Maghembe: Tanzania sio koloni la Kenya

Maghembe: Tanzania sio koloni la Kenya

Top Ten tourist destination in Africa

1. South Africa: Main Attractions (Kruger National Park, Table Mountain, Cape Winelands)
2. Seychelles : Main Attractions (Anse Intendance, Morne Seychelles National Park, Marine National Park)
3. Mauritius: Main Attractions (Black River Gorges National Park, Gabriel Island, Casela Nature Park)
4. Morocco: Main Attractions (Djemaa el Fna, Essaouira, Chefchaouen)
5. Namibia: Main Attractions (Etosha National Park, Fish River Canyon, Skeleton Coast)
6. Kenya: Main Attractions (Maasai Mara National Reserve, Malindi, Lake Naivasha)
7. Tunisia: Main Attractions (El Djem Amphitheatre, Sidi Bou Said, Bulla Regia)
8. Egypt: Main Attractions (Great Pyramid of Giza, Egyptian Museum, Valley of the Kings)
9. Cape Verde: Main Attractions (Cabo Verde Safari, Mindelo, Museu Municipal)
10. Main Attractions: Okavango Delta, Tswapong Hills, Mokolodi Nature Reserve

12. Tanzania (duniani ya 93) maajabu yenyewe ukitoa (attraction za Egypt) kila kitu kilichopo nchi nyingine na kwetu kipo in bigger size. Thats the tip of the iceberg hakuna nchi duniani inaishinda Tanzania kwa geological wonders apparently ata a good gaze into the heavens during the night Tanzania gives a better view of Andromeda Galaxy sio mimi nimemuona mzungu kwenye science documentary andai hivyo.

Hiyo Helium tunayoishangilia imegundulika sijui Kigoma chanzo chake 'Olduvai George' ambapo chini inafukuta na mzungu mwingine kwenye science documentary anadai afrika iko tayari kuachia (in pangea) style na ushahidi wa gesi inayotoka chini kwa kasi upo Tanzania kupitia olduvai george volcano; apparently the first gas which is emitted in natural combustion is helium ndiyo hiyo mnayoishangalia.

In short nchi ina kila kitu kuzidiwa na nchi kama Kenya kwa idadi ya utalii ni kipimo cha uzembe wetu; tatizo ni watu kama huyu Maghembe badala ya kufikiria kushindana analeta nyodo za viongozi wa Tanzania these people tend to think very highly of themselves and arrogant wakiwa mawaziri wakati ovyo kweli wengi wao Phd (my foot).
 
Safi saana! Hii ndiyo aina uongozi niliyoisubiri maisha yangu yote, dadadeki!
Hatutaki Watalii masikini wa kugombania chips mayai na sisi kitaani, tunataka Watalii wa kuspend hela ndefu, hao watalii masikini kwanza wanaharibu mazingira yetu!
le mbebez maskin kumbe mko wengi kha si kwa comment hii
 
Sasa utalii wa kenya na Tanzania unafanana isipokuwa sisi tuna mlima Kilimanajro iweje tusiwaangalie? Naonaga kampuni ambazo zinauza bidhaa zinazofanana lazima zinaangaliana na kupanga kuendana na mwingine ili kuvutia wateja, why nitembelee Tanzania nilipe $1000 kwenda kuona simba, wakati naweza muona kenya kwa $500. Hawa maprof wa Tanzania ni wa ajabu Mno! Yaani maghembe ni mwepesi kichwani kama tissue!
Kunautofauti wamazingira mkuu..... Kumwona simba tarangile ni tofaut na kenya..... Mazingira mkuu..... Hilo kwanza(movie kuiangalia cinema ni tofauti na kuangalia movie hyo hyo nyumbani)
 
Raisi Magufuli ni genius watu mediocre hawawezi kumuelewa, hivi wewe unajua Kagame ni nani Dunia hii?
Unajua influence ya Kagame wewe kwa Wazungu?
Waulize Ufaransa na Ujerumani, Kagame ndiyo raisi pekee hapa Afrika anayeweza kuongea na wakubwa wa hii Dunia, Kagame ni namba nyingine usiguse kabisa ...
poor think capacity so what is he can ?
 
...bali Tanzania ni koloni la Rwanda.

Moshi. Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amesema Tanzania siyo koloni la Kenya kwamba kila mipango yake ya maendeleo itegemee Taifa hilo.

“Kenya siyo sehemu ya Tanzania na sisi (Tanzania) si koloni la Kenya. Kenya ni nchi tofauti, Uganda ni nchi tofauti, Uingereza ni nchi tofauti,” amesema Profesa Maghembe.

Profesa Maghembe ametoa kauli hiyo kufuatia malalamiko ya mawakala wa utalii wanaodai hatua ya Serikali kutoza Vat kwenye utalii kutaathiri sekta hiyo na kwamba, watalii wengi wamesitisha safari zao na wengi wameamua kwenda Kenya kwa vile nchi hiyo imeondoa kodi hiyo.

“Hizi ni kodi ndani ya Tanzania. Kenya ina mazingira tofauti kabisa na Tanzania. Hatuwezi kupanga kodi kwa maendeleo ya nchi yetu tukiwatazama wao,” amesema.

Chanzo:Mwananchi online
 
Hivi watu wanaofanya Kazi TTB au wizara ya Mali asili na utalii au Wizara ya Fedha

Wafanyakazi wa TANAPA, Ngorongoro ......

Woote hakuna member JF?

Wanasoma siasa za Jeuri za Boss wao??? Wanamchukuliaje?

Watanzania, wekeni siasa pembeni...angalieni figures and facts........
 
Coca cola inauzwa 1000 na Azam Cola inauzwa 700.. Still Coca cola inauza zaidi ya hiyo Azam Cola.. Tusiwe watu wa kulaumu tu, tusubiri tuone tutakachovuna kwenye Utalii mwaka huu alafu tukifananishe na kile cha mwaka jana..

SWOT analysis haimaanishi tu uangalie bei anayotoz competitor wako.. Lakini Strength and his Weaknesses.. Wakenya bado wana jinamizi la ugaidi na Mtalii yeyote makini na mwenye uwezo mzuri hatokubali kwenda kuhatarisha maisha yake Kenya hasa kipindi hiki cha jinamizi la kujitoa muhanga..
Jidanganye na hiyo SWOT analysis yako uliyoisomea sijui zoom poltechnique ama maana kwa suala la utalii ndugu ni more that SWOT ya kawaida sasa subiria hata hao 1m utawaskia kwa majirani wako na huku kuporomoka kwa uchumi duniani watu wanabana matumizi si matajiri wala maskini wanaenda na strong budget ,value for money and customer service.Mwenzio weakness yako kaifanya strength chezea.
 
Ni kweli kabisa. Watalii hujiandaa muda mrefu na kuja kuona kivutio fulani kinachopatikana sehemu fulani hela kwao sio issue hivyo hata hao wakenya wakifanya bure kabisa na vivitio hivyo vipo bongo itabidi waje walipe tuu
 
Mzee Magembe weka hakiba ya maneno baba,hizi nchi zipo jirani na zina shabihiana hasa kwenye mali za asili,sasa wadau wa utalii wanapokushauri au kukuambia jambo ujue kuna jambo wameliona baba.
Waende tu huko kenya, huku hamna vya bure!!
 
Ndugu zangu watanzania wapenda maendeleo na wadau wa biashara ya utalii napenda niwasilishe kwenu masikitiko yangu baada ya kusikia kwamba sereikali yetu imepitisha ongezeko la 18% kwa tozo za wageni wanao tembelea taifa hili lililo jaliwa vivutio vya kila aina.

Ongezeko la 18% litapunguza kwa asilimia kubwa idadi ya watalii wanaotembelea Tanzania, kwani mpaka sasa Tanzania nighali kwa 7% ukilinganisha na nnchi zingine kama vile, Kenya, Zimbabwe, Botswana, South Africa na zingine wakati nchi washindani wanapunguza tozo sisi tunaongeza.
Pia ongezeko hilo litapunguza ajira kwawatanzania wengi, kwani secka hii imeajili vijana wengi sana,

mfano: mtalii 1 anaekuja kupanda mlima Kilimanjaro kwa siku 6 atambatana na watanzania wasio pungua 9 , ikiwa ni waongoza watii , wabeba mizingo na wapishi na madereva, kwa maana hiyo tukimkosa mtalii mmoja tunapoteza ajila kwa watanzania 9. Pia wafanya biashara wa vyakula masokoni na madukani watakosa wateja.

Tangu serikali ilipotangaza kuongezeko la tozo kuna kampuni imepokea Cancelation 1500, ina maana wageni hao hawatakuja tena Tanzania , can you imagine tutakuwa tumepoteza ajila ngapi kwa watanzania na serikali itapoteza mapato kiasigani???, hiyo ni campuni moja, na Tanzania kunamakapuni mangapi ya waongoza watalii ???

Pia ikumbukwe kwamba wageni wanao kuja sasa walishafanya booking zao mda mlefu na kunakampuni zingine nzimesha pokea malipo ya booking za wageni wao hadi mwaka 2017 , leo hii unaongeza 18% katikati ya msimu hicho kiasi kinacho ongezeka kitatoka wapi, kiukweli siokwamba tunakataa kulipa kodi lakini sasa serikali yetu sikivu ingeliangalia hili kwa umakini maana tutahaliku kabisa secta ya utalii.

Kwa upande mwingine wizara ya maliasili ijalibu kulinganisha wenzetu wanafanyaje ili kukuza utalii, Kwamfano majirani zetu Kenya, Wana ndege zao zinazo litangaza taifa lao kimataifa, sisi hatuna ndege wala badgeti inayopangwa haitoshi hutangaza Tanzania kimataifa. Tusiangalie kuongeaza kodi kabla ya kuboresha .
Jambo lingine la kusikitisha ni Tanzania kuto shiriki mamonyesho ya kimataifa ya ITB yanayo fanyika ujerumani , kwastail hii tunaongezaje idadi ya watalii Tanzania , na hiyo 18% tutamchaji nani wakati hatujitangazi???,

Kuna sekta zingine sio za kuzifanyia mchezo kwenye suala la kukuza uchumi wa nchi, ukizingatia Utalii ndo unaongoza kwa kulipatia taifa pesa za kigeni.

Mungu ibariki Tanzania
Bora umesema wasikie! Hii wizara ni kubwa Mno kwa prof maghembe! Wakati wadau wa utalii mnalalamika lazima pia mseme tatizo ni maghembe, msilalamike tu bila kusema tatizo ni nini! Maghembe hajui utalii anajua magogo na misitu tu msione aibu kusema kuliokoa taifa.
 
Back
Top Bottom