Maggid Mjengwa ana Virus?

pamoja na kwamba kunaweza kuwa na ukweli mama aliniambia umbea haumfai mtoto wa kiume.
ngoja nichambue kama hakuna umbea napita baadae.
 
Hapo kwenye rangi, una maanisha aliyemlipa sio? kwa hiyo habari zake na matukio anayoripoti ni kwa kuwa anatumika! ananunulika kifupi unataka kumaanisha kuwa sura na kalamu yake vinaonesha bei yake!!!

ata mie apo mmeniacha waungwana,inamaana ufundi wake wa kupangilia maandishi ndio mtaji wake!??
 
michuzi jr hawezi kupost picha za vinega na akaacha kuweka picha za clouds kwa sababu jamaa kaajiriwa clouds kama MPIGA PICHA
 
Nasapoti vinega. Tutazidi kuwascan virus wote. Magid hata abane vipi no one can stop this. Nguvu ya umma nguvu ya umma, msilete uk(scratch) fik fik fik
 
Tunaongelea vyombo vya habari je ni sahihi Mjengwa kutoweka picha za Tamasha hili? unafahamu kinachoendelea wewe au unadhani tunauza sura hapa? wapenda haki hatuwezi kukaa kimya tukaangalia watu wakitumia pesa zao kunyanyasa wengine, Issue hapa ni kwa nini Mjengwa hajaupload hizi picha za Tamasha la Anti virus wakati hakuhitajika kupeleka mpiga picha pale uwanjani bali zipo humu humu kwenye internet? na nina uhakika anazo.

Nimejenga hoja, ukiweza pangua hoja na ulete hoja na hatuhitaji Viroja.

We matola sikiliza sepa hata mod wa JF wanaweza kuifuta post yako kama haina mshiko vile vile kwa mjengwa ile ni blog yake moral authority ya kumtaka afanye utakacho wewe kwa matakwa yako unaitoa wapi?

Ile udhamini anautafuta mwenyewe..na wanao mdhamini wanapenda wenyewe...wewee hauko kwenye nfasi ya kumpagia nini afanye na nini apost..na kwanini vinega acha kutanguliza ushabiki wako wa kijinga na kutaka kufanya wengine tuamini kama umekamata primus uko bar..unataka kutuaminisha..kwenda uko hii ni jukwaa huru kila mtu anachangia anachoona ni sahihi..kutochangiwa mada zako na mjengwa inakuuma sana..kama mada zako hazina mshiko? achangie..

Lazima tukifike tukubali kutokubaliana....kalale.Shutdown.
 
Light click, scan virus, then delete,
Haya ni mawazo ya misukule, mtu aliegoma kuushirikisha ubongo wake unabaki kutokwa na povu bila sababu, na bado kwenye vita ya haki ushindi ni lazima. tupa kule.
 
Wewe Motala mbona unakuwa na akili fupi kama mkia wa mbuzi? Unataka Mjengwa hafanye kazi zake kwa mapenzi yako wewe? Kwanza unajua kama Sugu nae kawatia ndani pesa,baadhi ya wasaani kufanya shoo?
 
Wewe Motala mbona unakuwa na akili fupi kama mkia wa mbuzi? Unataka Mjengwa hafanye kazi zake kwa mapenzi yako wewe? Kwanza unajua kama Sugu nae kawatia ndani pesa,baadhi ya wasaani kufanya shoo?

Naunga Mkono Hoja.

316710_124060024372690_100003060783008_128462_96337878_n.jpg
 
Ndugu zangu,

Usiku huu nime-google jina langu ndipo nimekutana na habari hii. Ukweli imeniburudisha na kunipa elimu pia. Ama hakika, ishi ujionee na ujifunze kutoka kwa wanadamu wenzako.

Nalaumiwa kwa kuwa Mjengwablog haiku-post picha za tamasha la Anti- Virus. Na ni jana tu nimenunua kitabu cha Mr. Sugu kuhusu maisha yake- From Streets to The parliament.

Ndugu zangu,
Mie naishi na kufanya kazi Iringa. Ni mahali ambapo hata mtandao wakati mwingine ni wa shida. Na kublogu huku tunajitolea tu. Hata matangazo ya maana hatuna, Tunatumia senti za mifukoni mwetu. Na kazi ya kublogu naifanya nikiwa na wakati ziada.

Tena siku hizi nina mwanafunzi wangu aliye Dar na anayenisaidia wakati mwingine kuifanya kazi hiyo. Kuhusu picha za tamasha hilo linalosemwa nami niliziona zimetundikwa kwenye Mjengwablog.com na mwanafunzi wangu huyo.

Niwahakikishie, kuwa Mjengwablog ni blogu huru. Haijapata kununuliwa na haitakuja kununuliwa kufanya kazi za kishabiki. Na mimi kama mmiliki wa blogu ndivyo nilivyo. Sijapata kununuliwa na sitakuja kununuliwa nimfanyie mtu kazi ya kishabiki na isiyo na maslahi ya kitaifa.

Pamoja na yote hayo. Niseme tu, kwa hata mabaya yaliyoandikwa hapa juu yangu, sina kinyongo na mtu. Na nirudie, niliyosoma hapa usiku huu yameniburudisha pia. Nimebaki nikicheka mwenyewe kuona jinsi watu wanavyonifikiria, kunituhumu na kunihukumu, bila hata kunipa nafasi ya kunisikiliza.

Nawatakia usiku mwema.

Maggid,
Iringa.
.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom