Magari ya Hybrid yanayofanya vizuri Tanzania

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
19,204
50,470
Huku bei ya mafuta ikiendelea kupanda kila kukicha ndani ya hii miaka mitano (kutoka Tsh 2100/= hadi sasa Tsh 3300/=) na hamna "dalili" kuona bei ikishuka, ni muda wa Watumiaji kubadirisha muelekeo (adaptation). Kwa wanaotafuta gari, ni bora kuangalia "Fuel Efficient cars" au "Hybrid cars" huku tunasubiria "Electrical Vehicles" miaka miwili ijayo.

Tukumbushane tu kua, Hybrid cars, kama wadau kwenye nyuzi zilizopita walivyowahi kusema, inakuja na battery mbili. Moja ni ile ya kawaida (12 Volts battery) inayofanya kazi ya "kupower" gari na kuwasha. Na ya pili ndio "high Voltage hybrid" battery inayotumika kumsaidia engine au kumreplace engine kusukuma gari.

Kwahiyo kuna scenario mbili hapa: (1) Kuna muda gari inaendeshwa na hii hybrid battery tu. Kwahiyo engine haifanyi kazi kabisa. Na mafuta hayatumiki kabisa. (2) Kuna muda engine na battery ya hybrid vinasaidiana. Kwahiyo gari inakua efficient sana. By sana namaanisha sana.

Kwahiyo, lengo kuu la kununua hybrid cars ni kusave mafuta. Na ndio maana tunashauri anunue mtu anaekaa mji wenye msongamano (trafic jam), we anaeendesha sana gari kwa siku au mwaka gari yake na mwisho angalau akae nayo iyo gari kwa miaka 3 kwenda mbele ndio ataona faida. Wale wazee wa kila miezi 6 kubadirisha gari hii kwake itakua haina "faida".

Ebu tujuzane magari ya Hybrid yanayofanya vizuri au tunayoshauri mtu wa kipato cha kati anunue.

1. Toyota Prius
Wenyewe wanasema huyu ndio king wa Hybrids. Prius ana generations tano (5) hadi sasa hivi. Tuipata 2nd generation sio mbaya ila 3rd generation ni nzuri pia.

Hii hapa ni 2nd generation 2003 hadi 2008. Unaweza kuipata jumla (CIF na ushuru) kwa chini ya mil 15.
2008_Toyota_Prius_(NHW20R)_liftback_(2012-06-24).jpg


Hii hapa ni 3rd generation, mwaka 2009 hadi 2013 unaweza kuipata kwa angalau Mil 19 na kuendelea kutoka Japan.
Hii gari ishawahi pata tuzo nyingi sana. Highly recommended.
Toyota_Prius_ZVW30_front_20100725.jpg


Combined Fuel economy ya Prius inafika 25 km/L na ukiwa dereva mzuri inaweza kufika ata 30 km/L au zaidi.


2. Toyota Aqua (aka Prius C, C for City!)

Huyu ni mdogo wake Prius aliekua designed kwaajili ya kuendeshwa mjini. Kidogo ni mdogo, mwepesi na ana fuel economy kubwa zaidi.

2012_Toyota_Prius_c_(NHP10R)_hatchback_(2015-07-03)_01.jpg


Ana generations mbili, ila tunatumia zaidi ya kwanza 2011 hadi 2020 maana hii ya pili inaanza 2022 tuassume ipo nje ya budget yetu.
Huyu ndio kipenzi cha Uber na Bolt drivers kwa sasa kwakua anaweza kwenda hadi 38 km/L hapa mjini.

3. Honda Insight
Honda nae havumi lakini yupo. Anachuma zake Hybrid kadhaa ila Honda Insight ni moja ya hybrid insyofanya vizuri.

Huyu ana generations tatu (3) hadi sasa. Ya kwanza ya mwaka 1999 ilikua ya kiwaki sana shape yake. Sijui madogo wa field ndio walikuja na Ile idea?

HondaInsight.jpg

Ila kuna wabishi walinunua. Aisee.

Ila second generation ya 2009 hadi 2016 ipo poa na Bongo zipo za kutosha. Inafanana sana na Prius hadi wengine wanasema kuna mtu aliuza ramani. Sasa hatujui nani kwasababu almost zote zimetoka mwaka mmoja (Honda Insight 2nd gen 2009 na Prius 3rd gen 2009).

2010_Honda_Insight_LX_in_Alabaster_Silver_Metallic,_Rear_Left,_12-15-2021.jpg


Hii Insight ukitulia Beforward unaweza ipata kwa Mil 15 na mafuta haipishani sana na Prius. Ukichagua yoyote utaenjoy.

4. Honda Fit Hybrid na Honda Fit Shuttle Hybrid
Honda alifanya unyama kutuletea kagari kadogo kama IST flani akakaita Honda Fit. Best selling compact car kutoka kwa Honda. Kwa kuona haitoshi akaamua kukapa Hybrid. Aisee kama unatafuta gari dogo ambalo linanusa wese mara mbili ya IST basi ishi na Honda Fit Hybrid.
Hapa kuna generations nne (4) hadi tunavoandika huu uzi. Ila tuachane na 1st generation ni ya zamani sana na tuachane na 4th generation, bei sana. Tuishi na 2nd generation na 3rd generation.
Hii ni 2nd generation 2007 hadi 2012. Ukitaka Hybrid yake ipo, ukitaka isio Hybrid ipo, ukitaka Sports Edition (RS) ipo. Shindwa wewe.
1280px-2008-2010_Honda_Jazz_(GE)_hatchback_(2011-10-25).jpg

Hii unaweza ukapata kutoka Japan kwa chini ata ya Mil 14 ukifanya uchunguzi vizuri.

Hapa tuna Fit Hybrid 3rd generation kuanzia 2014 hadi 2020 aisee. Imeboreshwa muonekano, engine na ndani ina unyama sana.
1280px-2017_Honda_Jazz_EX_Navi_i-VTEC_CVT_1.3_Front.jpg

Honda Fit ina consumption ndogo pia inaweza kwenda hadi 30km/L hapo mjini town.

Pia, Honda alikuja na Honda Fit Shuttle ambayo ni "kubwa" ya Fit ya kawaida. Kilichobadirika ni shape tu. Hii kwa lugha ya wataalamu wanasema ni station wagon shape ya Honda Fit.

1280px-Honda_Fit_shuttle_1.5L-Model.jpeg

Kwahiyo kama unapenda Fit ila haujapenda size yake, twende na Hii. Ingawa utasacrifice fuel economy kidogo kwasababu hii ni kubwa (heavy).

5. Harrier Hybrid
Harrier ina generations nne (4) hadi leo. Ila Hybrid engine walianza kutengeza kwenye 2nd generation (2003 hadi 2013). Hii almaarufu tako la nyani (usishangae logo ya Lexus, picha tu ila same car)
1280px-2004-2005_Lexus_RX_330_(MCU38R)_Sports_Luxury_wagon_(2011-04-02)_01.jpg

Kama uchumi sio tatizo unaweza kwenda na 3rd generation kuanzia 2014. Mchawi pesa ila hii chuma kali kifala.

1280px-2018_Lexus_RX_450h_Luxury_CVT_3.5_Rear.jpg

Kidogo bei za Harrier sio rafiki kwasababu 2nd gen chini ya Mil 35 haupati na 3rd gen bila Mil 70 hauchomoi. Ila tuneona tuiweke kwa maboss.

Tufanye hesabu kidogo:
1. Tufanye Mshana amenunua IST inatumia mafuta 15 km/L na Bwana PureView Zeiss kanunua Toyota Aqua inayoenda 35 km/L na wote wanedesha 40 km kila siku kwenda na kurudi kazini.

2. Mshana kwa siku anatumia Lita 2.5 kwa bei ya leo ya Tsh 3300/= anatumia Tsh average ya Tsh 9,000/= kwa siku.
Kama anaendesha kila siku 365 za mwaka atatumia Tsh 3,285,000/= kwenye mafuta.
Tuassume amekaa na gari miaka mitano, kwahiyo tuzidishe na tano tunapata Mil 16.5 za mafuta.

3. PureView Zeiss yeye kwa siku anatumia Lita 1.2 za mafuta ambazo ni kama Tsh 4,000/= tu.
Kwa mwaka (siku 365) ni kama Tsh 1,460,000/= tu.
Nae amekaa na kiberiti chake kwa miaka mitano, tukizidisha tunapata Mil 7.3 tu.

4. Najua hesabu za ivo ni za motivation speakers ila my point kuonesha kwamba Hybrid inaweza save nusu ya gharama kwenye mafuta.

NB:
1. Bei nilizoandika ni estimation. Zitabadirika kutegemea na hali ya gari na kikokotoo cha TRA.
2. Fuel consumption nilizoandika nj estimation za mitandaoni. Zinaweza kupanda zaidi au kushuka kutegemea na mtumiaji.
3. Hybrids zina perfom vizuri kwenye low speed na mjini kuliko highway.
4. Hybrids nyingi zina options tatu. Eco, EV na Sport. Kama unaweka Eco muda wote tegemea ulaji mzuri wa wese kuliko anaeweka Sport.
5. Kama ilivyo battery ya simu yako, pia battery ya Hybrid inakufa (degradation) kutokana na muda na matumizi.
6. Unavyotafuta hybrid car online. Kilometa za kwenye odometer zisikudanganye. Usiangalie namba ndogo. Hii topic ya siku nyingine.

Nimeona tuziweke izo gari tano (5) ingawa hybrids siku hizi zipo nyingi sana kwahiyo kila mtu anaweza kuja na list yake. Natumai wachangiaji wataongeza hybrids pendwa zingine na wengine wataongezea nyama kwenye izo tulizodiscuss.

Karibuni
 
Somo zuri sana hili. ....Mkuu hivi zile Harrier New Model (Toyota Harrier Z Hybrid) kuna moja nimekuta Engine ni 1990CC kama sikosei na pia ni hybrid ....Hii gari ni nzuri au niipotezee tuu maana nilikua nawaza mpango wa kuvuta Subaru FORESTER XT 2013 ila sio Hybrid
Yeah kama uko njema wese sio shida. Sio tatizo. Hizi Hybrid kwaajili yetu wabahili.
 
Hizo subar (sports car dah ni pasua sana ) kwakuw unaagiza nje ni sawa na kama unajimidu vzr)
Mimi naona kama ukomae na Toyota haria hybrid
Somo zuri sana hili. ....Mkuu hivi zile Harrier New Model (Toyota Harrier Z Hybrid) kuna moja nimekuta Engine ni 1990CC kama sikosei na pia ni hybrid ....Hii gari ni nzuri au niipotezee tuu maana nilikua nawaza mpango wa kuvuta Subaru FORESTER XT 2013 ila sio Hybrid
 

Attachments

  • 1713151418023.jpg
    1713151418023.jpg
    143.1 KB · Views: 3
Aisee umepiga hesabu Kali Sana kwenye upande wa hybrid maana wengi wetu hatuna hesabu za mwaka tunatumia kiasi gani cha pesa kwenye mafuta..
Kwangu Mimi nazikubali Sana hybrid car kuliko EV's

Toyota Prius anaongoza Kwa mauzo nchini Japan hili ni gari-pendwa Kwa wajapan,
 
Nawaza tu bei ya hizo betri zake itakuwaje baada ya hizo gari kuanza kutumika.
Ili kuna siku nitaliongelea ila kuna mwamba Mr DIY aliwahigusia akasema:

Hybrid battery ikifa hainamaana imekufa yote, ila baadhi ya "cells" ndio zimekufa. Mfano, Prius 2010-2015 imeundwa na izo "cells" 24 ambazo zimewekwa kwa pair kwenye block 14. Prius C (Aqua) yenyewe inazo 20 ambazo zimewekwa kwenye blocks 10 kila block mbili.
Mfano wa picha ya battery ikiwa kwenye gari hii:
images (8).jpeg

Hapa chini ikiwa imetolewa:
images (7).jpeg

Hapa ilifunguliwa kuonesha izo cells:
images (6).jpeg

Sasa kama nilivosema ikifa haifi yote, ila kuna cells zinakua zimekufa. Unampelekea fundi anafanya "cell swaps". Hizo cells unaweza kuagiza eBay au popote online. Cells sio gharama mfano cell moja ya Prius 2010 ni $25 hadi 40 kutegemea unaponunua ingawa shipping cost itabidi uwe mjanja (battery gharama sana kuship).

Screenshot_20240418-183733.png


Ila kununua battery nzima ni gharama kiasi chake:
Screenshot_20240418-183641.png


Ila Prius zinafika kilometa 300k kwa original battery nyingi sana. Na zinaenda fresh kabisa.

Na sio kwamba battery ikifa gari haiendi, inaenda fresh, sema hybrid inakua haipo.

Msiwe waoga (in dalali's voice).
 
Back
Top Bottom