Magreat Thinkers ninaowafeel........... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magreat Thinkers ninaowafeel...........

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mohammed Shossi, Jan 29, 2011.

 1. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #1
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Nabofya kibodi yangu, salamu nazituma,
  Kwenu marafiki zangu, natumai mu wazima,
  Nawaombea kwa Mungu, mjaliwe yalo mema,

  Nilham usiyechoka, asubuhi na jioni,
  Nyumbani kuwajibika, halafu pia kazini,
  Kisha huachi andika, kutujuza kulikoni,

  Ni wewe ulieniteka moyo wangu
  Nikaamua kukutokea kimizungu
  Nikubalie mpenzi niachane na machangu

  AfroDenzi
  , nakuzimia tangu MWANZONI,
  Fikra zake ni huru, pia zina burudani,
  Nami ninamshukuru, hachoki tangu zamani,

  Yupo dadetu
  Festiledi, yeye hupenda MAISHA,
  Kamwe hawezi kusita, mazuri kutuonesha,
  Thanks tele azipata, maana huelimisha,

  Michelle
  yupo, hutaka TUJIELEWE,
  Daima aandikapo, vichwa vyetu tusuguwe,
  Sifa zake zipo, muhimu apewe,

  Dr W. Slaa
  nasaha tumepeyana, tena tukanufaika,
  Mafumbo tukafumbana, kwa furaha na kucheka,
  Na mara tukabishana, na wengine tukachoka
  Kisha ukarudi tena, huku tumeshachamka.


  Mzee Mwanakijij
  i, MZEE WA CHANGAMOTO,
  Haishi kutuambia, mambo yalo motomoto,
  Habari hutupatia, yenye midundo mizito,

  Hashycool
  anza tangaza, ni kwako yamechimbuka
  Watunzi waagiza, ushauri kuwataka
  Yaseme kwenye baraza, hii ni mbiu ya mwaka.

  Kaa la moto
  Chochote unachoweza,hima weka mchangoni
  Hilo ndilo unalowaza,tukakawa hatulioni
  Ila sala memaliza,ndio ukatia udhu

  Madela wa Madilu
  keri hazi ghasi, nyimbounawaimbia
  Mwenye kukerwa huhisi, hujali humuingia
  Hawi zimwi asikisi, ikawa bure tabia.

  Pakajimmy amejieneza,sifa zakejamvini,
  Jambo analoliwaza, taarifa kuwapeni,
  Si vizuri kunyamaza, bora awajulisheni,

  Kaiza
  kaka yetu sote, jitu liloshiba,
  Mengi hutaka tuyapate, yale yaliyoshiba,
  Asichoke asisite, ajaze hata kibaba,

  Gsana
  Naingia jamvini, hapana tena ajizi
  Nazikubali shukrani, kwa juhudi zangu hizi
  Kushajiisha jamvini, watunzi wa zama hizi
  Kheri ipo kwa manani, Mpaji kanijaalia.


  Katavi
  na LazyDog ipambeni JF wananeti mwasikia
  Tenzi na mashairi nyeti, wengi watafurahia
  Uridhi ndani ya beti mmfiche mmesikia?

  Shishi na
  Mpevu hoja za kweli toeni, faida kutupatia
  Aso ubavu wavuni, shimoni atakimbia
  Mtenza mwenye nguvu makini, hadharani nawambia
  M_bongotz
  acha woga, wananeti yetu hiba.

  Kuwa fundi si ajabu, hilo kwanza eleweni,
  Kuwa fundi ni thawabu, aliyanena Manani,
  Msijempa adhabu, kwa maswali ya kwa nini?
  Drphone ameshasilimu, sasa naitwa FUNDI.


  Rose
  naye ni rafiki, hutumia DARUBINI,
  Kazi yake haichoki, popote ulimwenguni,
  Kwenye siasa na urafiki, hutujuza kulikoni,

  Mwanajamvi
  Aspirin, hutuonesha MWANGAZA,
  Makala zenye hekima, na mambo kuyachunguza,
  Kwa ushairi ni vema, post zake zapendeza,

  Zion Daughter
  Si wakuamsha daku,walo macho wameona
  Hashindani na kuku,kula wanacho kiona
  Wala havai kikuku,kuwaiga walonona


  Miss Judith
  huyo, ana UPANDE MWINGINE,
  Yale ayaandikayo, hupendwa nao wengine,
  Kwa mawazo si mchoyo, hufanya tushikamane,

  Gbolin
  umesibu, umenena ya hakika
  Tena nimetaajabu, posti zako za haraka,
  Wajibu tena wajibu, wanajamvi kukusanyika
  Jamvini bila tabu, sote twaburudika.

  Wa ndima
  Mgosi vipi unadhani, nasaha zipi azizi?
  Nianze upande gani, kuepusha jinamizi?
  Ni ipi ile ya ugoni, kutanguliza malezi?

  MwanajamiiOne
  pia, hutuambia AMKENI,
  Hachoki kutuletea, yatokeayo nchini,
  Daima hukumbushia, tutoke usingizini,

  October
  mwenzetu, utujuzaye maisha,
  Wewe ni darasa kwetu, maarifa yaso kwisha,
  Wafunza juu ya utu, mengi watuelimisha.

  Teamo
  bado kuchoka, upo kwenye msafara,
  Ungali kwenye pilika, kwa zako huru fikra,
  Nakuombea baraka, uzidi kuwa imara,

  Mwenzetu
  ni mwanaharakati, daima usiyechoka,
  Wautumia wakati, pasipo yoyote shaka,
  Maisha kuwa na chati, daraja la uhakika,

  Inkoskaz
  Upo kwenye mapambano, ujenzi walo taifa,
  Hujalala kama pono, wastahili nyingi sifa,
  Washika yetu mikono, ili tuzizibe nyufa,

  Kiraka
  mwendo ukaze, usiache harakati,
  Mawazo uyaeleze, tena kwa kila wakati,
  Ili nasi tujifunze, nawe uwe katikati,

  Voiceofreason
  , mapenzi umeandika,
  tangu siku za zamani,
  Yale yaliyokufika, na yale ya majirani,
  Na kwako alozimika,umesema ya moyoni,

  Ndugu yetu
  Preta, kabobea kwa MAVAZI,
  Vitu vyake ni vizuri, hilo mbona lipo wazi,
  Yupo kwenye mstari, hachoki kufanya kazi,

  Fidel80
  nayakumbuka, manenoyo jamvini,
  Hakika niliridhika, nami nikakuamini,
  Kwako hayakufichika, hata yale ya moyoni,
  Hashima siku hizi hakuna labda zamani

  Invisible
  tunamjua, mkuu wetu KIJIWENI,
  Sheria apambanua, ili asitupige ban,
  Sote tukajitambua, tujijue kina nani,


  Mkuu
  Klorokwini, posti zake ni KITAMU,
  Hatosahau daima, kutupa yote muhimu,
  Ujuzi wake kisima, haisaliti elimu,


  Mkuu
  Kashaijabutenge,nakuheshim zamani na sasa,
  Yeye wala hajalala, mengi ameshayaasa,
  Kabobea mijadala, ya jamii na siasa,

  Kimokole
  moyoni nafarijika, malenga tukikutanika,
  Ya haki kuyatamka, batili kuzifunika,
  Kheri ikaminika jamvini tukanufaika.
  Bwana Kimokole, nakushukuru hakika


  Magulumangu
  mshairi, USHAIRI MAMBOLEO,
  Mashairiye mazuri, tena yale ya kileo,
  Huukuza ushairi, na kuupa mwelekeo,


  Na
  Wiselady, siachi kumsifia,
  Elimu kutugawia, na picha kutuwekea,
  Mazuri hutuambia, ndani ya hii dunia,

  Maria Roza

  Posti zako laiti ni tarumbeta, kuvuma wakasikia
  Lakini wapi ni nta, sikioni wametia
  Lije kubwa la kivita, barugumu likalia

  Ndugu yangu
  Rutashunyuma, sitokuwacha nyuma
  Posti zako nii ghali sio kama uji
  Zinawakuna wa mbali mbaka Tabora na Ujiji

  Mjomba
  Bujibuji, mwingi wa burudani
  Posti zako adhimu, zinatupa burudani
  Sina wakufanisha hata na mmoja humu ndani.

  Nakumiss
  mzee wa malivdavi ulie kaburini
  Baada ya posti mbili wadau wakakupa bani
  Kifo chako historia ndo mana nakutilia ubani

  Ewe nawe
  The Finest usinung'unike,
  Tena uingie ndani nawe ufarijike,
  Utuambie amkeni, wanajamvi tubadilike
  Tushikane kwa imani wanajamvi tunusurike.

  Wozawoza
  wewe mshari jahili,
  Kama huoni dalili, kebehi si jambo kupigania,
  Twatetea kwa ukali, siambe tunatania
  Kiwa sio zetu sisi, dini hizi ni za nani?

  JF Moderator1
  huyu wa ajabu, wala hataki mchezo
  Kuwatia watu adabu, bila kuleta mizozo
  Katoa watu ububu kukumbatia kuozo
  Lazima tumpe thanks, Wanajamvi tumfurahie.

  JF Moderator2
  huyu ni hodari, Mtauni humkani
  SIHABA baba jasiri, wala hataki utani
  Hakuna kutafakari, mwanajamvi si muhuni
  Pongezi tumpe na jamvi kulifurahia.

  Mwenzetu huyu si mgeni,
  Samora10 mwamjua
  Mwenzetu si limbukeni, kusema anayoyajua
  Samora10 hana utani, kwenye uovu hufichua,
  Ni kijana muadilifu si kijana wakuchakachua.

  Jaluo Nyeupe
  mwamjua, bilashaka mwamuona
  Ni yeye tunaemjua, hakika yupo bayana
  Haki huitetea, bila kubaguana
  Jaluo Nyeupe
  ni rafiki hana kubaguana.

  Na
  Lizzy na Husniyo msisite, ikawa tusionane
  Wala tusijikokote, mlonayo muyanene
  Mllipo mji wowote, mambo tuelimishane
  Abebwae hujikaza, ukumbi tuuchangie

  Nyani Ngabu
  , Babaubaya, michango nileteeni
  Ninyi ndugu pia, shime tujitokezeni
  Muhimu ni zetu nia, na wala sio thamani

  Lizzy
  fanya kuniandikia, wapi yako maskani
  Ndipo nitapokwambia, mchango umpe nani
  Na mimi tafatilia, nizitie kibwetani

  Hongera niwatumie,
  Kibunango na Babu Atakasema sirisiri
  Na duwa tuwaombee, Rabi awape kivuli
  Mungu awazidishie, duniani na peponi

  Masikini_Jeurina
  na Gurudumu hawa harambee, wapiga debe jamvini
  Hawana ila ushee, imekuwa hamkani
  Wamejifanya wazee, wao ndio makarani
  Posti nyingi wanaandika hapa jamvini,

  Muhogo mchungu
  kwa siri au dhahiri , atoae yujamvini
  Uziitazo ghururi , mwenyewe amezibuni
  Unenayo yafikiri, usijeitwa fatani

  Mwaminifu
  thread ulozitunga,zitawafika wahunzi
  Wale wasije kulonga,uloanza mwanafunzi
  Wapita ukiwachonga,kwa vile una kurunzi

  Ki Mey
  hutenda mengi ya dini, habanduki kanisani
  na posti nyingi jamvini, hukaribisha na wageni
  na ibada za nyumbani, hatutaki hata wageni.

  WomanOfSubstance
  Na kama wapendelea, usitajwe hadharani

  Kwa kuwa unahofia, mambo fulani fulani
  Ninakuhakikishia, taweka siri moyoni


  Maxishimba
  uchunge mwenendo wako , wende mwendo wa kupima
  Utunze twabiya zako , ujuwe baya na jema
  Kama hujali wenzako , kutenda ya kuwauma
  Ngoja nawe siku yako , utendwe bila huruma

  Kakajambazi
  , yeye huyu si mwizi, na tena ye si jambazi
  Kanilaghai kiujuzi, kwa jinale jamvini
  Huyu yeye si jinamizi, akatuchuna na ngozi
  Kakajambazi ni mwema mwenzetu jamvini.

  Tatiana
  Kashika kuwasafisha, jamvini harufu waridi
  Kutwa atuhamakisha, kuwa yeye ni shahidi
  Posti zake zisokwisha, za tamu tena jadidi

  Sulphadoxine
  Unasi ghamu ghalati, siugenini jamvini
  Siraji ng'aza sirati, uongoze Furusani
  Chifunaga
  kapaza sauti, Mwamuska si mwoga jamvini
  MANYANZA
  taabani, hali hana hamu.


  Mawazo1109
  ni wetu sote, hima tusaidiane
  Wa mbele tuwafuate, haya tusioneane
  Kwa hili natusitete, bali tusikilizane
  Abebwae hujikaza, ukumbi tuuchangie.

  GT
  wake mdogodogo mwendo, wajulikana zamani
  Mwendo usio vishindo, haufeli abadani
  Asoweza huwa kando, awezae huwa ndani

  Mbongopopo

  Chunga heshima na cheo, na maovu usifikwe
  Fidhuli umjuapo, usimtoze neno lake,
  Takuudhi na wenzio, ushikapo pasishikwe
  Umjuaye kunyakwe, simnyishe penye watu....

  Godfrey Tajiri
  Kweli wewe si wasongi, malenga mashuhuri
  Umejikita kama kigingi, mwingi wa sururi
  Usia nakupa tena uukariri
  Usije oa shangingi maisha ukayaona shubiri
  Cheusimangala,
  Kadhalika nawe pia,usihi uko peke yako

  Ukadhani umesahaulika ukawaonea wivu wenzako
  Unaujuzi wakujitetea,kwa hoja zenye mashiko
  Basi iweze duniya,kwani ya kale hayako
  Upatapo tungo yako ,utaingiya jamvini  BLUE BALAA acha makeke, ushairi si mapene.
  Kalamu yake Nsiande, kali kaka ujuani
  Wapaswa kukaa chonjo, Rais msije mtaniani
  Watajakutoa mkojo, Segerea wala si uraiani
  [FONT=&quot]Nguli Jabali[FONT=&quot] wewe mbora, amekupamba Rabana,
  Tena umetia fora, posti hufana,
  Basi usiwe mkora, akiba uweke sana,
  Sihadawe na unyange na unyange una mwisho[/FONT]
  [/FONT]

  Vuvuzela
  Nakuambia wazi wazi,sitaacha kusema neno.
  Kwani jana sio juzi,ulimi si sawa na meno.
  Umalenga si kuna nazi,hili ukumbuke mno.
  Utunga hata kwa hirizi,uyawache majivuno.


  Mimi ningali mwanafunzi katika hii tansia
  Bado singuli kutunga nje ya tanzania
  Baraza watu mahiri Kimensera acha kutania
  Ila umetoa wazo zuri kazi talifanyia
  Sivibaya kuijenga lugha yetu sawia
  Nawe pia umo njoo tupige kasia
  Usijitoe kundini kusema utenzi ni kadhia

  Tungo huleta faraja penye dhiki na ghasia
  Malenga hutoa hoja za msingi na wosia
  Namaliza kukuomba tunga japo kwa kukisia.
  Wajuzi walo jamvini watakufunda kiintelejensia.

  DaMie nimeona na wewe nikutaje
  Mtoto uliye na hiba nikushau iweje
  Posti zako ni dawa zimeshinda mvuje
  Zina toa wosiwa dar mpak kivinje
  Usirudi nyuma jamvi usilikunje

  Mdondoaji hupo nyuma kuchangia jamvini
  Sasa noa panga na jembe tia mpini
  Nani asojua mchango wako jamvini?

  Superfisadi sasa amka, tenzi kutupatia
  Uzipange kwa ubeti sio za kutupia
  Utujuze hali yako na aila yako pia
  Usinisahau kwa dua pamoja na nabia
  Mungu akupe ya kheri na wanajamvi pia.

  X-PASTER upo wapi mbona umetulia
  Nini kimekusibu hoja hujachangia
  Najua upo buze dini kulingania
  Mungu akupe baraka na dhawabu pia.

  Nami MWAJAMVI MIMI, Mohammed Shossi
  Tungo zangu siwanyimi, nawapenda kiukweli,
  Tena mara kumi kumi, tena na kwa kila hali,


  Ambao sijawataja
  , lipo shairi jingine,
  Sote tungali pamoja, kwa mema tuombeane,
  Tusichoke zetu hoja, hivyo na tushikamane,
   
 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Mkuu shukrani za dhati,na we pia tunakufeel kwa mistari hii adimu,ukichanganya na Afodenzi basi hata studio mnaweza ingia mkatoa singo kali!!
  Keep it up Mohammed
   
 3. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #3
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Shukran sana mkuu hata mie nakukubali

  Umepewa utu wema,
  Wenye thamani daima,
  Moyo wangu wanituma,
  Sifazo kukupatia.
   
 4. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  IMETULIA HIYO.....!

  karibu sana mkuu
   
 5. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #5
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Asante sana mkuu...........nilikusahau ila nimekurusha hewani mkuu.:roll:
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hilo shairi twangoja, ulitoe hadharani,
  Usijefanya viroja, utuache mataani,
  Ulijazie na hoja, lipambwe na umakini

  Siku litakapokuja, twaomba tuwe hewani,
  Lituletee faraja, kama ile ya manani,
  Litujengee Umoja, tusiwe mahayawani
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu leo naona vina vimekaa na kutulia kichwani

  Hongera sana.
   
 8. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #8
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Nimeamka fresh mkuu....
   
 9. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #9
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Maneno nimesikia, ninayo mwangu moyoni,
  Yote unayonambia, natafakari kichwani,
  Endelea subiria, shairi lipo mbioni,
   
 10. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  du mkuu kichwa kmetulia maana mashairi yametulia cpati picha hlo linalokuja litakuwaje keep it mkuu
   
 11. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Jamani,sikujua crazy comments zangu hufanya watu wajielewe.......nilijua nawachanganya

  Nashukuru sana wakwetu Tanga.......you have made my saturday.....Have fun today!!!:clap2::clap2:
   
 12. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #12
  Jan 29, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Not bad
   
 13. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #13
  Jan 29, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Jana ulifika salama nyumbani???
   
 14. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Asante mzee wa mashairi,,uko vzr!nakukubali:clap2:
   
 15. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #15
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Haya,,,hawavumi lkn............
   
 16. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #16
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Nimeongeza hii beti....

  Ewe nawe The Finest usinung'unike,
  Tena uingie ndani nawe ufarijike,
  Utuambie amkeni, wanajamvi tubadilike
  Tushikane kwa imani wabnajamvi tunusurike.


  [FONT=&quot]
  [/FONT]
   
 17. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #17
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Asante sana mama mwenye busara zako............ tunajaribujaribu tu....
   
 18. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #18
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160

  :sad::sad:,mi na wewe basi.........
   
 19. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #19
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu you have got talent hongera sana...
  Kweli JF kuna talent za kutosha kwakweli tuki-Stand Together... ni mengi tunaweza kufanikisha....
  Tunaweza tukatumia Vipaji vya Watu Tofauti humu kwa Manufaa ya wengi..., Just Imagine nyie wanamashairi mkiungana mkawatungia wanamuziki wetu??????....... au mnasemaje?..... Hapa kuna Gold Mine ambayo hatutaki kuitumia.
   
 20. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #20
  Jan 29, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Huyu uliemtaja, hafui dafu jamani,
  Ni dada mwenye viroja, amezidisha matani
  Sifa zake nazitaja, upate kumbaini

  Huyu ni mtu wa kuja, atokea milimani
  Hawezi hata kungoja, subira haitamani
  zingine nitazitaja, wala hutomtamani

  Akikwambia "nakuja", kumbe yuko kitandani,
  Si mtu alo na tija, amekosa shukurani,
  Utakaa kumngoja, hayupo hata njiani
   
Loading...