Maggid Mjengwa ana Virus?

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
56,492
92,920
Wakuu kama mtakuwa ni wafatiliaji wazuri jumamosi ya tarehe 26 yaani juzi kwa upande wa burudani kulikuwa na matamasha mawili Jijini Dar ambayo yalibeba hisia na mitazamo tofauti, kulikuwa na Tamasha lile la clouds fm pale Leaders club na lile la wasanii wa Nyumbani Anti virus with no Apology, lakini cha kusikitisha huyu memba mwenzetu wa JF pamoja na mwenzake Michuzi, kwenye blog zao kwa makusudi wameamuwa kuonesha picha za Tamasha la clouds peke yake!

Swali linakuja je huyu member mwenzetu anastahili kuendelea kuaminiwa kama muandishi wa habari huru au ni njaa tu inamsumbuwa, amepewa vijisenti mbuzi na kina Kusaga ili kuwanyima Watanzania habari?
Hivi inawezekana vipi Tamasha kubwa kama hili na ndilo lilibamba kwa mahudhurio lisiripotiwe kwenye blog za hawa jamaa? ndio maana nauliza au hawa ni sehemu ya hawa VIRUS?
Nimewashitaki kwenu wadau:

Sister P akikamua

Zay B jukwaani

Daz baba akifanya kweli

DJ Sox akifanya mambo yake

Mkoloi akiwa kazini

Mr Simple, Diwani wa Ticket ya CHADEMA

Mashabiki wakipagawishwa

Sugu akifanya mambo

Wasanii wa kizazi kipya waliowahi kutamba zamani waliounda kundi la Vinega wakiongozwa na Mkurugenzi wa Deiwaka Entertainment, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (pichani juu) usiku wa kuamkia leo wamefanya onesho lililohudhuriwa na maelfu ya watu katika Viwanja vya Chuo cha Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam. Hapo juu ni baadhi ya matukio yaliyojiri kiwanjani hapo:.

Machizi mko fiti????? Mheshimiwa Mbowe (Mwenyekti wa CHADEMA) akiwasalimia mashabiki waliohudhuria tamasha viwanjani hapo

Mashabiki wakiitia salamu ya Mbowe, Tuko bomba ile mbayaaaa
source: wajanja club blogs
 
mbona michuzi alirusha picha za matamasha yote
Mjengwa? maana nina aleji na hiyo blog ya michuzi na isitoshe hapa nimemshtaki member mwenzetu mjengwa ni kwa nini ajaballance haya matukio? itakuwa ni kumuonea tukisema amepewa pesa na kina Kusaga? maana kila alie hapa mjini anajuwa aibu walioipata clouds na kila njia wanayofanya kuficha ukweli.
 
atakuwa kapewa offcourse
 
  • Joseph Mbilinyi
    TAARIFA:NASKIA LEO JAMAA WAMEAMKA NA JIPYA,KWAMBA SHOW YA VINEGA ILIKUWA MATUSI MATUPU!

    KWANZA SIO KWELI NA TUNATOA DVD NA UMMA UTAONA NA KUHUKUMU MANENNO YAO,PILI HIVI KUNA RADIO INA LUGHA CHAFU NA MATUSI KAMA CLOUDS FM??!!KWA MFANO TU,NI WAO WANAOPROMOTI UPUUZI UNAOITWA 'KANGA MOJA',YALE NI NINI KAMA SIO MATUSI NA UPOTOSHAJI WA MAADILI ULIOMBATANA NA UDHALILISHAJI WA WATOTO WA KIKE??!!

    OKOA MAADILI YA TAIFA KWA KUSUSIA KUSIKILIZA CLOUDS FM!!!
 
kanga moko laki si pesa
[video=youtube_share;8rxczvcWQOo]http://youtu.be/8rxczvcWQOo[/video]
 
Kila leo mi nasema maggid ni gamba tu, hukumbuki kipindi cha uchaguzi mkuu??
Namsubili kwa hamu sana wiki hii aje na makala zake za kipumbavu tafsiri yangu, ili nimchane live maana yeye Maggid huwa achangii thread za member wengine, sasa namsubili kwa hamu sana jaa kali kabisa huyu.
 
Mkuu Matola tujifunze kubadilika kutokana na wakati...km ilivyo siasa,kutofautiana kimtazamo kusijenge uadui...nafikiri hujasahau ya B.I.G na 2pac...Vinegar kimpango wao,Clauds kimpango wao...Clouds ni duka la sanaa,kila mtu yuko huru kuanzisha la kwake!
 
Tunaongelea vyombo vya habari je ni sahihi Mjengwa kutoweka picha za Tamasha hili? unafahamu kinachoendelea wewe au unadhani tunauza sura hapa? wapenda haki hatuwezi kukaa kimya tukaangalia watu wakitumia pesa zao kunyanyasa wengine, Issue hapa ni kwa nini Mjengwa hajaupload hizi picha za Tamasha la Anti virus wakati hakuhitajika kupeleka mpiga picha pale uwanjani bali zipo humu humu kwenye internet? na nina uhakika anazo.

Nimejenga hoja, ukiweza pangua hoja na ulete hoja na hatuhitaji Viroja.
 
Matola,sio sahihi kwa mdau yeyote wa tasnia ya habari kuegemea upande wowote ama kwa makusudi ama kwa bahati mbaya...naam,hilo nalitambua na ni saratani kwa baadhi ya wanahabari ambao ni wengi...ni dhambi sawa na hiyo hiyo ya kuegemea upande mmoja kwa mwakilishi wa watu,ama mtu anayesimamia maslahi ya watu mathalan kusimama kwenye majukwaa rasmi na kutumia mic vibaya...Namkubali Sugu,ni jembe na role model wangu tokea enzi lakini ktk mgogoro huu na bwana Ruge namtizama Sugu ktk sura tofauti...Maggid alihudhuria tamasha la clouds,mbali ya uandishi ana mapenzi yake binafsi na ndilo alilofanya...
 
Nakubali kutokukubaliana na wewe,........
 
  • Joseph Mbilinyi
    TAARIFA:NASKIA LEO JAMAA WAMEAMKA NA JIPYA,KWAMBA SHOW YA VINEGA ILIKUWA MATUSI MATUPU!

    KWANZA SIO KWELI NA TUNATOA DVD NA UMMA UTAONA NA KUHUKUMU MANENNO YAO,PILI HIVI KUNA RADIO INA LUGHA CHAFU NA MATUSI KAMA CLOUDS FM??!!KWA MFANO TU,NI WAO WANAOPROMOTI UPUUZI UNAOITWA 'KANGA MOJA',YALE NI NINI KAMA SIO MATUSI NA UPOTOSHAJI WA MAADILI ULIOMBATANA NA UDHALILISHAJI WA WATOTO WA KIKE??!!

    OKOA MAADILI YA TAIFA KWA KUSUSIA KUSIKILIZA CLOUDS FM!!!

Uhasama huu unatupeleka kubaya, watanzania tushirikiane kuwasuluisha watanzania wenzetu hawa" Mh. Mbilinyi na Ndugu Ruge". Vinginevyo endapo uhasama huu utaendelea kwa mbali naona 'replica' ya matokeo mabaya kabisa kuwahi kutokea ya uhasama wa B.I.G na 2Pac wa Marekani, My Living God forbid.
 
Kama kafanya hivyo kweli basi ni mtu wa kupiizwa kabisaaaa.................hatufai watz wa kzazi hiki...............clouds wenyewe wamejaa virus
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom