Maggid Mjengwa: Msimamo wa Serikali kuhusu mradi wa Bagamoyo ni Sahihi

Hatutaki Kujifunza, Sri Lanka Waliota Kama Sisi, Yakawafika..

Ndugu zangu,

Pichani askari wa Sri Lanka waliokuwa wakipambana na waandamanaji walioingia mitaani kupinga mji wa bandari yao kukabidhiwa Wachina.

Hambantota ni mji wa bandari ambapo WaSri lanka waliota kuwa ungejengwa na kuwa wa kisasa kuufanya kuwa mji wa pili kwa ukubwa nchini mwao. Ni kwa fedha za mkopo kutoka China dola za Kimarekani bilioni 16.

Kwamba bandari ya Hambantota yenye kina kirefu kupokea meli kubwa za dunia ingejengwa na kuwa ya kisasa zaidi. Ni pamoja na mji wenyewe wa Hambantota.

Ninavyoandika hapa Hambantota si sehemu tena ya Sri Lanka. Imekabidhiwa kwa Wachina Julai 31,2017. Haya yote si siri kwa tunaojaribu kuhangaika kutafiti. Yapo yameandikwa.

Nini kiliwatokea wenzetu?

Walikuwa na ndoto ya kupata bandari mpya na mji wa kisasa kwa fedha za mkopo. Mkopo ukawa na riba kubwa na mapato ya bandari yakawa kiduchu.
Serikali nayo hazina yake haikuwa na fedha za kutosha. Ukaja ugumu wa kulipa.

Ikafika siku ya kubwaga manyanga. Waziri Mkuu wa Sri Lanka Ranil Wicremesinghe Julai 31, 2017 kwa huzuni kubwa akaisalimisha bandari na mji kwa China Merchants Ports Holdings mpaka mwaka 2116. Ni mwaka elfu mbili mia moja na kumi na sita. Si ajabu wananchi wenye hasira waliingia mitaani kuandamana. Ni kampuni hiyo hiyo ambayo baadhi yetu wanaililia ije haraka katika masharti yatakayotupelekea kutufika kama ya wenzetu. Inashangaza.

Nani wa kulaumiwa?

Rais wa zamani wa Sri Lanka, Mahinda Rajapanska baada ya kukosa sapoti kwa nchi za Magharibi akakimbilia mikopo ya ujenzi kwa Wachina ili kubaki na umaarufu nyumbani.
Kumbe, aliwachimbia kaburi watu wake.

Tuna ya kujifunza, hata kama hatutaki, tujilazimishe.
Soma hapa: http://www.dailymirror.lk/article/SL-formally-hands-over-H-tota-port-to-China-141897.html
Maggid

View attachment 1099033View attachment 1099034
MJENGWA KAPOTEA SANA KWENYE SOCIAL NETWORKS HASA JAMII FORUM.

WAKATI WA JK ALIJITAHIDI SANA SIJUI KULIKONI??
 
Hakuna haja ya kumpa sifa yeyote katika hili,kikubwa ni kupata vigezo na masharti ya mkataba,hapo ndo pakubwa, halafu tutaazimia kwamba inafaa ama lah.
 
Hatutaki Kujifunza, Sri Lanka Waliota Kama Sisi, Yakawafika..

Ndugu zangu,

Pichani askari wa Sri Lanka waliokuwa wakipambana na waandamanaji walioingia mitaani kupinga mji wa bandari yao kukabidhiwa Wachina.

Hambantota ni mji wa bandari ambapo WaSri lanka waliota kuwa ungejengwa na kuwa wa kisasa kuufanya kuwa mji wa pili kwa ukubwa nchini mwao. Ni kwa fedha za mkopo kutoka China dola za Kimarekani bilioni 16.

Kwamba bandari ya Hambantota yenye kina kirefu kupokea meli kubwa za dunia ingejengwa na kuwa ya kisasa zaidi. Ni pamoja na mji wenyewe wa Hambantota.

Ninavyoandika hapa Hambantota si sehemu tena ya Sri Lanka. Imekabidhiwa kwa Wachina Julai 31,2017. Haya yote si siri kwa tunaojaribu kuhangaika kutafiti. Yapo yameandikwa.

Nini kiliwatokea wenzetu?

Walikuwa na ndoto ya kupata bandari mpya na mji wa kisasa kwa fedha za mkopo. Mkopo ukawa na riba kubwa na mapato ya bandari yakawa kiduchu.
Serikali nayo hazina yake haikuwa na fedha za kutosha. Ukaja ugumu wa kulipa.

Ikafika siku ya kubwaga manyanga. Waziri Mkuu wa Sri Lanka Ranil Wicremesinghe Julai 31, 2017 kwa huzuni kubwa akaisalimisha bandari na mji kwa China Merchants Ports Holdings mpaka mwaka 2116. Ni mwaka elfu mbili mia moja na kumi na sita. Si ajabu wananchi wenye hasira waliingia mitaani kuandamana. Ni kampuni hiyo hiyo ambayo baadhi yetu wanaililia ije haraka katika masharti yatakayotupelekea kutufika kama ya wenzetu. Inashangaza.

Nani wa kulaumiwa?

Rais wa zamani wa Sri Lanka, Mahinda Rajapanska baada ya kukosa sapoti kwa nchi za Magharibi akakimbilia mikopo ya ujenzi kwa Wachina ili kubaki na umaarufu nyumbani.
Kumbe, aliwachimbia kaburi watu wake.

Tuna ya kujifunza, hata kama hatutaki, tujilazimishe.
Soma hapa: http://www.dailymirror.lk/article/SL-formally-hands-over-H-tota-port-to-China-141897.html
Maggid

View attachment 1099033View attachment 1099034
Kuna baadhi ya viongozi wetu hawaitakii nchi yetu mema kwani siamini kama haya yote hawayafahamu. Ubinafsi na kujifanya miungu wadogo humu nchini na hodari sana kupiga kelele za kulaumu serikali pale ambapo mambo hayaendi kama wanavyotaka.
Uzuri mmoja tumeanza kuwafahamu kwani wanavaa majoho ya utukufu wakati wao ndiyo mashetani wanaotaka kuipoteza nchi hii.
Ninafurahi kuona serikali yetu inaendelea na misimamo ya kuiendeleza nchi yetu ili vizazi vijavyo vione fahari ya kizazi kilichopita.
 
Aliechanganua huu mradi alikuwa mwizi. Hata tupige kelele vipi hii bandari haina tija ni HASARA. Kwanza kutumia bilioni 9 kuondoa mchanga every year wakati kuna natural harbour Mtwara na Tanga ni ukichaa. Hongera Rais heri nusu shari kuliko shari nzima.
 
Mjengwa stori stori (in ibo voice)
Wakati mikataba Hii inasainiwa mlikuwa washauri wa Mzee wa Msoga sasa leo ndio mnayaona
Mnafurahisha sana mjue
Mikataba mibovu mingi tu
Ule wa Dodoma eti Wachina wanajenga
Nyie haya
 
Wachina hapo wanaenda kushika pabaya!! mfano mzuri ni majirani zetu Kenya, juzi kidogo China wachukue bandari ya Kenya kwa mchezo huu huu!!
Chonde chonde Ndugai na genge lake wasiuze nchi yetu! walizotuibia hazitoshi mpaka wanatake na kuuza nnchi yetu!!??
 
Hizo ndiyo data za reference wakati wa majadiliano na si kuwa kwa sababu ilikuwa hivyo Sri Lanka au na kwingine then mradi huo hautufai. Tunapaswa kujifunza kutokana na makosa ya wenzetu na kuweka terms and conditions ambazo zitaepusha nasi kuwa kama wao na si kukataa kwa sababu wengine walifanya makosa.

Tofauti na Sri Lanka, Tanzania haikopeshwi bali mwekezaji anakuja na mtaji wake 100%, hii ni tofauti na Sri Lanka. Haiwezekani mtu awekeze pesa zake na asiangalie risk za uwekezaji na ku calculate payback period na jinsi atakavyo pata faida. Kwa upande wetu tuangalie tu kuwa kuna faida yoyote tutapata au tuache Mbegani na Milongotini pabaki na mikorosho na wazee wetu wale.
Kuna ukweli kidogo sana kufuatana na mkataba uliyo, Masharti yeyote ambayo mwekezeji anataka uweke dhamana au umiliki wa halali wa mali yake basi inamaana huodio ukopeshaji una masharti!!!!

Kumilikisha Ardhi kwa miaka ama 66 au 99 ni kuweka hiyo mali kiudhamini. Anaekudai collateral kwa anacho kuazima ni lugha tuu maana yake anakuku kopesha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo ndiyo data za reference wakati wa majadiliano na si kuwa kwa sababu ilikuwa hivyo Sri Lanka au na kwingine then mradi huo hautufai. Tunapaswa kujifunza kutokana na makosa ya wenzetu na kuweka terms and conditions ambazo zitaepusha nasi kuwa kama wao na si kukataa kwa sababu wengine walifanya makosa.

Tofauti na Sri Lanka, Tanzania haikopeshwi bali mwekezaji anakuja na mtaji wake 100%, hii ni tofauti na Sri Lanka. Haiwezekani mtu awekeze pesa zake na asiangalie risk za uwekezaji na ku calculate payback period na jinsi atakavyo pata faida. Kwa upande wetu tuangalie tu kuwa kuna faida yoyote tutapata au tuache Mbegani na Milongotini pabaki na mikorosho na wazee wetu wale.
Yaan wewe ungekuwa mwanangu ningekuachia laana
 
Srilanka walikopeshwa wakashindwa kulipa wamenyanganywa.
Wakijenga kwa gharama zao watabaki na Bandari wakiiendesha kwa 99yrs au zaidi Mpaka warudishe gharama zao. Ktk kipindi hicho bandari zingine zinatakiwa zife au zidumae kwa kutoendelezwa, aidha serikali haitokuwa na uwezo wa kujua bidhaa au fedha inayoingizwa bila kuambiwa.
Mambo hayo tuliyaona wakati Barrick wanaingia kuchimba: walituambia wamekopa 3bl usd miaka ya 90 na kwamba haeatolipa kodi mpaka wakusanye hela yotebealuokopa.. bila kujua ukweli wa kiasi hicho au kama kweli zote zilituka kwa mradi. Bado tukawa hatuwezuli kuhakiki mapato. Kila mwaka wanatangaza kuingiza haasara mpaka reserve ikaisha na sasa tunaachiwa mashimo na vyoo.
Leo tunataka tuwape Wachina waanzishe CHINESETOWN hapa Bongo???
 
Tatizo kubwa ni usiri wa huo mkataba.
Haijulikani kama kweli wakoloni wapya wa Africa wanataka kuhodhi uchomi wetu wa bandari au wanakuja kama wawekezaji tutakaogawana nao fursa kwa haki

Back
Top Bottom