Mafisadi Wizara ya Ardhi

Mafisadi Wizara ya Ardhi

1. Wakuu Bongo Hakuna Haraka, ukiwa na Haraka Jasho litakutoka.

2. Kila section Imeoza na Inanuka. Tumeshindwa ku-organize utendaji wa Serikali kiasi ambacho kila mtu mahala alipo anaona sehem ya Ulaji, na huwezi amini hata rafiki yako anaweza kukutoa Upepo bila wewe mwenyewe kujua.

3. Tunafanya Utendaji uonekane Mgumu, mtu huwezi kushughulikiwa mambo yako hadi ujuane na mtu fulani ktk secta fulani, na ukiwa huna mtu mfuko wako lazima utoboke. Wachache wale wanaokhofia M/Mungu na Siku ya Mwisho ndio wanaweza kukushughulikia bila kukuuliza unatoka wapi au unafanyakazi wapi au....mtu anaangalia job description zake basi...

Labda na huku tunahitaji ku-"privatize" ili utendaji uende....

4. Kila Zoezi ktk Idara ya Ardhi ni Kero kwenda Mbele... Kupata Kiwanja tu kasheshe...na Ukikosa ukinunua kwa watu then ufanye Transfer..zoezi lake jasho litakutoka....baada ya Hapo utaambiwa nenda TRA ukalipie....Nako huko utazungushwa as if watu hawalipwi mishahara....sasa mtu anakufanyia hivyo as if wewe uliepeleka Faili unalipwa pesa nyingiiiiiii....

Labda wenzetu wa Mikoani nao watueleze...may be hii ni experience ya DSM au Mikoa ambayo Viwanja vyake ni VIPUSA.
 
Yaani nashukuru sana sana kwa wana JF kuhamia Wizara ya ardhi. hawa jamaa wana miradi waliyobuni inaitwa ujenzi wa vituo vya huduma za kijamii na kibiashara (satellite towns). Kwa kuanzia walianzia eneo la Luguruni Kibamba ambapo zaidi ya wakazi 259 walitakiwa kuhama kupisha ujenzi wa mji wa mfano wa Luguruni. baada ya hiyo pilot project watahamia Kigamboni, Kongowe, Pugu Kajiungeni, Bunju na Mji Mwema ambko kote kutaanzishwa vituo hivi vya kibiashara.

Cha kushangaza unyonyaji uliotendeka hapo ni wa kutisha sana. kaya hizi 259, zilifanyiwa uthamini wa mali zao Juni 2007 na kulipwa fidia Desemba 2007. Cha kushangaza wakati ambapo kiwanja cha Mita 20 X 20 sawa na 400 sq metres kilikuwa kinauzwa kwa bei ya kati ya Shs Milioni 4 hadi 6 sawa na Shs 10,000 hdi 15,000 kwa Sq Mita moja. Hawa mafisadi wa ardhi waliwalipa wananchi kila mita mraba Shs 300 sawa na Shs Milioni moja na Laki mbili tu bila ya kwa ekari moja bila ya aibu yoyote.

Hii ilikuwa ni sawa na 2-3% ya bei ya soko la ardhi kwa eno la Kibamba. Uthamini ulifanyika ulikuwa ni wa kiwizi wizi tu, badala ya kutumia nyaraka halali la Serikali kwa ajili ya Ukaguzi wa uthamini iitwayo VAL FORM 1, mafisadi hawa walitumia madaftari (counter books) kurekodi mali za wafidiwa. Nyaraka VAL FORM 1 hutumika kurekodi mali za wafidiwa katika eneo linalofidiwa iwe ni kiwanj, shamba au nyumba na kasha kusainiwa na mwenye mali, kiongozi wa eneo na mthamini mali.

Mwenye mali hupigwa picha mbel ya mali yake na picha hiyo kubandikwa upande wa nyuma wa nyaraka hiyo; ambapo pia mtaalamu wa michoro hutakiwa kufanya mchoro wa mali inayofanyiwa uthamini upande wa nyuma wa nyaraka hiyo na kuweka sahihi yake.

Kimsingi nyaraka hiyo ili iwe halali kwa ajili ya malipo halali kwa fedha za Serikali inatakiwa kuwa na sahihi nne kama ifuatavyo Mwenye mali, kiongozi wa eneo, mthamini mali na mtaalamu wa michoro. Mantiki ya waliotajwa kuweka sihihi zao ni kuthibitisha taarifa zilizojazwa katikan yaraka husika. Na endapo tarifa hizo itagundulika baada ya malipo kuwa kuna hitilafu yoyote, vyombo husika viweze kufanya ufuatiliaji. Nyaraka ya pili inayotakiwa kujazwa ni VAL FORM 2 ambayo taarifa zizlizoma katika VAL FORM 1 huhamishiwa katika nyraka hiyo na kisha mahesabu tya kiwango cha fidia hukokotolewa. Mkokotoa mahesabu hutakiwa kuweka sahihi yake.

Anayekagua hesabu hizo pia hutakiwa kuweka sahihi yake na mwisho Mthamini Mkuu wa Serikali hutakiwa kuweka sahihi yake na mhuri.( Tazama Attachments za mmoja wa waliolipwa jinsi nyaraka walizojaza watumishi wenyewe zisivyokuwa na sahihi zozote). Kwa mliwaji huyu kwa kutumia nyaraka hizi zisizo kuwa halali ikatayarishwa hati ya malipo na kisha hundi ya malipo ya fidia ya Shs 12,463,800/= Milioni Kumi na Mbili Laki nne sitini na tatu na Mia nane tu) zikiwa fedha za Serikali. na hivi ndivyo ilivyotkea kwa mradi mzima wa kuwafidia kaya 259 kwa mtindo huu.

Katika hali inayoonyesha kuwa viongozi na watumishi wa Wizara ya Ardhi washirikiana kufanya ufisadi waliwalipa waaathrika 259 wa mradi wa Luguruni zaidi ya Shs Bilioni moja za Serikali kama fidia pasipo nyaraka hizi kutumika. Nadhani watalamu wa mahesabu watanisaidia kuwa mafisadi hawa walitumia nyaraka zipi kama supporting documents kwa malipo hayo.

Licha ya fidia hizikuwa finyu bila aibu mafisadi hawa wakawapatia waathrika hawa notisi ya siku 30 wawe wamehama kutoka katika eneo huiska. Sheria ya Ardhi na 4 ya 1999 inataka notisi kuwa ya siku 90. Kwa hakika this was man made disaster. Ilibidi wanaharakati tuingilie kati to preveny man made disaster. Tulipiga kelele kiasi cha kumvuta Mhe Jiohn Magufuli, ambaye alitembelea eno hili tar 17 Januari 2008 na kuquash the illegal demolition order.

Akawaruhusu wananchi kuendelea kuisha eneo hilo hadi hapo atakapo toa tamko lingine. Na akakabidhi majina yote ya waliolipwa kwa vyombo dola kwa uchunguzi zaidi. Maskini hii ndio ilikuwa kazi ya mwisho Mzee Pombe pale Ardhi. Mama Sijaona Katibu Mkuu alikerwa sana na intervention ya Mzee Pombe akamtumia Ndg Luhanjo Katibu Mkuu kiongozi kumuundia wizara ya kitoweo, ili aweze kuwanusuru mafisadi wake.

Kutokana na evidence tuliyoweza kugather, ilimbidi Mhe John Chiligati aagize ufanyike uthamini mali upya kwa kuleta wathamini wapya kabisa na wake wa zamani kufichwa ofisisni badal ya kuchukuliwa hatua zozote za kinidhamu au kisheria. Uthamini wa mali mopya ulifanyika kwa kutumia nyaraka za Serikali halai yaani VAL FORM 1 & 2. Zoezi lilizaa malipo ya fidia ya nyongeza ya kati ya 85 to 600%; Kutoka Shs 300 to 2000/= per sq metre, au from Shs 1.2 M to 8.0 Milion per acre.

Swali hapa lilibaki fedha hizi za wananchi zilikuwa wapi? Nani alikuwa nazo? Zilihifadhiwa wapi? N.k Cha kushangaza licha ya Serikali kulazimika kuingia gharama za kufanya uthamini wa mali upya na kulipa fidia za nyongeza hakuna mtumishi hata mmoja ambaye amechukuliwa hatua zozote za kinidhamu au kisheria? Watumishi walifanya vitendop hivi waliondolewa briefly kupooza hasira za wananchi then wakaendelea na mradi huu eneo la Kwembe ambako walirudia ufisadi huu na mwingine mwingi.
 
Wewe ayebo Yebo haujawahi kukubwa na masuala ya fidia ndio maan unawasifia. Subiri wasfike mtaa wako ndio utajua kama wamejirekebisha au la?
 
Yaani nashukuru sana sana kwa wana JF kuhamia Wizara ya ardhi. hawa jamaa wana miradi waliyobuni inaitwa ujenzi wa vituo vya huduma za kijamii na kibiashara (satellite towns). Kwa kuanzia walianzia eneo la Luguruni Kibamba ambapo zaidi ya wakazi 259 walitakiwa kuhama kupisha ujenzi wa mji wa mfano wa Luguruni. baada ya hiyo pilot project watahamia Kigamboni, Kongowe, Pugu Kajiungeni, Bunju na Mji Mwema ambko kote kutaanzishwa vituo hivi vya kibiashara.

Cha kushangaza unyonyaji uliotendeka hapo ni wa kutisha sana. kaya hizi 259, zilifanyiwa uthamini wa mali zao Juni 2007 na kulipwa fidia Desemba 2007. Cha kushangaza wakati ambapo kiwanja cha Mita 20 X 20 sawa na 400 sq metres kilikuwa kinauzwa kwa bei ya kati ya Shs Milioni 4 hadi 6 sawa na Shs 10,000 hdi 15,000 kwa Sq Mita moja. Hawa mafisadi wa ardhi waliwalipa wananchi kila mita mraba Shs 300 sawa na Shs Milioni moja na Laki mbili tu bila ya kwa ekari moja bila ya aibu yoyote. Hii ilikuwa ni sawa na 2-3% ya bei ya soko la ardhi kwa eno la Kibamba. Uthamini ulifanyika ulikuwa ni wa kiwizi wizi tu, badala ya kutumia nyaraka halali la Serikali kwa ajili ya Ukaguzi wa uthamini iitwayo VAL FORM 1, mafisadi hawa walitumia madaftari (counter books) kurekodi mali za wafidiwa. Nyaraka VAL FORM 1 hutumika kurekodi mali za wafidiwa katika eneo linalofidiwa iwe ni kiwanj, shamba au nyumba na kasha kusainiwa na mwenye mali, kiongozi wa eneo na mthamini mali. Mwenye mali hupigwa picha mbel ya mali yake na picha hiyo kubandikwa upande wa nyuma wa nyaraka hiyo; ambapo pia mtaalamu wa michoro hutakiwa kufanya mchoro wa mali inayofanyiwa uthamini upande wa nyuma wa nyaraka hiyo na kuweka sahihi yake.

Kimsingi nyaraka hiyo ili iwe halali kwa ajili ya malipo halali kwa fedha za Serikali inatakiwa kuwa na sahihi nne kama ifuatavyo Mwenye mali, kiongozi wa eneo, mthamini mali na mtaalamu wa michoro. Mantiki ya waliotajwa kuweka sihihi zao ni kuthibitisha taarifa zilizojazwa katikan yaraka husika. Na endapo tarifa hizo itagundulika baada ya malipo kuwa kuna hitilafu yoyote, vyombo husika viweze kufanya ufuatiliaji. Nyaraka ya pili inayotakiwa kujazwa ni VAL FORM 2 ambayo taarifa zizlizoma katika VAL FORM 1 huhamishiwa katika nyraka hiyo na kisha mahesabu tya kiwango cha fidia hukokotolewa. Mkokotoa mahesabu hutakiwa kuweka sahihi yake. Anayekagua hesabu hizo pia hutakiwa kuweka sahihi yake na mwisho Mthamini Mkuu wa Serikali hutakiwa kuweka sahihi yake na mhuri.( Tazama Attachments za mmoja wa waliolipwa jinsi nyaraka walizojaza watumishi wenyewe zisivyokuwa na sahihi zozote). Kwa mliwaji huyu kwa kutumia nyaraka hizi zisizo kuwa halali ikatayarishwa hati ya malipo na kisha hundi ya malipo ya fidia ya Shs 12,463,800/= Milioni Kumi na Mbili Laki nne sitini na tatu na Mia nane tu) zikiwa fedha za Serikali. na hivi ndivyo ilivyotkea kwa mradi mzima wa kuwafidia kaya 259 kwa mtindo huu.


Katika hali inayoonyesha kuwa viongozi na watumishi wa Wizara ya Ardhi washirikiana kufanya ufisadi waliwalipa waaathrika 259 wa mradi wa Luguruni zaidi ya Shs Bilioni moja za Serikali kama fidia pasipo nyaraka hizi kutumika. Nadhani watalamu wa mahesabu watanisaidia kuwa mafisadi hawa walitumia nyaraka zipi kama supporting documents kwa malipo hayo.

Licha ya fidia hizikuwa finyu bila aibu mafisadi hawa wakawapatia waathrika hawa notisi ya siku 30 wawe wamehama kutoka katika eneo huiska. Sheria ya Ardhi na 4 ya 1999 inataka notisi kuwa ya siku 90. Kwa hakika this was “man made disaster”. Ilibidi wanaharakati tuingilie kati to preveny man made disaster. Tulipiga kelele kiasi cha kumvuta Mhe Jiohn Magufuli, ambaye alitembelea eno hili tar 17 Januari 2008 na kuquash the “illegal demolition order”. Akawaruhusu wananchi kuendelea kuisha eneo hilo hadi hapo atakapo toa tamko lingine. Na akakabidhi majina yote ya waliolipwa kwa vyombo dola kwa uchunguzi zaidi. Maskini hii ndio ilikuwa kazi ya mwisho Mzee Pombe pale Ardhi. Mama Sijaona Katibu Mkuu alikerwa sana na intervention ya Mzee Pombe akamtumia Ndg Luhanjo Katibu Mkuu kiongozi kumuundia wizara ya kitoweo, ili aweze kuwanusuru mafisadi wake.

Kutokana na evidence tuliyoweza kugather, ilimbidi Mhe John Chiligati aagize ufanyike uthamini mali upya kwa kuleta wathamini wapya kabisa na wake wa zamani kufichwa ofisisni badal ya kuchukuliwa hatua zozote za kinidhamu au kisheria. Uthamini wa mali mopya ulifanyika kwa kutumia nyaraka za Serikali halai yaani VAL FORM 1 & 2. Zoezi lilizaa malipo ya fidia ya nyongeza ya kati ya 85 to 600%; Kutoka Shs 300 to 2000/= per sq metre, au from Shs 1.2 M to 8.0 Milion per acre.

Swali hapa lilibaki fedha hizi za wananchi zilikuwa wapi? Nani alikuwa nazo? Zilihifadhiwa wapi? N.k Cha kushangaza licha ya Serikali kulazimika kuingia gharama za kufanya uthamini wa mali upya na kulipa fidia za nyongeza hakuna mtumishi hata mmoja ambaye amechukuliwa hatua zozote za kinidhamu au kisheria? Watumishi walifanya vitendop hivi waliondolewa briefly kupooza hasira za wananchi then wakaendelea na mradi huu eneo la Kwembe ambako walirudia ufisadi huu na mwingine mwingi.

Jatropha thanks kwa taarifa. imetulia. Mafisadi Kila Kona wapo. Bahati Mbaya tumebakia na vita vya baadhi ya watu badala ya MFUMO MZIMA wa UTAWALA.
 
Jatropha thanks kwa taarifa. imetulia. Mafisadi Kila Kona wapo. Bahati Mbaya tumebakia na vita vya baadhi ya watu badala ya MFUMO MZIMA wa UTAWALA.

Chuma,

Mimi imani yangu siku zote iko kwenye kubadili mfumo. na Sio watu kwa kuwa wote Mafisadi tu...

Ukiwauliza umeingia/unaingia kwenye siasa kwa sababu gani atasema nataka baadaye niwe waziri, niwe rais sio niweze kutumikia wananchi.

Kazi kwetu ni kuchagua wabunge wenye vichwa vizuri wakatunge sheria nzuri... sio wabunge wengi wa sasa wakati wa kujadili mswada wanasema wanaomba mradi blah blah... badala ya kujadili muswada kifungu kwa kifungu kama wabunge wachache sana less than 10% wanavyofanya.
 
Yebo Yebo Are you Serious? You must have a stake in this, or else you are among the dubious officers of Ardhi.


Mkuu GT na wengine...

Mara ya mwisho Title Deed yangu ulichukua miezi 6 lakini kwa kiwango kikubwa ni kwa sababu nilikuwa nje ya nchi hivyo sikuweza kufuwafuatilia kila wiki.

Siku nilipokuwa likizo na kuamua kuifuatilia nilienda Wizarani moja kwa moja, gorofa 5 kama sikosei, dirishani nikawakuta wahudumu 2 (wa kike na kiume), yule wa kike akachukua kitambulisho changu, na pia akanukuu namba ya Offer Letter kwenye kikaratasi, akageuka nyuma na kufungua droo iliyokuwa imejaa mafaili. Akachomoa faili moja lenye Title Deed yangu, akaniambia weka sahihi hapa....nikaweka sahihi nikatia faili kwapani nikatokomea zangu. Utaratbu wote siku hiyo haukunichukua dakika 10...

Kesi ya kufidiwa iliwahi pia kunikuta nilikuwa na kiwanja maeneo ya Pugu (sitasema kwa undani zaidi ya hapo), ingawa sikuwa na furaha kiwango walichonifidia lakini niliridhika kwa sababu eneo lenyewe halikuwa na kitu cha dhamani kama nyumba au mazao na pia, iwapo Serikali isingelichukua na kunipa fidia pengine wanakijiji wangeliuza na kunidhulumu eneo langu...kwa hiyo niliona bora nimepata chochote...huu mchakato nao ulichukua miezi kama 3 au 4; hili pia sababu kubwa ni kuwa sikuwepo nyumbani kufuatilia.

Huu ndio msingi na sababu ya kauli yangu kwamba Arthi kumebadilika sio kama zamani.

Ningependa kumalizia pengine mimi nilikuwa sina haraka [sio kwamba ni kosa kuwa na haraka] na ndio maana sikuona shida au pengine nilikuwa na bahati. Ila ninachojua ni kuwa sijawahi kuhonga hata senti 1 kwenye kesi hizo mbili.
 
Kwa maendeleo ya hivi karibuni wameteue assistant commissioners of lands kwa kila kanda, mbeya, dsm , mwanza na arusha kwa maana hiyo hati inaandaliwa na manispaa husika , inasainiwa na kamishna aliyeko kwenye kanda husika, inasajiliwa na msajili aliyeko huko, hakuna haja tena hati zote kusainiwa dsm

kama mpango huu ulioanza march 2009 utafanikishwa hati inaweza kuandaliwa kwa wiki moja, kamishna wetu hapa mbeya somebody luvanda amefika tayari na msajili tunae bwana kessy, nasikia hati za mwanzo zinatoka chapuchapu

Nyie wa huko Mbeya pengine mna bahati mambo yenu yanaimprove; sisi huku Singida it is still a nightmare to dream of getting your tittle deed!! Kuna syndicate ya watu wa ardhi hapa toka kwenye manispaa mpaka kwa mshauri wa ardhi pale mkoani ; kazi yao ni rushwa tu mimi naifahamu kesi ya mtu amekwisha liwa zaidi ya shilingi millioni lakini afisa wa ardhi bado wanamzungusha kupata title zake!

Chiligati na mama Sijaona pengine hawajui haya na kumbuka Chiligati anatoka mkoa wetu!
 
Jamani kabwe kaisha sema tutengeneze manati. Sasa wezi kama tunawajua kama rostam ni suala la kumpiga jiwa na manati walau atoke nundu kichwani na ikishindikana tutumie mishale.
 
naomba kujua kama nina kiwanja nataka kuapata hati ya kiwanja/title deed ni bei gani wanacharge hao watu wa ardhi?including some rushwa.

dudu
 
naomba kujua kama nina kiwanja nataka kuapata hati ya kiwanja/title deed ni bei gani wanacharge hao watu wa ardhi?including some rushwa.

dudu

Teh teheeee, mkuu umenivunja mbavu, kwani rushwa inakiwango? labda nao kama wameisha fikia daraja moja na traffiki ambao rushwa yao inajulikana ni book mbili, nasikia wengine hadi wanarudisha chenji. kwa hao ardhi sijui mkuu, but, usiwaendekeze, wakikuomba rushwa wabebee za moto!
 
sorry mkuu key board iliteleza nilikuwa namaanisha excluding rushwa.nilikuwa nataka kujua bei ya kupima ina range vipi
 
Mwenye matatizo yake ayaweke hapa, kisha aseme amemwona nani, na nani, na nani, na nani, nani alifanya nini, wakati gani, bosi akasema nini... hatua kwa hatua, mpaka kieleweke! Hawa watu si wa kuwaonea haya hata kidogo.... mishahara yao inatokana na KODI ZETU.... wako hapo KWA AJILI YETU.... wasitufanya sisi wajinga.... wakati wa kusema HAPANA umefika.... tajeni LIST OF SHAME ya hii wizara na nyingine zote!

./Mwana wa Haki

P.S. Ina maana hata mimi nitakaponunua kiwanja nitapata usumbufu wa aina hii? HAIWEZEKANIIIII!
 
mnapiga kelele tuu hapa mwatu wakianza kudrop majina mtaanza off haifai ohh hamisha ohhh this is not the way to go
 
GT,
Mkuu mimi niliwahi pata Title deed mwaka 1984 kiwanja Kitijonyama.. mwaka 1986, tulikuwa watu wanne wenye title deed kiwanja hicho hico.. wenzangu walikuwa ktk system ilibidi nikiteme na kumwachia Mungu..
Haya hayakuanza jana mkuu wangu sema mbinu ndizo hubadilika lakini siku zote Mlalahoi (mwenye kipato cha chini) ndiye hukamuliwa..
 
GT,
Mkuu mimi niliwahi pata Title deed mwaka 1984 kiwanja Kitijonyama.. mwaka 1986, tulikuwa watu wanne wenye title deed kiwanja hicho hico.. wenzangu walikuwa ktk system ilibidi nikiteme na kumwachia Mungu..
Haya hayakuanza jana mkuu wangu sema mbinu ndizo hubadilika lakini siku zote Mlalahoi (mwenye kipato cha chini) ndiye hukamuliwa..

Mkuu 1984 bado nipo secondary, hata mawazo ya kibanda cha kuku sikuwa nayo!
 
Mimi nina kiwanja Tegeta siku nyingi sana. Mwezi wa pili mwaka huu nilienda ardhi kuomba hati (kilishapimwa) nikaambiwa kuwa "FILE" limepotea. Chakushangaza ni kuwa wanazo details zangu zote kwenye systems/PC zao sasa sijui tatizo lipo wapi. Yaani kila nikienda napigwa kalenda tu...
PALE KUMEOZA!!

Nitalianika jina la huyu dada anayenisumbua nikienda tena!!
 
Pale ardhi pana Tool (kompyuta program) ya kuingiza kero. Hivi bado ipo? Hizo kero zinafanyiwa kazi? Wapeni PCCB washughulikie!
 
MAFISADI wizara ya ARDHI

Game Theory
user_online.gif
10th March 2009, 08:04 PM

Naam GT nimerudi tena baada ya kutoka THA ambako tayari Mheshimiwa JK anapashughulikia nadhani it would be fair tukahamia kule wizara ya ARDHI ambako haijulikani kwa nini TITLE DEEDS zinachukua karne kutoka,MAFAILI YANACHOMWA MOTO/ AU YANAPOTEA kwa kusudi ili kuwe na delays na matokeo yake wananchi ambao kipato chai ni cha chini wanalazimishwa kutoa RUSHWA

sasa nadhani its about time tukawaname and shame wahusika pale na kama wenye JF mkiamua kuihamisha au kuamua kuibadilisha header kama ile thread ya THA na rushwa then hatuna budi kusema kuwa mtakuwa ma mafisadi kama hao ambao tunajaribu kuwa expose

Tatizo si wao bali waliowaweka hapo.

Kamanda
 
Back
Top Bottom