Magreat Thinkers ninaowafeel...........

mmh nikitizima huo ubeti wa mwisho nashindwa hata kukubembeleza uendelee kutupa company hapa jamvini.
haya asante,nanyi mkalale salama.

Cheusimangala,
Kadhalika nawe pia,huko ambako sikwako
Unaujuzi wakujitetea,kwa hoja zenye mashiko
Basi iweze duniya,kwani ya kale hayako
Uwatapo tungo yako ,utaingiya jamvini
 

Nilham
Kipaji ni jambo bora, amekupamba Rabana,
Tena umetia fora, posti hufana,
Basi usiwe mkora, akiba uweke sana,
Sihadawe na unyange na unyange una mwisho

 

PJ congratulations
 

shosi wewe muwazi, hata kwa yako mavazi,
waona vyetu vivazi, kila upande kwa wazi,
hata Judith husazi, misi umemperuzi,
heri mejiweka wazi, filingi zako taenzi

wasema waja vingine, kwa wote ulosahau,
nusura mie nigune, mepozwa nazo nahau,
ingawa ni kama tone, chonde usinisahau
nitakodoa nione, tuko pamoja mdau
 

Nimeandika vizuri vina nimepangilia
Yale yaliyo ya kheri rahisi kuyagundua
Kwa anaefikiri vema kuyatambua

Tujitume kwa khiyari na jitihada pia
Tusitafute fahari kisha tukaumia
Zingatia shauri ujue wako wajibu
Usiingie kwenye hatari ukawacha ya wajibu
Mpongeze akupongezae, usimpongeze asokupongeza.
 
Asante mkuu, nilikuwa najaribu kukujibu kwa vina hapa lakini naona nachezea makaratasi tu ukizingatia nilikuwa na bifu na mwalimu wa kiswahili.
 

umejibu kwa wepesi, moyo wangu kusuza,
hata bila ya senkisi, heshima umenituza,
zi zako zote makisi, kwa yote ulonijuza
watunyosha kama pasi, vipaji vyetu kukuza
 
Asante mkuu, nilikuwa najaribu kukujibu kwa vina hapa lakini naona nachezea makaratasi tu ukizingatia nilikuwa na bifu na mwalimu wa kiswahili.

Shukurani nazipokea, Jaluo mwana Nyeupe.
Mola mi sinizuie, namsifu kwa si kwamapepe
Urithi ni thamanie, tunzoni pepepe
Shairi ni kipaji,weka vina kibindoni
 
umejibu kwa wepesi, moyo wangu kusuza,
hata bila ya senkisi, heshima umenituza,
zi zako zote makisi, kwa yote ulonijuza
watunyosha kama pasi, vipaji vyetu kukuza

Nimejibu kwa senks mpaka zote zimeisha
Nimekugongea reputations kukuongezea maisha
Wewe ni kiboko wengene gersha
Ole wao watakaoiga waitaishia kushuta
Nadhani ulighani tenzi ezi za umistumta
Usije acha kughani mpenzi ukajajuta

Alamsiki
 
mkuu wewe kwa utenzi kiboko

Vuvuzela
Nakuambia wazi wazi,sitaacha kusema neno.
Kwani jana sio juzi,ulimi si sawa na meno.
Umalenga si kuna nazi,hili akumbuke mno.
Atungae kwa hirizi, ayawache majivuno.

Alamsiki
 
Shukurani nazipokea, Jaluo mwana Nyeupe.
Mola mi sinizuie, namsifu kwa si kwamapepe
Urithi ni thamanie, tunzoni pepepe
Shairi ni kipaji,weka vina kibindoni


Asante Mohhamed Shossi, sasa naingia kichwa kichwa,
Ujinga kweli mkosi, hakika wapaswa kuachwa,
Najiunga rasmi na kikosi, chenye wachapa kazi kuliko mchwa.


Unikumbushe asubuhi nikiamka nijaribu tena kuandika.
 
 
Thanks Mohamed Shossi! This is so creative of u:clap2::clap2::clap2:

I will be back....
 
Asante Mohhamed Shossi, sasa naingia kichwa kichwa,
Ujinga kweli mkosi, hakika wapaswa kuachwa,
Najiunga rasmi na kikosi, chenye wachapa kazi kuliko mchwa.


Unikumbushe asubuhi nikiamka nijaribu tena kuandika.

Asubuhii mefika timiza ahadi
Shiri kulibandika kama ilivyo jadi
tenzi zilizo na ujumbe usituache gadi
tungo zenye utam si ukakasi wa magadi
utunge za kichochezi ukaitwa gaidi
tupe ladha ya lugha mwanajamvi tufaidi
 
Thanks Mohamed Shossi! This is so creative of u:clap2::clap2::clap2:

I will be back....

Shukran nazipokea kwa mikono miwili
Kwenye tungo nasifika nilisha pewa mwali
Asubuhi imefika nataka kukuza hali
Hujambo ndugu yangu ewe ulie mbali
Sisi tumeamka salama siku hii jumapili
 
mohammed mi hivi siwezi nifanyeje jamani??

Hakuna aliezaliwa akajua ya bayana
Kila mmoja kapawa kipaji na Rabana
Jaribu kupangia vina usiseme hapana
Ghani kwa shairi kwa urefu na mapana
Usijishuke kifani wakauna uso maana

Nilham una elimu umewashinda watwana
Wewe bint rashed mwenye siha mwanana
Usingoje kuonyesha kipaji alokupa Maulana

Tungo nazisubiri kutoka kwako muhibu
Kiswahili safi wakijua usijigeuze bubu
Kilichobaki hivi sasa jivute taratibu
Utunge tungo za dawa tena zakitabibu
Uwasuuze nyoyo mabibi na mababu
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…