – Afya, Lishe, Elimu nk); walijenga mahusiano mazuri na mataifa ya nje pamoja na trading blocks mbambali, na ilipofika mwaka wao kujiunga na ‘WTO’, wakaingia wakiwa wamejiandaa vizuri.


Ni kupitia maandalizi ya aina hii, China ikaanza kuonja mafanikio katika kila Nyanja ambapo wakaanza kujenga a ‘competitive advantage’ - localization of technological development, economies of scale, cheap labour, labor with skills and technology know how n.k.


Matokeo yake – China ikaanza kuuza bidhaa zake mbalimbali na zenye ubora katika soko la kimataifa, hasa katika nchi zinazoendelea, miongoni mwa bidhaa muhimu ni ‘textiles’ ambazo kwa Tanzania, hivi vilikuwa ni viwanda mama. Kutokana na mapungufu yetu mbalimbali ambayo baadhi yake tumeyajadili huko juu, ujio wa bidhaa za ‘textiles’ kutoka China ukapelekea viwanda vyetu ya nguo nchini kushindwa kuhimili ushindani na hatimaye vingi vikafa.


1.5.8 Je tunatokaje hapa tulipo?


Maswali muhimu ambayo yanapaswa kujibiwa na Serikali, kupitia Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa 2016/17-2020/21 pamoja na Sera ya Taifa ya Viwanda ni pamoja na haya yafuatayo:


· Katika miaka kumi chini ya mkakati huu wa viwanda (2016-2025), lengo kuu ni nini?

Ni muhimu tukawa na majibu sasa sio baadae ili kuokoa muda na kodi za wananchi kutumika masuala yasiyo na tija. Bila ya kuwa na lengo kuu linaloeleweka, ni rahisi kupoteza rasilimali nyingi (misallocation of resources).


· Kama Taifa, je tumeridhia ku ‘sacrifice’ nini kwa maana ya ‘kuchagua’ vya kufanya na kutofanya sasa?

Pamoja na umuhimu wa Uchumi wa Viwanda, wananchi walio wengi bado wanaishi katika hali duni na serikali inahitaji kuhudumia sekta hizo. Ni muhimu wananchi wakaelezwa mapema kwamba katika kipindi cha miaka kumi ijayo matumizi ya fedha zao (kodi) katika uchumi wa Viwanda utaathiri kwa kiasi gani huduma za kijamii na kwa muda gani? Serikali isipofanya hivyo mapema na baadae hali za maisha ya wananchi zikazidi kuzorota, upo uwezekano wa wananchi kutochangia ipasavyo katika mkakati unaohusisha uchumi wa viwanda, hasa pale watakapoona huduma za kijamii zinazorota na hivyo kutokuwa na moyo wa kuongeza uzalishaji, kulipa kodi n.k.


· Kama Taifa, tumejipanga vipi kuhamisha tekinolojia (technology transfer) kutoka kwa wawekezaji wa nje (FDIs)?

Mpango wa maendeleo husika una lengo la kuongeza kiasi cha uwekezaji kutoka nje (nje) kutokea kiwango cha sasa cha takribani Dola za Kimarekani Bilioni

2.1 kwa mwaka na kufikia Dola za Kimarekani Bilioni (5) tano kwa mwaka. Katika hili, tumejiandaa vipi ‘domesticate/localize’ tekinolojia itakayokuja na uwekezaji wa kiwango hiki?


Malengo ya kuongeza kiasi cha FDI ni mazuri lakini sio kwamba uchumi wetu haupo wazi kuvutia FDIs na tekinolojia. Hata wakati wa ujamaa, uwekezaji kutoka nje ulikuwepo pamoja na uingiaji wa tekinolojia ya nje. Lakini moja ya makosa tuliyofanya ni kwamba hatukuwa makini sana katika suala la localization of imported technology kwani sehemu kuwa ya tekinolojia iliyoingia nchini iliishia kuwa ‘transplanted’ badala ya kuwa ‘diffused and localized/domesticated’. Tuna miaka zaidi ya ishirini sasa ya uchumi wa soko huria, lakini tatizo lililopo ni kwamba uchumi huria haujaweza kuamsha ‘a competitive response’ ya kuvutia zaidi FDIs katika sekta muhimu kwa uchumi wetu kwa sababu hatuna nguvu kazi ya kutosha yenye ‘skills and capabilities’ inayoendana na mahitaji ya karne ya ishirini na moja. Uwekezaji mkubwa katika sekta za Elimu, Afya na Kilimo (lishe) ni muhimu katika hili.


Bila ya kuwa na mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji mkubwa kutoka nje, uwekezaji ambao sio tu unafuata rasilimali bali pia human capabilities, itakuwa ni vigumu sana kwa taifa kufaidika na uwekezaji wa nje katika sekta ya viwanda na kuwa na ‘multiplier effect’. Wawekezaji watakuja, wata ‘inflate’ bei za malighafi zao kutoka nje, watawalipa wafanyakazi wao kutoka nje wenye ‘skills’ mishahara minono, watafanya ‘transfer pricing’, na mwisho wake wataonyesha faida ndogo ili walipe kodi ndogo. Sisi kama taifa tutaendelea kuvuna kodi ndogo na wananchi wetu wataendelea kupata ajira zenye vipato duni.


· Kama Taifa, tumejipanga vipi kupambana na ushindani wa kikanda na kimataifa?

Muktadha wa uchumi wa viwanda umebadilika sana katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita. Ushindani umekuwa ni mkubwa kuliko huko nyuma kufuatia ‘economic liberalization & shrinking of economic distance’ kutokana na kukua kwa tekinolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA).


Ushindani umechukua sura mpya inayosukumwa na mabadiliko ya kasi katika tekinolojia, pamoja na kuibuka kwa mitandao mikubwa ya uzalishaji ya kimataifa (International production chains). Hali hii inahitaji ujuzi (skills) na uwezo (capabilities) za hali ya juu hata katika ‘entry level manufacturing’ or ‘basic manufacturing activities.’


· Serikali imejiandaa kwa kiwango gani na wataalam?

Moja ya changamoto zinazotukabili katika uendeshaji wa sekta ya umma ni pamoja na uhaba wa watendaji wenye skills, technical knowledge, entrepreneurial spirit, negotiation skills (with World Trade Organisation and Donor Community in general) and knowledge in industrial policy.


Hata katika awamu ya kwanza ya ujenzi wa uchumi wa viwanda (1975), mapungufu ya aina hii yalichangia mashirika mengi ya umma kukosa ufanisi. Bureaucrats wakiachiwa kuongoza mkakati huu bila ya kuwa na ‘entreprenurial drive’, kuna hatari ya kutofanikiwa.


Serikali inahitaji watu wenye uwezo na pia mfumo wa usimamizi, utekelezaji, udhibiti, kujifunza, na kujipanga upya.


·Mwisho, je tumeandaa taasisi zinazohitajika kusimamia ujenzi wa uchumi wa viwanda?

Awali tuliona kwamba katika awamu ya kwanza ya ujenzi wa uchumi wa viwanda (1975), mafanikio mengi yalitokana na uanzishwaji na ushirikishwaji wa taasisi muhimu kama vile taasisi za elimu ya juu (Vyuo Vikuu), TIRDO, TEMDO, SIDO, TISCO, n.k.


Umuhimu wa taasisi hizi ni kufanyia kazi changamoto zote zinazojitokeza katika ujenzi wa uchumi wa viwanda. Leo hii, nyingi ya taasisi hizi zipo katika hali mbaya kifedha, kitaalam, kihamasa na pia kuna weak link baina yake na sekta binafsi.


Mwisho wa Sehemu ya KWANZA



Bandiko linalofuata ni sehemu ya pili, tutaanza kwa kujadili:

Sehemu ya Pili – Majukumu ya Serikali katika Uchumi wa Taifa.
 
Sehemu ya Pili – Majukumu ya Serikali katika Uchumi wa Taifa.


Serikali ina majukumu maalum katika uchumi wa taifa yaliyogawanyika katika sehemu kuu tatu:


*Stabilization of the Macroeconomic environment (Uimarishaji/uthabiti wa Mazingira ya uchumi mpana wa nchi).

*Income Redistribution (mgawanyo wa mapato).

*Resource Allocation (mgawanyo wa rasilimali).


Kabla ya kuangalia kwa undani majukumu tajwa hapo juu, tuangalie kwa uchache nyenzo mbili kuu zitumiwazo na serikali kutekeleza majukumu tajwa matatu ambazo ni :


i) Fiscal Policy instrunments (kupitia serikali kuu/hazina)

ii) Monetary Policy instrunments (kupitia Benki Kuu).


2.1 Fiscal Policies


Nyenzo hii ipo chini ya Serikali kuu (hazina), ambapo serikali huratibu uchumi wa taifa kwa kutumia nyenzo kuu mbili:

*Kodi za aina mbalimbali – Lengo kuu ikiwa ‘to ‘influence’ vitu kama mapato ya wananchi (disposable income), matumizi ya vipato vya wananchi (consumption), mfumuko wa bei (inflation), na viwango vya akiba na uwekezaji ndani ya uchumi wa nchi. Tutayaona haya kwa undani baadae.


*Matumizi ya aina mbalimbali ya umma – Lengo kuu katika hili pia ni ‘to ‘influence’ mapato ya wananchi, uzalishaji ndani ya taifa (output), mfumuko wa bei, viwango ajira n.k. Matumizi haya ni pamoja na shughuli za ujenzi wa miundo mbinu kiuchumi (economic infrastructure) yenye lengo la kuzalisha ajira, kuongezea wananchi uwezo wa kumuda mahitaji (purchasing power), kutoa motisha kwa maendeleo ya viwanda nk.


2.2 Monetary Policies

Nyenzo hii ipo chini ya Benki Kuu ya nchi (e.g BOT), ambapo Kazi kubwa ya Monetary policies ni kusimamia na kudhibiti mambo makuu mawili:

-Monetary base katika uchumi (money supply) mzunguko wa fedha, ili hasa kudhibiti mfumuko wa bei (inflation).

- Viwango vya riba kudhibiti ‘money supply’ yenye athari katika viwango vya mfumuko wa bei (rate of inflation).


Katika kufanikisha masuala haya, Benki Kuu hutumia nyezo kuu tatu:

2.2.1 Open Market Operations

Kupitia nyenzo hii, Benki kuu huwa inaendesha minada ya kuuza na kununua dhamana za serikali (kwa Treasury Bills na Treasury Bonds) mara kwa mara. Hii ni sehemu kubwa ya soko la ndani la deni la taifa (domestic debt market). Kwa upande mmoja, iwapo lengo la serikali ni kupunguza mzunguko wa fedha katika uchumi kwa nia ya kudhibiti mfumuko wa Bei au kutafuta fedha kwa ajili ya shughuli za serikali (domestic debt/deni la ndani), Benki kuu inaweza kuuza dhamana za serikali kwa umma. Kwa upande mwingine, iwapo lengo la serikali ni Kuongeza mzunguko wa hela katika uchumi ili kuamsha shughuli za kiuchumi, Benki kuu inaweza kununua dhamana hizi kutoka kwenye umma.


Katika hali ya kawaida, mbali ya taasisi za kifedha, domestic debt market zinapaswa kushirikisha daraja kati kiuchumi ‘middle class’ ya nchi. Lakini kwa Tanzania, wadau wakubwa ni mabenki ya kibiashara na mifuko ya pensheni.

2.2.2 Discount/Window Lending

Hii ni nyenzo ya pili chini ya Benki kuu yenye lengo la kuongeza au kupunguza mzunguko wa fedha katika uchumi (Monetary base) kutegemeana na malengo yaliyokusudiwa. Ikumbukwe kwamba - Benki kuu ni benki mama ya benki zote za biashara ndani ya nchi. Benki Kuu inawajibika kutoa huduma mbalimbali za kifedha kwa mabenki ya Kibiashara (kwa mfano CRDB, Acces Bank nk), kama vle mabenki ya biashara yanavyotoa huduma za kifedha kwa umma.


2.2.2.1 Namna Benki Kuu inavyo athiri monetary base kupitia ‘discount window’:


Benki kuu hutoa huduma inayoitwa ‘discount loans’ kwa benki zote za biashara. Huduma hii pia hujulikana kama ‘discount window.’ Kwa upande mmoja, Discount rates zikiwa kiwango cha juu, Mabenki ya Biashara hayapati motisha ya kukopa kutoka benki kuu, hali ambayo inapunguza wingi wa fedha mikononi mwa benki hizi kwa ajili ya kukopesha wananchi na wafanyabiashara mbalimbali, hivyo kupunguza mzunguko wa fedha (monetary base). Kwa upande mwingine, ‘discount rates’ zikiwa katika kiwango cha chini, mabenki ya biashara hupata motisha ya kuchukua mikopo kutoka benki kuu na kuongeza wingi wa fedha mikononi mwa wafanyabiashara na wananchi, hivyo kuongeza mzunguko wa fedha katika uchumi (increase monetary base).


Discount lending ni muhimu katika nyakati za msukosuko wa uchumi. Kwa mfano, ikitokea wananchi na wafanyabiashara wanapoteza imani na mabenki ya biashara na kuamua kuondoa fedha zao (withdraw their deposits), hali hii itapelekea mabenki ya biashara kukumbwa na uhaba mkubwa wa ‘deposits’ kwa ajili ya kujiendesha kibiashara. Hali hii ikijitokeza, Benki kuu huwa ipo ‘standby’ kuziokoa benki za biashara kama ‘a lender of last resort’.

2.2.3 Changes in Reserve Requirements


Hii ni nyenzo ya tatu ya Serikali (kupitia benki kuu) yenye lengo ‘to influence’ the monetary base ndani ya uchumi wa nchi. Reserve requirements maana yake ni kwamba – Katika kipindi chochote, Mabenki yote ya biashara yanatakiwa kuwa na kiwango Fulani cha akiba Benki kuu, viwango ambavyo hubadilika kutokana na malengo ya Benki kuu katika usimamizi na udhubiti wa uchumi katika wakati husika. Kwa mfano, benki kuu inaweza kuwa na lengo la kuongeza mzunguko wa fedha au kupunguza mzunguko wa fedha katika uchumi wa nchi. Kwa upande mmoja, Maamuzi haya yana athari kwenye ‘liquidity’ ya mabenki ya biashara.


Kwa upande mmoja, Benki Kuu ikiongeza ‘reserve requirement’, athari yake ni mabenki ya biashara kulazimika kupeleka akiba kubwa zaidi benki kuu jambo litakaloathiri kiasi cha fedha mikononi mwa benki hizi kwa ajili ya mikopo kwa wananchi na wafanyabiashara. Matokeo yake ni pamoja na kwamba - mzunguko mdogo wa fedha katika uchumi wa ndani unapungua/unakuwa mdogo, hivyo kutatua tatizo lililolengwa, kwa mfano kudhibiti mfumuko wa bei ambao unachochewa na uwepo wa fedha nyingi katika mzunguko wa uchumi kuliko wingi wa bidhaa na hudma.


Kwa upande mwingine, Benki kuu ikikupunguza ‘reserve requirement, athari yake ni mzunguko wa fedha katika uchumi kuongezeka, hivyo serikali kufanikisha malengo ya kisera kama ilivyokusudiwa.


Swali muhimu katika hili ni je:

· Serikali/Benki Kuu hutekeleza Fiscal Policies & Monetary Policies kwa kuzingatia maslahi ya wananchi walio wengi?

· Wananchi walio wengi (maskini) wamekuwa wakinufaika vipi na sera hizi?



Baada ya kujadili njia kuu mbili (KISERA) ambazo serikali huzitumia kutekeleza majukumu yake katika uchumi, sasa tuangalie majukumu matatu ya serikali katika uchumi ni yepi,kama tulivyodokeza kwenye aya ya kwanza. Tutaanza na jukumu la kwanza ambalo ni:


Stabilization of the Macroeconomic environment (Uimarishaji/uthabiti wa Mazingira ya uchumi mpana wa nchi).
 
2.3 Stabilization of the Macroeconomic environment (Uimarishaji/uthabiti wa Mazingira ya uchumi mpana wa nchi).


Uchumi mpana una viashiria kadhaa vinavyotumika kupima Afya yake kwa faida ya wananchi. Katika sehemu inayofuata, tutajadili viashiria vichache muhimu ambavyo ni:

· Kasi ya kukua kwa ‘Pato la Taifa’ (GDP growth rate)

· Mfumuko wa bei (Inflation)

· Viwango vya Riba (Interest Rates)

· Viwango vya ajira katika taifa (Employment/Unemployment Rate)

· Balance of Payment/Current Account deficit


Wakati tukipitia viashiria hivi, inatakiwa tujiulize swali moja muhimu - Je:


Mafanikio katika maeneo yote haya ya uchumi wa NCHI yanaleta matokeo gani katika uchumi wa WANANCHI?


2.3.1 Kasi ya kukua kwa ‘Pato la Taifa’ (GDP growth rate)


Serikali ina wajibu wa kuhakikisha inajenga mazingira ya kuwezesha pato la taifa kukua kwa kasi itakayosaidia kuchochea shughuli za kiuchumi ili kutoa fursa kwa serikali kukusanya mapato zaidi kwa ajili ya kuendesha shughuli pamoja na kutoa huduma za kiuchumi na kijamii ili kuboresha maisha ya walipa kodi. Katika hali ya kawaida, kushamiri kwa shughuli za kiuchumi katika nchi (GDP growth) inatakiwa kuzalisha ajira kwa wananchi pamoja na kutoa fursa nyinginezo kwa wananchi, na kuchochea kasi ya kupungua kwa umaskini nk.


Ni katika muktadha huo wachumi wameeleza kwamba nchi maskini ikifanikiwa kukuza uchumi angalau kwa kasi ya asilimia 7 kwa mwaka kwa miaka 15 mfululizo, nchi hiyo ina uwezo wa kupunguza kiwango cha umaskini kwa asilimia sio chini ya hamsini. Kupitia mpango wake wa pili wa Maendeleo wa Taifa, serikali imetamka kwamba inatarajia kasi ya kukua kwa uchumi kutoa asilimia saba ya mwaka leo hadi asilimia kumi mwaka 2020. Hivyo basi matarajio ya wananchi ni kwamba kasi hii itaanza kuleta mabadiliko katika maisha yao kwa namna tulivyojadili hapo juu – kutoa fursa kwa wananchi kama vile ajira, kuchochea kasi ya kupunguza umaskini, kuongeza mapato ya serikali ya kusaidia kuboresha huduma za kijamii nk.


2.3.2 Mfumuko wa bei (Inflation)

Hiki ni kiashiria kingine muhimu cha kupima Afya ya uchumi mpana wa nchi. Swali ambalo linahitaji majibu chini ya serikali ya awamu ya tano, serikali ya “Mabadiliko” ni je, kuimarika kwa kiashiria hiki cha afya ya uchumi mpana wa “nchi” kinaleta matokeo gani kwenye uchumi wa “wananchi”


· Umuhimu wa kiashiria hiki upo katika maeneo kadhaa:


Kwanza mfumuko wa bei una uhusiano wa moja kwa moja na gharama za maisha ya wananchi (purchasing power), katka kumudu mahitaji yao yanayohitaji matumizi ya fedha.

Pili, kwa kufuatilia kasi ya mfumuko wa bei (inflation rate), ni rahisi kuona ni kwa kasi gani ‘real wages’ (viwango vya mishahara baada yaku-correct for inflation) inaongezeka katika taifa. Kwa mfano, iwapo mfumuko wa bei kutoka mwaka mmoja kwenda mwingine ni 7%, real wage inapaswa kuongezeka kwa kasi kubwa kuliko ‘inflation rate’ ili angalau mwananchi husika aweze kumuda gharama za maisha angalau kwa kiwango cha awali. Kwa maana nyingine rahisi, inflation rate ikiwa ni 7% kama mfano, maana yake ni kwamba gharama za maisha zimepanda kwa 7%. Real wage ikiongezeka kwa kiasi sawa na hii 7% maana yake ni kwamba mwananchi mwenye mshahara husika ataweza kumuda maisha yale yale ya mwaka uliopita. Lakini ili maisha yake yawe bora zaidi, ongezeko la mshahara wake ni lazima liongezeke kwa kasi kuliko ‘inflation rate’ ya 7%.


Vinginevyo holding other factors constant (Ceteris Paribus), kiwango cha mfumuko wa bei kikiwa kiatika tarakimu mbili (double digits), huwa ni ishara kwamba afya ya uchumi wa taifa sio nzuri. Na takwimu hii ikiwa katika tarakimu moja (single digit), ni ishara kwamba afya ya uchumi wa taifa ipo imara, kwa maana ya kwamba wananchi hawana haja na kuwa na wasiwasi juu ya mabadiliko ya gharama za maisha. Hii ndio sababu kuu kwanini Serikali wakati wote huwa inajitahidi kudhibiti mfumuko wa bei uwe chini ya 10%.



Kwa kipindi cha February 2015-February 2016, mfumuko wa bei (kwa wastani) ulirekodiwa kuwa karibia 6%. Kwa maana nyingine, katika kipindi husika, gharama za maisha ya mtanzania zilipanda kwa takribani 6%. Kwa wastani huu, maelezo ya kawaida ni kwamba serikali inafanya kazi yake vizuri kudhibiti mfumuko wa bei ili kuwezesha wananchi waendelee kumuda maisha yao ya kila siku.


Swali linalofuatia ni je – UHALISIA UPO VIPI?


Tukichukua ripoti ya mwezi wa pili Wastani wa mfumuko wa bei kwa kipindi cha mwisho kilichoripotiwa na serikali kupitia idara ya takwimu (NBS), wastani wa mfumuko wa bei kwa kipindi cha ‘January 2015 hadi January 2016’ ni kama 6%. Kwa wastani huu wa tarakimu moja (single digit), tafsiri ya moja kwa moja kama tulivyokwisha ona ni kwamba afya ya uchumi wa nchi ni nzuri, hivyo wananchi walio wengi kuwa katika nafasi nzuri ya kuendelea kumudu gharama za maisha kama kawaida. Lakini wastani huu huwa haielezei uhalisia wote upo vipi. Tujadili hili kidogo katika sehemu inayofuata:

Tukiachana na wastani wa mfumuko wa bei kwa katika kipindi husika 6%:

· Je hali ipo vipi katika bei ya bidhaa na huduma moja moja?

· Je, tukiangalia mfumuko wa bei katika bidhaa ambazo huchukua sehemu kubwa ya mapato ya wananchi walio wengi, tunaona nini?


Kwa mujibu wa idara ya Takwimu ya Taifa (NBS), bidhaa za vyakula na vinywaji (soft drinks) zinachukua karibia asilimia 40 ya matumizi ya kipato cha wananchi walio wengi. Kwa maana hii, mfumuko wa bei kwenye bidhaa moja moja za Vyakula ndio takwimu muhimu zaidi kwa Serikali kuithibiti ili kuhakikisha kwamba gharama za maisha kwa watanzania walio wengi haziongezeki kwa kiwango cha kutisha. Kwa mujibu wa ripoti ya Mwezi February 2016, kwa kipindi cha January 2015 hadi January 2016, mfumuko wa bei za bidhaa za chakula unaonyesha kukaribia 11%.


Kwa kigezo kwamba ‘inflation’ ikidhibitiwa ndani ya tarakimu moja (single digits), wananchi walio wengi wanaweza kumudu gharama za maisha, basi wastani wa 6% unakidhi kigezo hicho. Lakini kama tulivyokwisha gusia, takwimu ya wastani huwa inaficha uhalisia wa mambo. Kama tulivyoona, wakati wastani wa mfumuko wa bei ni 6% kwa kipindi cha January 2015-January 2016, mfumuko wa bei on ‘food and non alcoholic beverages’ katika kipindi hicho hicho ni karibia mara mbili ya 6%, kwa maana ya 11%. Ndio maana katika kipindi husika, wananchi wengi wameendelea kushangaa iweje serikali iseme kwamba mfumuko wa bei umethibitiwa wakati maisha yao yakiendelea kuwa magumu, kwa mfano kwa kuangalia bei ya bidhaa za vyakula kama vile sukari, nyama nk.


Hivyo basi kupitia jukumu la serikali la ‘uimarishaji na uthabiti wa uchumi mpana wa nchi kwa maslahi ya wananchi’ tulilojadili awali, wananchi wanatarajia ‘mabadiliko’ ya kweli ambayo yatahusisha pia udhibiti wa mfumuko wa bei za Vyakula, tatizo ambalo kwa miaka ming bado halijapatiwa ufumbuzi wa kudumu. Pia kama tulivyogusia awali, Serikali inatakiwa kuhakikisha kwamba ‘real wages’ kutoka mwaka mmoja kwenda mwaka mwingine zinaongezeka kwa kasi zaidi ya ile ya mfumuko wa bei katika ili wananchi waweze kumudu gharama za maisha yao ya kila siku.


2.3.3 Viwango Vya Riba (Interest Rates)

Viwango vya riba ni kiashiria kingine muhimu cha afya ya uchumi wa nchi kwa maslahi ya wananchi. Kiashiria hiki kina uhusiano wa moja kwa moja na hali ya maisha ya wananchi kwa maana zifuatazo:


-Gharama za mikopo wanazokabiliana wananchi na wafanyabiashara katika juhudi zao za kujiendeleza kibiashara na pia kuchangia ujenzi wa uchumi.

-Riba pia ina ‘influence’ motisha (incentives) za watu kujiwekea akiba, na ‘akiba’ ni chanzo muhimu cha uwekezaji wa ndani (domestic savings Equals domestic investments).

-Vile vile viwango vya riba vina ‘influence’ wingi au mzunguko wa fedha mikononi mwa wananchi (rejea mjadala wa awali juu ya monetary policies).


Swali muhimu hapa ni je – Viwango vya riba nchini vimekuwa vikinufaisha vipi wananchi walio wengi?


Tukiwa bado katika mjadala juu ya jukumu la kwanza la serikali – yani Stabilization of the Macroeconomic environment (Uimarishaji/uthabiti wa Mazingira ya uchumi mpana wa nchi), tutaendelea kuangalia viashiria vingine vya afya ya uchumi mpana wa nchi.
 
2.3.4 Viwango vya ajira

Hiki ni kiashiria kingine cha afya ya uchumi mpana wa nchi. Katika hali ya kawaida, kasi ya kukua kwa uchumi inapaswa kwenda sambamba na kukua kwa ajira. Hii ni kwa sababu, kasi ya kukau kwa uchumi ni matokeo ya ongezeko la shughuli mbalimbali katika sekta mbalimbali za uchumi wa nchi.


Swali muhimu hapa ni je – Kasi kubwa ya uchumi inayoendelea kutokea nchini Tanzania kwa miaka kumi na tano mfululizo (wastani wa 7% kwa mwaka), imekuwa ikizaa kiasi gani cha ajira – kwa maana ya ‘quantity and quality of jobs created?’


2.3.5 Current Account/Balance of Payments

Hiki ni kiashiria kingine muhimu cha afya ya uchumi mpana wa ‘nchi’. Current Account ni sawa na ‘balance sheet’ ya nchi.


2.3.5.1 Maana ya “Current Account”:


Tukichukulia Tanzania kama mfano, Current Account ni JUMLA ya haya yafuatayo:

BALANCE OF TRADE [Our exports of Goods and Services to the rest of the world] kutoa (minus) our imports from the rest of the World;


NET INCOME [Difference baina ya ‘mapato’ ya makampuni yetu yaliyowekeza kufanya biashara nje ya nchi na makampuni yaliyowekeza kufanya biashara ndani ya nchi yetu. Mapato yanayohusika hapa ni yale baada ya kutoa gharama za uendeshaji biashara kama vile malipo ya Kodi, Riba nk]; Na


NET TRANSFERS [Difference baina ya workers’ remittances (e.g in the Diaspora), donations, tax payments, foreign aid, grants, nk, kutoka nje ya nchi na zile zinazoingia kutoka nje ya nchi].


Kwa upande mmoja, Current Account SURPLUS (Chanya) huwa ni ishara kwamba nchi husika ni ‘net lender’ to the rest of the world. Kwa upande mwingine, Current Account DEFICIT (Hasi) huwa ni ishara kwamba nchi husika ni ‘net borrower’ from the rest of the world.


Muhimu pia ni kwamba - Current Account Surplus inaongeza ‘net foreign assets’ za nchi kwa kiwango cha surplus husika, na Current Account Deficit inapunguza ‘net foreign assets’ za nchi kwa kiwango cha deficit husika.


Ni jambo la kawaida kwa nchi maskini kama Tanzania kuwa na Current Account ‘Deficit’ kuliko ‘Surplus’. Hii ni kwa sababu nchi maskini zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa fedha za ndani kwa ajili ya kugharamia shughuli mbalimbali kama vile huduma za kijamii, uendeshaji wa shughuli za serikali nk. Kwa maana hii, nchi kuwa na “Current Account Deficit” maana yake ni kwamba nchi inarundika ‘external liabilities’ kutokana na kugharamia nakisi yake (deficit) kupitia fedha kutoka nje ya nchi kama vile mikopo nk, ili kukidhi mahitaji tajwa hapo juu na mengineyo.


2.3.5.2 Kwa kifupi, current account deficit ni matokeo ya:

-Nchi kuwa na mapato madogo ya ndani (mapato ya kodi na yasiyo ya kodi) ikilinganishwa na mahitaji.

-Nchi inapokuwa na viwango vidogo vya akiba (savings) ikilinganishwa na mahitaji ya uwekezaji (investments) wa ndani.

-Nchi inapokuwa na mapato madogo ya fedha za kigeni kutokana na mauzo hafifu ya bidhaa zake nje ya nchi. Nk.


Yote haya yanailazimisha nchi kuziba nakisi husika kwa kutegemea vyanzo vya fedha kutoka nje ya nchi kwa njia kama vile Misaada (Aid), government budget support, mikopo(deni la taifa), uwekezaji kutoka nje (FDI) nk.


2.3.6 Current Account Deficit kama Kiashiria cha Afya ya Uchumi wa nchi.


Kipimo cha Afya ya uchumi wa nchi kupitia kiashiria kinaangalia uwiano wake (Currenct Account) na pato la taifa (GDP), na kuwasilishwa kwa asilimia (as a percentage of GDP). Kama tulivyosema, nchi kuwa na ‘current account deficit’ ni jambo la kawaida. Swali muhimu ni kwa je:


· Is the Current Account Sustainable?


Iwapo haipo ‘sustainable’, huku deni la taifa (hasa la nje) nalo likiwa halipo ‘sustainable’, hapa kuna tatizo. Tutajadili kwa undani zaidi juu ya deni la taifa katika sehemu ya NNE.


2.3.6.1 Sustainability ya Current Account Deficit

Holding other things constant (Ceteris paribus), kwa mujibu wa ripoti ya ‘UN Economic Commision for Africa’ (UNECA), uchumi wa nchi unakuwa salama (safe zone) pale kiwango cha ‘current account deficit’ kinapokuwa (-5%) ya pato la taifa (GDP) au chini ya hapo.


Hivi sasa Current account deficit ya Tanzania ni takribani (-11%) ya pato la taifa (GDP). Kwa mujibu wa ‘UN Economic Commission for Africa (UNECA), kwa kipindi cha mwaka 1970 hadi mwaka 2005 (1970-2005), wastani wa current account deficit ilikuwa ni takribani (-9%) ya pato la taifa (GDP. Na kwa kipindi cha 2011-2015, wastani wake ilikuwa ni takribani (-11%).


2.3.6.2 Jinsi ya Kutathmini ‘Sustainability’ ya Current Account Deficit kwa nchi.


Ifuatayo ni orodha ya viashiria vinavyotumika kupima sustainability ya ‘current account’, vyote hivi vikiwasilishwa kwa uwiano wan a pato la taifa (% of GDP):


· High Trade Deficit (Nakisi ya biashara ya kimataifa)

Inayotokana na hali ya uchumi wa nchi to import zaidi kuliko exports. Current Account Deficit ikiambatana na high trade deficit, ni ishara yake ya kutokuwa ‘sustainable’. Pia huwa ni ishara ya uchumi/bidhaa zinazozalishwa nchini kutokuwa ‘competitive’, suala ambalo linapelekea bidhaa za nje kuingia zaidi na na pia kuathiri export performance ya nchi. Export performance kuwa duni, athari zake ni pamoja na taifa kutopata fedha za kigeni kwa kiasi cha kutosha kuendesha shughuli za maendeleo na shughuli za serikali nk. Hali hii inapelekea ulazima wa nchi kutegemea zaidi mikopo, na kuendelea kurundika deni la taifa. Tanzania ipo katika orodha ya nchi zenye ‘fastest growing deficit’, ambapo kwa sasa ni takribani ($-9.1 Billion)Tunabakiliwa na ‘high trade deficit’.

· Low Domestic Savings (akiba za ndani).

Akiba za ndani ni muhimu kwa uwekezaji wa ndani. Kiwango hiki kinapokuwa ni kikubwa, kinasaidia kupunguza utegemezi wa mikopo na mitaji kutoka nje ya nchi. Current Account Deficit ikiambatana na Low domestic savings, ni ishara ya current account kutokuwa sustainable. Hali hii inapelekea nakisi iliyopo kugharamiwa na akiba za wananchi wa mataifa mengine kwa njia za mikopo, misaada nk ili kukuza na kuendeleza uchumi, badala ya kazi hii kufanywa na fedha (akiba) za ndani ya nchi. Matokeo yake ni deni la taifa kuendelea kuwa kubwa. Wastani wa dunia (Gross National Savings as percentage of GDP) ni karibia 19%. Tanzania ni chini kidogo ya Wastani huu (takriban 17%). Nchi zinazoongoza barani Afrika ni pamoja na Botswana (38%), DRC (33%), Ethiopia (23%), Angola (19%) na Nigeria (19%).

· Low Foreign Direct Investments (uwekezaji kutoka nje ya nchi).

Current Account Deficit ikiambatana na Low Direct Investments, hii ni ishara kwamba ‘deficit’ haipo sustainable. FDIs ni chanzo muhimu na pekee ambacho kina uwezo wa kuziba ‘current account deficit’ kwa manufaa ya wananchi, tofauti na mikopo kutoka nje. Lakini hii itategemeana na jinsi gani serikali inakuwa makini na sera zake kuhakikisha kwamba nchi inavuna faida kubwa. Kupitia FDIs ‘a win-win situation’ baina ya wawekezaji na nchi mwenyeji (host country) inaweza kupatikana. Kwa mfano, FDIs zikiratibiwa vizuri na serikali ya nchi mwenyeji (host country), FDIs zinaweza kuleta faida nyingi ikiwa ni pamoja na kutengeneza wananchi ‘ajira bora’ (sio ‘bora ajira’), technology transfer kwa SMEs, kuchangia pato la taifa (GDP) na pia kuchangia mapato ya serikali (kodi). Tunakabiliwa na changoto nyingi, baadhi yake tumezijadili awali katika muktadha wa ‘uchumi wa viwanda’. Changamoto nyingine ni pamoja nan chi yetu kushindwa kuvutia FDIs katika sekta muhimu za uchumi wa nchi, sekta ambazo zina uwezo mkubwa wa kunyanyua hali za wananchi na pia kuchangia kukua kwa Viwanda vidogo vidogo nk (rejea mjadala wa awali juu ya mkakati wa Viwanda).

Lengo la Serikali ya awamu ya tano (kupitia mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano 2015-2020) ni kuongeza FDIs inflows kutoka kiwango cha sasa cha $2.1 Billion na kufikia $5Billion kwa mwaka ifikapo mwaka 2020. Pamoja na malengo haya, bado hayatoi uhakika kwamba Tanzania itakuwa miongoni mwa ‘top FDIs destinations” barani Africa, hasa iwapo bado tutaendelea kuwa na mazingira yasiyokuwa rafiki kwa wawekezaji. Changamoto nyingine ni kwamba, nchi kama Nigeria, Ghana, Algeria, DRC na South Africa ama tayari zimeshavuka malengo yetu ya $5billion (kufikia 2020), au tayari zipo katika kiwango hicho. Kwa mfano, kwa mwaka 2010, FDIs inflow katika nchi hizi ilikuwa ni kama ifuatavyo:

- Nigeria $9billion

- Afrika ya Kusini $5billion

- Ghana takriban $3billion

- DRC takriban $3billion

- Algeria takriban $2.6 billion

· Low GDP Growth (kasi ndogo ya kukua kwa uchumi wa nchi).

Current Account Deficit ikiambatana na low GDP growth, huwa ni ishara kwamba current account haipo sustainable. Kasi ndogo ya kukua kwa uchumi maana yake ni kwamba shughuli za uchumi (uzalishaji wa bidhaa na huduma) katika nchi ni duni/zipo chini/chache. Athari ya hili ni pamoja na serikali kuwa na vyanzo vichache vya mapato (tax revenues as percentage of GDP). Hali hii inalazimisha nchi kutegemea zaidi fedha za nje kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo, shughuli za serikali nk. Lakini kama tulivyojadili awali, kasi ya kukua kwa uchumi wa nchi ni kubwa lakini kasi hii inahusisha sekta zisizo kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na maisha ya wananchi kama vile utengenezaji wa ajira zenye viwango vizuri vya mapato, fursa za kibiashara down stream and up stream activities exposed to SMEs etc).

Asilimia sabini ya nguvu kazi bado ipo kwenye kilimo, sekta ambayo kama tulivyoona, kasi yake ya kukua (Kilimo) imeendelea kuwa karibia nusu ya wastani wa 7% unaosifiwa kwenye majukwaa ya siasa. Uchumi kukua nje ya Sekta ya Kilimo ni tatizo kubwa, hasa ikizingatiwa kwamba ndio chanzo kikubwa cha mapato/fedha za kigeni ambayo yanaendelea kuwa duni. Hali hii ikiambatana na current account deficit kubwa, ni dalili kwamba current account haipo sustainable.

· High National Debt and High Debt Service (As a percentage of tax revenues and commodity exports).

Jumla ya deni la taifa (au) kasi ya kukua kwa deni la taifa na pia malipo ya deni hilo kila mwezi (au) mwaka ya deni hilo yakiwa ni makubwa (kwa kuangalia uwiano wake na mapato ya kodi na pia mapato fa fedha za kigeni), na hali hii ikiambatana na ‘high current account deficit’, huwa ni ishara kubwa kwamba uchumi unashindwa ‘to maintain’ current account deficit’, hivyo deficit haipo sustainable. Tutajadili haya kwa undani zaidi katika sehemu ya nne na ya tano.

· Poor governance.

Ukosefu wa utawala bora (Good Governance) ukiambatana na uwepo wa ‘high current account deficit’, ni rahisi zaidi kwa current account kuendelea kuwa unsustainable kwa sababu utawala wa mabavu, kidikteta na usiojali haki na sheria za nchi mara nyingi huwa hauna motisha (incentives) kusimamia uchumi kwa maslahi ya wananchi. Utawala wa aina hii hugeuza ‘Uchumi’ uwe mtumishi wa ‘Siasa’ badala ya kuhakikisha kwamba ‘Siasa’ zinakuwa mtumwa mkubwa wa ‘Uchumi’, hasa uchumi wa wananchi.

Sehemu ya 2.3 hapo juu ilijikita katika kujadili Jukumu la kwanza la serikali katika uchumi – ambalo ni ‘Stabilization of the Macroeconomic environment (Uimarishaji/uthabiti wa Mazingira ya uchumi mpana wa nchi’). Katika sehemu inayofuata, tutaendelea kujadili Majukumu mengine mawili yaliyosalia ambayo ni – Redistribution of Income & Allocation of Resources.




Tukiwa bado kwenye sehemu ya pili, sehemu inayofuata tutajadili jukumu la pili na la tatu la serikali ambayo ni – redistribution of income & Allocation of resources.
 
2.4 Redistribution of income

Sera za ‘Redistribution of income’ hufanyika kwa njia mbalmbali, ikiwa ni pamoja na:


-Kupunguza pengo baina ya ‘walio nacho’ na ‘wasio nacho’ (kwa maana ya tofauti ya VIPATO).

-Kuwapatia wananchi wengi huduma bora (na sio bora huduma) za kijamii, lakini pia kwa gharama nafuu, kwa mfano elimu, afya, nk.


Serikali inaweza kusimamia/kutekeleza sera juu ya ‘redistribution of income’ kwa njia nyinginezo kama vile:


-Kwa kujenga ‘Mfumo’ imara wa kupambana na rushwa/ufisadi.

-Kwa kutaifisha mali za waalifu (kwa mfano wezi wa mali ya umma, wauza madawa ya kulevya).

-Kwa kugawa rasilimali ardhi kwa wananchi kupitia ‘land reforms’.

-Kwa kufanyia marekebisho mfumo wa kodi ili uwe ‘fair and jus’t kwa pande zote mbili yani - kwa kuhakikisha kwamba wasio nacho hawapati maumivu makubwa, lakini bila ya kwa kuhakikisha kwamba viwango vya kodi vilivyopo havileti athari hasi kwa ‘incentives’ kwa walio nacho, ambao wana umuhimu mkubwa wa kuendeleza uchumi wa nchi. Nk.


Kwa kufanya haya, maisha ya wananchi walio wengi yanaweza kuboreshwa zaidi kwa mfano – literates rates kuongezeka, life expectancy kuongezeka, mortality rate kupungua, mapato ya wananchi kuongezeka, umaskini kupungua nk.


Muhimu hapa pia ni kwamba – serikali itakuwa inatengeneza mazingira ya uwepo wa ‘social mobility’ (movement ya wananchi kutoka kadi ya chini, kada ya kati na kada ya juu) kutokana na juhudi za wananchi badala ya ujanja ujanja, ‘nepotism’, upendeleo wa kiitikadi za vyama n.k.


Muhimu

Kila shughuli ya serikali katika uchumi wa nchi huwa ina athari kubwa kwenye Kodi wanazotozwa wananchi. Kwa mfano Afya bora (na sio bora afya) au elimu bora (na sio bora elimu) maana yake viwango vya Kodi lazima vipande. Lakini kama kodi husika zitakuwa zinaendana na ubora wa huduma zinazotolewa, ni rahisi kwa wananchi kuendelea kujituma kujenga uchumi wa nchi lakini pia, ‘tax compliance’kuwa juu kwa sababu faida za kufanya haya zinakuwa zikionekana wazi pale serikali yao inapo wajibika ipasavyo kwa maslahi ya wananchi walio wengi. Kuna umuhimu wa serikali kuzifanyia kazi changamoto zilizopo ambazo zinafanya ‘tax compliance’ level kuwa katika kiwango cha chini sana ikilinganisha na nchi nyingine kadhaa katika ukanda unaotuzunguka.


Kama tulivyogusia hapo juu, Serikali pia ina haja ya kurekebisha mfumo wake wa kodi ili kuhakikisha kwamba haiumuzi pande zote mbili – walio nacho na wasio nacho. Vinginevyo, iwapo mfumo wa kodi hauwatendei haki wananchi wa kada hizi. Kwa mfano – kwa upande mmmoja - kwa walio nacho ambao wamejijengea mafanikio ya kiuchumi kupitia juhudi zao binafsi na kwa njia halali wanaweza wakakosa incentives za kuchangia maendeleo ya uchumi. Pia walio nacho kurasimisha shughuli zao (na kuongeza mapato ya kodi kwa serikali, na pia kulinda maslahi ya wafanyakazii wao kwa kulipa michango kwenye mifuko ya kijamii), yote haya yatategemeana jinsi gani mfumo wa kodi upo ‘fair and just’.


Na kwa upande wa wasionacho, mfumo wa kodi ambao una wakandamiza unaweza kuwafanya waje na maamuzi yenye kuleta athari kubwa katika uchumi. Kwa mfano, Tanzania inaongoza Afrika Mashariki kwa utitiri wa kodi (‘nuisance taxes’). Kwa wastani, mtanzania analipa aina za kodi zinazokaribia hamsini (50), huku nchi nyingine zote za Afrika Mashariki zikiwa na idadi ndogo zaidi. Wasio nacho ni kada muhimu sana katika uchumi kusaidia serikali kutimiza malengo yake ya kukusanya kodi. Lakini kada hii ita ‘comply’ pale tu itakapokuwa na imani kubwa na serikali kwamba mfumo wa kodi ulipo ni ‘fair and just.


2.5 Resource Allocation

Hili ni jukumu la tatu la serikali katika uchumi. Maana rahisi ya dhana hii ni – assignment ya ‘limited resources’ (fedha/mapato ya kodi) kukidhi ‘unlimited needs’ (mahitaji yasiyo na kikomo). Katika mijadala mbalimbali bungeni, hoja hii hujadiliwa kwa lugha ya ‘kasungura kadogo’.


Moja ya njia zinazotumiwa na serikali katika kutekeleza jukumu hili ni pamoja na utoaji wa huduma za kiuchumi na kijamii kwa umma (public goods and services) kupitia kodi za wananchi. Miongoni mwa huduma hizi ni pamoja na Elimu (bora na sio bora elimu), Afya (bora na sio bora afya), Maji (safi na salama na sio tu maji), Usalama wa Raia na Mali zao (jeshi la polisi lisilofuata itikadi za vyama), ujenzi wa Miundo Mbinu nk.


2.6 Mgawanyiko wa Majukumu ya Serikali


Katika sehemu ya tatu, tumejadili majukumu makuu matatu ya serikali katika uchumi. Pia tumejadili nyenzo mbalimbali zinazotumika na serikali katika kufanikisha majukumu husika (Fiscal and Monetary Policies). Katika utekelezaji wa majumu yake, lengo kuu la serikali linapaswa kuzingatia umuhimu wa mambo makuu mawili:

· Efficiency -

Uwezo wa kuepuka ‘wastes’ – ikiwa ni pamoja na vitendea kazi, nguvu kazi, fedha, na muda.

· Effectiveness -

Uwezo wa kutekeleza majukumu na kufanikiwa kufikia malengo husika.


Katika sehemu inayofuata, tutajadili mgawanyo wa majukumu makuu matatu ya serikali tuliyoyaona awali baina ya ngazi za serikali. Mgawanyo huu utazingatia ‘efficiency’ na ‘effectiveness’ baina ya ngazi kuu mbili za serikali katika utekelezaji wa majukumu tajwa. Ngazi kuu za serikali ni mbili:


1. Serikali Kuu.

2. Serikali za halmashauri.


Awali tulijadili kwamba - Jukumu la Kwanza la serikali katika uchumi wa nchi ni ‘Stabilization of the Macroeconomic environment’ - (Uimarishaji/uthabiti wa Mazingira ya uchumi mpana wa nchi).


Tukiwa bado katika sehemu ya pili, katika bandiko linalofuata tutajadili - JE - Baina ya ngazi ya Serikali Kuu na ngazi ya Serikali za Halmashauri, ni serikali ya ngazi gani inapaswa kulisimamia jukumu hili kwa vigezo vya ‘efficiency and effectiveness’?


Pia tutaangalia, je ni ngazi gani inastahili kusimamia jukumu la pili la serikali katika uchumi – jukumu ya “Redistribution of income”.
 
2.6.1 JE - Baina ya ngazi ya Serikali Kuu na ngazi ya Serikali za Halmashauri, ni serikali ya ngazi gani inapaswa kulisimamia jukumu hili kwa vigezo vya ‘efficiency and effectiveness’?

Jukumu la ‘Stabilization of the Macroeconomic environment’ - (Uimarishaji/uthabiti wa Mazingira ya uchumi mpana wa nchi) linapaswa kusimamiwa na SERIKALI KUU. Kama tulivyojadili awali, viashiria vya uchumi mpana wa nchi vinahusisha vitu kama – kasi ya kukua kwa uchumi (GDP Growth Rate), mfumuko wa bei, viwango vya riba, viwango vya ajira na ‘current account deficit/balance of payments’.


2.6.1.1 Sababu za kuachia jukumu hili lisimamiwe na Serikali Kuu

Ngazi ya serikali kuu ina motisha (incentives) zaidi katika kusimamia masuala ya Fiscal & Monetary Policies (rejea juu kuhusiana na maana ya masuala haya). Hii ni kwa sababu kuu mbili – sababu ya kwanza ni kwamba serikali ngazi za halmashauri hazina the necessary macro economic instruments (rejea mjadala juu ya viashiria vya uchumi mpana huko juu) kutekeleza sera za uchumi mpana. Pili, serikali ngazi za halmashauri zinakabiliwa na vikwazo mbalimbali vya kusimamia fiscal and monetary policies, hasa kutokana na uwazi (openness) wa serikali na uchumi ngazi ya halmashauri. Hali hii itapelekea uwepo mkubwa wa ‘externalities’ – maamuzi ya serikali ngazi ya halmashauri yataathiri makundi ya watu ambayo serikali haikudhamiria yaathirike na hatua husika za serikali.


Ufafanuzi juu ya ‘openness & externalities’ katika muktadha wa uchumi wa halmashauri/manispaa:


Kwa vile uchumi wa manispaa/halmashauri upo wazi (open) kwa watu kutoka maeneo mmbalimbali ya nchi kuingia na kutoka kwa kadri wanavyopenda, serikali ngazi ya halmashauri ikiamua kwa mfano kusimamia suala la mfumuko wa bei kwa kiwango tofauti na maeneo mengine ya nchi na kupelekea gharama za maisha katika manispaa moja kuwa na utofauti mkubwa sana na kwingine, wananchi wengi kutoka halmashauri nyingine ambao hawakulengwa na sera hizi wataamua kuhamia katika halmashauri husika (externalities) na hivyo kuleta athari za kiuchumi ambazo zitabomoa kuliko kujenga.


Kwahiyo jukumu hili la ‘Stabilization of the Macroeconomic environment’ - (Uimarishaji/uthabiti wa Mazingira ya uchumi mpana wa nchi), linapaswa kubakia katika ngazi ya Serikali Kuu ili kuepuka athari hizi na nyinginezo.



2.6.2 Jukumu la Pili la Serikali katikaUchumi – ‘Income Redistribution’:


· Je baina ya Serikali Kuu na Serikali za Halmashauri, ni ngazi ipi inapaswa kusimamia jukumu hili kwa vigezo vya ‘efficiency and effectiveness’?


Jukumu hili pia linapaswa kubakia mikononi mwa serikali kuu. Awali tuliona kwamba nyenzo kuu ya Serikali katika kutekeleza jukumu la ‘income redistribution’ ni pamoja na KODI. Uzoefu unatuonyesha kwamba ‘tax bases’ nyingi zipo mobile. Maana ya ‘a mobile tax base’ ni vile vyanzo vya kodi ambavyo vinahamika kirahisi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.


2.6.2.1 Mifano ya ‘mobile taxes’ ni pamoja na:

- Corporate taxes’ kwa maana ya kwamba – iwapo sehemu moja ya nchi (kijiografia) inatoza kiwango cha kodi ya aina hii tofauti na sehemu nyingine za jiografia, ni rahisi kwa makampuni mbalimbali kuamua kuhamia kwenye ‘low tax rate jurisdictions’.

- Mfano mwingine wa mobile tax bases ni pamoja na - Personal taxes, taxes on capital and income taxes.

2.6.2.2 Mifano ya kodi zisizo ‘mobile’ ni pamoja na:

- Kodi ya majengo/property taxes. Majengo hayahamishiki.

- Natural resources taxes. Rasilimali ni kitu ambacho hakihamishiki. Mfano dhahabu, shaba, chuma, gesi, mafuta, vivutio vya wanyama nk.

- Kodi za mazao/Commodity taxes – uzalishaji wa mazao mengi huwa unaendana na hali ya kimazingira, kijiografia nk, suala ambalo linapelekea uzalishaji husika usiweze kuhamia sehemu nyingine kwa urahisi kwa sababu tu ya mabadiliko ya viwango kodi. Kwa mfano (Ceteris Paribus), sio rahisi kwa zao la Korosho kustawi Singida, au zao la Pamba kustawi Pwani, nk nk.


Hitimisho katika hili:

Ikiwa lengo/sera la serikali kupitia kodi ni kupunguza pengo baina ya walio nacho na wasio nacho - ‘income redistribution’, halafu jukumu hili likaachiwa serikali ngazi ya halmashauri, itakuwa ni rahisi kwa ‘walio nacho’ kuhamia kwenye halmashauri/manispaa ambayo/zo zitakuwa zinatoza viwango nafuu vya kodi na kuleta athari zifuatazo:


Wasio nacho watakimbilia kwenye halmashauri/manispaa yenye kodi nafuu ili kufaidika na viwango vidogo vya kodi pamoja na huduma zitokanazo na kodi husika. Hali hii itapelekea ‘over load’ kwa upande wa ‘matumizi’ ya halmashauri watazohamia, na hivyo kuzifanya zilemewe kibajeti;


Kwa upande wa ‘walio nacho’, hali hii itawafanya wahamie kwenye halmashauri/manispaa zenye unafuu wa kodi. Kwa vile hawa ni vyanzo muhimu vya mapato, kuhama kwao kutapelekea ‘starvation of revenues’ kwa manispaa watazozikimbia.


Athari nyingine pia ni kwamba, kuachia jukumu la ‘income redistribution’ liwe chini ya serikali ngazi za halmashauri itapelekea ushindani wa viwango nafuu vya kodi baina ya halmashauri/manispaa mbalimbali. Athari ya hili ni kwamba, net gain (kwa ujumla wake) ya serikali kimapato (kodi) itakuwa ni chini.


Katika bandiko linalofuata tunaendelea kujadili mgawanyo wa majukumu baina ya serikali kuu na serikali za halmashauri kwa kuangalia jukumu la tatu ambalo ni “Allocation of resources.
 
2.6.3 Jukumu la Tatu la Serikali katika Uchumi – ‘Resource Allocation’:


· Je baina ya Serikali kuu na Serikali ngazi ya halmashauri, ni ngazi ipi inapaswa kusimamia jukumu hili kwa vigezo vya ‘efficiency and effectiveness’?


Katika majukumu yote matatu ya Serikali katika Uchumi, jukumu la “Resource Allocation” ndio jukumu pekee ambalo linapaswa kuwa chini ya Serikali ngazi za halmashauri. Kama tutakavyojadili punde, Suala hili linaendana na dhana ya ‘fiscal decentralization’. Katika sehemu inayofuatia, tutajadili kwa kina juu ya sababu kwanini jukumu la ‘resource allocation’ linapaswa kutekelezwa na serikali ngazi ya Halmashauri/Manispaa, na Sio Serikali Kuu:

· Kwanza, fiscal decentralization (kusogeza majukumu na maamuzi ya kibajeti ngazi za chini za serikali/kwa wananchi) inasaidia kuondokana na utamaduni wa serikali kuu kwa miaka mingi ambao umehusisha– ‘extraction of resources’ (hasa kodi) kutoka ngazi za chini (hasa small peasants) na kuzitumia bila ya faida zozote za kiuchumi na kijamii katika ngazi ambazo kodi husika hutoka. Hatua ya kukabidhi jukumu la resource allocation ngazi za serikali za halmashauri linapelekea ‘resources’ nyingi zaidi zibakie katika serikali ngazi za chini ili kusaidia utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo kwa faida ya wananchi wa ngazi husika, na kwa matokeo ambayo yanaweza kuonekana au kufuatiliwa kwa urahisi.

· Pili, kusogeza jukumu hili la ‘resource allocation’ ngazi ya serikali za halmashauri inapelekea kushamiri kwa shughuli nyingi za kiuchumi na kijamii ngazi za halmashauri (economic and social activities). Hali hii inasaidia kuzipatia halmashauri uwezo wa kutengeneza fursa mbalimbali kwa wananchi wenye ujuzi/utaalam (technological, managerial, leadership) na kuwafanya wabakie katika ngazi za chini badala ya kukimbilia fursa zilizopo katika ngazi ya serikali kuu (hasa mijini). Hali hii itasaidia kupunguza tatizo la urban – rural migration na pia tatizo la ‘brain drain’, hivyo kuongezea halmashauri uwezo (capacity) kusimamia masuala ‘yao wenyewe’ na pia nafasi ya kuongoza shughuli na mikakati ya maendeleo wao wenyewe. Moja ya changamoto kubwa zinazozikabili halmashauri zetu ni pamoja na uhaba wa wataalam wenye ujuzi wa aina mbalimbali (technological, managerial, leadership nk).

· Tatu, kusogeza jukumu hili la ‘resource allocation’ ngazi ya serikali za halmashauri inasaidia halmashauri zetu kuja na mipango na mikakati kwa ajili ya maendeleo yao wenyewe kwa jinsi wanavyoona inafaa. Katika hali hiyo, halmashauri zetu zitaweza ‘identify’ fursa zilizopo katika mazingira yao, wataweza identify rasilimali zinazo wazunguka na pia identify ‘competitive advantage on which development can be based. Suala hili litapelekea maendeleo kuwa ‘locally driven’ badala ya kuwa driven and determined by external agents (kwa mfano bureucrats serikali kuu) ambao mara nyingi huwa wapo pre-occupied na vipaumbele vingi na lakini pia wasio na uelewa wa kutosha kuhusu potential local development katika halmashauri zetu mbalimbali.

· Nne, mipango shirikishi ya maendeleo (participatory development projects) inawezekana zaidi iwapo michakato inahusisha wadau mbalimbali kuja na ‘collective vision’ kwa ajili ya ‘local development’, ambapo pia wanaweza kuja na makubaliano juu ya ‘common goals’ pamoja na mikakati ya kufanikisha malengo husika. Tafiti nyingi zinzendelea kuonyesha kwamba ‘participation of local communities’ katika mikakati ya maendeleo husaidia sana kupunguza kasi ya umaskini.

· Tano, mahitaji ndani ya taifa hayalingani. Kwa mfano, kutokana na sababu mbalimbali, zipo sehemu (halmashauri) ambazo kipaumbele kinaweza kuwa ni elimu, na kwingine kikawa ni afya au usalama wa raia na mali zao nk. Kila halmashauri ina ‘tastes, preferances, priorities, needs’ ambazo sio lazima zifanane na kwenye maeneo mengine.

· Sita, ni kufuatana na dhana ya ‘economies and diseconomies of scale. Serikali kuu inaweza kujikuta inatoa au kuzalisha huduma ‘at an increasing cost per unit produced’ kutokana na changamoto mbalimbali kwa mfano za kijiografia (umbali), population density nk. Katika hali hii, serikali ngazi ya halmashauri inaweza kuwa katika nafasi nzuri na bora zaidi ya kuzalisha au kutoa huduma huku ‘per unit cost’ ikishuka kwa jinsi service provision inavyoongezeka.

· Saba, tax compliance inaongezeka kwa sababu taxes are felt locally.

· Nane, inakuza uwajibikaji (accountability)

Serikali za halmashauri zipo karibu zaidi na walengwa wa miradi ya maendeleo/wananchi. Serikali ngazi hizi zipo better equipped to extract information on local preferances and needs kwa ufanisi zaidi kuliko serikali kuu. Pia serikali ngazi za halmashauri zinaweza kuwajibika vizuri zaidi to local residents kuliko serikali kuu.

· Tisa, uimarishaji wa Demokrasia

Kwa kuwapatia wananchi ‘sauti’ katika maandalizi na utekelezaji wa mikakati, sera na miradi mbalimbali ya maendeleo, wananchi wanaweza kufaidika from greater choice in the goods and services delivered to them.

Tuangalie Sekta ya Elimu kama ‘Case study’ ya Jukumu hili:

Kitaifa, serikali kuu ina wajibu wa kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na nguvu kazi yenye elimu na ujuzi unaohitajika katika kusukuma gurudumu la uchumi na maendeleo kwa kufuatana na mahitaji ya uchumi na dunia ya leo.

Lakini vile vile katika ngazi za halmashauri, nguvu kazi yenye sifa hizi inahitajika pia. Tafiti mbalimbali zinaonyesha kwamba katika ngazi za serikali za mitaa, ‘absorption capacity’ katika usimamizi na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inakabiliwa na vikwazo vikubwa kama vile uwezo mdogo to attract, recruit and retain qualified and professional staff.

Katika suala la huduma ya kijamii kama Elimu, utoaji wa huduma hii unaweza ukawekwa katika ‘sub functions’ kadhaa baina ya serikali kuu na serikali za halmashauri:

· Gharama za kifedha/bajeti – jukumu hili linapaswa kuwa ni la serikali ngazi ya halmashauri, hasa ‘capital expenditures.’

· Kutengeneza mitaala – jukumu hili linapaswa kuwa ni la serikali kuu lakini ‘supplemented’ na mitaala kutoka katika ‘local areas’

· Certification ya walimu – jukumu hili linapaswa kubakia ngazi ya serikali kuu ili kuweka ‘standard’.

· Kuajiri watumishi (elimu), mipango na malipo ya mishahara na kuwawajibisha (kwa mfano kuwasimamisha kazi) – jukumu hili linapaswa kuwa chiji ya serikali ngazi ya halmashauri.

· Vitabu (textbooks) – jukumu hili linapaswa kusimamiwa na serikali ngaz za halmashauri.




1. Sehemu ya Tatu: Mamlaka ya Kodi na Mapato katika ngazi za Serikali Kuu na Serikali za Halmashauri - (Taxation and Revenues Powers).


Katika sehemu iliyotangulia, tulijadili mgawanyo wa majukumu kati ya serikali kuu na serikali ngazi za halmashauri kwa kuzingatia vigezo vya ‘efficiency and effectiveness. Katika sehemu inayofuata, tutajadili ‘taxation and revenue powers’ katika ngazi hizi mbili za serikali. Pamoja na mengineyo, tutatazama urali “Fiscal Imbalances” katika ngazi hizi mbili na jinsi gani changamoto zake zinapaswa kutatuliwa kwa ushirikiano baina ya ngazi mbili kuu za Serikali.


Serikali ngazi ya halmashauri zina umuhimu wa kipekee katika utoaji wa huduma za kijamii na kiuchumi kwa wananchi. Halmashauri zetu zinakusanya karibia asilimia tano ya mapato yote ya ndani ya serikali. Lakini serikali katika ngazi hizi zinawajibika kwa zaidi ya asilimia ishirini ya matumizi yote ya huduma za kiuchumi na kijamii kwa wananchi. Pengo husika huwa linazibwa na ‘fiscal transfers’ kutona serikali kuu (tutajadili hili kwa undani baadae).


Serikali zetu ngazi za halmashauri zinakabiliwa na changamoto kubwa za kifedha, na miongoni mwa changamoto hizi ni pamoja na ‘unpredictable fscal transfers’ kutoka serikali kuu, ambazo ni muhimu katika kuziba ‘the fiscal gap/imbalance’ tuliyojadili huko juu. Hali hii umepelea uwepo wa huduma duni za kiuchumi na kijamii kwa wananchi.


Iwapo serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais JP Magufuli imenuwia kuwaletea wananchi mabadiliko ya kweli katika maisha yao, serikali kuu inapaswa kuleta na kusimamia ‘a sound framework’ kwa ajili ya mfumo wa fedha za halmashauri zetu ili kuleta ufanisi katika matumizi na utoaji huduma za kiuchumi na kijamii kwa wananchi.

clip_image001.gif


Iwapo serikali za halmashauri zinapewa uwezo wa kujitegemea kimapato kwa nia ya kujenga nidhamu ya fedha za umma, decentralization italeta faida kubwa kwa maana ya ufanisi na uwajibikaji na kupunguza gharama/hasara zinazojitokeza katika serikali ngazi za halmashauri kutokana na matukio katika uchumi mpana kisera, muktadha ambao haupo mikononi mwa serikali ngazi ya halmadhauri.


Kanuni ya ‘Fiscal Equivalence’

Njia bora ya kuleta ufanisi na uwajibikaji katika kuhudumia wananchi ni pampja kuhakikisha kwamba serikali inatekeleza kanuni ya ‘Fiscal Equivalance’ kwa kadri inavyowezekana. Kwa mujibu wa kanuni hii, ngazi ya serikali yenye majukumu ya matumizi Fulani - kiuchumi na kijamii kwa wananchi, ni inapaswa pia kuwa na majukumu ya kutafuta mapato kwa ajili ya matumizi hayo. Vinginevyo ikitokea kwamba ngazi moja ya serikali ikawa na matumizi makubwa kuliko kiwango inachopaswa kuwajibika kukusanya (kodi/mapato), athari zake ni pamoja na ‘externalities’ ambalo tulijadili huko juu.


Hivyo basi serikali kuu na serikali ngazi ya halmashauri zinapaswa kugawana vyanzo vya mapato, na mgawanyo huo uzingatie ‘mobility of tax bases’ ambapo kama tulivyo kwisha jadili, mobile tax bases zinapaswa kusimamiwa na serikali kuu na immobile tax bases zinapaswa kusimamiwa na serikali ngazi ya halmashauri. Lakini pia, ngazi hizi mbili za serikali zinaweza kugawana mapato kutoka kwenye ‘mobile tax bases’ kwa uwiano utaokubalika. Tutaona hili baadae.


Katika bandiko linalofuatam tutajadili:


Urali [“Fiscal Imbalances”] katika ngazi za Manispaa/Halmashauri na jinsi ya kutatua changamoto husika.
 
3.1 Urali [“Fiscal Imbalances”] katika ngazi za Manispaa/Halmashauri na jinsi ya kutatua changamoto husika.


Urari (fiscal imbalances) katika ngazi za manispaa/halmashauri maana yake ni uwepo wa ‘a mismatch between functions and finances. Hali husababishwa na vitu viku viwili:


- Vertical imbalances

- Horizontal imbalances


3.1.1 Vertical Imbalances

Urari huu hujitokeza pale serikali ngazi za chini (Halmashauri) inapokosa uwezo wa kukusanya mapato ya kutosha kuwiana na majukumu yake ya matumizi. Katika hali ya kawaida, serikali kuu huwa na ‘tax bases’ zenye uwezo wa kukusanya mapato makubwa na mengi zaidi kuliko serikali ngazi za halmashauri na manispaa. Tax bases kubwa katika uchumi wa nchi mara nyingi huwa ni pamoja na - VAT, Corporate Income tax, trade taxes nk.


Urari huu (Vertical Fiscal imbalance) linaweza kuzibwa kwa njia kuu mbili:


-Revenues sharing

-Grants.


Revenue Sharing

Revenue sharing ni njia moja wapo ambayo serikali inaweza kuitumia kuziba urari (vertical fiscal imbalance). Hili linaweza kufanyika kwa njia ya serikali kuu kuzipatia serikali ngazi za halmashauri sehemu (‘gawio’) ya kodi zinazokusanywa na serikali kuu katika maeneo (jurisdictions) ya Manispaa/Halmashauri husika. Kwa mfano kodi zinazohusisha au mapato yatokanayo na mauzo ya rasilimali kama vile madini, mafuta, gesi nje ya nchi; mapato yatokanayo na vivutio vya utalii; lakini vile vile kodi/mapato yatokanayo na mauzo ya ‘primary commodities’ nje ya nchi kama vile mazao ya biashara nk. Revenue sharing inaweza kufanywa ‘on tax to tax basis’ au kwenye ‘pool’ yote ya mapato ya serikali kuu.


Grants

Hizi ni fedha (non – repayable) zinazotolewa na serikali kuu kwenda katika serikali ngazi ya halmashauri/manispaa. Zipo aina tatu ya grants:

- Unconditional grants – ambapo hutolewa na serikali kuu kwa ujumla wake kwenda serikali ngazi za halmashauri kwa lengo la kututua urari (fiscal imbalance) bila ya masharti juu ya jinsi gani fedha hizo zitumike.

- Conditional grants – hizi pia hutolewa na serikali kuu kwenda ngazi za serikali za halmashauri. Grants za aina hii huambatana na masharti juu ya jinsi gani zitumike. Masharti hayo yanaweza pia kuhusishwa na ‘performance’ ya miradi iliyolengwa.

- Equalization – Tofauti na (conditional & unconditional grants) ambazo zinahusisha serikali kuu na serikali ngazi za halmashauri, ‘equalization grants’ zinahusisha zaidi ‘fiscal imbalance’ baina ya halmashauri/manispaa moja na manispaa nyingine. Lengo kuu hapa ni kuhakikisha kwamba halmashauri zote zinatoa ‘a national standard level of public goods & services’.


Horizontal Imbalances

Horizontal imbalances ni zile zinazojitokeza baina ya halmashauri moja na halmashauri nyingine. Hii ni tofauti na Vertical imbalance tulizoona awali, ambazo zinahusisha ‘imbalance’ baina serikali kuu na serikali ngazi za halmashauri.


Urari wa aina hii (Vertical Imbalances) hujitokeza kwa sababu zifuatazo:

- Maeneo ya kijiografia katika nchi huwa hayafanani kwa maana ya – uwepo wa rasilimali (natutal resources), aina ya vyanzo vya mapato/kodi, uwezo wa wananchi kiuchumi (hasa taxable income), na pia utofauti wa mahitaji (huduma za kijamii na kiuchumi) baina ya jamii moja na nyinginezo. Kwa mfano, mara nyingi ‘tax base per capita’ baina ya halmashauri za mijini na zile za mijini huwa zinatofautiana sana.

- Pia mahitaji ya huduma za kijamii na kiuchumi huwa zinatofautiana kwa sababu sehemu Fulani ya nchi inaweza kuwa na idadi kubwa zaidi ya watoto wenye umri wa kwenda shule, idadi kubwa zaidi ya watu wazima, exposure ya aina Fulani ya magonjwa kutokana na mazingira husika nk, tofauti na maeneo mengine. Lakini pamoja na uhalisia huu, unakuta serikali bado ‘treats the most unequal jurisdictions in a universal manner’ (one size fits all approach). Kama tulivyoona awali, kila ‘locality’ (mfano halmashauri) ina - tastes, preferences, needs & priorities ambazo haziwezi kufanana na za maeneo mengine. Kutokana na uhalisia huu, manispaa hazitakiwi kuwa treated in a uniform and homogenous manner.

- Pia ‘tax bases’ baina ya halmashauri moja na nyingine zinaweza kutofautiana. Kwa mfano, Halmashauri zenye relatively small tax base haziwezi kuziba fiscal imbalance kwa kuongeza viwango vya kodi kwani kama tulivyokwisha ona, kwa sababu hali hii inaweza ikapelekea biashara (makampuni), wananchi na hata wataalam wengi kuhamia kwenye halmashauri zenye kodi nafuu.

- Gharama za kutoa huduma za kijamii na kiuchumi haziweza kufanana baina ya halmashauri moja na nyingine. Hii ni kwa sababu pamoja na mengineyo, halmashauri zinaweza kutofautiana in terms of ‘population density’, ‘geographic location’, nk. Kama tulivyojadili awali, masuala haya yanaweza kupelekea utoaji wa hudumu kufanyika at an increasing cost per unit produced badala ya at a decreasing per unit cost kwa kadri utoaji hudumu unavyoongezeka.

Jinsi ya Kutatua Horizontal Imbalances

Solution on horizontal imbalances inahitaji kuhusisha ‘equalization’ kwa maana ya kwamba halmashauri zenye uwezo mkubwa wa kiuchumi zinatakiwa kufanya fiscal transfers kwenda kwenye halmashauri zenye uwezo mdogo kiuchumi, na kushindwa kukidhi mahitaji yake ya kijamii. Equalization formula haina budi kuzingatiwa kwa kupima ‘fiscal needs’ na ‘fiscal capacity’ za kila halmashauri/manispaa.

Lakini mara nyingine imbalance inaweza isiwe katika ngazi ya halmashauri moja na nyingine, badala yake ikawa ni ‘income inequality’ ndani ya halmashauri moja (baina ya wakazi au jamii Fulani ndani ya halmashauri husika). Katika hali hii, matumizi ya ‘equalization’ formula hayawezi kuleta the desired results. Katika hali hii, kinachohitajika ni ‘targeting’ ya makundi mbalimbali yanayohitajika kusaidiwa ndani ya jamii.

Iwapo jamii (communities) zitapewa mamlaka makubwa to influence serikali zao ngazi ya halmashauri, kutakuwa na uwezekano mkubwa wa sehemu kubwa ya local public funds kutumikia zaidi maskini.



Katika sehemu inayofuata, tutajadili deni la taifa kwa kuligawanya kati ya deni la ndani na deni la nje.
 
Sehemu ya Nne:


4.1 Deni la Taifa


Katika Sura ya TATU, tulijadili sababu mbalimbali zinazopelekea nchi kuwa na deni la taifa, hasa deni la nje. Tuliona kwamba Deni la Taifa ni matokeo ya uwepo wa ‘Current Account Deficit’ katika uchumi wa nchi. Hali hii inapelekea nchi kurundika ‘external liabilities’ kwa sababu ya ulazima wa kugharamia nakisi yake (deficit) kwa kutegemea vyanzo vya fedha kutoka nje ya nchi. Haya ni matokeo ya nchi kukabiliwa na uhaba wa vyanzo vya fedha za ndani kwa ajili ya kugharamia shughuli za uchumi, huduma za kijamii, kuendesha serikali nk.


4.1.1 Sura ya Deni la Taifa - Tanzania


Kwa mujibu wa ripoti ya Benki kuu (BOT) ya Mwezi February 2016, kufikia Mwezi January 2016, Jumla ya Deni la taifa (ndani na nje ya nchi) lilikuwa ni Dola za Kimarekani 19.5 Billion.

Kwa exchange rate iliyotumika katika ripoti husika ($1=TZS 2150), hii ni sawa na takribani TZS Trilioni Arobaini na Mbili (TZS 42 trillion), katika mgawanyiko wa maeneo makuu mawili

4.2.1 Deni la ndani.

Kufikia mwezi Januari 2016, jumla ya deni la NDANI ilikuwa ni Dola za kimarekani takribani Bilioni NNE (Sawa na karibia TZS Trillioni tisa). Hii ni sawa na asilimia 21 ya jumla ya deni lote la taifa.

4.2.2 Deni la nje.

Kufikia mwezi Januari 2016, jumla ya deni la NJE ilikuwa ni Dola za kimarekani 15.4 Billion (sawa na takribani TZS Trilioni 33). Hii ni sawa na asilimia 79 ya jumla ya deni lote la taifa.


Ili tupate uelewa wa kina juu ya athari za deni la taifa kwa uchumi wa “NCHI” na uchumi wa “WANANCHI” (walipa kodi), uchambuzi wa deni la hunafanywa tofauti na uchambuzi wa deni la nje. Tutafanya hivyo katika sehemu inayofuata:


4.2.2.1 Deni la Ndani:

Deni hili husimamiwa na Benki Kuu ya nchi (BOT), na kuendeshwa kwa sarafu ya ndani tu (local curreny only). Ni deni la muda mfupi (mara nyingi kati ya siku 35 na miaka 15 kutegemeana na aina za debt instrunments – tutaona baadae kwa undani), huiva kipindi kifupi, na riba zake huwa ni za juu. Kwa vile Deni la ndani huiva ndani ya muda mfupi/malipo yake huitajika kufanywa ndani ya kipindi kifupi, iwapo inatokea deni hili kuana kuelemea uchumi wa nchi, mara nyingi waathirika ni walipa kodi wa kikazi kilichopo.

Deni la ndani linahusisha amana za serikali (government securities) zinazouzwa kwenye soko la ndani la deni la taifa (Domestic Debt Market) kupitia minada maalum inayoratibiwa na Benki Kuu (BOT).

Kwa maana hii:

Deni la ndani ni fedha tunazodaiana wenyewe ndani ya taifa (tuajadili kwa undani punde). Malipo yake amana zinapoiva ni lazima yabaki katika zunguko wa ndani ya uchumi wa nchi kwa manufaa ya nchi na wananchi/walipa kodi.

Deni la ndani linapaswa kushirikishwa jamii kwa wigo mkubwa iwezekanavyo kwa maana ya ushiriki wa wananchi katika soko la ndani la deni (Domestic Debt Market). Kwa sasa, ushiriki wa umma katika soko hili ni mdogo sana. Soko limehodhiwa na benki za kibiashara.

4.3 Mgawanyiko wa Deni la Ndani:

Deni la ndani linahusisha amana mbali mbali za serikali ambazo zimegawanyika katika makundi makuu mawili:

· Marketable Government Securities

· Non – Marketable Government Securities


4.3.1 Marketable Securities.

4.3.1.1 Treasury Bills:

Treasury Bills ni aina ya kwanza ya ‘Marketable Securities’. Zipo ambazo zinaiva (matures) katika kipindi cha (Siku 35, 91, 182, na 364).

4.3.1.1.1 Pricing Assumptions

Miaka mitatu iliyopita (2013), Yields za Treasury Bills zilikuwa takribani 13%. Kwa mwaka huu wa 2016, zimefikia 18%. Kutokana na amana hizi kuwa ‘lucrative’, Mabenki mengi ya biashara yamekuwa ndio wanunuzi wakubwa wa amana hizi, suala ambalo lina athari kubwa katika uchumi wa ndani, hasa uchumi wa wananchi (tutajadili kwa undani).


4.3.1.2 Treasury Bonds:

Treasury Bonds ni aina ya pili ya ‘Marketable Securities. Katika kundi hili, kuiva kwake (maturity) pia hupishana, kwa mfano zipo za (Miaka 2, 5, 7, 10, na 15).

4.3.1.2.1 Pricing Assumptions

Hizi pia ‘yields’ zake ni za juu. Kwa mfano, katika kipindi cha hivi karibuni:

· Kwa Treasury Bonds za miaka miwili, ni karibia 17%.

· Kwa Treasury Bonds za miaka saba, ni karibia 16%.

4.3.2 Non – Marketable Securities.

4.3.2.1 Special Bonds & Stocks.

Non marketable securities ni special bonds and stocks ambazo zinakuwa issued for ‘recapitalization’ ya CRDB, NMB na PPF pamoja na accumulation ya BOT’s advance kwa serikali ambazo zimekuwa converted into ‘special bonds’.


4.4 Mgawanyiko wa Deni la ndani (by ‘Debt Instrunments’) – TZS Trilioni karibia Tisa:

· Treasury Bonds 63.3% (Sawa na Karibia TZS Trilioni 5.7 ya deni lote la ndani).

· Treasure Bills 32.8% (Sawa na karibia TZS Trilioni 2.9).

· Government Stocks 2.9% (Sawa na karibia TZS Bilioni 262).

· Non – Securitized Debt 1% (Sawa na karibia na TZS Brilioni 900).



Katika sehemu inayofuata, tutajadili,

Je, ni akina nani wanashikilia Deni letu la ndani la taifa?
 
4.5 Je, ni akina nani wanashikilia Deni letu la ndani la taifa?

4.51 Mgawanyiko wa Deni la Taifa (By ‘Holder Category) Iwapo tunajumuisha marketable & non marketable instrunments:

- Mabenki ya Biashara (51%) Takribani TZS Trilioni 4.5

- Mifuko ya Pensheni (16.1%) Takribani TZS Trilioni 1.4

- Benki Kuu (18%) Takribani TZS Trilioni 1.6

- Mifuko ya Bima (7.2%) Takribani TZS Bilioni 648

- Others (3.4%) Takribani TZS Bilioni 306


Lakini kama tulivyokwisha jadili, Non marketable securities ni special bonds and stocks ambazo zinakuwa issued for ‘recapitalization’ ya CRDB, NMB na PPF pamoja na accumulation ya BOT’s advance kwa serikali ambazo zimekuwa converted into ‘special bonds’. Kwa maana hii, tukiondoa ‘non marketable instrunments’, sura ya deni la taifa nikama ifuatavyo:


- Benki Za Biashara (60%)

- Mifuko ya Pensheni (21%)

- Mifuko ya Bima (10%)

- Benki Kuu (3%)

- Wengineo (Taasisi zisizo za kifedha, watu binafsi nk), kiasi kilichobania.


4.5 Contingent Liabilities

Mbali na madeni haya tuliyojadili (deni la ndani na deni la nje), pia kuna contingent & actual liabilities ambazo sio mara zote zinajumuishwa katika jumla kuu ya deni la taifa ingawa mwisho wa siku zinaishia kuwa ni madeni ya serikali yanayopaswa kulipwa na kodi za wananchi.


4.5.1 Contingent Liabilities

Kwa miaka ya hivi karibuni, ‘government guarantees’ zimekuwa zikitumika kama vyanzo vya fedha kutoka Mifuko mbalimbali ya pensheni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Hizi ‘Guarantees’ zimepelekea ongezeko kubwa na la ghafla la ‘contingent liabilities’ kwa upande wa serikali, suala ambalo linaongeza ‘fiscal burden’ katika mfumo wa sasa wa bajeti taslimu (cash budget). Government Contingent Liabilities ni pamoja hizi zifuatazo:

· Guarantees issued na serikali kusaidia mashirika ya umma kifedha.

· Guarantee Schemes kwa Sekta binafsi (makampuni binafsi ya ndani) binafsi kuzisaidia zipate mikopo.


Hizi ni contingent liabilities kwa serikali kwa sababu mwisho wa siku, mdaiwa asipolipa, ni serikali ndio inayowajibika kupitia kodi za wananchi.


Mbali ya hizi contingent liabilities zitokanazo na ‘government guarantees, zipo contingent liabilities nyingine kwa mfano:

· Unpaid government employment contributions kwenda mfuko wa PSPF. Hizi zinakadiriwa kufikia TZS trilioni NNE. Kati ya hizi, inasemekana kwamba kufikia 2013, TZS trilioni 1.2 zilikuwa zimeshalipwa kwa wastaafu wa serikali na PSPF, na TZS trilioni 2.8 ni madai ambayo yalikuwa yanasubiriwa kuhakikiwa na Serikali.

Kati ya hizi trilioni 2.8, kiasi kilichohakikiwa kufikia Mwaka 2013 kilikuwa ni TZS trilioni 1.22 (sawa na 42%), lakini zilizokuwa zimelipwa zilikuwa ni TZS bilioni 60 tu, na kuacha outstanding DEBT kuendelea kuwa kubwa.


Kwa mujibu wa Medium Term Debt Management Strategy (2013) kiwango cha contingent liabilities (Government Exposure) kufikia June 2013 kilikuwa ni TZS Trilioni 3.73. Kati ya hizi:


TZS Trilioni 2.8 zilikuwa ni contingent liabilities zilizohusiana na Unpaid government employment contributions kwenda mfuko wa PSPF.

TZS 645 Billioni zilikuwa ni contingent liabilities zilizotokana na government guarantees kusaidia mashirika ya umma kifedha.

· TZS 266 Bilioni zilikuwa ni contingent liabilities Makampuni binafsi kupitia ‘credit guarantee schemes’ kuzisaidia kupata mikopo.


Contingent Liabilities mara nyingi huwa hazihusishwi moja kwa kwa moja na deni la taifa, suala ambalo sio sawa kwani kama tulivyodokeza hapo juu, ‘any defaults’ hupelekea serikali kutumia fedha za walipa kodi kulipa such liabilities hizi. Ushahidi katika hili ni jinsi serikali ya awamu ya tano inavyoendelea kutenga fedha nyingi za walipa kodi kila mwezi kulipa such contingencies.


Kwa mujibu wa mkakati wa deni la Taifa (2002), mkakati huu unalenga kuhakikisha kwamba serikali inakopa kwa gharama nafuu na bila ya kuathiri mazingira ya kisera ya uchumi mpana (monetary policies) au kuathiri sekta ya fedha/kibenki ndani ya nchi. Kwa mfano, moja ya mikakati ya kufanikisha haya ni pamoja na kuhakikisha kwamba ‘Net Domestic Finance’ as percentage of GDP haivuki 1% (pia IMF inahimiza hili). Hii ni kwa sababu deni la taifa (ndani) likizidi 1% ya GDP, matokeo yake ni sekta binafsi ndani ya uchumi kukabiliwa na uhaba wa mikopo (crowding out effect).

Lakini kama tulivyokwisha jadili, kutokana na yileds zake kuwa kubwa (18%), amana za serikali zimekuwa ni kivutio kikubwa sana kwa mabenki ya kibiashara ambapo karibia robo tatu ya wanunuzi wa amana hizi ni mabenki ya biashara nchini, kwa mfano benki ya CRDB nk. Tumeona kwamba ushiriki mkubwa wa taasisi za kifedha katika soko la ndani la deni la taifa umekuwa ukienda sambamba na ushiriki ‘finyu’ wa wananchi.

Tukichukulia sura ya bajeti ya mwaka ujao wa fedha kama mfano (2016/17), Serikali inatarajia kukopa TZS Trilioni 5.4 kutoka katika soko la ndani. Tukichukuliwa pato la taifa kwa sasa (GDP) kufikia karibia TZS Bilioni 100, mkopo wa ndani kufikia kiwango cha TZS trilioni 5.4 maana yake Net Domestic Finance ni takribani 5%, kiwango ambacho ni kama mara tano zaidi ya kiwango kinachotakiwa (sio zaidi ya 1%) kwa mapendekezo ya IMF. Kiwango cha 1% kinawekwa kwa kusudio la kuzuia ‘crowd out effect’ ya private/SME sector katika kupata mikopo ya kibenki. Lakini kwa kiwango hiki cha 5%, itakuwa ni vigumu kwa serikali kushirikisha sekta binafsi nchini katika mkakati wake wa uchumi wa viwanda kwa sababu sehemu kubwa ya ‘domestic credit’itakuwa inatolewa na mabenki ya biashara kwa serikali kuliko domestic SME sector/private sector.

clip_image001.gif


Mkakati wa Deni la Taifa (2013) unalenga kuhakikisha kwamba muda wa maturity (kuiva) kwa madeni ya ndani unasogezwa mbele zaidi. Upo mkakati huu pia wa kuhakikisha kwamba deni la ndani linahusisha zaidi amana (securities) zinazoiva kipindi kirefu kijacho. Lengo katika haya ni kuhakikisha kwamba Serikali inapunguza kasi ya matumizi ya kodi za wananchi kwenda kulipa madeni mara kwa mara badala ya kutumika kutoa huduma muhimu kwa wananchi. Lakini katika hili pia, tumeona matokeo yakiwa ni kinyume. Kwa mfano, kwa mwezi January – Aprili 2016, serikali imetumia sehemu kubwa sana ya mapato ya kodi kulipa madeni yanayoendelea kuiva kuliko kiasi kilichoenda kwenye huduma za kijamii, miradi ya maendeleo nk.



Katika sehemu inayofuata tutajadili (risks) hatari mbalimbali kuhusiana na deni la ndani.
 
4.6.1 Risks


Risks

Kuna risks kadhaa kuhusiana na debt portifolio ya Tanzania. Lakini katika sehemu hii, tutaangalia risk moja ambayo ni ‘interest rate risk. Baadae tutaangalia risks nyinginezo kama vile exchange rate risks nk.

Refinancing Risk

Refinancing Risk - maana yake ni uwezekano wa deni kuwa ‘rolled over’ (kutolewa tena upya) baada ya deni kuiva kabla halijalipwa lote. Kwa kawaida, mkopo unapochukuliwa mara ya kwanza huwa unakuja na makubaliano juu ya riba itakayoendana na mkopo husika. Mkopo mzuri ni ule ambao utakuja na ‘fixed interest rate’ badala ya ‘variable/floating interest rate’. Hii ni kwa sababu, chini ya ‘fixed rate’, payment obligations zitaendelea kuwa katika riba ile ile chini ya makubaliano ya awali bila ya kujalisha baadae mabadiliko gani yatakajitokeza katika uchumi wa nchi na kupelekea viwango vya riba kupanda. Kwahiyo iwapo inatokea kwamba Deni linaiva kabla ya malipo kumalizika, ‘creditor’ na serikali wanaweza kuingia katika makubaliano ya kusogeza deni mbele, suala ambalo ‘creditor’ anaweza kuamua kukubali au kukataa.

Iwapo inatokea ‘roll over of debt’, such a ‘roll over’ itaambatana na kiwango kipya cha riba ambacho kwa kawaida huwa ni cha ghali zaidi kuliko kile cha awali. Na iwapo creditor ataamua kufanya ‘roll over’ kwa ‘variable or floating interest rate’, mzigo wa deni kwa serikali utakuwa ni mkubwa zaidi.

Zipo njia kadhaa zinazotumika kupima ‘refinancing risk’, lakini njia kuu ni pamoja na njia inayotazama kiasi cha deni (asilimia) la ndani linaloiva ndani ya mwaka mmoja. Takwimu zinaonyesha kwamba mwaka (2010), jumla ya deni la ndani ilikuwa ni TZS trilioni 2.7. Kati ya hizi, 25.6% ilikuwa ni madeni yanayoiva ndani ya mwaka mmoja, kiasi ambacho kilikuwa sawa na takribani TZS Bilioni 700. Kwa maana hii, Serikali ilitakiwa ama ilipe kiasi hiki chote au iingie katika makubaliano ya debt roll over. Serikali haikulipa kiasi hiki chote kumaliza deni husika, badala yake kiasi kikubwa kilikuwa ‘rolled over’ katika kiwango kipya cha riba.

Kwa mwaka 2015, takwimu zinaonyesha kwamba jumla ya deni la ndani ilikuwa ni TZS trilioni 11.1. Kwa maana hii, ndani ya miaka mitano tu, deni la ndani liliongezeka zaidi ya mara nne ya kiwango cha mwaka 2010. Kwa mwaka huo (2015), deni la ndani ambalo lilikuwa linaiva ndani ya kipindi cha mwaka mmoja ilikuwa ni 21.6% ya jumla yote (yani TZS trilioni 11.1). Kwa kutazama kwa ‘asilimia’, tunaweza kusema kwamba ni jambo jema kama kiasi cha deni lililoiva kilishuka kutoka 25.6% (mwaka 2010) na kufikia 21.6% (mwaka 2015). Lakini uhalisia ni kwamba:

Pamoja na kiasi husika kupungua kwa ‘asilimia’ kati ya mwaka 2010-2015, kwa kutazama haraka haraka, tunaweza kusema kwamba serikali ilifanikiwa kupunguza mzigo wa malipo ya madeni ya ndani. Lakini ukweli ni kwamba katika kipindi hiki, ‘Net Present Value’ ya deni la ndani as Percentage of GDP ilipanda kutoka 9.1% mwaka 2010 na kufikia 18.2% mwaka 2015, mara dufu ndani ya miaka mitano tu. Ndio maana tukichunguza kwa undani zaidi, tutagundua kwamba ‘the percentage decrease is deceiving’.

Ukweli upo katika thamani kwa Shillingi. Kwa mwendo wa “shillingi”, jumla ya deni lililoiva kwa mwaka 2014/2015 lilikuwa ni kubwa zaidi ya kiasi cha mwaka 2009/2010. Kwa mfano, ukichukua jumla ya deni la ndani 2009/2010 (TZS 2.7 Trilioni) kisha kuchukua kiasi kilichoiva katika kipindi hicho (25.6%), unapata takribani TZS Bilioni karibia 692. Lakini kwa mwaka 2014/2015, ambapo deni la ndani lilifikia (TZS trilioni 11.1), na tukachukua 21.6% kama deni lililoiva, maana yake ni kwamba kiasi hiki kilikuwa ni karibia TZS 2.4 trilioni. Hii ni sawa na ongezeko la TZS trilioni 1.7.

Kama ilivyokuwa kwa kipindi cha 2009/2010, sehemu kubwa ya deni hili haikulipwa na badala yake ikawa rolled over at a much higher interest rate.


Changamoto nyinginezo

- Deni la ndani linakabiliwa na changamoto mbalimbali kubwa ikiwa ni pamoja na ‘limited activity’ kutokana na ‘one way liquidity’ katika mfumo husika, small investors base, na pia utamaduni wa ‘issuance of new securities’ katika kila mnada wa amana za serikali, badala ya uwepo wa ‘secondary markets’.

- Ingawa sehemu kubwa ya deni la ndani lipo katika instrument ya Treasury Bonds (63.3%), kwa kawaida hizi huwa zipo under subscribed tofauti na Treasury bills ambazo kwa miaka kadhaa sasa zimekuwa over subscribed. Hii ni kwa sababu, pamoja na mengineyo, Treasury Bills zinaiva haraka na zina yields yenye mvuto (hadi 18%) katika kipindi kifupi (mfano siku 264).

- Kwa kipindi cha Mwaka mmoja - January 2015 hadi January 2016, deni la ndani liliongezeka kwa zaidi ya TZS Trilioni 1.3.

- Mwezi January 2016, serikali ilikopa ndani kwa ajili ya kuendesha shughuli mbalimbali za serikali, kiasi cha TZS Bilioni 633. Hii ilikuwa ni ongezeko la asilimia 32 (kutoka kiwango cha TZS 430 Bilioni January 2015). Kama tulivyojadili awali, sababu kubwa ya ongezeko kama hili kutokea ni kutokana na ‘kuiva’ kwa deni la awali kabla ya malipo ya deni kumalizika, hivyo kulazimisha ‘roll over’ of the debt kwa kipindi kingine. Na tumeona pia kwamba ‘rolling over’ huwa inaambatana na kiwango kipya cha riba ambacho huwa ni cha juu kuliko kile cha awali.

- Kwa upande wa Treasury Bonds outstanding ni zaidi ya TZS Trilioni NNE. Kwa kipindi cha mwaka 2017 na 2018, inatarajiwa kwamba:

* Karibia 20% ya Treasury Bonds za Miaka saba kitakuwa kimeiva, hivyo kuhitaji fedha za walipa kodi kulipia deni hili.

*Karibia 25% ya Treasury Bonds za miaka kumi zitakuwa zimeiva, pia kuhitaji fedha za walipa kodi kulipa deni hili.

*Karibia 15% ya Treasury Bonds za Miaka kumi na tano zitakuwa kimeiva, vile vile kuhitaji fedha za walipa kodi kulipia deni hili.

- Kwa mujibu wa Sura ya Bajeti iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha (Dr Mpango) hivi karibuni, Serikali inatarajia kukopa TZS Trilioni TANO kutoka kwenye vyanzo vya ndani. Vyanzo hivi vitatokana na debt instrunments ambazo tumeshajadili huko juu.


Katika sehemu inayofuata, tutajadili deni la nje.
 
4.7 Deni la Nje


Katika Sura ya TATU, tulijadili sababu mbalimbali juu ya kwanini nchi kama Tanzania inakabiliwa na madeni makubwa ya nje. Tulijadili kwamba Deni hili ni matokeo ya uwepo wa ‘Current Account Deficit’ katika uchumi wa nchi na tukaeleza sababu zake. Awali tumeona kwamba kufikia mwezi Januari 2016, jumla ya deni la NJE ilikuwa ni Dola za kimarekani 15.4 Billion (sawa na takribani TZS Trilioni 33). Hii ni sawa na asilimia 79 ya jumla ya deni lote la taifa.


4.7.1 Sifa Kuu za Deni la Nje:

Deni la nje lina sifa nyingi lakini muhimu ni pamoja na hizi zifuatazo:


(a) Deni la nje linasimamiwa na kuratibiwa na Wizara ya Fedha (Hazina). Hii ni tofauti na deni la ndani ambalo tuliona kwamba msimamizi wake mkuu ni Benki Kuu (BOT).


(b) Deni la nje ni fedha zinazotoka nje, hivyo kumaanisha kwamba ni za wananchi/walipa kodi wa mataifa nje.


(c) Deni hili hulipwa na serikali kila mwaka/mwezi/miezi kwa hutumia Kodi za wananchi.


(d) Deni la nje kwa kawaida huiva baada ya kipindi kirefu zaidi kuliko deni la ndani. Hii inafanya mzigo wa deni la nje kuwa mzigo mkubwa kwa vizazi vya baadae. Kwa maana hii, – serikali isipotumia vyema madeni ya nje kwa manufaa ya vizazi vijavyo, vizazi hivyo vitakuja deni ambalo halikuwa na manufaa kwao. Ukweli huu unathibitishwa na taariza za World Bank kwamba sehemu kubwa ya mikopo ya serikali kutoka nje inatumika kwenye MATUMIZI YA KAWAIDA.


(e) Deni la nje pia lina athari zake kwa kizazi cha sasa pale madeni ya nyuma yanapoiva kipindi hiki. Badala ya malipo ya madeni haya kubakia/kuzunguka ndani uchumi wa ndani, malipo yake yanakwenda nje ya nchi. Kwa maana nyingine, ‘we are giving away FEDHA’ ambazo leo zingetumika kuboresha maisha ya wananchi badala ya kunufaisha wananchi wa nchi za nje.


(f) Deni la nje likiongezeka kwa kasi kubwa kuna kila sababu ya wananchi kuwa na wasiwasi kwa sababu deni la nje linatengeneza shimo kubwa zaidi kwenye mfumo wa fedha wa nchi (fiscal hole). Kwa mfano, deni la nje likiwa ni $Bilioni MOJA kwa exchange rate ya $1 = TZS 2,180, ili kulipa deni hili, tutahitajika kukusanya fedha za ndani kwa exchange rate hii ili kuipata hiyo $1B. Lakini thamani ya Shilingi ikishuka dhidi ya dola na kuwa tuseme $1 = 2,400, tutahitaji kukusanya ‘madafu’ mengi zaidi kutoka kwa walipa kodi kulipa deni kiasi kile kile cha $1B. Suala hili linajulikana kama ‘Exchange Rate Risk’. Hili ni tatizo kubwa sana kwa nchi kama yetu ambayo bajeti yake inafuata mfumo wa ‘fedha taslimu’ cash budget.


(g) Deni la nje linaondoa sovereignity (uhuru) wa nchi inayodaiwa, kiuchumi lakini mara nyingine hata kisiasa. Hii ni kwa sababu mikopo huwa inaambatana na masharti yanayopendelea zaidi wakopaji ‘creditors’. Tutajadili hili baadae katika muktadha wa Public – Private Partnerships katika miradi ya ujenzi wa miundo mbinu, umeme nk.



4.8 Mgawanyiko wa Deni la Nje (Kwa mujibu wa ‘Creditors):

Makundi makuu ni haya yafuatayo:

· Concessional Bilateral Lenders

· Concessional Multilateral lenders

· Semi Concessional Lenders

· Non – Concessional Lenders


Ni muhimu tukafafanua maana ya dhana za Multilateral, Bilateral, na pia Concessional & Non – Concessional loans’:


4.8.1 Bilateral Loan(s):

‘Bilateral Loan(s)’ ni aina ya mkopo/mikopo inayohusisha ‘a single lender’. Kwa mfano, inaweza kuwa ni mkopo kutoka nchi moja kwenda kwa nchi nyingine, au taasisi moja ya kifedha kwenda nchi nyingine. Mifano ni pamoja na Mikopo kutoka nchi kama Japan, Sweden nk.


4.8.2 Multilateral Loan(s):

‘Multilateral Loan(s)’ ni aina ya mikopo inayohusisha taasisi au nchi nyingi zinazotoa mkopo kama kundi moja kwenda kwa nchi nyingine. Mifano ni pamoja na mikopo kutoka taasisi kama World Bank, IMF, AfDB n.k, taasisi ambazo zinajumuisha wadau wengi ndani yake.



4.8.3 Maana ya Concessional & Non – Concessional Loans:


4.8.3.1 Concessional loans

Hii ni mikopo yenye masharti nafuu kwa maana ya kwamba: Kwanza gharama yake/riba ni ndogo sana ikilinganishwa na riba zilizopo katika masoko mengine ya fedha; Pili, mbali ya riba kuwa nafuu, riba hizi huwa ni ‘fixed’ (fixed interest rate) kwa kipindi chote cha mkopo husika;

Tatu madeni ya aina hii huchukua muda mrefu sana kuiva (hadi miaka 40), hivyo kupunguza ‘fiscal pressure’ kwa serikali zinazokopa (mfano Tanzania) za kujikuta zinatumia fedha nyingi za walipa kodi kulipa madeni yanayoiva badala ya kuelekeza fedha kwenye huduma za kijamii;

Nne, mikopo ya aina hii inaambatana na na ‘grace period ndefu’ (miaka hadi kumi), kabla ya serikali kutakiwa kuanza kulipa mikopo husika.


4.8.3.1.1 Concessional Multilateral lenders wakubwa ni hawa wafuatao:

- International Development Finance (IDA), ‘a concessional window ya World Bank.

- International Fund for African Development/IFAD (chini ya Umoja wa Mataifa).

- Norway Development Fund (NDF).

- African Development Fund (chini ya African Development Bank).


4.8.3.1.2 Concessional Bilateral wakubwa ni pamoja na:

- Sweden.

- Japan.


4.8.3.2 Non – Concessional loans


Kama tutakavyojadili punde, katika kipindi cha hivi karibuni, serikali imekuwa ikihamia zaidi kwenye ‘non concessiona loans’ kutoka nje. Mikopo ya aina hii inakuja na masharti magumu na gharama kubwa kwa walipa kodi.


Kwa kipindi karibia chote cha uhuru hadi kufikia miaka ya mwisho ya 2000, sehemu kubwa ya deni la nje llikuwa ni mikopo yenye masharti na gharama nafuu “Concessional Loans”. Kutokana na hali hii kwa kipindi kirefu sana, sehemu kubwa ya deni la nje lilikuwa in ‘fixed interest rates’, hivyo kusaidia nchi kuepukana na risks related to interest rates movements. Kwa mfano, kufikia mwaka 2010, takribani 95% ya deni la nje lilikuwa in ‘fixed interest rate’, tofauti na 2015 ambapo kiasi hiki kilishuka na kufikia karibia 80%. Inatarajiwa kwamba mikopo mingi ya nje itaendelea kuja in ‘floating/variable interest rates’.


Sababu kubwa kwanini wahisani waliamua kuanza kupunguza mikopo ya aina hii (concessional lending) ni pamoja na kwamba, serikali zao zilianza kupata shiniko kutoka kwa walipa kodi wao ambao hawakuwa wakiridhishwa na matumizi ya mikopo hiyo, lakini hasa kutoridhishwa na kasi ya kupungua kwa umaskini. Kutokanana mabadiliko haya, concessional loans zinatarajiwa kuendelea kupungua zaidi.

clip_image001.gif



4.9 Mgawanyiko wa Deni la Nje by Creditors (Kwa mujibu wa Medium Term Debt Management Strategy, Mwaka 2010 & 2015):

Jedwali #1

Chanzo Cha Mkopo

Mwaka 2010

Mwaka 2015

Concessional Multilateral mfano IDA, IFAD, NDF, AfDB

85.93%

60%

Concessional Bilateral mfano Japan, Sweden nk.

11.52%

8%

Non – Concessional:

·Commercial Banks - example Standard Bank, ING Bank, HSBC, Shanghai and Hong Kong Bank.


·Export Credit Agencies - example Exim India and China.


2.53%







0.02%


32% (Jumla ya Commercial & Export Credit Agencies).


Kupungua kwa vyanzo vya nje vyenye gharama na masharti nafuu kumeenda sambamba na kuongezeka kwa deni la nje. Kama tunavyoona, vyanzo vyenye gharama kubwa na masharti magumu vinazidi kuchukua nafasi ya concessional lending kwa kasi kubwa. Kwa mfano, tukitazama jedwali hapo juu, ndani ya kipindi kifupi sana (miaka mitano), vyanzo vya ‘non-concessional lending’ (yani commercial banks and Export Credit Agencies) vimeongezeka kutoka 2.55% ya jumla ya deni lote la nje mwaka 2010 na kufikia 32% mwaka 2015.


Kama tutakavyoona baadae, non – concessional loans ni gharama kubwa zaidi – kwa maana ya kuwa na riba kubwa, kuja na “floating interest rates” zaidi kuliko “fixed interest rates”, kuja na shorter grace period and pia shorter debt maturity. Mabadiliko haya yana athari kubwa kwa uchumi wa nchi na uchumi wa wananchi, masuala ambayo tutayajadili kwa undani muda sio mrefu.




Katika sehemu inayofuata tutajadili Mgawanyiko wa Deni la nje (Kwa mujibu wa Sarafu).
 
4.10 Mgawanyiko wa Deni la nje (Kwa mujibu wa Sarafu):

· Dollar za Kimarekani (23.2%)

· Speacial Drawing Rights (SDR), hizi ni (52%). SDR zinaratibiwa na IMF. Hii ni nyenzo muhimu sana ya kuisaidia IMF kutekeleza majukumu yake ya msingi katika mfumo wa fedha wa kimataifa hasa ‘macro economic stablization’ na pia ‘liquidity’ wakati wa dharura/misukosuko.

· Australian Currency (11%).

· China – Yen (4.9%).

· Euro (4.1%).

· Japan – Yen (3.0).

· Sarafu nyinginezo (1.8)


Muhimu:

Sehemu kubwa ya SDRs zinatolewa katika sarafu ya Dollar ya Kimarekani. Kwa maana hii, sehemu kubwa ya deni la nje lipo katika sarafu ya DOLA. Suala hili linafanya deni la nje kuwa ‘exposed to exchange risk’ kila wakati Sarafu yetu (TZS) inaposhuka thamani dhidi ya Dola ya Kimarekani. Tutaona hili kwa undani baadae.


4.11 Je Mashati ya Mikopo ye nje yakoje? Je Wakopeshaji Wakubwa ni akina nani?


Uendeshaji na usimamizi wa mikopo Tanzania unaongozwa na sheria ijulikanayo kama – ‘Government, Loans, Guarantees and Grants Act Cap. 134’. Sheria hii inataka mikopo yote ya nje ya nchi iwe na ‘Grants’ ya angalau 35% ya concessional loans. Lakini kama tulivyokwisha ona, serikali imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa kutokanana aina ya nje inayopatikana, hasa kupungua kwa mikopo yenye masharti na gharama nafuu (concessional loans).


Kama tulivyojadili, mbali ya concessional lending, serikali pia imekuwa ikikopa kupitia vyanzo vingine vya fedha nje ya nchi ikiwa ni pamoja na semi – concessional loans (mfano France, Austria) na pia Export Credit Agencies (China & India Exim Banks). Vile vile serikali imekuwa ikiendelea na juhudi za kutafuta fedha kutoka kwenye masoko ya kimataifa ya mitaji kwa ajili ya kugharamia mahitaji yake mbalimbali hasa ujenzi wa miundo mbinu. Ifuatayo ni ‘summary’ ya masharti ya mikopo ya nje pamoja na orodha ya wakopeshaji wakubwa (major creditors):


Jedwali #2

Instrunment

Creditor(s)

Repayment Structure(Maturity)

Repayment Structure (GracePeriod)

Cost i.e Interest Rates (%)

Multilateral Concessional (Fixed).

Kwa mujibu wa Medium term Debt Management Strategy (2013), serikali ilitarajia kiasi cha $500 millioni kwa mwaka kwa miaka mine ijayo.


IDA(World Bank), ADF, NDF, IFAD, AfDB

40

10

0.75%

IFAD/EXKOR/NORDIC (Fixed)

IFAD, NORDIC, JICA, Korea (bilateral)

40

10

0.10%

Concessional Fixed


Kwa mujibu wa Medium term Debt Management Strategy (2013), serikali ilitarajia kiasi cha $200 kutoka kwa baadhi ya wadau.


BADEA, AUSTRIA (bilateral), FRANCE(bilateral), JAPAN (bilateral), SWEDEN (bilateral) and EIB

25

5

1.75%

Semi – Concessional Fixed


Kwa mujibu wa Medium term Debt Management Strategy (2013), serikali ilitarajia kiasi cha $200 millioni kutoka kwa wadau.


OPEC, KUWAIT

20

5

2%

Semi – Concessional Floating


ADB, AFD

20

5

2%

Export Credit Agences – Fixed.


Gazeti la ‘The Citizen’ la tarehe 16 March 2016, liliripoti taarifa kutoka Exim India kwamba serikali ya Tanzania inatarajia kukopesha Dola za Kimarekani Bilioni KUMI kutoka Exim India kwa ajili ya miradi ya miundo mbinu. Jumla ya mkopo huu unatarajiwa kuwa ni Dola za kimarekani Bilioni 10.4, sawa na takriban TZS 23 trilioni.


Kati ya hizi, Shirika la Taifa la Nymba (NHC) peke yake linatarajia kuchukua jumla ya TZS Trilioni 6.2.


Exim China, Exim India, HSBC

15

3

2%

Export Credit Agences – Floating


Exim China, HSBC

15

3

Libor + 4.3%

Sovereign Bond (Commercial fixed)


Kwa mujibu wa Medium term Debt Management Strategy (2013), serikali inatarajiwa wakati wowote to issue hati fungani yenye thamani ya USD 700 milioni.


Kwa kutazama muda wa kuiva kwa deni hili (miaka kumi), na gharama ya mkopo (8.5% interest rate), hii ni risk kubwa sana kwa uchumi wa nchi na uchumi wa wananchi.

International capital market

10

9

8.50%

Commercial Loans (floating).


Kwa mujibu wa Medium term Debt Management Strategy (2013), serikali ilitarajia kiasi cha $500 millioni kwa mwaka kwa miaka mine ijayo.


Standard Bank, Hongkong & Shanghai Bank, ING,

7

2

Libor +7%

Source: Medium Term Debt Management Strategy, 2013 & 2015



Katika sehemu inayofuata, tutachambua masuaa muhimu tuliyoyaona hapo juu.
 
Back
Top Bottom