Mafuriko makubwa yatokea wilayani Dumila,barabara ya Morogoro-Dodoma yafungwa

mh poleni sana walioathiriwa na tukio hili kwa namna moja au nyingine. picha imedhihirisha ukubwa wa janga lenyewe.
 
Aisee poleni sana,kwamba wa Dodoma hukohuko na wa Morogoro hukohuko,poleni wasafiri wanatumia njia ya barabara
 
mafuriko yamesomba daraja la Dumila sasa hivi watu wanazunguka arusha wengine mbeya no road cnnctn betwn moro and dom
 
Pombe anapiga ten percent tu

Ni kweli mkuu sisi wana dumila tuna hasira na Magufuri na Mkulo, kuna mkandarasi wa kichina hapa anajenga barabara tangu 2010 hadi leo hajamaliza hata kilimita 50, hili daraja lilitelekezwa na tanroad kwa kuwa tayari mkandarasi alikuwa site lakini yaliyotokea leo mungu anajua.
NI KWAMBA kuna mashine za mchele jirani zina hali mbaya maji yameingia hadi kwenye maghala inakadiriwa tani zaidi ya 30 za mchele na mpunga zimelowa maji.Kwa ujumla hali ni tete
 
Wadau daraja la dumila linalounganisha Dodoma na Morogoro limekatika kutokana na mvua kubwa.

Hakuna mawasiliano kati ya dar na dodoma.Inaonekana ni tatizo litakalokaa muda mrefu.Wasafiri na malori wanashauriwa kupitia Singida na Chalinze!.

Source:Radio One
 
Serikali imefunga barabara ya Moro-Dom kwa muda usiojulikana kufuatia kubomoka daraja la Dumila, yashauri wasafiri kutafuta njia nyingine.source mwananchi breaking newz
 
Serikali imefunga barabara ya Moro-Dom kwa muda usiojulikana kufuatia kubomoka daraja la Dumila, yashauri wasafiri kutafuta njia nyingine.source mwananchi breaking newz

Radio one wanasema ni barabara ya dodoma - moro. Sijui tushike lipi.
 
Back
Top Bottom