Hiyo kauli yako ya mwisho inaonesha una kitu moyoni juu ya huu mchakato, kama si kitu basi hujafikiria sawasawa.Sina hakika kama hata hawa wanopewa bure ni ruhusa kisheria.. Basi hakuna maana ya kufanya interview.
Anyway, kazi ni kwenu vijana.... Toeni pesa mpate form jamani...
Ngoja nikupe kitu kidogo, kila kazi huwa zina upendeleo, hata nafasi kama Rais huwa anapewa favour flani, anaeza akafa yeye ila kodi zetu zitaigharamia familia yake ambayo haijafanya chochote kwa nchi ila ni baba.
Kama Mbunge pia anapewa favour, iwe kwa wakuu wetu wa vyombo vya usalama!? Na nikujurishe tu kuwa sio Tanzania ila ni duniani kote iko hivyo, vyombo vya Usalama waTaifa na Jeshini kwa maaskari wake huwa kuna Spirit flani ambayo inatembea ndani ya familia ndo maana wanawapa hizi nafasi kwa ajili ya familia zao na ndugu zao wa karibu. Na ktk hizo form kuna sehemu ya udhamini hapo na yeye anaweza kuhusika.
Hao maaskari form wanapewa bure kabisa, huu utaratibu haujaanza jana wala leo, tangu miaka hiyoooo ila kwa sasa haya majeshi yamekuwa ni kimbilio kubwa saba kwa vijana tofauti na zamani.
Sasa kama unavyojua sehemu yenye mlo huwa ushindani ni mkubwa sana, na sehemu yenye ushindani popote pale duniani hususani Afrika ni lazima utoe hata ela ya maji.
Na hio sio Jeshini tuu, nenda TANAPA, BANK etc ni ngumu kupata kazi kama hauna mtu wa kukubeba, na kama hauna hapo lazima ujiongeze.