Mi inaonekana siridhiki, na sitakaa nifanikiwe kimaisha (sijui wenzangu), maana;
Mwaka 1995 (form 1); niliamini siku nikiweza kusoma hadi nikafika chuo kikuu cha SUA nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha...
Mwaka 1998 (form 4); wakati wa kombe la dunia, niliamini siku na mimi nikwa nakaa kwenye nyumba yangu (hata chumba cha kupanga), huku nikiwa na TV yangu naangalia kombe la dunia, nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha...
Mwaka 2000 (form 6, bado sijafika SUA, sina TV), nikaongeza 'hitaji', kuwa siku nipate kazi, niwe najitegemea nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha
Mwaka 2002 (first year SUA); niliamini siku nikifanikiwa kuajiriwa kama mwalimu wa chuo kikuu nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha
Mwaka 2006 (4th yr, SUA); niliamini siku nikiwa na ajira inayonilipa kama laki nne hivi nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha
Mwaka 2007 (graduating SUA), niliamini siku nikiwa na ajira, nikaoa mke ninayempenda, nikawa na gari aina ya chaser, nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha
Mwaka 2008 (nimeshaajiriwa, nimeshaoa), niliamini siku nikiwa na mtoto, nikiwa na Masters, nikiwa na ajira nzuri zaidi... nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha...
Mwaka 2010; ninaamini siku nikiwa na nyumba yangu mwenyewe (ghorofa), kipato cha kutosha niende ninapopenda wakati wowotena mke wangu, nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha...
2011; ???
2012; ???
n.k ...
Conclusion; Asilimia 99 ya vitu nilivyokuwa natamani hadi 2008 nimeshavipata, lakini kwa sasa najiona niko duni sana kimaisha, natamani, natamani natamani, na natamani niibadilishe Tanzania ifanane na Netherlands (can you imagine?!!)
Nikiwaza watu 'waliofanikiwa' kimaisha (kifedha), wanavyoendelea kufight kutafuta pesa, nikiangalia watu waliofanikiwa kijamii na kisiasa wanavyoendlea kutafuta kufanikiwa zaidi, inabidi niamini hakuna siku nitakokaa 'nifanikiwe kimaisha'
Decision; Nimeamua kuwa nitatumia 60% ya kipato changu 'kuifurahisha nafsi yangu na ya familia yangu na 40% kuwekeza kwa ajili ya baadae, maana nimeshaona kuwa hakuna siku nitakayorizika eti nimeshavuna sasa nianze kula...
...ahsante sana gaijin kwa ufafanuzi wako...dahhh,....angalau nakuangalia kwa jicho la afadhali yako unayejua dira ya maisha yako..hongera sana...
nadhani definition ya "mafanikio kimaisha" inatofautiana mtu na mtu kwa sababu inakuwa influenced na vitu vingi sana ikiwemo malezi, mazingira mtu aliyokulia, utamaduni wa eneo husika, pamoja na elimu
m
Huwa inasikitisha sometimes mtu yuko radhi kuvunja mahusiano kwa ajili ya pesa 'ndogo' kwake... Kwa mfano mtu ana kipato cha zaidi ya laki nne kwa mwezi, lakini yuko radhi agombane hata na mtaa mzima kwa kukataa kuchangia 3000 za kufanya lets say ukarabati kwenye mtaro wa maji machafu hapo mtaani!
...umesema vyema.
sasa utawezaje kuyachanganya hayo yote kuweza kufanikisha maisha yako?
MbuKusema ukweli, kufanikiwa kimaisha (being successful) is a very subjective term ambayo mara nyingi huwa pia inategemea na societys standards. Kwa wengine mafanikio au kufanikiwa inamaanisha kuwa responsible, you make more than enough to pay your bills, you're married with children, you have a college degree and you have a prestigious job. Sure, kila mtu atakuangalia na kukudefine kama mtu mwenye mafanikio. Mara nyingi wengi wetu tunaishi kwa jinsi jamii inavyotumould na kujikuta mtu unajihesabu umefanikiwa kwa kuangalia acknowledgement ya wengine kwako kuwa umefanikiwa. Kwamba kwa wewe kujiita mtu aliyefanikiwa ni lazima kuwe na a general acknowledgement kutoka katika jamii, mfano watu wengi tunamwona Mzee Mengi kama mtu mwenye mafanikio sana
Lakini kama alivyosema Gaijin hapo juu nani alishawahiuliza kama hawa tunaowaona wana mafanikio kama wana furaha, upendo na amani ndani ya mioyo, familia na nyumba zao?
So to me, being successful ni kuweza kuishi maisha yako to the fullest, ukiwa happy, umezungukwa na amani na upendo no matter una pesa kiasi gani, elimu kiasi gani au materials gani. Uwe na amani, upendo na furaha kiasi cha kuweza kufulfil malengo yako uliyojiwekea maishani.
Mhhh mkuu Mbu
Safari ya maisha bado ndefu sana na haina mahali utasema hapa nimefikia mwisho.
Hata safari yangu ya maisha japo nina vitu basic ambavyo ni vya muhimu kwa maisha bado natamani hiki na kile
Bado natamani niwe na kile na kile na hiki na hiki
Kweli maisha ni safari na sidhani kama nitafikia sehem ambako nitasema hapa nimefikia kilele cha mafanikio.
peace of mind is everything to me
Angalia kule Hollywood ambako watu wengi wa kule wamejaliwa kila kitu lakini asilimia kubwa unakuta maisha yao wengi wao yamejaa migogoro ya aina mbali mbali na hivyo kusababisha hata ndoa za nyingi zisiwe za muda mrefu na mafanikio.
Tuko,good analysis. Kuna ndoto tumeota tukiwa watoto,some of them tumezipata tukagundua it was nt such a big deal. Mwisho wa siku u lead ur heart and follow through. Nakubaliana na mwl pia.kuwa na amani na upendo ndo mafanikio muhimu kuliko yote kwangu,japo kuna basic materials ambazo zisipokuwepo amani inatetereka.hata kama itabidi mie kushuka ama kupunguza priority zangu ili amani iwepo nitajisikia kufanikiwa
...umezungumza mambo ya msingi sana mwj1...
mzee wangu bw mengi namjua mapungufu yake maskini,...acheni tu ajifaidie pesa zake mzee wa watu...ametokea mbali,
bahati mbaya ndio hivyo tena, maisha sio kama vile tunataka yawe...
nisingependa kumjadili mtu, ila nitagusia tu kwamba pamoja na mafanikio yote, failed marriage, losing a dear son,
na mengineo ya hapa na pale pia ni disappointments ambazo kwa kiwango kikubwa zina athari kwenye
mafanikio ya mtu... au?
hilo la amani na upendo kiasi cha kufulfil malengo uliyojiwekea inapingana na ile hoja ya mafanikio ya mtu kwenye jamii zetu yanatokana na muonekano wako wa nje.
hudhani hilo litakupelekea kuwa "a slave" of your own success?..mfano; Michael Jackson pamoja na kutufurahisha mamilioni ya watu tangu miaka ya 70's kwa cheza kwa stepu...kumbe mwenzetu alikuwa hawezi kulala bila chloroform, like wise kwa kina Elvis Presley, nk...
...umesema vyema.
sasa utawezaje kuyachanganya hayo yote kuweza kufanikisha maisha yako?
The whole trick is in balancing. Don't chew more than u can bite,no matter how tempting it looks
Hii thread inanisaidia sana kupanua wigo wa uwezo wangu wa kufikiri. Aksante Mbu kwa kuileta na aksante Gaijin na wachangiaji wengine.
Gaiji umezungumzia aspect ya mahusiano. Nadhani happiness inafall pia kwenye hiyo aspect na vile vile success kwenye angle hiyo inatofautiana kwa mtu na mtu.
Kwa upande wangu, mafanikio kwa upande huu ni kuwa na mahusiano mazuri (nikimaanisha kimapenzi zaidi) kwani naelewa hii huchukua sehemu kubwa ya maisha ya binadamu. Pamoja na kuwa na mwenza anayekuthamini, kujali na kukupenda but awe pia ni mwenza niliyempenda for who he is and not what he can give or make me..............na mwenza huyo akalitambua hilo na kulithamini. Si kuwa na mtu anayehisi kuwa you are after something from him, kitu ambacho kinawezasababisha akaabuse love yako. Na itakapotookea kuwa sijabahatika kumpata mtu wa aina hii haimaanishi sitojihesabu myself as successful kwa sababu nitajiaminisha kuwa at least I tried. I will sit down na kumshukuru MUNGU kuwa haya ndio maisha alonipangia so yasi-get into my way ya kujiona mwenye mafanikio.
...umenigusa kwenye jambo la muhimu sana maishani mwangu.
nadhani binafsi katika kitu muhimu kinachokosekana maishani mwangu kuweza ku justify
mafanikio ya maisha yangu ni mwenza wa aina hiyo....pheewww!
mwj1 tuoane basi, nipo tayari kukuombea talaka kwa mumeo...lol!