Mambo yaliyombeba Dkt. Dotto Biteko kupata Unaibu Waziri Mkuu na mtihani ulio mbele yake

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,270
9,716
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa upande wangu nimemsoma na kumuelewa vyema sana Mh Rais Samia juu ya Aina ya uongozi wake na aina ya watu na viongozi ambao angependa kufanya nao kazi Muda Wote. Rais Samia Tangia awali Ameonyesha kwa maneno ,kauli ,matamko na matendo kuwa anapenda kufanya kazi na watu wenye moyo wa utulivu,wachapa kazi,waadilifu,wazalendo,wenye moyo wa kujituma,kujitolea,wabunifu katika kazi ,wenye kuleta matokeo chanya,wenye kuzingatia sheria,kanuni,taratibu na miongozo mbalimbali.Rais samia anapenda kufanya kazi na watu wanaoongea kidogo na kufanya kazi sana,anataka watu wa matendo na siyo maneno.

Anataka watu wenye uwezo wa kusimamia kazi na kujisimamia.Hataki watu wenye kusubiri maelekezo au kutaka kusukumwa kwa kila jambo,anataka watu wanaojiamini katika kazi na maamuzi lakini wenye kuzingatia katiba na sheria za nchi. Anataka watu wenye kufanya kazi kama watu wazima na siyo kusubiri kupewa amri kwa kila jambo na kufokewa kila mahali ,ndio maana ikifika hatua hiyo kwa mtu kutoweza kuelewa ni lazima uione haraka sana barua ya utenguzi.

Rais Samia hapendi mtu au watu au viongozi wenye mihemuko, mikurupuko, wenye kutoa matamko au maneno yenye kuleta Taharuki au sintofahamu katika jamii au jumuiya ya kimataifa. Hataki mtu mwenye kutoa maneno au matamko yenye kuhatarisha diplomasia yetu au ujirani mwema au undugu miongoni mwetu watanzania. Anataka kufanya kazi na watu wenye kuchunga ndimi zao na kupima kauli zao kabla ya kuzitoa,anataka watu wenye hofu ya Mungu na wenye kujuwa kuwa cheo ni dhamana na wenye kutenda haki muda wote katika maamuzi yao,anataka watu wenye kujuwa kuwa ofisi za umma ni kwa ajili ya kuwahudumia wananchi na siyo pahala pa kuchumia utajiri na mali, anataka uongozi wa alama na siyo uongozi wa moshi ambao upepo ukipita nao unafutika.

Sasa ukimuangalia na kurudi kwa mh Dkt Doto Biteko Unaona Anaingia katika mfumo ,mahitaji na kukidhi vigezo vya mh Rais Dkt Samia Suluhu Hasssan.Kwa kuwa Dkt Doto Biteko ni mtu na kiongozi Mtulivu na mwenye Utulivu wa hali ya juu sana,Ndio maana huwezi ukaona kauli zake zikileta mtafaruko au sintofahamu katika jamii au jumuiya ya kimataifa,licha ya kushika na kuongoza wizara nyeti ya Madini lakini alikuwa ni mtu mwenye kuchunga ulimi wake kabla ya kuzungumza.

DKT Doto Biteko ni kiongozi mwenye kutaka kuona jambo linafika mwisho na kuleta matokeo chanya kwa Taifa letu,Ndio maana tuliona sote namna alivyoamua suala la uanzishaji wa masoko ya madini katika mikoa mbalimbali hapa nchini linafika mwisho na kufanikiwa ,ambayo ilisaidia sana na kuchochea biashara ya madini,lakini pia ilichochea na kusaidia serikali kupata mapato yake halali pamoja na kuongeza mapato serikalini,lakini pia kupitia yeye wachimbaji wadogo wadogo walianza kunufaika sana na shughuli za uchimbaji wa Madini.pia ni kupitia yeye akiwa waziri tuliona utoroshaji wa Madini kwa njia za panya ukipungua nchini na hata yalipofanikiwa kuvuka nje ya nchi kwa njia za uchochoroni yalikwenda kukamatiwa sehemu zingine.

Mh Dkt Doto Biteko ni kiongozi mchapa kazi sana na anayefanya kazi pasipo kuhitaji kusukumwa au kusimamiwa kama mtumwa,yeye ni mtu wa kuzingatia sheria na kuhakikisha kuwa kazi zinazo Songa mbele kwa mujibu wa sheria na matokeo chanya yanapatikana,ni mtu anayetimiza wajibu wake kwa kadiri ya uwezo wake,ni mtu ambaye muda na wakati wote yupo maeneo yanayohitaji majibu , maelekezo na muongozo wa wizara pasipo kuhitaji kusukumwa. muda wote unamuona akiwa kazini na siyo kukaa ofisini, ndio maana kero na changamoto kwa wizara hii ya madini zilipungua sana wakati wake.

Dkt Doto Biteko ni mfuatiliaji sana wa mambo,ndio maana unaona kila kitu kinachofanyika na kilichokuwa kikifanyika katika wizara ya madini kilikuwa kiganjani pake,Takwimu zote na mipango yote ilikuwa mkononi mwake Hii ni kutokana na Tabia yake ya ufuatiliaji wa mambo na kutaka kila kitu kinachofanyika akifahamu kwa undani,ndio maana ulikuwa ukiona anaelezea mafanikio ya wizara,mipango na hata mikakati ya wizara kwa siku zijazo bila shida yoyote ile.

Ni kiongozi asiye na mihemuko wala jazba wala kufanya mambo kwa Hasira au kukurupuka ,ni kiongozi mwenye kufanya kazi kwa ushirikiano na mwenye uwezo mkubwa wa kuwaunganisha watu,ndio maana wizara ilifanikiwa kupata mafanikio makubwa kwa kuwa kila mmoja alijiona ni sehemu ya wizara na anao mchango wa kuipeleka mbele wizara hasa secta ya madini tuliyopewa na mwenyezi Mungu.

Ili watu wasitembee vifua wazi au nguo zimechanika mabegani kwa umasikini au kukosa milo bora ya chakula wakati wanatembea juu ya ardhi iliyobarikiwa kila aina ya madini yenye thamani kubwa sana.Alitaka kuona watu wa maeneo ya madini wananufaika na madini yaliyo katika maeneo yao na siyo kunywa maji machafu yenye sumu kutoka migodini au wakipigwa risasi na kumwaga Damu katika Ardhi yao na watu wanaoitwa wawekezaji, au kupita katika barabara zilizojaa vumbi na matope huku zikipitisha madini ya thamani ya mabilioni kwa mabilioni kwenda nje ya nchi.

Mtihani na mifupa iliyo mbele ya Mh Dkt Doto Biteko na ambayo akifanikiwa kuivuka na kuuvunja basi ataingia na kuweka historia ya kipekee sana katika Taifa letu kama kijana,lakini pia itamsaifishia njia zaidi ya kisiasa kwa siku zijazo kama watu walivyoanza kutabiri juu ya kuja kushika uwaziri mkuu siku zijazo huko mbele panapo majaliwa ya mwenyezi Mungu. Mitihani hiyo ni Suala la Umeme pamoja na Nishati ya mafuta hasa petroli na Dizeli.

Nitaanza na suala mafuta. Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa kukijitokeza changamoto za upatikanaji wa mafuta hasa petroli na dizeli kwa baadhi ya maeneo hapa nchini hasa inapoelekea mwishoni kwa mwezi,mimi mwenyewe nimeshuhudia kwa maeneo niliyopo. Hisia za watu wengi ni kuwa Kuna Baadhi ya wafanyabiashara wakishirikiana na baadhi ya watumishi waliopo Serikalini wamekuwa wakitoa na kuvujisha siri na Taarifa juu ya Bei mpya ya mafuta kwa mwezi unaofuata ,Hivyo wafanyabiashara na wamiliki wa sheli wakishafahamu bei za mwezi unaofuata kuwa zitapanda huanza kuficha mafuta yao wanayokuwa nayo kwa wakati huo.

Hali hii imekuwa ikileta kero kubwa sana kwa watu ,kwa kuwa mafuta machache yanayokuwa yakipatikana katika baadhi ya maeneo yamekuwa yakiwa ni ya foleni kubwa na kwa bei kubwa sana ,lakini pia nimeshuhudia sheli zikifanya hadi zamu ya kuuza mafuta yaani leo mafuta yanakuwa yanauzwa sheli fulani tu siku nzima halafu kesho yanakuwa yanapatikana kwa mwingine tu,hali inayoonyesha kuwa ni mipango ya wafanyabishara wenyewe katika kuhakikisha kuwa wanabakiwa nayo mengi ili wauze pale yatakapo kuwa yamepanda bei.

Hali hii inaleta maumivu makubwa sana kwetu wananchi kwa kuwa hata nauli kuanzia bodaboda,bajaji na magari zimekuwa zikipanda bila utaratibu hasa kwa maeneo ya pembezoni mwa miji na kwa magari yanayobeba mizigo ,hali inayopelekea mtu anayefanya biashara ya usafirishaji kutopata faida ya aina yoyote ile ikiwa anasafiriaha mzigo kama vile mahindi au chochote kile kupeleka sokoni.

Hivyo ni mtihani na mfupa ambao mh Dkt Doto Biteko anatakiwa autafitie suluhu na majibu ya haraka sana ili kuondoa changamoto hii inayogusa maisha ya watu wengi sana uwe na gari au usiwe na gari lazima uguswe tu kupitia kupanda kwa nauli au kupanda kwa bidhaa madukani. Mh Naibu waziri mkuu akifanikiwa kulimaliza Tatizo hili kwa hakika ataandikwa jina lake kwa wino wa Dhahabu katika mioyo ya watanzania wengi sana.

Mtihani wa pili ulio mbele yake ni kuhakikisha kuwa Umeme unapatikana muda mwingi na kuondoa matatizo ya kukatika katika kwa umeme . watanzania wengi wanatambua juhudi za serikali katika kukabiliana na tatizo la umeme na kuhakikisha kuwa umeme wa uhakika unapatikana muda wote na maeneo mengi,tunatambua pia kuwa Bwawa la mwalimu Nyerere linakwenda kuanza udhalishaji wa umeme mapema mwakani na hivyo kuondoa tatizo hilo.

Hivyo ni busara wakati huu kutafuta njia na mbinu au mikakati mbadala hasa kwa miezi hii ambayo huwa hata kina cha maji mitoni au katika mabwawa yetu ya kuzalisha umeme yanapungua na hivyo kuathiri uzalishaji wa umeme .kuhakikisha kuwa watanzania wanapata umeme muda mwingi ,hasa kwa kutambua kuwa Umeme ni injini ya uchumi wetu na vitu vingi sana au shughuli nyingi sana na mambo mengi sana yanategemea uwepo wa umeme, ukikata umeme unakuwa umekata matumaini ya familia nyingi sana kupata mahitaji na milo mitatu kwa siku,unakuwa umekata ndoto za watu kupata pesa kwa siku husika ,unakuwa umekata mipango ya watu wengi,unakuwa umekata minyororo ya kujipatia kipato kwa kaya nyingi sana,unakuwa umekata njia za wajasiriamali wengi sana kama mafundi welding,wauza samaki wabichi,matunda,watu wa saloon,gereji,viwandani, steshenari N.k katika kujipatia fedha.

Hivyo Mh Dkt Doto Biteko akifanikiwa kuuvunja mfupa huu kwa hakika jina lake Halitafutika katika mioyo ya watanzania,litaandikwa kwa wino usiofutika ,litabaki kama alama katika mioyo ya watanzania na kubakia katika kumbukumbu za watanzania pamoja na kuimbwa na kila mtanzania mwenye kinywa hai.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
CCM ina wenyewe kijana hata namba zao za simu hawaziweki wazi hivyo na wanapigiana .

Hebu angalia mtu kama Pindi Chana aliwekwa benchi kwa muda tu ila unaona alivyorudishwa na anavyohama wizara?

Namba ya Pindi Chana ulishawahi kuiona hapa jukwaani?

Kama wewe ni mkulima kweli kama unavyodai focus na jembe tu, Pinda alijiita mtoto wa mkulima je unaweza kunipa picha ya Pinda akiwa na jembe la mkono achilia mbali tractor?
 
CCM ina wenyewe kijana hata namba zao za simu hawaziweki wazi hivyo na wanapigiana .

Hebu angalia mtu kama Pindi Chana aliwekwa benchi kwa muda tu ila unaona alivyorudishwa na anavyohama wizara?

Namba ya Pindi Chana ulishawahi kuiona hapa jukwaani?

Kama wewe ni mkulima kweli kama unavyodai focus na jembe tu, Pinda alijiita mtoto wa mkulima je unaweza kunipa picha ya Pinda akiwa na jembe la mkono achilia mbali tractor?
Hapana Ndugu yangu mimi naendelea na kilimo changu na shughuli za kilimo na siingii hapa jukwaani kuandika kwa ajili ya kusaka uteuzi.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa upande wangu nimemsoma na kumuelewa vyema sana Mh Rais Samia juu ya Aina ya uongozi wake na aina ya watu na viongozi ambao angependa kufanya nao kazi Muda Wote. Rais Samia Tangia awali Ameonyesha kwa maneno ,kauli ,matamko na matendo kuwa anapenda kufanya kazi na watu wenye moyo wa utulivu,wachapa kazgu.

0742-676627.
Tafuta kazi nyingine ya kufanya hii ya kulamba viatu haina dili kwa sasa
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa upande wangu nimemsoma na kumuelewa vyema sana Mh Rais Samia juu ya Aina ya uongozi wake na aina ya watu na viongozi ambao angependa kufanya nao kazi Muda Wote. Rais Samia Tangia awali Ameonyesha kwa maneno ,kauli ,matamko na matendo kuwa anapenda kufanya kazi na watu wenye moyo wa utulivu,wachapa

0742-676627.
Huo ni Mtama kwa watoto kuwaghilb watu wa kanda ya ziwa lakini tunasema hivi:- HATUDANGANYIKI !!!
 
Kweni Ripoti ya CAG iliongeleaje WizMad?
Hakuna mahali ambapo ilimhusisha mh waziri kuwa ametumia madaraka yake vibaya. Sote tumeona juhudi zake kubwa katika kupambana kuhakikisha kuwa madini yanatoa mchango mkubwa katika pato la Taifa.
 
Huo ni Mtama kwa watoto kuwaghilb watu wa kanda ya ziwa lakini tunasema hivi:- HATUDANGANYIKI !!!
Rais Samia anakubalika kanda zote na maeneo yote ya Taifa letu ,kutokana na kupeleka maendeleo kila eneo pasipo upendeleo wala ubaguzi wa Aina yoyote ile.
 
Hivi wewe haukuwahi kujifunza ku summarize hadithi, maneno meeengi kumbe unarudia rudia tu!
Andiko limekuwa refu kwa sababu lina pande mbili,ambapo pande moja inazungumzia sababu za kuteuliwa kwake na vitu vilivyombeba ,wakati sehemu ya pili inazungumzia changamoto au mitihani iliyo mbele yake .na wakati huo huo nilikuwa ninetangulia nimeelezea aina ya watu au viongozi ambao Rais samia anapendelea kufanya nao kazi kulingana na sifa ambazo nimezielezea mwanzoni kabisa.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa upande wangu nimemsoma na kumuelewa vyema sana Mh Rais Samia juu ya Aina ya uongozi wake na aina ya watu na viongozi ambao angependa kufanya nao kazi Muda Wote. Rais Samia Tangia awali Ameonyesha kwa maneno ,kauli ,matamko na matendo kuwa anapenda kufanya kazi na watu wenye moyo wa utulivu,wachapa

0742-676627.
Mwambie baba ako akupe shamba ukalime. Unajipendekeza hadi inakera. Ccm ina wenyewe mzee shtuka
 
Mwambie baba ako akupe shamba ukalime. Unajipendekeza hadi inakera. Ccm ina wenyewe mzee shtuka
😄😄😄 Mimi Tayari ninayo mashamba na ninaendelea kuchapa kazi kwa juhudi,bidii na maarifa.pia shambani siyo jera kuwa muda wote natakiwa kuwa huko.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom