Mohammed Hamad
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 3,988
- 1,308
- Thread starter
- #161
Hakika umetamba,
Tenzi kutaramba,
Mods kuwapamba,
Members kuwaimba,
Niaba ya Robot MTAMBA,
Shukurani kutoifumba,
Kwako tumeiumba,
Kwa tungo kujiramba
SHOSSI umebamba
Kanuni shika,
Hutoguswa hakika,
wale mlahaka,
walo na dhihaka,
JamiiForums siyo chaka,
Ni kiota kwa wahajaka,
SHOSSI umesomeka
Mkuu umesomeka, Kanuni nitazifata
JF si kichaka, hilo nimelipata
Hakika nimefarijika, kwa shukrani zako kuzipata
Kumbe wewe mshairi, mbona ulikaa kimya?
Au uliiunda safari, kukifungua kinywa?
Beti zako murua mistari yako hatari
Tungo yako ni muwa, wenye utamu wa sukari
Kaditama namaliza nakuombea ya kheri
Mwaka tuumalize bila kupata ya shari