Katika gazeti la Mwananchi la Tarehe 17/09/2013 kuna taarifa yenye kichwa cha habari
"TFDA yatahadharisha mafuta ya alizeti mitaani".
Habari yenyewe ni kama ifuatavyo:-
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imesema mafuta ya alizeti yanayouzwa mitaani hayakidhi viwango vya usalama wa binadamu. Imesema, hali hiyo inatokana na wasindikaji wadogo kutumia mashine ambazo hazichuji vizuri mafuta hayo.
Habari hizo zimekuja wakati ambapo kumeibuka mjadala mkali baada ya TFDA kutoa taarifa kwamba mafuta yanayotokana na mbegu za ubuyu yana kiwango kikubwa cha kemikali. Inasemekana kemikali hiyo in athari kwa afya. Ofisa Uhusiano wa TFDA, Gaudensia Simwanza, alisema mwaka jana walianza mpango wa majaribio ya utafiti kuhusu mafuta hayo kutoka kwa wasindikaji wadogo Singida.
Maswali ya kujiuliza:-
1. Mafuta ya mitaani ni yapina wananchi watatofautisha vipi ya mitaani na ambayo si ya mitaani?
2. Kutokana na hii kauli ya TFDA ni nini wananchi wanatakiwa kufanya? Waache kutumia mafuta ya alizeti au vipi?
3. Mafuta ya alizeti hayajaanza kutengenezwa leo au jana. Yamekuwa yakitengenezwa kwa muda mrefu sana. Je, ni kwa nini TFDA hawakufuatilia ubora wa hizo mashine siku zote hadi sasa ambapo wananchi wengi wameshatumia mafuta hayo kwa muda mrefu, kiasi ambacho kama kuna madhara basi wengi tumeshaathirika?!
Kwa kweli imefika wakati hivi vyombo vyetu vinavyohusika na maswala yahayohusu afya za wananchi ikiwamo TFDA viache ubabaishaji. Kinyume na hivyo wananchi tutaendelea kuugua magonjwa ambayo hata chanzo chake ni vigumu kubaini!