Maeneo ya kambi za wakimbizi kurejeshwa Serikalini

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamis Hamza amesema Serikali inaendelea na jitihada za kupunguza tatizo la wakimbizi Nchini kwa kuwarejesha makwao wakishirikiana na Jumuiya za Kimataifa na Nchi wanazotoka

Akiwa Bungeni Dodoma, amesema "Baada ya Wakimbizi hao kuondoka maeneo yote ya kambi yatarejeshwa Serikalini ili Mamlaka husika ziweze kuyapangia matumizi stahiki"

Aidha, amesema hakuna mgogoro wa ardhi baina ya Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu na Kata ya Makere. Ameeleza hayo akimjibu Mbunge wa Kasulu Vijijini aliyehoji ni lini Serikali itatatua mgogoro huo
 
Back
Top Bottom