Mafuriko mwezi ujao (September 2012)

mkuu kiranga
muda wangu umeisha kesho. mungu akulinde na kuzidi kukupa afya njema kwikwiwwww
 
Bottom line, huwezi kuicheka sayansi kwa kutokuwa na majibu yote kwa sababu haijawahi kusema ina majibu yote.

Icheke dini kwa kutokuwa na majibu yote kwa sababu imesema kwamba ina majibu yote.

Mimi naikubali sana sayansi kuliko dini. Dini kwa kiwango kikubwa sana siikubali.

Aspects za dini ninazozikubali hususan ni zile ambazo zinazungumzia maadili kama baadhi ya zile so called amri 10 za mungu.

Na kwa hakika siwezi kuibeza wala kuicheka sayansi kwa ujumla. Ila ni baadhi tu ya nadharia zake ambazo mimi naona bado zina mapungufu makubwa na ambazo sikubaliani nazo - mfano hiyo nadharia ya evolution.

Lakini pia, uzuri wa sayansi ni kwamba yenyewe at least inaweka wazi kuwa jambo au kitu fulani ni 'nadharia'/ 'theory' tu na siyo undisputed fact. Sasa hata ukiangalia maana ya theory kwenye kamusi utaona kuwa inaacha mwanya wa uwezekano wa kutokuwa sawa au sahihi. Hebu cheki hizi definitions za theory kutoka M-W.


Najua unaweza kujua kwa nini kwenye hiyo def. ya kwanza wametumia neno 'intended'. Sasa hebu toa hilo neno 'intended' halafu toa na 'is' uone jinsi ambavyo maana inabadilika.

So I'm not at all anti-science or anything near that. It's just that when it comes to certain things I think science hasn't been able to convincingly explain their origin as of yet.
 

You got it. You would be surprised to see so many people do not get this.

Science admits to being fallible and at best convergent.

But who is this "science"?

You are welcome to pick up the baton and research and write papers etc. The scientific community welcomes that.

Try that shyt in religion and they will hang you even if you are certified as mentally challenged like this Pakistani girl.

And to think that sane people do this in the name of religion? They look like the ones who are insane.

No Bail Yet For Pakistani Girl Accused of Blasphemy « VOA Breaking News
 
mkuu kiranga
muda wangu umeisha kesho. mungu akulinde na kuzidi kukupa afya njema kwikwiwwww

muda lazima uishe, ngoma kali hii.

Kabla ya kuniombea mungu anilinde kwanza ni convince kwamba yupo, ama sivyo nitaona unanizuga tu.

Kama mie ninavyoweza kukuzuga kwa kukurudishia "Willy Gamba akulinde"
 

hana uwezo wa kuelewa huyo,anao wa kukariri tu. at the age of 11, alikuwa anakariri kama kasuku,na bahati mbaya kwake hata alipo attain majority bado ana ulemavu wa kujua kukariri tu pasipo kuwa na tafakari ya kumsaidia kuelewa maandiko. narudia 'kiranga' book sense 100% excellent, common sense 1% very poor.
mtu wa aina hii ni vigumu mno kujifunza kinyume na alivyo kariri...
 

Hapa ndo panaonesha uwezo mkubwa ulionao wa kukariri na kuaminisha uongo kwa jina la sayansi, umeandika evolution haiwezi onekana kwa kuwa scale ni ya mbali mno na inatumia mda mrefu 'billion of years'. ni antibiotic gani ambayo imetumiwa japo kwa miaka 500 tu ili kupata sifa ya kutufunza evolution, kitendo cha mtu kuadopt mazingira pia kwako ni evolution,mtu aweza kwenda shimoni kariakoo kwa mara ya kwanza atasikia harufu kali possibly na chafya,engineer wa miili yetu 'Mungu' aliitengeneza miili katika mfumo ambao ni wa kimchakato sio static hivyo inauwezo wa kujizoesha kulingana na mazingira ndiyo maana hata halufu ikiendelea kuwepo mwili utajibadili kuhimili na utakuwa huisikii tena,kwa wanasayansi na mabingwa wa kukariri kama wewe hiyo tu itakuwa na evolution ???!!! kama kwa binadam sio evolution kwanini kwa bakteria iwe evolution ? kama ni evolution basi, evolution haihitaji mamilioni ya miaka kama mnavyojidanganya ili kujificha, ma striker wa sayansi ni mabingwa wa kufunga kwa kuhamisha gori...
 

Scrap... what are those science many answers with their corresponding question,and what are the questions that religion lacks answers ?
 
Hapa ndo panaonesha uwezo mkubwa ulionao wa kukariri na kuaminisha uongo kwa jina la sayansi,

Huyu anasema nini? Hebu tumsikilize, labda ana gotcha.

umeandika evolution haiwezi onekana kwa kuwa scale ni ya mbali mno na inatumia mda mrefu 'billion of years'.

Nimeandika pia kuhusu scale, kwamba, kwa kuwa bacteria wanajigawanya kwa kasi sana ukiwalinganisha na binadamu (binadamu kuzaa mathalani ni mpaka miaka takriban 16, kwa hiyo mpaka mtu apate mjukuu itachukua si chini ya miaka 32 aghalabu) bacteria wanajigawa kila dakika 20. Na kwa sababu bacteria ni wadogo na wanajigawa sana, na kwa sababu evolution agent wake mmoja mkubwa ni mutation iliyo katika reproduction, basi utaweza kuona evolution ikiwa kazini kwa urahisi na haraka sana ukiangalia bacteria kuliko ukiangalia binadamu.

Soma zaidi kuhusu bacterial reproduction hapa Bacterial Reproduction



Habari yangu ya juu imefunga kipande hiki cha mjadala, labda kama unataka kuendekeza ubishi tu.

Ungeelewa somo la scale hata usingejiaibisha hivi.
 
Scrap... what are those science many answers with their corresponding question,and what are the questions that religion lacks answers ?

Nimeuliza hapo juu kwa nini mungu mwenye uwezo wote na upendo wote aumbe ulimwengu wenye mabaya, maovu, umasikini, magonjwa etc kama tulionao?

Watoto wachanga wanakufa bila hata kujua utamu wa maisha, tena vibaya vibaya, kwa maumivu makali.

Hata mie ningekuwa na uwezo wa kuumba dunia bila shurti nisingeumba dunia yenye mabaya kama hii, kwa nini huyu mungu mwenye uwezo wote na upendo wote karuhusu haya?
 
 
muda lazima uishe, ngoma kali hii.

Kabla ya kuniombea mungu anilinde kwanza ni convince kwamba yupo, ama sivyo nitaona unanizuga tu.

Kama mie ninavyoweza kukuzuga kwa kukurudishia "Willy Gamba akulinde"

teeeee kwikwiwiiwwwwwi namfurahia sana willy gamba kama vile yupo kweli. mh nisimsifie sana nisijeachika bure kwa character wa kitabuni.
 
Kama vile kitabu cha "Njama" kilivyo cha Willy Gamba.

ulivyokitaja kitabu cha willy gamba umenikumbusha hadithi nyingine mishawahi kuisoma ya mafiction ya kufa mtu kinaitwa ZIRANI NA ZIRAILI. cha mkufya. kitabu hiki nilikipenda sana.maana kinaubishani kama wa hapa jamvini kuhusu mungu.
 

i dont have a problem with science for its efforts to try to expain things,and science is good. but to some of the things using science to gets answers is like using a best book to pass exam yet you fail everyday.will you be depending on it to pass the same exam?
 

Tatizo lako unapinga jambo/kitu bila wewe mwenyewe kuja na hoja baada ya kuvipitia 'Vitabu'. Maswali yako yote yanajibika, ila ungekuja na hoja moja kwa moja unayoipinga ndani ya 'Kitabu'
 
kiranga,
hapa ni sawa na kusema mpira huu hapa kuna aliyeuleta wewe unasema umejileta wenyewe nachurali hapa ndio tunapobishana.

Utajifunza lini ku quote? Karibu nakuchoka!

Nisha dismiss evolution for the sake of argument.

Hata nikisema sijui mpira umetoka wapi, hili halimaanishi ni lazima uwe umefumwa na bibi.

Kutojua maisha yameanzaje, hata kama evolution si kweli, hakuna maana kwamba mungu kaumba maisha.
 

swali lako ni la kipuuzi na haliendani na hoja uliyoulizwa hapo juu. wewe ndiye unaye define hayo unayosema ni mabaya kwa kuwa huko ndani ya mpango wa Mungu,yeye ndiye Muumba na ndiye mpangaji wa standard,yapi ni mabaya, yapi ni matatizo yeye ndiye anayejua na kwa tuliowake majibu yapo ndani ya kitabu chake hatuna shida nayo.MAJIBU YAKE YAPO WAZI KABISA KWENYE MAANDIKO, wewe una vigezo vyako vya utambuzi wa mabaya lakini si lazima viwe ndiyo vigezo vya Mungu, Maisha na Kifo ni shida kwetu sisi wanadam lakini si kwa Mungu,amka kiranga.

Toa majibu ya kisayansi na maswali yake, toa pia maswali ya kiimani yaliyokosa majibu.Tatizo unataka upewe majibu ya kidini kisayansi hapo ndipo madhara ya kukariri yanapojionesha.
Swali la kidini linajibiwa kidini,kama ilivyo swali la kisayansi linajibiwa kisayansi. kinyume chake ni ujinga tu.
 


red. Ukitaka kuwa mkweli ungeandika,HAKUNA MAANA KWAMBA MUNGU KAUMBA AU HAJAUMBA MAISHA.
 
Tatizo lako unapinga jambo/kitu bila wewe mwenyewe kuja na hoja baada ya kuvipitia 'Vitabu'. Maswali yako yote yanajibika, ila ungekuja na hoja moja kwa moja unayoipinga ndani ya 'Kitabu'

Sihitaji kupinga chochote kuonyesha idea ya kuwepo kwa mungu haijajitosheleza.

Nahitaji kuuliza maswali tu.

Na ukishindwa kujibu maswali nitakuwa nishapinga vya kutosha.

Na mpaka sasa umeshindwa kujibu maswali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…