Mtangoo
JF-Expert Member
- Oct 25, 2012
- 6,163
- 5,623
Kwa chereko nyingi tu niwapongeze wasimba au kwa kiswanglish wanaitwa madevelopa wa Bongo kwa mambo makubwa yaliyofanyika nchi hii. Kwa kweli tunahitaji pongezi sana. Kwa wale wasiojua mafanikio yetu nitaweka machache ili waungane nami kutupongeza:
Kabla sijafunga naomba kujua kiswahiki cha neno Satire...!
Wasalaam
OPed on LinkedIn
- Tumeondoa kabisa longolongo na utapeli. Sasa hivi madevelopa wa Bongo tuko vizuri kabisa. Utapeli umeisha asilimia 100%. Madevelopa tunapiga kazi bila utata na tunamaliza kwa muda. Kama wapo ambao ni matapeli, asilimia haifiki tano (5%). Makofi Tafadhali!
- Tunajua kugonga vitu kwenye "Code". Yaani we leta tatizo lolote na tunalitatua. Tunajua kuweka mambo katika mstari. Yaani tuko vizuri kona zote. Ukiona kuna anayeleta longolongo hajui kuandika Code vizuri huyo ndio wale wa chini ya asilimia 5!
- Tuna sauti Moja. Yaani hata ulaya tumewapiga gepu. Kuna "meetup" kibao zipo na tuna ushirikiano sana. Kiukweli tumepiga hatua sana katika hili. Ukiwa unahitaji msaada kwa muktadha wa Kibongo utaupata fasta! Tuna forum nyingi za kibongo na zimefanikiwa saana. Hatutaki ujinga kabisa na hivi karibuni tutaipita stackoverflow!
- Kwa sababu ya umoja wetu huu tumeweza kuifikia hata serikali na kuomba serikali ibadilishe baadhi ya sheria ambazo zimekuwa kikwazo kwa maendeleo ya Teknohama Bongo.
Kabla sijafunga naomba kujua kiswahiki cha neno Satire...!
Wasalaam
OPed on LinkedIn