Mafuta ya ubuyu hatari kwa afya

Mafuta ya ubuyu hatari kwa afya

Kuna uzi nilimuuliza mdau hapa kuwa ni wapi tafiti imefanyika juu ya mafuta ya ubuyu?Watu wameshatajirika kwa biashara hiyo,bongo bana chochote ukiuza pesa
 
Du, tanzania kila kitu ni janga. Watu walianza kunywa na kupaka mafuta ya ubuyu kwa kasi ya ajabu tena kwa bei juu na wahusika wa ubora wa vyakula waliona na hawakulifanyia kazi hadi leo, ingawa siamini hizi taarifa kama za kweli, Ndumyana hebu tupe habari inayoeleweka, ikibidi source ya taarifa hii.
 
Hahahaha biashara za watu hizi zimeingizwa mchanga. Kuna jitu lilinitumia sms eti 'nauza mafuta ya ubuyu litre sh 70,000/=. Ukinywa unang'aa bila mkorogo. Sijui unapungua weight ....'
I was polite enough not to reply! MziziMkavu njoo utulize tufani hapa
 
Last edited by a moderator:
Hiyo Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) na hao TBS naona hawafanyi kazi yao ipasavyo....
Muda wote tangu hayo mafuta yameanza kutumiwa na wananchi leo hii ndio wanaibuka na kusema ni hatari kwa Afya?
Ni Watanzania wangapi watakuwa wameshadhurika na hayo mafuta mpaka taarifa hii inapotolewa?
Hii nchi kila kitu hovyo hovyo tuu..!
 
OKI NA VIKING pia jana zimetangazwa kuwa ni hatari!

Aah! Ubwege na ukenge huu. OKING na OKI havijaanza kuingizwa nchini leo wala jana!
TFDA nayo haijaundwa leo wala jana!
Nina mashaka na nahyo taarifa kama hawajapewa rushwa ili mfanyabiashara fulani afaidike.
Kwanini wasiseme haya mafuta c mazuri miaka yote hiyo?
Kuna kipindi uvumi ulienea kuwa mafuta hayo ni kwa ajili ya kutengenezea sabuni lakini hawakusema chochote, leo miaka zaidi ya 10 baadae wanasema c salama? Wameathirika watu wangapi!
 
Mkuu si umeambiwa ni TDFA? Au na yenyewe huiamini?

TFDA wanasema mafuta ya ubuyu ni mazuri kwa matumizi ya binadamu tena ni tiba na kinga kwa magonjwa anuai!
Sasa hao TDFA wako sijui umewaokotea wapi!ni nini hiko kwani mi sielewi
 
Hiyo Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) na hao TBS naona hawafanyi kazi yao ipasavyo....
Muda wote tangu hayo mafuta yameanza kutumiwa na wananchi leo hii ndio wanaibuka na kusema ni hatari kwa Afya?
Ni Watanzania wangapi watakuwa wameshadhurika na hayo mafuta mpaka taarifa hii inapotolewa?
Hii nchi kila kitu hovyo hovyo tuu..!

Nakumbuka enzi hizo miaka ya 90 watu tulitumia mafuta ya tura zaidi ya miaka kumi then ikaja kupigwa marufuku miaka ya 2000 pamoja na sabuni ya jaribu waliyokuwa wanatumia wakina dada......Chezea BONGO wewe,bado tuna usingizi mbaya na tukiamka bado tuna maruweruwe,hivyo tunarudi kitandani tena.MBONA MDA WA KUAMKA BADO SANA,NDO SAA 1:15 USIKU
 
Kuna wengine walikuwa wanayapaka kwenye kipochi manyoya ili kurejesha "mnato"...

Sasa sijui ndio kusema vipochi manyoya vitadebweda!!
 
Mtoa uzi ingekuwa vyema kama ungetuwekea na chanzo cha habari hii kwa taarifa zaidi.
Kwa kuwa mafuta haya ya ubuyu yameshatumiwa na watanzania wengi kuliko hata KIKOMBE CHA LOLIONDO.

Gazeti la Habarileo
 
Du, tanzania kila kitu ni janga. Watu walianza kunywa na kupaka mafuta ya ubuyu kwa kasi ya ajabu tena kwa bei juu na wahusika wa ubora wa vyakula waliona na hawakulifanyia kazi hadi leo, ingawa siamini hizi taarifa kama za kweli, Ndumyana hebu tupe habari inayoeleweka, ikibidi source ya taarifa hii.

Imechapishwa Jumatatu, 08 Julai 2013
00:50
Imeandikwa na Theopista Nsanzugwanko
Imesomwa mara: 273
BAADA ya kuonya wananchi wanaotumia
dawa za tiba mbadala ambazo
hazijathibitishwa, Mamlaka ya Chakula na
Dawa Tanzania (TFDA), sasa inawataka
wananchi kuacha kutumia mafuta ya ubuyu
kwa kunywa kama dawa.
Akizungumza na gazeti hili juzi katika
Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa
ya Dar es Salaam, msemaji wa TFDA,
Gaudensia Simwanza, alisema Mamlaka
hiyo ilipima na kubaini mafuta hayo yana
tindikali ya mafuta.
Alifafanua katika maonesho hayo maarufu
kama Sabasaba yanayoendelea katika
viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, kwamba
mafuta hayo hayafai kuliwa na binadamu na
anayekunywa kwa wingi, yuko hatarini
kupata saratani za aina tofauti tofauti.
“Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la
wajasiriamali wanaouza mafuta ya ubuyu
kama dawa, kwa kuwaelekeza wananchi
kunywa. Napenda kuwataarifu kuwa mafuta
hayo ni hatari kwani yana tindikali ya
mafuta,” alisema.
Gazeti hili lilipata sampuli ya vielelezo vya
matumizi yake na manufaa yake mwilini,
kama inayotangazwa na wajasiriamali katika
maeneo mbalimbali na hata katika
mitandao.
Matangazo
“Ni mafuta yatokanayo na mbegu za ubuyu
{au kokwa}. Hukamuliwa kiini chake na
kutoa mafuta. Yana ubora kuliko mafuta
mengine ya kupikia, yana Vitamin A, B, C, D
na F. Pia yanatibu magonjwa mbalimbali,”
kielelezo kimoja kilinadi ubora wake katika
mitandao ya jamii.
Mafuta hayo yamedaiwa kutengeneza seli
zote ndani ya mwili, kuzuia ngozi isiharibike
wala kupata makunyanzi, kuondoa mafuta
ndani ya mishipa ya damu na yanapunguza
uzito uliozidi.
Pia inadaiwa yanarutubisha ini na figo,
yanaleta hamu ya kula, yanaimarisha
mifupa, kucha na nywele, yanaongeza kinga
ya mwili (CD4), yanaondoa sumu na
yanatengeneza sukari iwe katika kiwango
kinachotakiwa.
Maelezo hayo yameendelea kusifu kwamba
yanasaidia kuona vizuri na kujenga
kumbukumbu, yanapunguza vitambi na
matumbo makubwa, yana virutubisho vyote
vinavyohitajika mwilini.
Katika ngozi yametajwa kuondoa madoa,
chunusi, fangasi, upele, mba na muwasho,
yanafaa kwa walemavu wa ngozi (albino).
Pia huondoa hamu ya kutumia dawa za
kulevya na kuponyesha vidonda vya tumbo.
“Endelea kutumia mafuta bora ya ubuyu, ni
bidhaa asilia ya kitanzania. Ni mafuta
yasiyochanganywa na kitu chochote, ni
mafuta asilia,” yamesifiwa katika maelezo
hayo.
Kisukari
Mtumiaji ameelezwa kama ana ugonjwa wa
kisukari, atumie kijiko cha chakula kimoja
tu. Anatakiwa kutumia dozi hiyo ya kwanza
nusu saa kabla ya kula chochote kwa muda
wa siku 15.
Dozi ya pili na ya tatu kwa wagonjwa hao,
inatakiwa kufuata baada ya siku 15 kisha
mgonjwa apumzike wiki moja, huku
akiendelea kupima kila wiki. Kipimo hapo
ni cha hospitali.
Vidonda vya tumbo, figo, ini
Kwa wagonjwa wa vidonda vya tumbo, figo
na ini, wameelekezwa na wajasiriamali hao
kunywa kijiko cha chakula kimoja asubuhi
kabla ya kula chochote, na usiku kijiko cha
chakula kimoja kabla hajala chochote kwa
muda wa siku 15 kwa dozi ya kwanza.
Baada ya hapo, mgonjwa anapumzika wiki
moja kisha siku 15 zinazofuata dozi ya pili,
mapumziko wiki moja halafu siku 15
nyingine dozi ya tatu.
Maelezo ya dozi hiyo ya kutibu ugonjwa wa
vidonda vya tumbo, yanaendelea kumtaka
mgonjwa baada ya dozi ya tatu, aanze
kunywa kila wiki mara moja kijiko cha
chakula kimoja asubuhi, tena nusu saa kabla
hajala chochote kwa muda wa wiki nne.
Dozi inaendelea ambapo mgonjwa
atatakiwa kunywa kijiko kimoja cha chakula
kila mwezi mara moja asubuhi, kabla hajala
chochote kwa muda wa wiki nne, kisha
kunywa kila mwezi mara moja, asubihi
kabla hajala chochote kwa muda wa miezi
sita mfululizo.
Utoaji sumu, CD4
Kwa utoaji wa sumu, mgonjwa ametakiwa
kunywa kijiko cha chakula kimoja asubuhi
kila siku kwa muda wa siku 14, kisha
kunywa kila mwezi mara moja kwa muda
wa miezi sita mfululizo.
Kwa kuongeza CD4 mwilini, ametakiwa
kupata kijiko cha chakula kimoja asubuhi
nusu saa kabla ya kula chochote, na usiku
kijiko cha chakula kimoja nusu saa kabla ya
kula chakula cha usiku kwa muda wa miezi
mitatu.
“Mgonjwa aanze kunywa baada ya kipimo
cha mwisho (cha CD4) alichopima. Mafuta
yanapatikana kuanzia ujazo wa lita moja na
zaidi,” imesifiwa dawa hiyo.
Onyo
TFDA imeonya kuibuka kwa tabia ya
wananchi kutaka matibabu ya haraka, kama
ilivyo kwa baadhi ya watu kutaka utajiri wa
haraka, na imehadharisha ni vema kabla ya
kutumia dawa zinazoibuka kila siku, waulize
kama zina ubora kwa afya zao.
“Nawasihi wananchi kuacha kukimbilia dawa
ngeni mara tu baada ya kutangazwa… kama
haya Mafuta ya Ubuyu, yamekuwa
yakielezwa ni dawa na wajasiriamali tu, na
wengi wamekuwa wakitumia bila kusikiliza
mamlaka husika zinasemaje,” alisisitiza.
Semwanza alisema Mamlaka hiyo iko katika
mkakati wa kuanza kuelimisha jamii kuhusu
matumizi ya mafuta hayo, ambayo wengi
wanayaamini na kuyanywa kama dawa.
Teknolojia, matumizi sahihi
Kwa mujibu wa Semwanza, baada ya
kupima mafuta hayo na kubaini hatari hiyo,
waligundua pia inawezekana tindikali hiyo
kutenganishwa na mafuta hayo, lakini
imebainika utaalamu na teknolojia hiyo
haipo nchini.
Hata hivyo, alisema Mamlaka hiyo
haijabaini madhara ya matumizi mengine
ya mafuta hayo kama kipodozi.
Msako Sabasaba
Kutokana na mvuto huo wa kibiashara, na
shauku ya kupona haraka ya wananchi,
Semwanza alisema TFDA imekuwa ikifanya
msako wa dawa mbalimbali zinaouzwa na
wajasiriamali katika maonesho hayo.
Alisema kuwa kuna baadhi ya waandaaji
wanaowaalika wajasiriamali bila kufuata
kanuni na sheria za kuingiza dawa hizo
katika maonesho.
Kwa mujibu wa Semwanza, wanakagua dawa
na kama wakikuta hazijathibitishwa na TFDA
na mamlaka nyingine, wanamuamuru
mjasiriamali kuacha kuzitangaza mpaka
apate kibali na kuwaasa wanaowaleta
wajasiriamali katika maonesho hayo ya
kimataifa kuhakikisha wanafuata vigezo.
Wiki iliyopita TFDA, ilionya wananchi dhidi
ya matumizi ya dawa za tiba mbadala,
zikiwamo zinazokuza maumbile, ambazo
bado hazijasajiliwa na Mamlaka hiyo baada
ya kuchunguza usalama, ubora na ufanisi wa
dawa hizo.
Mamlaka hiyo ilieleza kuwa, ilitoa nafasi ya
watoa tiba mbadala kwenda kusajili dawa
zao, lakini mwitiko umekuwa hafifu.
TDFA yenye dhamana ya kusimamia ubora
na usalama wa bidhaa za vyakula na dawa,
ikiwa ni pamoja na dawa za mitishamba,
vipodozi na vifaa tiba vinavyouzwa katika
soko la Tanzania, imeeleza kuwa watoa
huduma wa tiba mbadala, wengi hawako
tayari kubainisha aina ya mchanganyiko wa
dawa hizo jambo ambalo ni hatari kwa
walaji
 
TFDA wanasema mafuta ya ubuyu ni mazuri kwa matumizi ya binadamu tena ni tiba na kinga kwa magonjwa anuai!
Sasa hao TDFA wako sijui umewaokotea wapi!ni nini hiko kwani mi sielewi

Sawa..
 
Kuna wengine walikuwa wanayapaka kwenye kipochi manyoya ili kurejesha "mnato"...

Sasa sijui ndio kusema vipochi manyoya vitadebweda!!

Hahahaaa...vipochi manyoya ndio nini mkuu?
 
The Tanzania Food and Drug Authority (TFDA) yesterday warned the public against drinking baobab oil, saying it contains substances that have carcinogenic effects. The baobab, scientifically known as Adansonia digitata, is tree species, spread in many parts of Africa and people use it for many purposes including relish, preparation of juice and of late "cure-all oil medication."

The government has also strongly cautioned the public against buying and using of drugs without prescription of qualified medical professionals.

The drug and food watchdog cited reckless use of Diclopa and Diclofenac, which are popular pain killers, as examples, noting that there were various unpleasant side-effects associated with the drugs.

TDFA, however, said people may continue using baobab oil as a cosmetic and not medication purposes.


Kwa maelezo zaidi ifuatilien hapa chini....

Mafuta ya Ubuyu ni Hatari

Mchungaji Masanilo hebu pita hapa
 
Back
Top Bottom