Magari yote yangekuwa Manual transmition kusingekuwa na Foleni nchi nzima

Mkuu nifafanulie
Kiongozi Anti Blocking system (ABS) ni mfumo ulio tengenezwa kuzuia tyre ya gari isisimame (skiding) kwa sababu isiwe 0 friction force which means no braking. Sasa waza kuna lamu yenye maji inateleza na unatumia AT usiyoweza kucontrol speed na torque, si majanga hayo

..!
 
Automatic zinahandle utelezi vizuri tuu..huko kwenye ice and snow si ndo kuna etelezi balaa na wengi wao wana magari automatic
Nani kakuambia? Najua ninachokisema. Nimeendesha magari miaka mingi kwenye ice na snow, barabara za kokoto na vumbi, zneye matope ya mfinyanzi etc zadi ya miaka 40.
 
Napenda sana ku drive stick shift kiukweli, ila kwa sasa ni kama ziko too primitive. Zamani madereva wote waliendesha manual so hata kama auto zisingekuwepo bado watu wangejifunza na wangeendesha tu manual na foleni ingekuwepo kama kawaida
Kumbe Gear lever sometimes inaitwa stick shift??? Nimeipenda hii, kama uliwahi kuona movie za Fast and Furious utaona uzuri wa gari za manual
 
Kumbe Gear lever sometimes inaitwa stick shift??? Nimeipenda hii, kama uliwahi kuona movie za Fast and Furious utaona uzuri wa gari za manual
Uzuri mkubwa unakuwa in full control of generating and motoring mode (jifunze). Ulaya wengi hawapendi AT
 
Mie natumia Toyota V8 manual ninakwenda speed ninayota katika mvua hizi since speed - torque characteristic is 100% in my control
Kwenye mvua huwezi kwenda spidi unayotaka, unatakiwa upunguze mwendo kwa sababu ya hydroplaning, gari kuelea juu ya layer ya maji, traction inapungua na control inapungua, huwezi kuwa na 100% control na kwenda spidi unayotaka, that is just insanely ridiculous to say.

I mean, sio sifa kusema mimi naenda spidi yeyote wakati wa mvua. Isitoshe, visibility inapungua wakati wa mvua, au kama wewe una macho ya bundi ujue wenzio barabarani hawakuoni, sasa ukitaka driver's license kwenye nchi zinazojali maswala ya road safety unaambiwa yote haya. Lakini kwenye vi nchi vyetu hivi tunakonunua leseni kwa mapolisi ndio unakuta mtu anasema mimi naenda spidi yeyote wakati wa mvua! How preposterous is that.
 
Hii nimeigundua nilipotaka kuuza gari yangu mpya yenye gia ya manual kwa bei rahisi. Kila aliyeiona aliipenda na katika kuiangalia mtu akiiona kuwa ni manual basi mjadala wa kuuziana ndo unaishia hapo. Hakuna madereva watu wengi wanaogopa gari za manual

Mimi nilijifunza gari enzi hio automatic walikuwa wanasema mbovu!gari ilikuwa manual tu! Lakini trust me nikipewa option ya auto na manual nachukua AUTO! Tangu link mtu aka opt manual machine instead of automatic one if both have same specs?! BTW siku hizi zipo semi auto if u wanna shift up and down manually!
 
Kiongozi Anti Blocking system (ABS) ni mfumo ulio tengenezwa kuzuia tyre ya gari isisimame (skiding) kwa sababu isiwe 0 friction force which means no braking. Sasa waza kuna lamu yenye maji inateleza na unatumia AT usiyoweza kucontrol speed na torque, si majanga hayo

..!

Anti-locking Brake System......Locking ndio kitendo cha tairi kusimama na gari kuendelea kuserereka,system hii inazuia hilo kwa kukamata na kuachia harska Sana!
 
Anti-locking Brake System......Locking ndio kitendo cha tairi kusimama na gari kuendelea kuserereka,system hii inazuia hilo kwa kukamata na kuachia harska Sana!

Yap mdau. Ni tofauti na mdau alivyotuaminisha kule juu. Mfumo huo hauruhusu tairi kuslide. Hali hiyo ikijitokeza sensor ya mafuta ya breki inakata mafuta haraka na tairi litaanza kuzunguka na papo hapo mafuta ya breki yataanza kuja na kushika breki tena. Tendo hilo ni la haraka sana na hufanyika automatically, hivyo dereva huwezi kuhisi kama kuna jambo linafanyika.
Pamoja na faida za Manual transmission, lakini kimsingi mfumo huo uko superceded kwa sasa, ndo utaona hata lorry za kisasa zina Automatic gearing system!
 
Nani kakuambia? Najua ninachokisema. Nimeendesha magari miaka mingi kwenye ice na snow, barabara za kokoto na vumbi, zneye matope ya mfinyanzi etc zadi ya miaka 40.

Mimi naendesha automatic kwenye ice na snow every winter for the last 15 years na inamudu vizuri tuuu hata wakiwa hawajasafisha automatic iko okay mbona
 
Mimi naendesha automatic kwenye ice na snow every winter for the last 15 years na inamudu vizuri tuuu hata wakiwa hawajasafisha automatic iko okay mbona

Kuna watu bado wako 16th century! Hizo gari auto zina anti skid,traction control,decent control,hill decent control hata kuwe na snow ice kiadi gani na ICE MODE special kwenye icy conditions!
 
Mimi naendesha automatic kwenye ice na snow every winter for the last 15 years na inamudu vizuri tuuu hata wakiwa hawajasafisha automatic iko okay mbona
Ni suala la personal experience na perception, kwa hiyo siwezi kupinga. Hata mimi nimeendesha kwenye ice na snow miaka zaidi ya 25 kwa hiyo experiences, preferences ni tofauti.
 
Ni suala la personal experience na perception, kwa hiyo siwezi kupinga. Hata mimi nimeendesha kwenye ice na snow miaka zaidi ya 25 kwa hiyo experiences, preferences ni tofauti.

Gari za kisasa vitu ambavyo ukiwa na manual unavifanya kupambana na hali mbaya zinafanya zenyewe automatically. Kuna ice mode,kuna traction control,kuna hill decent control,anti skid etc.

Lakini kama Una gari auto ya kawaida ya kizamani isiyo na hizo options nilizotaja kwenye hali mbaya mfano snow na unashuka mlima itakutoa nishai ila manual unaweza kujitetea!
 
Automatic kwenye long trip unaweza kusinzia kwa uwezekano mkubwa sana kama upo mwenyewe
 
kwa taarifa yako gari nyingi kama siyo zote ni manuap. nenda bergium au germany. auto ji uchafuzi wa mazingira zikichoka
 
Back
Top Bottom