Mafisadi + CCM ngao imara ya Freeman Mbowe

Status
Not open for further replies.

Ni kweli GQ,

Lakini pia, alichoandika huyo siku ikifika hapa JF kwa muda sasa (Soma post zake), kina uhusiano na yaliyotokea kwenye kampeni ya Zitto ya kutaka uenyekiti wa CHADEMA.

Labda Jokakuu anampa Zitto nafasi ya kumkana sikuikifika hapa JF.
 
Asante sana Phillemon Mikael.

Umenena mambo ya maana.

Hata mke na mume wanakwaruzana ndani ila wakitoka nje wanacheka.
 
PM amini usiamini makada wa chama cha kijani wako hapa kazini kama kawaida yao na mimi ni mmoja wa wale wanaopuuzia ujinga wao.
Wajinga ndio watanaswa na mtego wao!
Hapa ni akili mkichwa. Kaa mbali na kanda mbili na kundi lake!
 
Naomba kumuuliza huyu mjinga aliyeandika pumba hizi hivi hawa wachaga waliojaa kila idara za serikali, mashirika ya umma na hata TRA je wamewekwa na Mbowe pia?
Wacha nchi tuwape wachaga kuliko wakwere wezi!
 
PM amini usiamini makada wa chama cha kijani wako hapa kazini kama kawaida yao na mimi ni mmoja wa wale wanaopuuzia ujinga wao.
Wajinga ndio watanaswa na mtego wao!
Hapa ni akili mkichwa. Kaa mbali na kanda mbili na kundi lake!

MF,

Ni ukweli usiopingika kwamba watanzania wengi wanaopenda kuona ustawi wa demokrasia ya kweli nchini walitegemea sana chama kama CHADEMA kuwa mfano wa kuijenga demokrasia ya kweli.
Lakini tulichoshuhudia katika kipindi hiki cha vuguvugu la uchaguzi ndani ya chadema ni vituko juu ya vituko.
kwahiyo kuna watu wamesikitishwa kwa namna wazee wa chadema walivyotumia busara zao kumshinikiza Zitto ajitoe kugombea uenyekiti wa chama chake, ingawa pia kuna wale ambao wamefurahia uamuzi huo.

Kwahiyo sidhani kama wote wasiokubaliana na uamuzi wa wazee wa chadema watakuwa ni ccm, au wanatumiwa na mafisadi. Kuna wanachadema wazalendo tena kwa nia safi kabisa wamepingana na busara za wazee wa chadema na ambao walikuwa wanamuunga mkono zitto na bado wataendelea kumuunga mkono.

kwahiyo sio kila anyeonekana kuwa against na mbowe mnamshambulia kuwa ccm, fisadi na mambo mengine kama hayo ingawa pia ccm wanachekelea kuona chadema mnavyokorogana.

CCM kwa upande wao wanaendesha mchakato wa kura za maoni kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa, na wamechapana makonde sana huko lakini watu hawawafuatilii kama wanavyowafuatilia chadema, kuna sababu ya msingi watu kufuatilia uchaguzi wa chadema na si kufuatilia mambo ya nambari wani.

watu wangetegemea kuona demokrasia inashamiri ndani ya chadema na zaidi sana watu wanataka wajivunie kuwa na chama mbadala wa ccm na chadema kilionekana kuwa mbadala, sasa huu mtafaruku wa uchaguzi usiwafanye mkaanza kuvuana nguo, safari bado ni ndefu na ndio kwanza mnaanza kupiga hatua.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…