Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,068
- 151,315
Moshi. Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amesema Tanzania siyo koloni la Kenya kwamba kila mipango yake ya maendeleo itegemee Taifa hilo.
“Kenya siyo sehemu ya Tanzania na sisi (Tanzania) si koloni la Kenya. Kenya ni nchi tofauti, Uganda ni nchi tofauti, Uingereza ni nchi tofauti,” amesema Profesa Maghembe.
Profesa Maghembe ametoa kauli hiyo kufuatia malalamiko ya mawakala wa utalii wanaodai hatua ya Serikali kutoza Vat kwenye utalii kutaathiri sekta hiyo na kwamba, watalii wengi wamesitisha safari zao na wengi wameamua kwenda Kenya kwa vile nchi hiyo imeondoa kodi hiyo.
“Hizi ni kodi ndani ya Tanzania. Kenya ina mazingira tofauti kabisa na Tanzania. Hatuwezi kupanga kodi kwa maendeleo ya nchi yetu tukiwatazama wao,” amesema.
Chanzo:Mwananchi online