Magreat Thinkers ninaowafeel...........

Magreat Thinkers ninaowafeel...........

Aisee mheshimiwa Muddy sikujua kama unanifeel asee?

Sijui nikujibu kwa ushairi au hii inatosha?

Nimekugongea senksi kule, kakague.

Wewe tena mwenye hoja za maana
Siwezi kukusahau post zako mwanana
Umeelimika hoja dhaifu husema hapana.................

Shukran mkuu tupo pamoja
 
Mimi nipo poa mambo, bado nayaangalia
vijana wenye vijambo, hoja mkizichangia
Naogopa kwenda kombo, nisije kuwaharibia
Nipo naogopa shombo, msije kunimwagia


Mvuvi anapovua, samaki kukusanyika,
akikosa anajua, leo Mungu Hakutaka,
hawezi kujisumbua, kununa kukasirika
Lazima kitakufika, kile kilichoandikwa.


Mkulima hushtushwa, shamba moto likiwaka,
ajue akiulizwa, kama ametoa zaka,
asiseme kasakamwa, au mkosi umefika,
Lazima kitakufika, kile kilichoandikwa.


Biashara ikifanywa, na ukifungua duka,
kama hukufanikiwa, uache kunung'unika,
pengine hudhulumiwa, watu kwako hupunjika,
Lazima kitakufika, kile kilichoandikwa.


Yote yamesajiliwa, Mungu Ameshaandika,
kalamu kuinuliwa, wino umeshakauka,
kudura imeshapangwa, hakuna kubadilika,
Lazima kitakufika, kile kilicho andikwa.


Tangu bado kuzaliwa, vyote vimeandikika,
riziki imegawiwa, na ajali kadhalika,
utajiri ukipewa, usisahau sadaka,
Lazima kitakufika, kile kilicho andikwa.
 
Mimi nipo poa mambo, bado nayaangalia
vijana wenye vijambo, hoja mkizichangia
Naogopa kwenda kombo, nisije kuwaharibia
Nipo naogopa shombo, msije kunimwagia



Tangu bado kuzaliwa, vyote vimeandikika,
riziki imegawiwa, na ajali kadhalika,
utajiri ukipewa, usisahau sadaka,
Lazima kitakufika, kile kilicho andikwa.

Ninakuaminia kofia nakuvulia
Usiogope ushandani wewe vumilia
Ukienda kombo nitakushikilia

X-PASTER
Mashairi hayataki nipo kwenye simanzi............
 
Ninakuaminia kofia nakuvulia
Usiogope ushandani wewe vumilia
Ukienda kombo nitakushikilia

X-PASTER
Mashairi hayataki nipo kwenye simanzi............

Pole kwa yano kukuta, ushindani si kushinda
Kama ye ukumpata, Mwingine atakupenda
kutafuta si kupata, maneno si kutenda

Kitaka mke tawakali, tafuta mke muumini

Oa mke Muumini, funga ndoa tawakali,
Mke aloshika dini, na kila siku kuswali,
Hijaab iwe kichwani, afunike yote mwili,

Funga ndoa tawakali, oa mke Muumini.

Usitafute uzuri, au yule mwenye mali,
Chagua tabia nzuri, alotulia akili,
Aloleleka vizuri, kidini na kiasili,

Funga ndoa tawakali, oa mke Muumini.

Tafuta mke haraka, ukijiona kamili,
Ikufikie baraka, ya Mola Wako Jalali,
Utulie kwa hakika, tabia mbaya badili,

Funga ndoa tawakali, oa mke Muumini.

Fadhila zake ni nyingi, uliza kila pahali,
Huo ndio ni msingi, wa maisha ya halali,
Ni kinga kwa mambo mengi, kwa madhambi mbalimbali,

Funga ndoa tawakali, oa mke Muumini.

Kuoa ni utulivu, tumeshaona dalili,
Huyaondoa maovu, na mambo huwa sahali,
Hukufanya mtulivu, shida ikikukabili,

Funga ndoa tawakali, oa mke Muumini.

Wajibu wako timiza, nyumbani mpo wawili,
Mkikaa kuzungumza, na mambo kuyajadili,
Mjaribu kueleza, muelezane ukweli,

Funga ndoa tawakali, oa mke Muumini.

Mume ni msimamizi, kwa mali na kila hali,
Ayaonyeshe mapenzi, maneno kama asali,
Katika masimulizi, asiseme kwa ukali,

Funga ndoa tawakali, oa mke Muumini.


Mungu awape watoto, hao ni rasilmali,
Mke ni mama watoto, awe mwema na mkali,
Awatazame watoto, wasikuwe kijahili,

Funga ndoa tawakali, oa mke Muumini.

Mke ni nguzo nyumbani, kama vile matofali,
Na mume ndio rubani, huona yaliyo mbali,
Kamba ya Mungu shikeni, ibada iwe awali,

Funga ndoa tawakali, oa mke Muumini.

Mungu Watunze vigoli, pamoja na wanawali,
Wawe kama wa awali, kama zama za Rasuli,
Nimemaliza kauli, hapa nafunga kufuli,

Funga ndoa tawakali, oa mke Muumini.




A Bin E
 
Kwako Mohamedi Shosi, Ahsante nakugaia,
Kunipatia nafasi, Ya unaofagilia,
Kwako sina wasiwasi, Wote ulowasemea.

Magreti thinka makini, hakika umewataja.

Hukuweka kachumbari, Umesema ya moyoni,
waziwazi umekiri, Umeweka thiredini,
Hapa ninatafakari, Hata mimi Asprini?

Hapa nimevimba bichwa, Najiona jemedari.

Na. Big Braza ODM Asprin (Babu wa wajukuu)
Kaunta ya Juu
KingStar-Boko.
 
Kwako Mohamedi Shosi, Ahsante nakugaia,
Kunipatia nafasi, Ya unaofagilia,
Kwako sina wasiwasi, Wote ulowasemea.

Magreti thinka makini, hakika umewataja.

Hukuweka kachumbari, Umesema ya moyoni,
waziwazi umekiri, Umeweka thiredini,
Hapa ninatafakari, Hata mimi Asprini?

Hapa nimevimba bichwa, Najiona jemedari.

Na. Big Braza ODM Asprin (Babu wa wajukuu)
Kaunta ya Juu
KingStar-Boko.

huyo ndo odm mwenyewe a.k.a fildi masho,babu mewata etc,,,lol!uko juu
 
Unamtaka?...namba zake 0899300104-boko!...m'DIPU!

Aisee PJ inakuwaje unatoa namba za babu hadharani?

Unataka waniDIPU?
Ili wanipe majiPU?
Wanipake maupuPU?
Wanitie kwenye kaPU?

Babu nitaadhiriKA,
Kisha nitachokachoKA,
Nitashindwa kugeuKA,
Kurudia kwenye HulKA.
 
Aisee PJ inakuwaje unatoa namba za babu hadharani?

Unataka waniDIPU?
Ili wanipe majiPU?
Wanipake maupuPU?
Wanitie kwenye kaPU?

Babu nitaadhiriKA,
Kisha nitachokachoKA,
Nitashindwa kugeuKA,
Kurudia kwenye HulKA.
Uko kamili kiongozi!

Usiogope kuchoka.
Au kuingia chaka,
Hatutafanya dhikaha
Au kukuchekacheka.
 
Mohammed..................Hongera sana,shairi zuri sana hili..................Hakika una kipaji.....Guess what!!!!!.......Shairi lako hili limemtoa nyoka pangoni.......lol
 
Kwako Mohamedi Shosi, Ahsante nakugaia,
Kunipatia nafasi, Ya unaofagilia,
Kwako sina wasiwasi, Wote ulowasemea.

Magreti thinka makini, hakika umewataja.

Hukuweka kachumbari, Umesema ya moyoni,
waziwazi umekiri, Umeweka thiredini,
Hapa ninatafakari, Hata mimi Asprini?

Hapa nimevimba bichwa, Najiona jemedari.

Na. Big Braza ODM Asprin (Babu wa wajukuu)
Kaunta ya Juu
KingStar-Boko.

Mkuu kwa uchache wa maneno nakupa hongera sana inaonyesha hizi siku ulizokaa kimya ulitafuta kamusi na kitabu cha nahau ukaona mizinguo ukaamua kushusha mistari kutoka kichwani. Niliona kimya nikajua umechanja mbuga. Safi sana mkuu upo juu kama kichwa cha twiga. Nipo safarini nikifika nitakujibu kwa vesi.
 
Unamtaka?...namba zake 0899300104-boko!...m'DIPU!

Mkuu ukiingia humu mie naanza kujipanga kumtetea mama wa busara mpotezee leo mie sipo kwenye mudi ya kupoza maneno yako makali dhidi yake na isitoshe mnajua mtu na mtani mwenzie heheheheh
 
Mohammed..................Hongera sana,shairi zuri sana hili..................Hakika una kipaji.....Guess what!!!!!.......Shairi lako hili limemtoa nyoka pangoni.......lol

Shukrani sana mkuu Mungu akubariki...
 
jibaba hakika unatisha , katika hii fani
umetusambaratisha, malenga wa chochoroni
manzi umewadatisha, wewe kweli championi
halaf umetupaisha, senks from klorokwini.

kaka uko fiti! yaani we acha tu! keep it up bro halaf senks bana kwa kuinclude jina langu , mie nilikuwa naonaga nafuja tu hapa jamvini kumbe asavali kuna watu wananifeel. dah!
 
punguza maangaiko basi,hebu rudi kuleeeeeee,usiusononeshe moyo wangu kama pj

Mama wa busara, wakuu Asprin na PJ mwenzenu ninaugua ugojwa wa mahaba ninahitaji ushawishi wenu juu ya huyu binti nimezunguka humu JF nikaona yeye ndie anaenifaa kitabia, ucheshi wake na mwandiko wake. Mtakuwa mmefanya ya mbolea na busara ikiwa na nyie mtatoa mchango wenu na thanks maana mistari nimeshuka watu wamebana lol https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/107026-nakusihi-nilham-rashed.html
 
Back
Top Bottom