NADHARIA Mafuta ya nywele ya Body Luxe yanasababisha Mvi za mapema kwa Mtumiaji

Taarifa hii ni nadharia tu, tumeitolea ufafanuzi kwa kadiri ilivyowezekana
Matumizi ya muda mrefu ya mafuta ya nywele aina ya body luxe (body luxe hair oil) husababisha mvi kuota kwa kasi katika umri mdogo.

Hapa nazungumzia haya mafuta ya nywele ya body luxe yenye kopo la pink lenye picha ya mwanamke ana nywele ndefu.

luxe_hair_oil.jpg

Picha: Muonekano wa chupa za mafuta ya Body Luxe kwa upande wa mbele

1678951749583.png

Picha: Chupa ya mafuta ya Body Luxe ikionesha sehemu ya Viambato (Ingredients)

Hii ni kutokana na uzoefu wangu (personal experience) kwangu mwenyewe, kaka yangu na jamaa mwingine ambaye tunaishi naye mtaa mmoja. Wote tumeota mvi katika umri mdogo na tumekuja kugundua shida ni haya mafuta.

Mimi nilikuwa sijajua, nimeambiwa na kaka yangu jana kuwa mafuta ya nywele yanasababisha kuota mvi, nilioomuuliza alikuwa anatumia mafuta gani akasema Body Luxe.

Wadau, bila kujali hii ni brand na biashara ya watu, naomba tufanye uchunguzi juu ya hili.

Karibuni
 
Tunachokijua
Mvi ni hali ya nywele za binadamu kubadilika rangi kutokea nyeusi au blonde na kuwa nyeupe, kijivu au silver. Wataalamu wanaeleza kuwa Nywele za binadamu zina chembechembe za seli ambazo zinazotengeneza Melanini, hii ni kemikali inayosaidia kuzipa nywele na ngozi yako rangi yake. Hivyo, unapozeeka, seli hizi hupungua na kuanza kufa. Hali hii inapotokea hupelekea nywele kuanza kuwa nyepesi na kupoteza rangi yake kwa kuwa nyeupe, kijivu au silver.

Je, kuna uhusiano kati ya mafuta ya nywele na kutokea kwa mvi?
Wataalamu wa afya na kemia wanaeleza kuwa baadhi ya bidhaa za nywele hutengenezwa kwa kutumia kemikali ya ‘hydrogen peroxide’ ambazo zinaelezwa kuwa na madhara kwa nywele na zinaweza kusababisha kuota kwa mvi.

Inaelezwa kuwa matumizi ya vipodozi pamoja na unyoaji wa ndevu mara kwa mara umesababisha vijana wengi kuwa na mvi za mapema hususani kidevuni. Baadhi ya vipodozi vilivyofanyiwa uchunguzi katika saluni za kiume ni pamoja na Aftershave, Shampoo, Super magic, Super black, Facial mask, Scrub, poda na spiriti kwa kuwa vinatengenezwa kwa kutumia kemikali mbalimbali zikiwemo za asili na viwandani.

Je, mafuta ya Body Luxe yanasababisha mvi?
Kwa upande wa mafuta ya nywele yaitwayo Body Luxe hakuna utafiti rasmi wa kubainisha namna mafuta haya yanachochea kuota kwa mvi. Kopo la mafuta haya linaonesha kuwa yametengenezwa kwa kutumia viambato vya Mafuta yaliyochanganywa (Blended oil) na Manukato (Fragrance) kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu. Mchanganyo wa viambato hivi katika mafuta hayo haujathibitika kusababisha mvi.

Hivyo, kwa hatua ya sasa kulingana na aina ya taarifa tulizokusanya, JamiiForums imejirisha kuwa madai haya ni nadharia kwakuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaothibitisha hoja za mdau.

Aidha, zaidi ya bidhaa hizi za nywele pia mvi huweza kusababishwa na mambo yafuatayo:

Sababu za kijenetiki (Jeni)
Kwa baadhi ya watu suala la nywele kubadili rangi huwa la kiukoo. Ikiwa wazazi au babu zako walikumbwa na tatizo hili, basi kuna uwezekano mkubwa kwamba wewe pia utapitia hali hiyo. Kwa bahati mbaya, hakuna jambo ambalo linaweza kufanyika ili kuepuka.

Msongo wa mawazo
Kila mtu hukabiliana na msongo wa mawazo mara kwa mara. Matokeo ya msongo yanaweza kujumuisha matatizo ya usingizi, wasiwasi, mabadiliko ya hamu ya kula na shinikizo la damu. Ikiwa umeona kuongezeka kwa idadi ya nywele nyeupe, msongo wa mawazo unaweza kuwa chanzo.

Upungufu wa virutubisho vya vitamini
Ukosefu wa virutubisho vya kutosha vya vitamin B12 mwilini pia waweza sababisha ngozi na nywele kubadili rangi. Aidha, upungufu huu waweza kusababisha anemia (ambapo seli za damu hazina himoglobini ya kutosha, kiungo muhimu kinachobeba oksijeni mwilini kote). Kwa kawaida, Vitamin B12 hupatikana kwenye nyama ya ng’ombe, mayai na bidhaa zingine zinazotokana na wanyama.

Masuala ya homoni
Iwapo (thyroid gland) haifanyi kazi ipasavyo, huenda uwezo wa mwili wako kuzalisha melanini ukapungua na hivyo kusababisha nywele zako kubadili rangi mapema. Tezi dundumio ni kikoromeo kidogo kinachopatikana katika sehemu ya mbele ya shingo lako. Thyroid gland ni tezi yenye umbo la kipepeo iliyoko chini ya shingo yako.

Kushabuliwa kwa kinga za mwili
Inaelezwa kuwa ikitokea magonjwa yanayoshambulia kinga ya mwili na seli zake huweza kusababisha nywele kupoteza rangi yake. Aidha, inaelezwa kuwa magonjwa kama alopecia na vitiligo, huweza kushambulia kinga za mwili na kupelekea nywele kupoteza rangi yake.

Hivyo kwa msingi huo, tunashauriwa kuwa makini tunapoteua mafuta ya nywele kwa kutazama viambato vyake kabla ya kuanza kutumia. Pia, tunashauriwa kutumia vyakula vyenye vitamini B12.
Hata mimi na rafiki yangu imetutikea na tukikuwa watumiaji wazuri wa hayo mafuta.
 
Kuna mafuta flani nilitumia mara 1 tu kesho nikakuta mvi ambapo sikuwa na mvi hata 1, niliyatupilia mbali kabisa na hadi leo ni eneo lile tu ndiyo lenye mvi pekee.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Mvi nadhani huwa zinatekea kwa moja ya hizi factors:-

1. Umri
2.Upungufu wa madini
3.Vipodozi.

=> Kuna Umri ukifika kunakuwa hakuna namna lazima mvi zije
=>Kuna baadhi ya watu wanakuwa wanakosa baadhi ya madini hivyo mvi zinamuanza at 20s.
=>Kuna baadhi ya mafuta yanasababisha nywele kuwa na mvi ,nilisikia wale wanaonyoa ndevu/nywele kwa kutumia chemical flani nimeisahau huwa wanatoka na mvi mapema sana.
 
Ebhana eeh!

Hivi kwa nini wizara ya afya isitoe maelekezo watafiti wetu kutoka NIMR au hata TMDA wakachunguza hicho kitu tukapata majibu ya nadharia.

Wagharamie kila kitu kuanzia utafiti hadibuenezaji, ma video people wawe wanalipwa na kodi zetu wanaunda documentari za tafiti na taarifa za kina.
 
Mafuta mazuri kwaajiri ya nywele ni mafuta ya nazi. Unanunua zile kopo za kuspray, unachukua mafuta ya nazi pure sio yaliyopitishwa viwandani. Unatia perfume kidogo sana ili kuongezea harufu nzuri maana mafuta ya nazi yenyewe yananukia utamu kama wali.

Then unatia na maji kidogo sana halafu huu mchanganyiko unatikisa kisha unakuwa unajispray wakati wa kuchana nywele. Utaona nywele zako zitakavyokuwa zinanoga.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom