Maeneo haya yakiboreshwa, yatapunguza foleni mahospitalini pamoja na umauti kwa wagonjwa

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,474
40,474
Nimejaribu kutembelea baadhi ya mahospitali, changamoto kubwa niliyokutana nayo ni msongamano wa wagonjwa, kuwa kwenye foleni ili kupata huduma.

Wengine wanakuwa wametoka majumbani tangu asubuhi na wanamaliza siku nzima wanakuwa hawajapata huduma kwa wakati.

Kwa mtazamo wangu, hii changamoto inaweza kutatuliwa kwa kufanya yafuatayo, ingawa ni gharama lakini italeta unafuu kwa wagonjwa:-

A. Mapokezi
Angalau kuwepo na madirisha kumi kwa ajili ya mapokezi, ili kuepusha msongamano wa wagonjwa (foleni) pamoja na kupunguza adha au maumivu makali kwa mgonjwa aliyezidiwa au anayekaribia kuzidiwa; aweze kupata huduma haraka ili kuepusha umauti.

B. Madaktari
Kuwepo na 'section' angalau tano za madaktari wanaosikiliza wagonjwa, pamoja na kutafsiri vipimo vya maabara ili mgonjwa aweze kuanza tiba kwa haraka. Hii itaepusha misongamano ya wagonjwa kusubiri kuingia kumuona daktari mmoja; na pia itaepusha adha na umauti kwa mgonjwa.

C. Maabara
Angalau kuwepo na watu kama watano kwa ajili ya kuchukua 'sample' kwa mgonjwa na kufanyia vipimo; hii itaondoa misongamano na kumuwaisha mgonjwa kupata huduma kwa wakati pamoja na kuepusha vifo.

D. Matibabu
Kama sehemu A, B na C zitatekelezwa kwa ufanisi na kwa haraka, wagonjwa wengi watapona kwa kupata matibabu kwa wakati na kuepusha vifo visivyokuwa na ulazima.​
 
Mkuu hayo umesema vzr lkn utekelezaji wake mgumu maana Kasi utoaji wa ajira ni ndogo, VP kuhusu Vitendea Kazi vipo? Yaani lawama zinarudi kwa serikali maana uhaba wa vifaa tiba na watumishi ni juu yao
Ukitatua hapo Basi umefaulu pakubwa Sana
 
Back
Top Bottom