Mafuta ya Alizeti nayo hatari kwa afya - TFDA

Mafuta ya Alizeti nayo hatari kwa afya - TFDA

Katika gazeti la Mwananchi la Tarehe 17/09/2013 kuna taarifa yenye kichwa cha habari

“TFDA yatahadharisha mafuta ya alizeti mitaani”.

Habari yenyewe ni kama ifuatavyo:-


Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imesema mafuta ya alizeti yanayouzwa mitaani hayakidhi viwango vya usalama wa binadamu. Imesema, hali hiyo inatokana na wasindikaji wadogo kutumia mashine ambazo hazichuji vizuri mafuta hayo.

Habari hizo zimekuja wakati ambapo kumeibuka mjadala mkali baada ya TFDA kutoa taarifa kwamba mafuta yanayotokana na mbegu za ubuyu yana kiwango kikubwa cha kemikali. Inasemekana kemikali hiyo in athari kwa afya. Ofisa Uhusiano wa TFDA, Gaudensia Simwanza, alisema mwaka jana walianza mpango wa majaribio ya utafiti kuhusu mafuta hayo kutoka kwa wasindikaji wadogo Singida.

Maswali ya kujiuliza:-
1. Mafuta ya mitaani ni yapina wananchi watatofautisha vipi ya mitaani na ambayo si ya mitaani?

2. Kutokana na hii kauli ya TFDA ni nini wananchi wanatakiwa kufanya? Waache kutumia mafuta ya alizeti au vipi?

3. Mafuta ya alizeti hayajaanza kutengenezwa leo au jana. Yamekuwa yakitengenezwa kwa muda mrefu sana. Je, ni kwa nini TFDA hawakufuatilia ubora wa hizo mashine siku zote hadi sasa ambapo wananchi wengi wameshatumia mafuta hayo kwa muda mrefu, kiasi ambacho kama kuna madhara basi wengi tumeshaathirika?!

Kwa kweli imefika wakati hivi vyombo vyetu vinavyohusika na maswala yahayohusu afya za wananchi ikiwamo TFDA viache ubabaishaji. Kinyume na hivyo wananchi tutaendelea kuugua magonjwa ambayo hata chanzo chake ni vigumu kubaini!
Nadhani hawa wajasiriamali wanapata mashine zao toka SIDO na ndiko ambako TFDA wanatakiwa watoe msisitizo wa ubora wa mashine huko kwa kushirikiana na TBS,sasa wakisema tu mafuta ya mtaani hayana ubora sisi watumiaji wanakua hawatusaidii ipasavyo na hawawasaidii wajasiriamali pia
 
TFDA nayo ni hatari kwa afya! mkianza kukamua mafuta ya karanga nayo watasema ni hatari kwa afya! bwahahahaahha. Mafuta asili ya alizeti yanakuwaje hatari ya afya, hebu watoe ripoti ya kitaalam zaidi tuone, siyo blaah blaah za maneno matupu kama vilaza!
Nilivyoelewa mimi tatizo ni mashine zinazotumika kuchujia..na hili si tatizo la wajasiriamali bali ni tatizo la SIDO wanakopata mashine hizo
 
Apa kuna mpango wa fisadi limoja limeagiza machine au mafuta ya alizeti kutoka nje,
 
Mkuu nadhani swali lako lina mantiki, ila wanachodai TFDA ni kuwa mashine zinazotumika hazichuji vizuri! Sababu ya kutokuchuja vizuri haieleweki kama ni kutokana na ubora mdogo wa mashine au ni namna (process) ya kukamua inavyofanyika.

TFDA wangeweka wazi ili wananchi waelewe kabisa kuwa tatizo hasa ni nini.

hata wao hawajui wamesikia tu....
 
Hawa jamaa wa TFDA sijui wanafikiria nini. Hivi Tanzania ya leo wanafikiri tunaweza danganyika kihivyo? Kazi yao nazani kuwatetea walaji sasa leo hii wanakuja na ngonjera sa mafuta ya alizeti wakati washatuchanganya na mafuta ya ubuyu, nikiunganisha hapo napata jibu kwamba kuna wafanyabiiashara wanaitumia TFDA hili kupata soko kwenye bidhaa zao.

TFDA badala ya kushirikiana na wakulima wadogo kuja na suluisho la kukamua mafuta ya ubuyu na alizeti nyie mnatutisha tu. Tanzania jamani tubadilike tufanye kazi kwa manufaa ya nchi yetu sio manufaa ya nchi za nje. TFDA badilikeni pendeni bidhaa zetu, fanyeni tafiti za kutosha, tupeni matokeo sio kutudanganya tu. Nashangaa sana Dr. au Prof. mzima unakubali kutumiwa kisa pesa ya kula siku chache kweli? Embu tuchape kazi kwa uadilifu.
 
Hamna mafuta salama kama ya nguruwe, soon tutawasikia Mamlaka ya chakula na dawa wakisema
Hawatakuwa wamekosea, na mengine bora kwa viwango vya juu ni "LUZIZI" Kitu murua kutoka SANGARA INDUSTRIES!.
 
Kuna mgongano wa kibiashara hapa! Tfda wameongwa waje kuaribu masoko ya alizeti,washaaribu soko la mafuta ya ubuyu sasa wanataka waje kuaribu soko la mafuta ya alizeti,hatutaki mafuta ya korie,oki wala nini yana rehemu.
 
Nakumbuka zamani huku kwetu zenji tulikua tunatumia mafuta ya nazi, tunanunua nazi tunakuna then tunapika mafuta safi kabisa, sasa sijui yalikuja kupotea baada ya nazi kupungua zenji. Mana kama vp itabidi turudi tena tulikotoka. Au na haya ya nazi pia yalipigwa marufuku na hao wajamaa?
 
ni bora nitumie mafuta ya kuku au ngedere maana naona sasa TFDA hawaeleweki kabisa katika upimaji wao
 
Jamaa anajaribu kujasiria.amna sumu yoyote kwenye mafuta ya alizeti,ingekua kuna sumu,mifugo yote ingekufa au kudhurika.
 
enzi za babu zangu TFDA haikuwepo.sikuwahi kusikia maneno kama haya sasa hivi ni lazima kila mtu atumie akili yake'"AKILI YA KUAMBIWA ONGEZEA NA YA KWAKO '"
 
Kuna mgongano wa kibiashara hapa! Tfda wameongwa waje kuaribu masoko ya alizeti,washaaribu soko la mafuta ya ubuyu sasa wanataka waje kuaribu soko la mafuta ya alizeti,hatutaki mafuta ya korie,oki wala nini yana rehemu.
Mkuu unafikiri ni rehemu tu, kuna additives chungu mzima! Nasikia wakati mwingine wenye viwanda wana changanya mafuta ya mawese, alizeti na tallow oil, naona watafikia hatua ya kuongeza transformer oil mambo yakiwa magumu, who knows? - Yaani wanatulisha mchanganyiko maalum wa kutumaliza, nilisha yapiga marufuku nyumbani kwangu!! Awana utu hata kidogo, juzi juzi hapa walitaka ushuru wa mali ghafi ya mafuta ya kupikia kutoka nje yasilipiwe ushuru - hata sijui wanaposema mali ghafi wana maana gani wakati mafuta yanaletwa nchini complete/semi refined, bila ya Bunge kuwashtukia walikuwa na nia ya kuua viwanda vidogo vidogo vya walala hoi huko Singida na kwingeneko - kama ushuru ungetolewa kama walivyo kuwa wamependekeza basi bei ya mafuta kutoka viwandani ingekuwa ya chini sana kuliko bei ya waswahili - matokeo yake viwanda vidogo vidogo vya waswahili vingekufa. Hawa jamaa wana mbinu nyingi sana na wamekwisha tujulia Waswahili tulivyo, wanatutumia kuhangushana sisi wenyewe kutokana na tamaa ya pesa, uzalendo hatuna kabisa.
 
Katika gazeti la Mwananchi la Tarehe 17/09/2013 kuna taarifa yenye kichwa cha habari

“TFDA yatahadharisha mafuta ya alizeti mitaani”.

Habari yenyewe ni kama ifuatavyo:-


Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imesema mafuta ya alizeti yanayouzwa mitaani hayakidhi viwango vya usalama wa binadamu. Imesema, hali hiyo inatokana na wasindikaji wadogo kutumia mashine ambazo hazichuji vizuri mafuta hayo.

Habari hizo zimekuja wakati ambapo kumeibuka mjadala mkali baada ya TFDA kutoa taarifa kwamba mafuta yanayotokana na mbegu za ubuyu yana kiwango kikubwa cha kemikali. Inasemekana kemikali hiyo in athari kwa afya. Ofisa Uhusiano wa TFDA, Gaudensia Simwanza, alisema mwaka jana walianza mpango wa majaribio ya utafiti kuhusu mafuta hayo kutoka kwa wasindikaji wadogo Singida.

Maswali ya kujiuliza:-
1. Mafuta ya mitaani ni yapina wananchi watatofautisha vipi ya mitaani na ambayo si ya mitaani?

2. Kutokana na hii kauli ya TFDA ni nini wananchi wanatakiwa kufanya? Waache kutumia mafuta ya alizeti au vipi?

3. Mafuta ya alizeti hayajaanza kutengenezwa leo au jana. Yamekuwa yakitengenezwa kwa muda mrefu sana. Je, ni kwa nini TFDA hawakufuatilia ubora wa hizo mashine siku zote hadi sasa ambapo wananchi wengi wameshatumia mafuta hayo kwa muda mrefu, kiasi ambacho kama kuna madhara basi wengi tumeshaathirika?!

Kwa kweli imefika wakati hivi vyombo vyetu vinavyohusika na maswala yahayohusu afya za wananchi ikiwamo TFDA viache ubabaishaji. Kinyume na hivyo wananchi tutaendelea kuugua magonjwa ambayo hata chanzo chake ni vigumu kubaini!

Jamaa hawapo against na matumiz ya mafuta ya alizet wao wanapinga mafuta ya alizet ambayo hayajathibitishwa ambayo wameyapa jina kuwa ni ya mtaani.kitu ambacho mimi naona ni sahihi kabisa
 
Mi nitaendelea tu kuyatumia na familia yangu halafu nione mwisho wake
 
hii ni Janja ya wahindi na wafanyabiashara ambao wanatumia bandari bubu za pwani kuingiza mafuta haya; kwani baada ya kuzalishwa kwa wingi meni ya nje yamedoda madukani; sasa ndio wameanza kampaini
wAHINDI WAMEANZA KUTUMIA
TFDA KUTETEA MAFUTA YAO YANAYOTOKA NJE BAADA YA KUBAINI WATANZANIA SASA
WAMEANZA KUHAMIA AITRTEL (ALIZETI ASILIA) HAWA TFDA LAZIMA WAELEWE KUWA
WATANZANIA SASA WANATAKA TUMIA KILICHO CHAO ASILI NA SIYO MAFUTA
ARTIFICIAL YA KUTOKA NJE.WAHINDI IKULA KWAO MIMI NA MAFUTA YA ALIZETI NI
SAWA NA PUA NA KAMASI
 
Hii mamlaka imenunuliwa na wenye pesa imesahau jukumu lake inaweweseka kwa ajili ya pesa za watu. Kuna watu wanaona biashara zao hazitoki basi wamenunua TFDA wameiweka mfukoni wanadictate terms. Hii nchi imekaa kifisadi zaidi kila mwenye uwezo wa kupaza sauti na kusikika anatafuta jinsi ya kujinufaisha bila kujali athari kwa wananchi. Wananchi tutachagua wenyewe kipi tutakula na kipi ni hatari kwetu maana bado kidogo tutaambiwa hewa ya Tanzania haifai inabidi itoke India. Pambafu.
 
Back
Top Bottom