Magazeti Yetu na JamiiForums

hata TBC husema habari zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii wakati issue ipo hapa pekee! Waseme tu source Jamii Forums!

Hiii ni kutokana na mtandano kuitwa jamiiforums, sio jamiiforum, ndio maana na wao wanaichukulia in plural sense.
 
Lakini na sisi humu tunahamisha mengi toka kwenye hayo magazeti. Magazeti hayatoi tu shukrani kwa JF kama wanaJF wafanyavyo wanapoyanukuu. Nyumba tunajenga ni moja. Tusigombee fito.

Wana JF huweka source ya maandiko, kama hukuweka source wana JF wanakuzozomokea humu wakidai source, kwa hili sikuungi mkono.
 
Mleta mada hujaleta ushahidi kama ulivyoombwa, tukuamini vipi? kuna uzi humu mtu ana mada inayofanana na yako lakini katukinaisha wote kwa kutuwekea ushahidi kamili. Nadhani hata wewe umekuwa "inspired" na hiyo mada.
 
Mkuu wa Uchambuzi JF kuwa a giant media chini kwa chini haijaanza leo .Muulize hata Mwakyembe na mambo yake ya ufisadi alikuwa anashinda hapa na wengine tulimpa msaada mwingi kuupata ukweli kule US.JF ni kigingi mkuu na ukiona kuna habari za magazetini ina maana yanaletwa kwa mijadala pekee ila kwa kuibua issue JF ndiyo penyewe kama unabisha muulize Salva .

mkuu, umeongea vizuri sana, JF inaibua issues, magazeti yana-report.
Huo ndio ukweli.
 
Mchambuzi, wakiitaja jf ni source yao ya habari gharama atalipa Maxence, manake JF kama unakumbuka ni 'adui' wa amani ya CCM. I can just imagine wanaogopa kujivurugia, japo ni muhimu hata waseme ' Source withheld'
 
..unajua mpaka sasa bado sijamwelewa mchambuzi..!dizayn kama unataka attention hivi..watu wautambue uwepo wako...

kuna siku utakuja kulia lia hapa ili mwananchi au majira wereva waandike source:mchambuzi wa jf
 
Mkuu Mchambuzi ebu weka link za makala zako na makala za hayo magazeti yanayofyonza habari JF.
Hata mimi nna ham ya kuziona hizo 'link'. Haya, kazi kwako Mchambuzi, weka mambo hadharani! Tuchambue kama karanga.
 
Makala ya kwanza ni hii hapa:

Nape Anaifahamu Katiba ya CCM?

Na Salum Maftah - Imechapwa 18 January 2012



 
Imekuwa jadi kwa baadhi ya magazeti yanayotoka Jumatano na Jumapili kuchapisha content nyingi sana kutoka humu JF. Binafsi nimeona content zangu lifted kama zilivyo, neno kwa neno, kwenye matoleo na magazeti kama manne tofauti. Wakishindwa kubadili angalau maneno ili yaendane na mawazo yao, na badala yake kuamua to lift neno kwa neno, ingekuwa jambo la busara sana kama waandishi hawa angalau wangetoa credit kwa jamiiforums, kwani huko ni kujengana kama media platforms. Hawana haja ya kutaja majina ya wachangiaji au watoa mada humu kwani wengi wetu tuna majina ya uongo, lakini angalau watoe credit kwa jamiiforums. Huo ni mtazamo wangu binafsi.

Nakumbuka THIS DAY walikua na staha ya ku-quote... ila hawa wenzetu wa sasa wameamua kabisa kurahisisha kazi

plagiarism@work
 
...., but JF nimeona ikitajwa sana na raia mwema na mwanahalisi....
Ni kweli kbs mkuu, magazeti hayo mawili huwa yana 'acknowledge' sana JF, mara nyingi nimeona wakirejea chanzo cha habari zao kutoka JF. Tuwape heshima yao kwa hilo. Mengine huwa ni copy and paste bila kutoa source
 
Ni busara acknowledged source ya habari!
Na hata msipofanya ivyo JF bado iko juu na itaendelea kuwa juu.
Mbona sisi tukiqoute magazeti tunawacknoledge
 
Back
Top Bottom