Magreat Thinkers ninaowafeel...........

ewe cheusi mangala, salamu nakutmia,
mola anayetawala, akupe nyingi jalia,
usijeingia hila, nduguzo kutuchukia
...upatapo siku mbili, moja ututembelee.

uliondoka ghafula, ukatuacha na njia
ndege ukaidandila, ukapotea sawia
hatuna hamu ya kula, hata maji kunawia
...ile namba ya nduguyo,

Natamani kukujibu kimalenga ila kila nikijaribu nashangaa najiwa na kigugumizi,
nashukuru kwa kunitakia mema Pj.
hapo pekundu,hilo haliwezekani,niliwapenda mwanzo,nilifurahia muda wote niliokuwa nanyi na nitawapenda siku zote.
hapo pa blue tuko pamoja.
 
Cheusimangala upo? Mudy Shossi hajasahau,
Labda beti lijalo umo, ataghani kwa nahau,
Wala usiwe na kinyongo, kwenye listi hatakusahau.

mim nipo nimejaa tele,
usiwe na hofu kinyongo sio moja ya sifa zangu,ukinifahamu vizuri utadhibitisha hilo.
 
Kazi unayonituma, sina budi ujira kupatana Utaweza kubali, matai tusije kamatana Nataka nyama ilonona tena mwanana Sitakiutumbo japo wachanga wanapikia banana Walasitaki yakidadi kwenye meno yashikana Wala sitaki ya mbuzi hata iwe kilo nane Nataka paja la swala alienona mwanana Wiselady nauliza je wajua kuwinda?

Malipo ya swala utapata uwindaji ntasaidiana na kimakole,shaka ondoa ila kumbuka nimeomba msaada:typing:
 
Nimechoka, nimechoka mie, nataka enda mie jama,
Wajibu nikatimizie, wangu ubavu unalalama,
Hizi kazi nisisingizie, kumbe JF nimezama

Mudy Shossi tutaonana, huenda kesho ya Maulana,
PakaJimmy sijamuona, namuaga hata kama,
Cheusimangala mama, nakutakia usiku mwema

Mwandani kanikonyeza, anitega kinamna,
Vidole kavitembeza, kunako akanibinya,
Nikaona mmh anichokoza, cha moto atakiona
ooooooh kibodi siwezi bonya......
 
Wa kuwinda Wiselady? Sijui wamaanisha nini,
Au wataka weledi, watufumba tuachwe mjini,
Asije akamaindi, akakasirika mwandani
kusaidiana ni jadi, akuomba Wiseladi

kimokole do ze needful basi maana masharti ya shossi yako juu,either umjibu PJ au tuwinde swala wa MS
 
Wanajamvi mbona mmeingia mitini Au tungo zenye vina Vimeishia kichwanI Mwanakijiji hajanena au yupo kazini
 
gt humu tu wawili, japo moja ni wa longi
gt mimi nipo tuli, wanajamii siwasongi
tena bado sina mwali, bado naruka vigingi
punde taweka tangazo, nami nipate mwandani

GT wake mdogodogo mwendo, wajulikana zamani
Mwendo usio vishindo, haufeli abadani
Asoweza huwa kando, awezae huwa ndani
 
Kaka Mo mie najitolea kuwa meneja wako ili kusiwe na piracy ya kazi zako. Big up to yourself
 
gt humu tu wawili, japo moja ni wa longi
gt mimi nipo tuli, wanajamii siwasongi
tena bado sina mwali, bado naruka vigingi
punde taweka tangazo, nami nipate mwandani

Kweli wewe si wasongi, malenga mashuhuri
Umejikita kama kigingi, mwingi wa sururi
Usijeoa giningi, walakwa waikwiriri
Usije oa shangingi maisha ukayaona shubiri
 
Mkuu, ingawa maneno mengine ya kiswahili yamenipiga chenga but it is so creative of you, many thanks
 
Nimechoka, nimechoka mie, nataka enda mie jama,
Wajibu nikatimizie, wangu ubavu unalalama,
Hizi kazi nisisingizie, kumbe JF nimezama

Mudy Shossi tutaonana, huenda kesho ya Maulana,
PakaJimmy sijamuona, namuaga hata kama,
Cheusimangala mama, nakutakia usiku mwema

Mwandani kanikonyeza, anitega kinamna,
Vidole kavitembeza, kunako akanibinya,
Nikaona mmh anichokoza, cha moto atakiona
ooooooh kibodi siwezi bonya......

mmh nikitizima huo ubeti wa mwisho nashindwa hata kukubembeleza uendelee kutupa company hapa jamvini.
haya asante,nanyi mkalale salama.
 
mazito maneno yako, yameshamiri busara
shangingi wanambeleko, washikapo mtu hasara
nitatumia viwiko, nakukopa busara
umakini tatumia, kumpata wangu mwanana

Kweli wewe si wasongi, malenga mashuhuri Umejikita kama kigingi, mwingi wa sururi Usijeoa giningi, walakwa waikwiriri Usije oa shangingi maisha ukayaona shubiri
 
jamani jamani jamani sijui kwanini nimechelewa kwenye thread yako..... heheheh kumbe na mie nimoo ee kwa kuchangia jf....haya shukran mohammed.birthday yako ikifika nambie nikuletee bonge ya zawadi ukumbini,,, umeskia ee??..:msela::msela::msela::msela::msela::msela:
 
Kaka Mo mie najitolea kuwa meneja wako ili kusiwe na piracy ya kazi zako. Big up to yourself

Realman wanichesha, meneja uso kitambi
Tungo hujasherehesha, usije niwacha kwa kumbi
Nadhani mdomo wakuwasha,ukazungumza kimatumbi
Kana unaumwimbi,si ungekula tambi?
Duh nimechoka maneno sina
 
Katu sinalo neno, Muddy Shossi ninakiri
wako tenzi msumeno, wanifanya nifikiri
hata ingekuwa memo, ningeshindwa ninakiri
Utenzi huu pekee, umenigusa mtima


Aksante
 
Bora iweke moyoni , hiyo siri mwana flani
Siri ibaki sirini, siyo tena hadharani
Hapo utaweza wini, ewe mtunzi makini

Wakuu safi sana ndio nawasoma saizi, mko fiti, kumbe WOS sio mchezo, nilikuwa nakutafuta sana sisteri umepotelea wapi?? Mohamed unatisha mkuu, uko juu, vina vimetulia kinoma. Kweli watokea Tanga.
 
Mkuu nimeuvulia kofia! Heshima kwako maana umetishaa na kushine kiukweliii ! Thx sana.
 
Back
Top Bottom