Magembe: Walioniita 'Waziri mzigo' wataisoma wao...

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,806
48,960
Aliyekuwa waziri wa Maji awamu ya 4 ambaye kateuliwa kuwa waziri wa Maliasili na utalii, Prof. Maghembe baada ya kuapishwa juzi kasema waliokuwa wanasema yeye ni waziri mzigo hawakufanya utafiti wowote.

Nakumbuka katibu mkuu wa CCM Kinana na katibu wa itikadi na uenezi Nape Nnauye ndio walikuwa mstari wa mbele kuwaita wengine mizigo.

Kitendo cha rais Magufuli kumteua Maghembe ni kuonyesha hakubaliani na katibu wake mkuu.

Waziri kaapa kula sambamba na majangili,

Asiyempenda kaja.
 
Last edited:
Naona mzee wa kupeleka bajeti ya maji bilioni 3 jimboni kwake yupo katika ubora wake
David Silinde (Chadema-Mbozi Mashariki), alisema anashangazwa na namna Jimbo la Mwanga ambalo mbunge wake ni Waziri wa Maji lenye wakazi wasiozidi 130,000, kutengewa Sh. bilioni 1.4 kwa ajili ya miradi ya maji mwaka wa fedha wa 2013/14 na Sh. bilioni 1.7 kwa mwaka wa fedha wa 2014/15 huku Jimbo lake la Mbozi Mashariki lenye watu zaidi ya 350,000, likitengewa Sh. milioni 400 mwaka wa fedha wa 2013/14 na Sh. milioni 900 kwa mwaka wa fedha wa 2014/15.
 
Hivi Kinana na Nnauye waliwataja kwa majina hao waliokuwa Mawaziri Mizigo?
Au Wananchi ndio waliotathimini utendaji wao?
 
Hivi Kinana na Nnauye waliwataja kwa majina hao waliokuwa Mawaziri Mizigo?
Au Wananchi ndio waliotathimini utendaji wao?
Mbali na wabunge na wananchi kuwataja Maghembe na wenzake kama mawaziri mizigo bado Kinana na Nape walikuja na kuwaita ni mawaziri Mizigo.
 
Huyu sio mzigo tu ni furushi kule jimboni hakuna kitu amefanya wapare wanalalamika anawapa posho wamchague ......
 
Jf sasa inasumbua balaa,kulogin ni kama unafanya mtihani wa havard,hata ukifanikiwa ukichepuka kidogo unatakiwa tena ulog in ,

magembe ni jembe
 
Ni kweli kabisa kuwa Maghembe ni waziri mzigo, tena Mzigo mzito sana. Kwa sababu
1/Amekuwepo Serikalini kwa zaidi ya miaka 15 sasa, Aliingia kipindi cha Pili cha Mkapa 2000, kisha vipindi vyote viwili vya Kikwete, lakini hakuwahi kuonyesha chochote cha maana katika utendaji wake.

2/Amewahi kuongoza wizara za Maji, Mifugo, Kilimo, Ushirika na Chakula, Elimu, Maliasili nk. Lakini hakuwahi kabisa kutatua changamoto zozote za msingi katika wizara hizo.

3/Aliwahi kuwa waziri wa Maliasili, lakini utendaji wake ulizaa mambo mabaya zaidi kama Kuongezeka kwa ujangili, kupungua kwa thamani ya mazao ya misitu, utoaji holela wa vibali vya uwindaji, kushamiri kwa migogoro kati ya wafugaji na mamlaka za wafanyamapori, kusafirishwa kwa magogo kimagendo nje ya nchi, kudorora vibaya kwa sekta ya utalii.
 
Ingekuwa vyema ccm na kamati ya uteuzi itueleze kwa nini imeamua kumbebesha JPM na watanzania mzigo huu.....
 
Ni mzigo tu, wala hakuna jina lingine mbadala.....hapo ninachoona ni JPM kafunika kombe kwa angalau kaskazini nako patoe waziri, ila ukweli utabaki pale pale kuwa waliomuita mzigo hawakukosea.
 
HONGERA KWA KUTEULIWA TENA KUIONGOZA WIZARA NYETI KATIKA AWAMU YA TANO,PAMOJA NA KUANZA NA MAJANGILI PIA KUNA WABAYA ZAIDI YA MAJANGILI HAPO WIZARANI WANAJIITA TFS TANZANIA FOREST SERVICES HAWA NI WABAYA KULIKO MAJANGILI KWANI WANATUMIA KIVULI CHA KUKUSANYA MAPATO YA SERIKALI HUKU WANAHARIBU MAZINGIRA VIBAYA KIASI HATA HAO TEMBO HAWAWEZI KUISHI KATIKA MAENEO WANAYOFANYIA SHUGHULI ZAO HILO NI JIPU TUMUA MAPEMA KWA FAIDA YA MAZINGIRA YETU
 
waliwataja kwa majina ya wizara zao ikiwemo ya Maji chini ya Maghembe na Elimu chini ya Kawambwa.

Maghembe ahakikishe anamdhibiti jangili Kinana kudhihirisha yeye sio mzigo.
Ataweza?, akae Kimya tu, chama kikianza propaganda atatolewa kwenye uwaziri
 
Back
Top Bottom