Maeneo mengi wilaya ya Temeke yakosa umeme kwa zaidi ya masaa 24

mchakavumlasana

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
389
212
Ndugu TANESCO.

Ni masaa 24 sasa toka mkate umeme huku Kijichi

Asante kwa kasi ya kuangaza maisha maana baadhi yetu askrimu zimeyeyuka, wateja tumekosa, senti mbili tatu tayu.

Hapa yamebaki mawazo tu.

Habari wakuu,

Tangu jana baadhi ya maeneo ya wilaya yaTemeke hakuna umeme na watu tulio wengi hatujui chanzo cha kukosekana kwa umeme katika mitaa yetu.

maeneo ambayo hakuna umeme ni Vetenari,Mwembeyanga,Deviscorner,Tandika,Mtoni,Mbagala na baadhi ya mitaa ya temeke.

Tanesco tupeni taarifa rasmi tatizo ni nini na lini mtaturudishia huduma?
 
Wanasema transformer imeungua na hawajui utarejea lini ila mafundi wapo kazini, tuombe Mungu atusaidie
 
Kwani wewe hukuwa na taarifa kuwa kituo cha kupoozea umeme huko Mbagala kimeungua.
 
Mkuu hilo tatizo limeenea mpaka temeke, mtoni, na tandika.. Nasikia walitangaza kuna hitilafu imetokea kwenye substation ya mbagala huko.. Na mafundi wanaendelea kurekebisha.. Ila hawajasema litaisha lini..
 
Ndio matatizo ya kutosikiliza Radio na kuangalia taarifa za Habari,Jana ITV walitangaza kwamba kuna kituo cha umeme kimeungua mbagala.
 
tatizo letu watanzania tunajifanya wajuaji.unadhani lawama mitandaoni zitasaidia? piga kwa emergency ili uweze kujua kuna tatizo gani na tujenge utaratibu wa kusikiliza vyombo vy habari
 
38833.jpg
38833.jpg
38833.jpg
38833.jpg
pole mpaka umenua kila k2
huu umeme Mbagala ni majanga sasa sijui usiku kutalalika?
 
.....jana usiku kituo cha kupoozea umeme Mbagala kiliungua moto,hivyo maeneo ya mbagala na kigamboni kukosa umeme,Tanesco wanaendelea kulishughulikia hilo.
#rilaxx!
 
Hovi tanesco hawanaga plan B???

Maana kama ubungo au huko kinyerezi yakitokea ya mbagala nchi si itakuwa gizani?

Inaudhi sana unelipia huduma halafu hupati na watu wapo comfortable kabisa kusema kituo kimeungua....(hitilafu hazina budi kutokea)...ila plan b ni nini????
 
Back
Top Bottom