Mafuta ya Alizeti nayo hatari kwa afya - TFDA

Mafuta ya Alizeti nayo hatari kwa afya - TFDA

Hivi hawa TFDA wameanza kazi lini? Maana nakumbuka maisha ya boarding enzi zile. Ule msosi ulikuwa sumu tosha. Maharage yale yalikuwa hayafai hata kuliwa na wanyama. Tumeshakula sumu sana tuu.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Olive oil ndio mafuta pekee ambayo yako salama. Mengineyo ni hatari kwa afya yako

Haya yanapatikana wapi mkuu maana TFDa wako makini sana huenda na hii wakaipiga marufuku muda si mrefu!
 
Olive oil ndio mafuta pekee ambayo yako salama. Mengineyo ni hatari kwa afya yako

Hata hayo yakianza kutengenezwa mitaani TFDA watakuja na taarifa kuwa siyo salama.

Mafuta ya alizeti hayana tatizo kabisa labda tatizo ni hao wanaoyatengeneza though yamekuwa yakitengenezwa locally kwa muda mrefu na bila madhara yoyote.
 
Sie alizeti tunalima shambani kwetu tunatwanga kwenye kinu na kupikia wenye,TFDA wakashughurike na hao waliowalisha ARVs zilizochakachukuliwa watanzania

Si ndiyo hata mimi nashangaa. Kwetu tumelima alizeti tokea utotoni kabisa na zilitumika kuzalishia mafuta.

Udhaifu wa TFDA wasituletee huku shamba.
 
Katika gazeti la Mwananchi la Tarehe 17/09/2013 kuna taarifa yenye kichwa cha habari

“TFDA yatahadharisha mafuta ya alizeti mitaani”.

Habari yenyewe ni kama ifuatavyo:-


Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imesema mafuta ya alizeti yanayouzwa mitaani hayakidhi viwango vya usalama wa binadamu. Imesema, hali hiyo inatokana na wasindikaji wadogo kutumia mashine ambazo hazichuji vizuri mafuta hayo.

Habari hizo zimekuja wakati ambapo kumeibuka mjadala mkali baada ya TFDA kutoa taarifa kwamba mafuta yanayotokana na mbegu za ubuyu yana kiwango kikubwa cha kemikali. Inasemekana kemikali hiyo in athari kwa afya. Ofisa Uhusiano wa TFDA, Gaudensia Simwanza, alisema mwaka jana walianza mpango wa majaribio ya utafiti kuhusu mafuta hayo kutoka kwa wasindikaji wadogo Singida.

Maswali ya kujiuliza:-
1. Mafuta ya mitaani ni yapina wananchi watatofautisha vipi ya mitaani na ambayo si ya mitaani?

2. Kutokana na hii kauli ya TFDA ni nini wananchi wanatakiwa kufanya? Waache kutumia mafuta ya alizeti au vipi?

3. Mafuta ya alizeti hayajaanza kutengenezwa leo au jana. Yamekuwa yakitengenezwa kwa muda mrefu sana. Je, ni kwa nini TFDA hawakufuatilia ubora wa hizo mashine siku zote hadi sasa ambapo wananchi wengi wameshatumia mafuta hayo kwa muda mrefu, kiasi ambacho kama kuna madhara basi wengi tumeshaathirika?!

Kwa kweli imefika wakati hivi vyombo vyetu vinavyohusika na maswala yahayohusu afya za wananchi ikiwamo TFDA viache ubabaishaji. Kinyume na hivyo wananchi tutaendelea kuugua magonjwa ambayo hata chanzo chake ni vigumu kubaini!

chezea 10 percent wewe..
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Labda tuanze kwa kuuliza, kitaalamu kabla alizeti haijakamuliwa ina madhara gani kiafya? Maana inakoelekea tutaambiwa hata ugali una madhara kiafya ili watu wale kachori.
ni kweli mdau unga wa mahindi ukikaa sana huwa sumu
 
tumieni blue band sasa acheni na mafuta ya waganga wa kienyeji
 
Kuna watu wameenda kuanzisha viwanda vya hayo hayo mafuta huko singida na naona soko haliendi vizuri maana bado watu wanakimbilia yale yaliyokamuliwa na hizi mashine za wakulima wadogo wadogo ambayo yanaaminika hayajachanganywa na kitu maana unayaona wewe mwenyewe yanavyopelekwa kwenye mashine na kukamuliwa na kuwekwa kwenye vidumu
Sijui TDFA walikuwa wapi wakati hizi mashine za wakulima wadogo ziko miaka na miaka zinakamua mafuta leo tunakuja kuambiwa zina madhara
Hata waseme vipi tutaendelea kuwaunga mkono wakulima wa singida na kwingineko kuyanunua maana ndio mafuta angalau salama yaliyobaki ambayo hayajachakachuliwa
nayatumia mimi na familia yangu na sitaacha kuyatumia maana nilitumia sana mafuta haya ya kununua madukani kila siku watoto wana vipele mwili mzima nilipoacha kuyatumia na kuanza kutumia mafuta ya alzeti sijawahi ona hilo tatizo tena
Nitawaunga mkono sana wakulima kuyanunua haya mafuta mpaka hao TFDA wakawaelimishe hao wakulima namna ya kukamua mafuta yao vyema au waambie wakulima ubovu wa mashine zao na sio kusema yana madhara badala ya kuwasaidia wakulima wanaohangaika au walaji wa yale mafuta ambao wengi wanayatumia

Si ndiyo hapo mkuu, enzi hizo ulikuwa ukienda mashine kusaga, kuna mashine ya kusagia mahindi, kukobolea makande, kusaga ulezi, kukoboa karanga na ya kukamua mafuta ya alizeti. Halafu kila kitu kilikuwa kinafanywa live mbele yako bila kuchanganya takataka nyingine.

Sema kuna wakati unakuta mafuta yameisha (kwetu kulikuwa hakuna umeme) so inabidi uache mzigo pale ili mwenye mashine akirudi town kununua mafuta anakamua fasta usiku au asubuhi na mapema, kesho mnaenda kuchukua na kulipia. Wala walikuwa hawachakachui.

Otherwise, mashine zinawashwa kila siku kuanzia saa kumi jioni. Ilikuwa pia fursa ya wadada kutoka kwenda mashine kusaga na kutongozwa. lol.

Sasa leo tunambiwa mafuta haya yana sumu? Hata wale samaki pale Mgogoni watatumbia wana sumu ili watu wananunue wale wa maboksi kutoka Afrika ya kusini.

Mamlaka husika zifanye kazi ipasavyo kwa kuhakikisha wananchi wanapata vyakula vyenye afya lakini na siyo kuwakataza kutokula vyakula fulani kisa mamlaka hizo zimeshindwa ku-regulate ipasavyo.

Kumtangazia mwananchi asitumie mafuta ya alizeti kwa vile hayakidhi viwango vya usalama wa binadamu kwa kuwa wasindikaji wadogo wanatumia mashine ambazo hazichuji vizuri mafuta hao ni kushindwa kufanya kazi ya ku-regulate machine zinazoingizwa nchini au wamiliki.

Kama hawajashindwa ku-regulate basi kuna mkono wa mtu hapo.

 
Mimi naamini kuwa Tfda ni moja ya nyenzo zinazotumika kuhakikisha tabaka la chini linabaki huko huko chini au linapotea kabisa na tabaka la juu linaendelea kutawala.Nathubutu kusema wanatumika sana na wafanyabiashara wenye asili ya kiasia.Wanafanya kazi kisiasa sana na ukitaka kujua hilo,waambie wapime usafi wa hewa ya jiji la Dar.Nina uhakika watakuja na matokeo ambayo yatakushangaza kv hewa ya Dar imejaa bacteria hatari!Haifai kuvuta... ingawa bado wako watu hapa wanaitwa 'wasomi' watayasapoti na kutoa mapendekezo!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Hii taarifa yao haina tofauti na zile taarifa za habari za mkoloni. Ni sawa na kuwaambiwa wale wanaoishi sehemu zenye madini ya dhahabu na almasi eti wahame haraka kwa vile madini hao yana madhara kama kupata cancer ya ngozi na uwendawazimu.

Hata hivyo, wananchi hao wamekuwa wakiishi katika maeneo hayo miaka nenda rudi lakini hawajawahi kuumwa cancer au kuwa na wendawazimu.


[video=youtube_share;pwbFlJMGCAg]http://youtu.be/pwbFlJMGCAg[/video]
 
Mkuu nadhani swali lako lina mantiki, ila wanachodai TFDA ni kuwa mashine zinazotumika hazichuji vizuri! Sababu ya kutokuchuja vizuri haieleweki kama ni kutokana na ubora mdogo wa mashine au ni namna (process) ya kukamua inavyofanyika.

TFDA wangeweka wazi ili wananchi waelewe kabisa kuwa tatizo hasa ni nini.

Kama mashine ya unga haisagi vizuri basi huo unga utakuwa siyo mzuri kwa matumizi ya binadamu?

Kama mashine zinazotumika hazichuji vizuri, then alizeti ambazo bado hazijachujwa zina sumu?
 
Naomba kujua,hivi hayo mafuta ya alizeti wanayosemea TFDA,ndo SUNOLA kwa jina lngne?isije ikawa nakula sumu,mana mimi hapa ndo natumia hiyo Sunola,ila ni product ya sunflower!emu nijuzeni!

Umaanisha haya?

sunola.jpg


Mie naongelea zile alizeti ambazo unapanda, unavuna, unaziweka kwenye gunia wewe mwenyewe na kuzipeleka mashine, zinachujwa mbele yako, unabeba debe lako la mafuta unarudi home na kuanza kutumui mpaka unasahau.

Hayo ya SUNOLA nafikiri yanatengenezwa na Sunola Oil Mills. Ni sawa na mkazi wa Dar kununua samaki wa maboksi kutoka South Afrika wakati anaweza kupata samaki fresh pale Magogoni.
 
tumieni blue band sasa acheni na mafuta ya waganga wa kienyeji

Mie natumia siagi itokanayo na maziwa ya ng'ombe wangu, mwisho mtakuja kuniambia kuwa siagi ina sumu kwa vile sichuji vizuri ili muuze blue band yenu.
 
Hivi hawa TFDA wameanza kazi lini? Maana nakumbuka maisha ya boarding enzi zile. Ule msosi ulikuwa sumu tosha. Maharage yale yalikuwa hayafai hata kuliwa na wanyama. Tumeshakula sumu sana tuu.
Kuku wetu TFDA ndo wanarejea, tuwapokee tu, maake tumewapokea wenyewe
 
kuna watendaji tfda wanataka waonekane wachapakazi kwa gharama yoyote ile
na ina onesha hakuna waku wazuia kabisaaa
 
Kama mashine ya unga haisagi vizuri basi huo unga utakuwa siyo mzuri kwa matumizi ya binadamu?

Kama mashine zinazotumika hazichuji vizuri, then alizeti ambazo bado hazijachujwa zina sumu?


Halafu iweje mashudu (makapi) yanayotokana na alizeti yawe chakula bora kabisa kwa mifugo? Si yangepaswa kuwa sumu?
 
Hii nchi ina mambo sana, yaani watu wamekaa kimaslahi sana. Yaani huyu yupo radhi kuongopa ili kuwapatia hao Wahindi soko. Hii haiitaji uwe daktari, kama alizeti haina sumu hata kama haijakamuliwa vizuri haifanyi kuwa na sumu.
 
Hapa ni wenye viwanda na wafanya biashara wakubwa,wamewapa kitu kidogo ili watuenezee uongo,ili wajasiria mali wadogo bidhaa yao isinunuliwe.wazushi tu hawana lolote!lakini ndo serikali ya magamba ilivyo ni kukandamiza mtu wa chini asitoke.
 
Back
Top Bottom