Nilishafanya mitihani mingi hasa ya shule nikamaliza,sikujua kama ntakuja kukutana na mtihani mwingine kama huu!
Nilijiuliza nitawezaje kulala chumba kimoja na binti mrembo kaa yule nma nisiwaze kumgusa!
Baada ya kumwambia vile kuwa nimeambiwa nilale naye mle ndani,yule binti alinikaribisha ndani huku akionyesha kutokuwa na wasiwasi wowote jambo lililozidi kunitia wasiwasiw!
Yule binti alitandika chini kisha akataka mi nilale kwenye kile kitanda cha chuma chenye kigodoro cha pamba!
“Hapana wewe lala hapo juu mi ntalala chini!”
“hapana kaka wewe lala kitandani tu,wewe ni mgeni!”
Tulibishana sana ila sikukubali kulala kitandani,mwisho yule binti ambaye nilisikia yule mzee anamuita Regina akakubali kulala kitandani!
Nililala pale chini baridi lilikuwa kali kiasi cha kushawishi kumkumbatia yule dada tupeane joto!Ila nilipowaza kauli ya yule mzee kuwa nisifanye naye chochote nilituliza nyege zangu!
“Huku kutafutana ubaya tu,huyu mzee ananitafutia sababu tu aniroge anipeleke Gamboshi huyu!Anawezaje kumlaza Simba kwenye banda la swala?Ila hanipati kudadeki!”
Nilijisemea japo hisia zilikuwa kali,shetani alikuwa kazini anafanya kazi yake,usingizi ulikuwa mgumu sana siku ile!
Sijui nililala sangapi nilikuja kushtuka asubuhi jogoo anawika,nilifumbua macho nikaangalia kitandani sikumuona yule binti,nikajua tu alishaamka zamani,mabinti wa kijijini huamka mapema siyo kama wale wa mjini wanaokesha whatsap na insta!
Nilikurupuka nikajinyoosha,kwa mbali nilihisi mbavu zinauma sababu ya kulala chini,ila nilishukuru sababu nililala ndani kuliko kulala nje,halafu sehemu yenyewe ni Sumbawanga sasa!
Nilitoka nje nikamkuta yule mzee amewasha moto halafu amekaa pembeni yake,nilisogea pale sababu kulikuwa na baridi sana!
Nilichukua kigoda nikakaa pembeni ya yule mzee ambaye niligundua kwenye ule moto alikuwa anachoma viazi vitamu!
“Karibu kijana!”
“Ahsante sana shkamoo mzee wangu!”
“Marahaba kijana!”
Bado nilikuwa sijiamini amini,nilikuwa nawaza itakuwaje yule mzee akisema nimefanaya mapenzi na binti yake?
Ukimya ulitawala kati yetu muda huo yule mzee akatoa kiazi kimoja kwenye ule moto akanipatia!
Nilikipokea nikakiweka chini maana kilikuwa cha moto hatari,sijui hata yule mzee aliwezaje kukishika!
Muda huo yule binti alikuja akiwa amebeba maji,nikajua tu anatoka kisimani,nilipata muda sasa wa kumuona vizuri mrembo yule!
Dah!nilijisifu sana kuushinda mtihani ule,moyoni nilikiri nimekuwa sasa maana siyo kwa mtihani ule duh!
Nilipogeuza shingo kumuangalia yule mzee,nilikuta ananiangalia nikainama chini kwa aibu maana kaniona nilivyokuwa namtathimini binti yake!
“Hahahahahahah kijana!”
Alicheka yule mzee nisijue anacheka nini?nilikuwa mtu wa mashaka mashaka tu bado sikujiamini kabisa!
“Hongera kijana wewe ni mwanaume,uanaume siyo kufungua zipu tu hata ukijifunza kuifunga ni uanaume tena uanaume wa kweli!”
“Unamaanisha nini mzee wangu?”
“Namaanisha usiwe kama mbwa kila mgeni unambwekea tu ukiamni ni mtu mbaya!unaonekana utakuwa mgeni wa tofauti kuliko wageni wengine,kwa ajili yako naweza kuwaza kukishauri kijiji changu kianze kupokea wageni tena!”
“Wageni!!!!”
Niliuliza kwa mshangao cha ajabu yule mzee akaondoka zake huku anacheka,nilianza kuwaza namna nilivyopokelewa na wanakijiji wa pale,nilipounganisha na maneno ya yule mzee nilishindwa kuelewa,nikabaki na maswali mengi kichwani!
“WAGENI WANA NINI KWENYE HIKI KIJIJI?”
Licha ya kilichonileta nilitamani pia nifanye uchunguzi nijue kuna siri gani ya kile kijiji na wageni!
Yule binti alimaliza kuchota maji akachemsha uji na viazi tukanywa,muda ule yule mzee hakuwepo,alikuwa ameshaondoka zake!
Nilianza utafiti wangu kwa ajili ya kitabu changu kwa kumuuliza mambo mbali mbali yule binti ambaye alinipa ushirikiano wa kutosha kabisa!
Baada ya kumuuliza maswali yangu karibu yote ndipo nikaamua kumuuliza hili duku duku langu kuhusu wageni!
“Hivi Regina!”
“Rabeka!”
“Kuna kitu nataka nikuulize!”
“Kitu gani kaka halafu hujaniambia unaitwa nani?”
“Naitwa Jack Mambo!”
“Mmh aya unataka uniulize nini?”
“Oooh!nataka kujua kuna nini kwenye hiki kijiji mpaka wageni haw apokelewi vizuri?”
Swali lile lilimfanya Regina ainame chini na uso wake ukabadilika,ghafla akainuka akaacha kula na kuondoka!
Nilibaki njia panda yule mzee kasikia wageni kainuka akaondoka,Regina naye hataki kusema chochote,kuna nini katika kijiji hiki?wageni walikosea wapi?
JE NINI WAGENI WALIKOSEA WAPI HAPA KIJIJINI?USIKOSEEE