Magari yanayopaa kuanza kutumika 2030

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Kampuni ya Hyundai imesema imepiga hatua kubwa katika kutengeneza magari yanayoweza kupaa, na kuwa ndoto yake ya kuwa na magari hayo inaweza kutimia kufikia mwishoni mwa muongo huu.

1625050569906.png

Kampuni hiyo ya Korea Kusini imesema ina matumaini kuwa usafiri wa magari ya anga unaweza kuwa fursa kubwa ya kuondoa msongamano katika miji mikubwa, kupambana na hewa ya ukaa na kurahisisha usafiri ndani ya miji au kati ya miji, ikitaja magari yanayopaa kama “sehemu ya kesho yetu.”

Kampuni hiyo ilionesha mpangilio wa jinsi magari hayo yatakavyokuwa, ikishirikiana na kampuni ya usafirishaji ya Uber kuandaa mpangilio huo katika maonesho ya magari yaliyofanyika Las Vegas nchini Marekani mwezi Januari mwaka huu.

Kampuni hiyo pia inashirikiana na Uingereza kutengeneza uwanja wa ndege usiokuwa na barabara ya ndege kupaa na kutua (runway) kwa ajili ya ndege zinazoweza kupaa na kutua bila kulazimika kutafuta kasi ya kupaa kwa kukimbia, ukitarajiwa kuanza kufanya kazi katika mji wa Coventry nchini Uingereza baadaye mwaka huu.

Mwaka 2019, Kampuni hiyo ilisema inakusudia kuwekeza dola trilioni 1.8 (sawa na Tsh. trilioni 4,076) kwa ajili ya kufanikisha mradi huo kufikia mwaka 2025, ikitarajia kuanza kutumika kibiashara kufikia mwaka 2028.

Chanzo: The Guardian

 
Back
Top Bottom