Mafuriko mwezi ujao (September 2012) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafuriko mwezi ujao (September 2012)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Elisha Ray, Aug 1, 2012.

 1. Elisha Ray

  Elisha Ray JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 302
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wakuu, I hope wote mko poa kabisa.

  Nataka kuwashirikisha jambo. Kuna hali ya mafuriko makubwa yanayokuja kutokea Tanzania mwezi ujao. Kuna watu ambao Mungu amesema nasi ili tuombe toba kwa ajili ya nchi ili hali hii isitokee na hasa kama itatokea basi isilete madhara ambayo yanaweza kutokea kama hatutaomba Mungu atunusuru na maafa.

  Nchi yetu 'imemezwa na chatu'. Hii maana yake ni kwamba nchi hii imetumbukia katika uchawi na kumwabudu shetani as nyoka ni shetani as well as uchawi/ushirikina. Watu waliopewa dhamana kwenye taifa hili iwe serikalini au katika kanisa wamesahau wajibu wao na badala yake wanamkumbatia shetani na kazi zake zote i.e uuaji na umwagaji wa damu zisizo na hatia, uchawi, wizi, uongo na pia ukahaba umekithiri, uaminifu umepungua sana, ufisadi, upagani, ibada za mizimu, kuabudu shetani na mambo mengine yote yafananayo na hayo na kumchukiza Mungu na amekasirika. Mambo yote haya tunayaona day in day out. Na watu wanafurahia watu waovu na uovu kuliko uadilifu na watu wanaotetea haki.

  Mungu anaipenda sana Tanzania lakini anachukia uovu huu ndio maana ameonyesha nini kinakuja ili tuombe toba atusamehe na atunusuru na hali hiyo na kama bado itatokea basi isilete madhara makubwa au yasitokee kabisa.

  Picha ya mafuriko yanayokuja yanaonyesha mvua kubwa sana ya kutisha na nusu ya Dar ikiwa imemezwa na maji ambayo yamechanganyika na maji ya bahari. Hii inaashiria gharika au kimbunga chenye mvua kubwa.

  Kwa yeyote mwenye mzigo wa kuliombea Taifa hili tafadhali omba toba kwa ajili ya nchi yetu na ufunge kwa siku tatu kawaida na sio tatu kavu (utachagua mwenyewe siku za kufunga) ili Mungu atuepushie na balaa hili. Tafadhali mshirikishe na mwenzio.
  Nimewashirikisha ili isije kula kwetu tuliopewa huu ujumbe kama tutakaa kimya bila kushirikisha wengine pia waombe.

  Usichangie kwa kukashifu na kama huna mchango au huamini basi wewe pita tu na Mungu atakubariki.

  Mathayo 18:18, 2 Nyakati 7:14, Isaya 62:6, 45:11
   
 2. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  lol haya bwana naona kizazi cha joshua wa emmanuel tv kipo Tanzania pia
  Mungu alishesema hataangamiza tena binadamu kwa gharika kama ilivokuwa wakati wa Nuhu
  kama wewe umefunuliwa hivo basi yelekea Mungu alitoa ahadi ya uwongo pale alipotupa ishara ya Upinde wa mvua.Genesis 9:8 hadi 11.
  kama mafuriko yatakuepo ni kwa vile sisi wenyewe tumeharibu mazingira au ni matetemeko ya kawaida hayahusiani na ghadhabu ya Mungu.
  hata hivo sikatai kuwa tanzania imetumbukia katika uovu wa kutisha hata shetani mwenyewe anatushangaa
  nakuunga mkono kuwa tusali daima kuomba msamaha na tuwe na toba ya kweli
  ila tusiseme ni ghadhabu ya Mungu kwani ametupa uhuru wa kuchagua kumfuata yeye au kumfuata Ibilisi;
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,191
  Trophy Points: 280
  Hamna mungu wala shetani.

  Kama idara ya hali ya hewa inaona mvua zinakuja na kukuarifu, na wewe unakaa mabondeni bado, wewe ndiye shetani wako mwenyewe.

  Ukiheshimu mazingira na kuhama utakuwa mungu wako mwenyewe.

  Kwingine kote tnasingizia tu kwa kukosa kujua.
   
 4. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #4
  Aug 2, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu tumia akili au kalale mchana kwani kwetu Bara ni Kiangazi kikali mwezi huo, halafu huko ulikoota wala hujafika na wala aliyefika hajarudi kuja tueleza kukoje. Nyie ndio mliosema mwisho wa Dunia ulikuwa uwe 21 May 2011
  Mimi naomba tukutane Oktober 2012 Maanani atujalie tukuimbushane, kwani kuna Amri ya 10 nya MUNGU aliyompa MUSA iansema USIMSHUHUDIE JIRANI YAKO UONGO km huu ni kutishana Mvua ya Kiangazi
   
 5. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Inawezekana Mungu amesikia kilio chetu. Angemuangamiza kwanza baba riz ningekuwa na amani ya moyoni...
   
 6. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,339
  Likes Received: 2,664
  Trophy Points: 280
  Mkuu mleta uzi huu nina maswali kadhaa kwako:
  1. Ujumbe ulioupata uliletewa kwa njia ya ndoto,ishara,ujio wa malaika,sauti, maono au?
  2. Baada ya kupata huo ujumbe ni nini ulichoambiwa kifanyike ili kuepuka na hiyo gharika.
  3. Wakati wa Nuhu au Lutu, Mungu aliwatenga wana wake na kiama kilichokuwa kinawakabili, je katika huo ujumbe uliopewa waathirika watakuwa ni watu wote au? hakuna wateule wenye kutengwa?
  4. Hiyo gharika itagharikisha Dar es Salaam tu au nchi nzima.

  "Ikiwa watu wangu walioitwa kwa JINA langu watageuka na kutubu, nitaiponya nchi yao..."
   
 7. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,223
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Kama ulivyoshauri ndugu mtoa hoja,mimi ngoja nipite tu kimya kimya!
   
 8. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #8
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Gosh!!, who will resque this land?, people still live in idealistic world while the world is in post-modern stage. Floods Tanzania in September!!!! real!!, are you crazy??!!!!
   
 9. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  hoja hii msiibeze, shauri yenu
   
 10. jamiif

  jamiif JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 2,417
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  sasa mbona mtoa mada kasepa??? mh, hizo zitakuwa mvua za vuli au masika? SIOGOPI!
   
 11. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Source?
   
 12. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #12
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  ahahahahahaaaaaaaaaaa_chezea kiranga wewe!
   
 13. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #13
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Toy soldier,.......
   
 14. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #14
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,108
  Likes Received: 6,581
  Trophy Points: 280
  Nimekusoma mkuu.
   
 15. HP1

  HP1 JF-Expert Member

  #15
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 3,353
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  God forbid!
   
 16. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #16
  Aug 2, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Mungu hajawahi kusema na watu weusi!!!
   
 17. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #17
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Hili nalo neno_ingawa watu hawapendi kulisikia kwa sababu za kujiliwaza.
   
 18. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #18
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Mungu yupi..wa_waisrael ama wa_waarabu,...maake hao ndio tunajipendekeza kwao.

  Anyway'miafrika ndio tulivyo'...by Nyani Ngabu..a jf member
   
 19. Kizamani

  Kizamani JF-Expert Member

  #19
  Aug 2, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mtoa mada ni mfuasi wa kakobe nini? Mbona kala kona kama kakobe katachia tukilumbana tu!
   
 20. Bwana Mapesa

  Bwana Mapesa JF-Expert Member

  #20
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,926
  Likes Received: 660
  Trophy Points: 280
  We ni Wakala wa Mamlaka ya hali ya hewa?.....au ndo life ishakupiga unata kuanza uzushi...?
   
Loading...