Uchaguzi 2020 Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Jumanne Maghembe apata ushindani mkali Mwanga, Kilimanjaro

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
Waziri wa zamani aliyetenguliwa, Jumanne Maghembe, apata ushindani mkali Mwanga Kilimanjaro

MNANDI MNANDI, Mtia nia wa ubunge katika jimbo la Mwanga mkoani kilimanjaro, leo amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa/ kupitishwa kuwa mgombea wa ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi CCM.

Mnandi amechukua fomu leo hii majira ya saa nane mchana, katika ofisi ya CCM Wilaya ya Mwanga ,akiwa ameongozana na mke wake, Samira Manento.

Mbunge wa sasa wa jimbo la Mwanga ni aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye alitenguliwa Jumanne Maghembena Rais John Pombe Magufuli.

Jummane anakabiliwa na upinzani mkali ndani ya chama cha Mapinduzi ambacho wanachama wake wamejitokeza kutia nia ili kuomba ridhaa ya chama hicho kugombea ubunge.

Kwa mjibu wa KATIBU wa CCM Wilaya ya Mwanga, Sixtus Mosha, amesema mpaka saa nane mchana leo, watia nia 27 wa kuomba ridhaa ya CCM, wamechukua fomu ya kugombea ubunge wa Jimbo la Mwanga.

IMG20200714142521.jpg


IMG20200714141808.jpg


IMG20200714142522.jpg
 
Huyo mzee zama damu bado analazimisha kuwa mbunge! Tena chaguzi zenyewe hizi za kishenzi?! Kweli mzee amekosa aibu.
 
Huyo mzee zama damu bado analazimisha kuwa mbunge! Tena chaguzi zenyewe hizi za kishenzi?! Kweli mzee amekosa aibu.

Samahani shemeji, mbona umekuwa mkali sana kuhusu uchaguzi huu? Nyuzi kibao nakuona unasiriba kinoma! Kulikoni shemeji!!
 
Kuna chama ili mgombea chaguo la mfalme awe peke yake, imelazimu kumvua uwenyekiti wa wilaya (mtia nia ), kuvunja kamati nzima ya utendaji ya wilaya na kufanya uchaguzi mwingine kwa siku moja.😂😂
 
Samahani shemeji, mbona umekuwa mkali sana kuhusu uchaguzi huu? Nyuzi kibao nakuona unasiriba kinoma! Kulikoni shemeji!!

Shemeji mimi sio muumini wa chaguzi za kihuni, hivyo nazipinga na kuzishushia credit kwa nguvu zangu zote.
 
Wanamwanga hawana Cha kujivunia juu ya Maghembe labda usangi na ugweno ambapo wanaamini bila Maghembe wasingepata umeme tokea awamu ya nne.

Hana hata la kutamba .2015 aliponea chupuchupu kuachia Jimbo kwa kileo was chedema .ila kilichomuokoa ni sarakasi za Kura zilizofanyika kule usanga vtc
 
Back
Top Bottom