Mafunzo ya JKT kwa kujitolea kwa mwaka 2016

Mafunzo ya JKT kwa kujitolea kwa mwaka 2016

Si ndio hapo, sijui degree inaongeza uwezo wa kula. Mi nadhani hizi nafasi zingekuwa wazi kwa vijana wote wanaotaka "kujitolea" sababu inaeleweka wazi sio ajira zile so sidhani kama kunakuwa na kulaumiana. Kama tatizo ni hizi bachelor basi vyuo vifungwe coz ni vingi mno na vinazalisha graduates wengi tofauti na mahitaji halisi.
Mkiziruhusu fkra kufikili zaidi ya hapo mtapata majibu mazuri kuhusu hilo.....

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
 
Hapo lazima kutakuwa na hili la degree muhimu yenye uhitaji wa kwenda huko jeshini ndiyo maana wengine watakuwa wanakatwa
 
kama swala ni logistics ,
Kwanini sasa wanabagua graduates wanawachukua kidogo? Si wawachukue kwa uwiano sawa? Kama kula si wanakula wote?
Sababu no 1

Mfumo wa utawala na madaraka wa jeshi
Mfumo wa jeshi upo kama wa vile ulivyokua mfumo wa elimu wa kikoloni, yaani una shepu ya piramidi ( pyramid ). Yaani jeshi linakua na maofisa wa ngazi za juu wachache, wa ngazi za kati wengi kidogo na maaskari ambao ndo wapiganaji wengi. Kama ilivyo piramidi, inakitako kikubwa / kipana, na kadri linavyozidi kwenda juu ndo linazidi kupungua kwa kua jembamba. Kwaiy jeshi lazima lichukue wasomi kwa kuzingatia huo mfumo, maana wasomi ni viongozi / maafisa wa ngazi mbali mbali katika mfumo. Kwaiy hawawezi chukua watu alfu wakakosa majukumu ya kuwapa kutokana na kua wengi au wakakosa kupata nafasi za madaraka wanazostaili kutokana na elimu zao, ikitokea ivyo kutakua na manung'uniko maengi katika jeshi, na kukishakua na manung,uniko ya kukosa stahiki basi ata ufanisi katika utendaji wa kazi utapungua.

Sababu no 2
Logistics. Maafisa wa jeshi, kama nilivyoeleza hapo juu, wapo katika makundi mengi, na hawa watu wana stahiki nyingi mno, hasa kuanzia ngazi ya majenerali, kuna mafao, mishahara, marupurupu na mambo mengi wanayostahili kupata pindi wakiwa kazini / ofisini na pindi wakistaafu. Kutokana na wingi wa stahiki izo, lazima hawa watu wawe wachache ili kuipunguzia serikali mzigo mkubwa wa malipo ya stahiki zao.

Nadhani nimeeleweka. Namalizia yai langu
 
hahaaaaa! poa mkuu japo umenitusi but nashukuru kwa kuweka na link!
Haja kutusi kakuambia ukweli weka hiyo website yako uliyokuwa una peruzi ili siku nyingine usaidiwe kama neno website ndio tatizo kwa kisukuma ni tovuti kaka
 
Nafasi zimeshaanza kutangazwa ktk baadhi ya wilaya zenu hivyo kwa wale wanaohitaji nenda ktk wilaya yako husika ktk office za mshauri wa mgambo
430615db541eb94305fd3c27653afcbd.jpg
54639a4f587a961997fd5c08cde08986.jpg

Kwa wale wa wilaya ya kinondoni mkoa wa dar es salaam hiyo hapo juu

===================

TANGAZO

180681_158735330845567_2210285_n.jpg

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, anawatangazia vijana wenye sifa za kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea kwa mwaka 2016.

Barua zilizoainisha sifa za kijana kujiunga na mafunzo ya JKT zimetumwa kwa Waheshimiwa Wakuu wa mikoa. Mchakato wa zoezi la kuwapata vijana wenye sifa unaanza Aprili 2016 hadi tarehe 20 Mei 2016.

Sifa za mwombaji ni kama zifuatazo:-

1. Awe raia halisi wa Tanzania.

2. Umri. Kwa vijana wenye elimu ya Darasa la saba hadi kidato cha sita ni miaka 18 hadi 23.Vijana wenye elimu ya Stashahada umri ni miaka 18 hadi 26 na Vijana wenye elimu ya Shahada na kuendelea umri ni miaka 18 hadi 30.

3. Awe na afya njema, akili timamu.

4. Asiwe na alama yeyote ya michoro mwilini (Tattoo).

5. Mwenye tabia nzuri, hajapatikana na hatia Mahakamani na hajawahi kufungwa.

6. Kwa vijana waliomaliza elimu ya Sekondari kidato cha nne wawe waliomaliza kuanzia mwaka 2010, 2011, 2012, 2013 na 2014 wenye ufaulu ufuatao:-

(a) Waliomaliza 2010 hadi 2012 wawe wamefaulu na wawe na alama (Points) zisizopungua 32.

(b) Waliomaliza 2013 wawe wamefaulu na wawe na alama (Points) zisizopungua 38.

(c) Waliomaliza 2014 wawe wamefaulu na wawe na GPA isiyopungua 0.6.

7. Awe na elimu ya msingi aliyehitimu darasa la saba.

8. Awe na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate).

9. Awe na cheti halisi cha kumaliza shule (School Leaving Certificate)

10. Awe na cheti halisi cha matokeo (Original Academic Certificate/Transcript).

11. Asiwe ametumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au KMKM wala kuajiriwa na Idara nyingine Serikalini.

12. Asiwe amepitia JKT Operesheni za nyuma.

13. Asiwe amejihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, bangi na yanayofanana na hayo..

Waombaji wenye sifa wapeleke maombi yao kwa Waheshimiwa wakuu wa mikoa. Makao Makuu ya JKT hayatapokea na hayapokei maombi yoyote, kwa vijana watakaoomba nafasi hizo wazingatie maelekezo yatakayotolewa kuepuka usumbufu.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Habari na Uhusiano

Makao Makuu ya JKT

Tarehe 05 Aprili 2016

Chanzo: TANGAZO MAALUM VIJANA WA KUJITOLEA 2016
Kama kuna mtu aliyeomba ILEMELA anicheki 0769576704
 
Mara nyingi jkt huwa wanapenda kuchukua degree za kilimo,animal science,veterinary,food science,education,nursing,medicine na mechanic engineering.ukiona una degree tajwa hapo juu na umeachwa,basi kuna walakini.fani nyingine sio sana kivile.
 
Mara nyingi jkt huwa wanapenda kuchukua degree za kilimo,animal science,veterinary,food science,education,nursing,medicine na mechanic engineering.ukiona una degree tajwa hapo juu na umeachwa,basi kuna walakini.fani nyingine sio sana kivile.
Education Mkuu goja tuone
 
Mara nyingi jkt huwa wanapenda kuchukua degree za kilimo,animal science,veterinary,food science,education,nursing,medicine na mechanic engineering.ukiona una degree tajwa hapo juu na umeachwa,basi kuna walakini.fani nyingine sio sana kivile.
Da watu mnauaaaa mbaya...mbona kuna nwanangu BA.KISWAHILI anasubiri commision..
 
Mara nyingi jkt huwa wanapenda kuchukua degree za kilimo,animal science,veterinary,food science,education,nursing,medicine na mechanic engineering.ukiona una degree tajwa hapo juu na umeachwa,basi kuna walakini.fani nyingine sio sana kivile.
Mimi ni BSc in mining engineering na nimechukuliwa na wakilimo walikuwepo na wamepigwa chini
 
Back
Top Bottom