Sasa utalii wa kenya na Tanzania unafanana isipokuwa sisi tuna mlima Kilimanajro iweje tusiwaangalie? Naonaga kampuni ambazo zinauza bidhaa zinazofanana lazima zinaangaliana na kupanga kuendana na mwingine ili kuvutia wateja, why nitembelee Tanzania nilipe $1000 kwenda kuona simba, wakati naweza muona kenya kwa $500. Hawa maprof wa Tanzania ni wa ajabu Mno! Yaani maghembe ni mwepesi kichwani kama tissue!
Ndugu zangu watanzania wapenda maendeleo na wadau wa biashara ya utalii napenda niwasilishe kwenu masikitiko yangu baada ya kusikia kwamba sereikali yetu imepitisha ongezeko la 18% kwa tozo za wageni wanao tembelea taifa hili lililo jaliwa vivutio vya kila aina.
Ongezeko la 18% litapunguza kwa asilimia kubwa idadi ya watalii wanaotembelea Tanzania, kwani mpaka sasa Tanzania nighali kwa 7% ukilinganisha na nnchi zingine kama vile, Kenya, Zimbabwe, Botswana, South Africa na zingine wakati nchi washindani wanapunguza tozo sisi tunaongeza.
Pia ongezeko hilo litapunguza ajira kwawatanzania wengi, kwani secka hii imeajili vijana wengi sana,
mfano: mtalii 1 anaekuja kupanda mlima Kilimanjaro kwa siku 6 atambatana na watanzania wasio pungua 9 , ikiwa ni waongoza watii , wabeba mizingo na wapishi na madereva, kwa maana hiyo tukimkosa mtalii mmoja tunapoteza ajila kwa watanzania 9. Pia wafanya biashara wa vyakula masokoni na madukani watakosa wateja.
Tangu serikali ilipotangaza kuongezeko la tozo kuna kampuni imepokea Cancelation 1500, ina maana wageni hao hawatakuja tena Tanzania , can you imagine tutakuwa tumepoteza ajila ngapi kwa watanzania na serikali itapoteza mapato kiasigani???, hiyo ni campuni moja, na Tanzania kunamakapuni mangapi ya waongoza watalii ???
Pia ikumbukwe kwamba wageni wanao kuja sasa walishafanya booking zao mda mlefu na kunakampuni zingine nzimesha pokea malipo ya booking za wageni wao hadi mwaka 2017 , leo hii unaongeza 18% katikati ya msimu hicho kiasi kinacho ongezeka kitatoka wapi, kiukweli siokwamba tunakataa kulipa kodi lakini sasa serikali yetu sikivu ingeliangalia hili kwa umakini maana tutahaliku kabisa secta ya utalii.
Kwa upande mwingine wizara ya maliasili ijalibu kulinganisha wenzetu wanafanyaje ili kukuza utalii, Kwamfano majirani zetu Kenya, Wana ndege zao zinazo litangaza taifa lao kimataifa, sisi hatuna ndege wala badgeti inayopangwa haitoshi hutangaza Tanzania kimataifa. Tusiangalie kuongeaza kodi kabla ya kuboresha .
Jambo lingine la kusikitisha ni Tanzania kuto shiriki mamonyesho ya kimataifa ya ITB yanayo fanyika ujerumani , kwastail hii tunaongezaje idadi ya watalii Tanzania , na hiyo 18% tutamchaji nani wakati hatujitangazi???,
Kuna sekta zingine sio za kuzifanyia mchezo kwenye suala la kukuza uchumi wa nchi, ukizingatia Utalii ndo unaongoza kwa kulipatia taifa pesa za kigeni.
Mungu ibariki Tanzania